Upload
jackson-m-audiface
View
41.088
Download
15
Embed Size (px)
Citation preview
Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii ya Wizara ya Nishati na Madini
Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]
Habari za nisHati &madini
Toleo No. 90 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Oktoba 23 - 29, 2015
BulletinNews
Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya Nishati na Madini
Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]
http://www.mem.go.tz
HABARI ZA NISHATI &MADINI
Toleo No. 51 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Tarehe - 23-29 Januari , 2015
JWTZ wapongezwa kunusuru mtambo wa Msimbati-Uk4
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, anayeshughulikia Madini Stephen Masele
Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Charles Kitwanga
Mkurugenzi Mtend-aji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba
Mkurugenzi Mkuu wa REA, Dk. Lutengano Mwakahesya
Wabunge Soma habari Uk. 2
Waimwagia sifa MEM, TANESCO, REA
WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AZINDUA RASMI BODI YA TANESCO -Uk2
Soma habari
Uk. 2Serikali kukomesha uchimbaji, uuzaji haramu madini
UMEME waongezeka Gridi ya Taifa
Mitambo ya kuzalisha umeme Kinyerezi I
2 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini
Zuena Msuya na Nuru Mwasampeta S
hirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limewasha mtambo mwingine wenye uwezo wa kuzalisha umeme wa kiasi cha Megawati 35 na
hivyo kufikisha jumla ya Megawati 70 zinazozalishwa kutokana na gesi
asilia inayotoka Madimba hadi kituo cha kufua umeme cha Kinyerezi I jijini Dar es salaam. Megawati 35 za awali ziliwashwa mnamo tarehe 17 Septemba, 2015.
Akizungumza kituoni hapo Meneja mradi wa Kinyerezi I, Mhandisi John Mageni amesema mtambo huo umewashwa ili kuendelea kuimarisha upatikanaji wa huduma ya umeme nchini kwa kuwa hivi sasa vyanzo vya maji vinavyotegemewa kuzalisha umeme vimeanza kukauka kutokana na ukame.
“Huduma ya umeme itaendelea kuimarika kwani sasa tunawasha mtambo namba 3 baada ya kukamilika kwa kuufanyia majaribio yote na kuridhika nayo kwamba uko tayari kuanza kazi ya uzalishaji wa umeme na hivyo kuongeza kiwango cha umeme unaoingia katika gridi ya taifa,” alisema Mageni
Aliongeza kuwa kwa sasa mkoa
wa Dar es Salaam unapata umeme wa uhakika baada ya kuwasha ule mtambo wa kwanza wa megawati 35, hivyo zoezi la kuwasha mitambo iliyosalia ili kufikisha Megawati 150 litaendelea ili kuimarisha huduma ya upatikanaji wa umeme nchini nzima.
Alisema pindi mitambo yote itakapowashwa katika kituo hicho itakuwa na uwezo wa kuzalisha umeme kiasi cha megawati 150, ambazo zimeanza kuingizwa katika gridi ya taifa.
Kituo cha Kinyerezi 1 kilizinduliwa tarehe 13 Oktoba, 2015 na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete ambaye aliitaka Tanesco kuongeza kasi ya kuzalisha umeme unaotosheleza mahitaji ya Watanzania.
Mitambo miwili kati ya minne inayokamilisha Kinyerezi 1 imewashwa na miwili iliyosalia itaendelea kuwashwa kadri siku zinavyoendelea.
Megawati 35 zaongezwa Kinyerezi I
Mohamed Saif na Clinton Ndyetabula
Imeelezwa kwamba Serikali imejizatiti katika kuhakikisha inakomesha uchimbaji na uuzaji haramu wa rasilimali ya madini yaliyopo nchini kwa manufaa ya
sasa na ya vizazi vijavyo.Hayo yameelezwa hivi karibuni
na Kamishna Msaidizi wa Madini sehemu ya Leseni, Mhandisi John Nayopa kwa niaba ya Kamishna wa Madini wakati wa ufunguzi wa warsha kuhusu utekelezaji wa mpango wa kupambana na uchimbaji haramu wa rasilimali kwa nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR) ujulikanao kama ICGLR Regional Initiative Against Illegal Exploitation of Natural Resources (RINR).
Mhandisi Nayopa alisema lengo la warsha hiyo ni kufafanua hatua ya utekelezaji wa mpango wa RINR kwa kuzingatia mazingira ya Tanzania; kuongeza uelewa wa wadau kuhusu
mpango wa RINR, na kuandaa mpango kazi sahihi ikiwa ni pamoja na mkakati wa utekelezaji wa RINR nchini.
Alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi 12 za Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR) ambazo zimeridhia itifaki zenye lengo la kuimarisha amani, utulivu, demokrasia na utawala bora kwenye nchi husika.
Alisema Wakuu wa Nchi 11 za Jumuiya ya Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR) walikutana jijini Dar es Salaam mwezi Oktoba, 2014 na kukubaliana kwa pamoja kuimarisha maendeleo, usalama na utulivu jambo ambalo anasema linathibitisha dhamira yao ya kubadilisha ukanda wa Maziwa Makuu kuwa na amani endelevu kwa mataifa hayo na kwa wananchi wake, ikiwemo utulivu wa kisiasa na kijamii na ukuaji wa maendeleo ya pamoja.
Mhandisi Nayopa alisema makubaliano hayo yanaitwa Tamko la Dar es Salaam, la Mwaka 2014
ambayo yanajulikana kama The Dar es Salaam Declaration of 2014.
“Ili kufanikisha hili, nchi za ICGLR zilisaini makubaliano ambayo yalizaa itifaki mbalimbali na miongoni mwake ni itifaki ya kupambana na uchimbaji haramu wa madini,” alisema Mhandisi Nayopa.
Alisema kwamba mojawapo ya changamoto kuu kwenye baadhi ya nchi za ICGLR ni kukithiri kwa uchimbaji haramu wa madini jambo ambalo linatumika kuchochea migogoro na pia ni chanzo cha fedha kwa wababe wa kivita.
Mhandisi Nayopa alisema Tanzania imejaaliwa rasilimali nyingi ambazo zinapasa kuleta maendeleo endelevu kwa jamii na Taifa kwa ujumla ikiwa ni pamoja na kukuza uchumi utakaoleta mabadiliko chanya.
“Licha ya mafanikio ambayo Tanzania imekuwa nayo katika kuvutia uwekezaji mkubwa katika Sekta ya Madini na katika kurasimisha idadi
kubwa ya wachimbaji wadogo, bado inakabiliwa na changamoto lukuki,” alisema.
Alisema kupitia Mpango huo wa RINR, Serikali inatarajia matokeo makubwa yenye tija katika kupambana na uchimbaji haramu wa madini yaliyopo nchini. “Lengo letu na matarajio yetu ni kwamba faida zitokanazo na uchimbaji madini zitaongezeka maradufu na hivyo jamii kwa ujumla kunufaika,” alisema Mhandisi Nayopa.
Warsha hiyo ya siku mbili imehudhuriwa na Kamishna Wasaidizi wa Madini kutoka Kanda mbalimbali, watumishi wa Wizara ya Nishati na Madini hususan kutoka Idara ya Madini, wawakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani, wawakilishi wa wachimbaji wadogo na washirika wa Maendeleo wa Canada wajulikanao kama Partnership Africa Canada (PAC).
Kamishna Msaidizi wa Madini, Sehemu ya Leseni, Mhandisi John Nayopa katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha. Wa kwanza kushoto waliokaa ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Mrimia Mchomvu na wa kwanza kulia ni Mwakilishi kutoka PAC, Stephen Turyahikayo.
Serikali kukomesha uchimbaji, uuzaji haramu madini
Washiriki wa warsha wakifuatilia uwasilishaji mada kuhusu utekelezaji wa mpango wa kupambana na uchimbaji haramu wa rasilimali kwa nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR) ujulikanao kama ICGLR Regional Initiative Against Illegal Exploitation of Natural Resources (RINR).
3BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini
TahaririMEM
Na Badra Masoud
Five Pillars oF reForms
KWa HaBari PiGa simU KitenGo cHa maWasiliano
Bodi ya uhariri
MharIrI Mkuu: Badra MasoudMsaNIfu: Lucas Gordon
WaaNdIshI: Veronica simba, asteria Muhozya, Greyson Mwase Teresia Mhagama, Mohamed saif, rhoda James ,
Nuru Mwasampeta na Zuena Msuya
increase eFFiciencyQUality delivery
oF Goods/service
satisFaction oF tHe client
satisFaction oF BUsiness Partners
satisFaction oF sHareHolders
tel-2110490FaX-2110389
moB-0732999263
Makubwa yamefanyika sekta ya Nishati
tel-2110490FaX-2110389
moB-0732999263
Tuzungumzie Gesi Asilia
Wengi tutakumbuka wakati Rais wa Awamu ya Nne Mhe. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete alipoingia madarakani mwishoni mwa mwaka 2005 nchi yetu ilikuwa katika mgawo wa umeme na hadi ilipoingia mwaka 2006 mgawo huo wa umeme uliendelea kuwa mkali.
Mgawo huo ulitokana na kukauka kwa Mabwawa ambayo yanatumika kuzalisha umeme ambayo kwa kipindi hicho ndiyo yalikuwa chanzo kikubwa na pekee cha kuzalisha umeme.
Baadhi ya watafiti na wana mazingira walieleza kwamba kukauka kwa mabwawa hayo kunatokana na sababu kubwa mbili ambazo ni mabadiliko ya tabia nchi pamoja na kilimo kinachofanywa na baadhi ya watu katika vyanzo vya maji (upstream) ambapo huchepusha maji na kushindwa kufuata mkondo wake.
Kutokana na mgawo huo wa umeme Serikali hiyo ya Awanu ya Nne kupitia Wizara ya Nishati na Madini iliamua kuchukua hatua za makusudi na madhubuti kuanza kukabiliana na hali hiyo ya mgawo na kipaumbele kikiwa ni kujenga mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia nishati mbadala hususan gesi asilia.
Serikali iliruhusu Kampuni binafsi kuchimba gesi na kusafirisha pamoja na kuwauzia Makampuni binafsi, viwanda na TANESCO ili TANESCO nayo iweze kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia.
Ilipofika mwaka 2008 Serikali ilikamilisha ujenzi wa mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia wa Ubungo I wenye uwezo wa kuzalisha Megawati 102.
Mwaka 2009 mtambo mwingine ulikamilika wa Tegeta wenye uwezo wa kuzalisha Megawati 45 na mwaka 2012 Serikali ilizundua mtambo wa Ubungo II (Megawati 105). Mitambo yote hiyo inazalisha umeme kwa kutumia gesi asilia na inamilikiwa na Serikali kwa asilimia mia moja.
Serikali pia ilijenga mitambo mingine ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia ya Mtwara (Megawati 18) na Somangafungu mkoani Lindi (Megawati 7.5).
Ili kuwa na umeme wa uhakika katika gridi ya taifa kwenye mikoa ya Kanda ya Ziwa, Serikali ilijenga pia mtambo mwingine wa kuzalisha umeme kwa kutumia mafuta mazito wenye uwezo wa kuzalisha Megawati 60 uliopo Nyakato, Mwanza.
Kutokana na gesi asilia kugundulika kwa wingi katika mikoa ya Kusini mwa Tanzania yaani Lindi na Mtwara, Serikali iliamua kujenga bomba kubwa la gesi kutoka Mtwara na Lindi pamoja na mitambo ya kuchakata ambapo gesi hiyo inazalisha na kusafirishwa hadi kwenye mitambo ya kuzalisha umeme kwani gesi inayozalishwa na kuuzwa na watu binafsi haitoshelezi katika kuzalisha umeme.
Aidha, kutokana na bomba la gesi kujengwa na mitambo yake, Serikali iliona ni busara kujenga mtambo wa Kinyerezi I wenye uwezo wa kuzalisha Megawati 150.
Mitambo yote ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia iliyojengwa na Serikali tangu mwaka 2008 hadi sasa 2015 imefikia jumla ya Megawati 484.5 ya umeme wote unaozalishwa na mitambo hiyo ya Serikali kupitia TANESCO. Hayo ni mafanikio makubwa katika sekta ya Nishati katika kipindi cha Serikali ya Awanu ya Nne.
Pamoja na kwamba Serikali ya Awanu ya Nne inaondoka madarakani mwishoni mwa mwaka huu lakini imeacha misingi mizuri na jitihada kubwa za kuendelea kuboresha sekta ya nishati hususan katika kuzalisha umeme.
Ni ukweli ulio wazi kwamba kukamilika kwa mtambo wa Kinyerezi I ndiyo mwanzo wa kuanza kwa ujenzi wa mitambo mingine ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia ya Kinyerezi II, Kinyerezi III na Kinyerezi IV kwani zipo kila dalili za kuandaa na kuendelea kwa ujenzi huo kuwapo kwa eneo lenyewe ambapo mitambo hiyo itajengwa na wahusika wameshaanza kazi.
Hivyo tuna kila sababu ya kuipongeza Serikali ya Awanu ya Nne inayoongozwa na Mhe. Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete kwamba imefanya juhudi kubwa katika kuhakikisha kwamba upatikanaji wa umeme unaongezeka ili Taifa la Tanzania litakapofika mwaka 2025 liwe ni taifa la uchumi wa kati na mafaniko hayo yote yatatokana na kuwapo kwa umeme wa kutosha na wa uhakika.
Hii ni dhahiri kwamba maendeleo ya nchi yoyote duniani yanatokana na upatikanaji wa umeme wa uhakika hivyo lazima wote tutambue kwamba bila umeme hakuna maendeleo hivyo, umeme ni maendeleo.
Kurasa hii inakupa fursa ya kuongeza uelewa kuhusu masuala yanayohusu sekta ndogo ya gesi nchini.
Yaliyoandikwa katika kurasa hii ni baadhi tu ya maswali ambayo yamekuwa yakiwatatiza wananchi.
Gesi asilia ni nini?Gesi asilia ni mchanganyiko wa molekuli
nyepesi za Carbon na Hydrogen mfano methane (CH4), Ethane (C2H6). Gesi asilia inatokana na kuoza kwa mata ogania (organic matter) kama vile uozo wa masalia ya mimea na wanyama miaka mingi iliyopita.
Ni kiasi gani cha gesi asilia kimegunduliwa hapa nchini? Kiasi cha gesi asilia kilichogunduliwa hadi
hivi sasa ni futi za ujazo trilioni 55.08 (Gas initially in place- kabla ya kuhakikiwa kiasi kamili kinachoweza kuvunwa). Kati ya hizo, futi za ujazo trilioni 47.08 ni kutoka vitalu vya kina kirefu cha bahari na futi za ujazo trilioni 8 ni kutoka vitalu vya nchi kavu.
Kwanini gesi asilia imepelekwa jijini Dar es Salaam na sio kubaki kwenye Mikoa
ya Lindi na Mtwara?Kwanza kabisa, kujenga miundombinu
hiyo kuliangaliwa uhitaji mkubwa wa gesi asilia ulipo nchini, kama viwanda, kuzalisha umeme na kadhalika.
Pili, uwepo wa miundombinu ya bomba
la gesi kwenda Dar es Salaam, hainyimi fursa kwa Mikoa ya Kusini kutonufaika na gesi asilia. Ikumbukwe kuwa mwaka 2006 kulijengwa Kituo cha kuzalisha umeme kwa Mikoa ya Lindi na Mtwara ambapo kituo hicho kinatumia gesi inayozalishwa Mnazi Bay, Mkoani Mtwara. Vilevile, miundombinu hiyo kwenda Dar es Salaam imejengwa kitaalam kuruhusu kutoa gesi asilia kwenda kila sehemu soko litakakopatikana. Mfano, ni uwepo wa kiwanda cha Saruji cha Dangote Mkoani Mtwara ambacho kinatarajiwa kutumia gesi asilia.
Je, kuna ukweli gani kwamba makampuni ya mafuta na gesi asilia yaliyogundua gesi katika kina kirefu
cha bahari yameshaanza kuvuna gesi asilia na kusafirisha nchi za nje?
Hapana, makampuni ambayo mpaka sasa yamefanikiwa kufanya ugunduzi wa gesi asilia katika tafiti za mafuta na gesi kwenye kina kirefu cha bahari ni BG, Statoil na washirika wake. Kwa sasa makampuni haya kwa kushirikiana na Serikali yapo kwenye mazungumzo ya kutafuta eneo la kujenga mradi wa kubadili gesi kuwa kimiminika “LNG” (Liquefied Natural Gas). Mradi huu utasaidia upatikanaji wa nishati ya gesi nchini, pamoja na kuuza gesi asilia nchi za nje na kuingizia Serikali fedha za kigeni ili kuchochea ukuaji wa uchumi. Kwa sasa hakuna uuzwaji wowote unaofanywa na Meli kwenda nje ya nchi.
Mitambo ya kuchakata Gesi Asilia, Madimba Mtwara
4 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava (wa tano kulia) na Balozi wa Brazili nchini Fransisco, Carlos Luiz (wa tatu kulia) katika picha ya pamoja na Wanafunzi 15 waliohitimu mafunzo ya lugha ya Kireno. Wanafunzi 7 kati yao walipata ufadhili wa kusoma masuala ya mafuta na gesi katika ngazi za Shahada ya Uzamili na Uzamivu nchini Brazil mwezi Machi, mwaka 2015.
Watanzania waliopata ufadhili wa masomo nchini China mwaka 2014, katika ngazi ya shahada ya uzamili na uzamivu katika fani ya mafuta na gesi wakiwa katika picha ya pamoja na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (aliyekaa) na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi (wa nne kutoka kushoto mstari wa nyuma) pamoja na watendaji wengine wa Wizara ya Nishati na Madini mara baada ya kuagwa rasmi katika Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini.Wengine katika picha (mstari wa mbele) ni Kamishna Msadizi Nishati anayeshughulikia Umeme, Mhandisi Innocent Luoga (wa kwanza kulia), Kamishna wa Madini, Mhandisi Paul Masanja (wa pili kulia), Kaimu Mkurugenzi Utawala – Bi. Caroline Musika (wa kwanza kushoto).
Waziri wa Nishati na Madini George Simbachawene (kushoto) akimkabidhi mmoja wa wanafunzi nyaraka za masomo kwenda nchini China. Anayeshuhudia katikati ni Kamishna Msadizi anayeshughulikia maendeleo ya nishati, James Andilile, Agosti 5, 2015.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eliachim Maswi akiwa na wanafunzi waliopata ufadhili wa masomo kupitia Wizara ya Nishati na Madini kusoma Shahada za Uzamili na Uzamivu katika masuala ya mafuta na gesi nchini China.Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali Watu Lusius Mwenda na wa tatu kulia ni Kamishna Msadizi anayeshughulikia Maendeleo ya Nishati, James Andilile, mwaka 2015.
Waziri wa Nishati na Madini George Simbachawene (kulia) akizungumza na wanafunzi 22 waliopata Ufadhili wa Masomo kupitia Serikali ya Watu wa China kusoma Shahada za Uzamili na Uzamivu kuhusu masuala ya mafuta na gesi nchini China.Hafla ya kuwakabidhi nyaraka za masomo ilifanyika mwezi Agosti, 2015
UFADHILI WA MASOMOTUMEWEZA
5BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Kayanza Pinda akikabidhi hundi za mikopo kwa wachimbaji wadogo. Mwaka 2013 Serikali ilianza utaratibu wa kutoa mikopo ya masharti nafuu na ruzuku kwa wachimbaji wadogo kupitia Benki ya Maendeleo ya TIB. Hundi za awamu ya kwanza za ruzuku hiyo zenye jumla ya Dola za Marekani 537,000 sawa na shilingi milioni 880.68 zilikabidhiwa mwezi Aprili, 2014 na Waziri Mkuu, Mizengo Kayanza Pinda kwa miradi 11.
Mjasiriamali anayejihusisha na biashara ya vito vya madini kwa kukata, kusanifu na kuuza, Susie Kennedy kutoka Arusha, akipokea mkataba kutoka kwa Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene wakati wa mafunzo kwa waliopata ruzuku awamu ya pili ya kuendeleza uchimbaji madini mdogo. Wengine pichani kutoka Kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Madini, Sehemu ya Leseni, Mhandisi John Nayopa, Mkurugenzi wa Usimamizi wa Fedha za Serikali kutoka Benki ya Maendeleo ya TIB, Prisca Chang’a na Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Madini Tanzania (FEMATA), John Bina. Mafunzo hayo ya siku mbili yalifanyika mjini Dodoma Oktoba 7 na 8, 2015.
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (wa pili kutoka kulia – waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wachimbaji madini wadogo kutoka Kanda ya Kaskazini waliopata ruzuku awamu ya pili kwa ajili ya kuendeleza uchimbaji madini mdogo.Ruzuku ya awamu ya pili ya kiasi cha shilingi bilioni 7.2 ilitolewa kwa vikundi 111 vya wachimbaji wadogo na watoa huduma mbalimbali katika sekta ya madini.
UTOAJI RUZUKUTUMEWEZA
6 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini
Na Veronica Simba
Hivi karibuni, Wizara ya Nishati na Madini iliendesha mafunzo maalum kwa wachimbaji madini ambao miradi yao
ilichaguliwa kupata ruzuku ya Serikali kwa ajili ya kuendeleza uchimbaji mdogo.
Miradi iliyochaguliwa kwa ajili ya kupata ruzuku ilikuwa ya aina mbalimbali na pia ilihusu jinsia zote. Miradi hiyo ni pamoja na ile ya uchimbaji madini, utoaji wa huduma za kiufundi, uchenjuaji madini, usanifu wa vito na pia huduma za mama lishe migodini.
Mafunzo hayo yalilenga kuwawezesha wachimbaji madini wadogo nchini kuendeleza shughuli zao kwa tija na yalihitimishwa kwa utoaji mikataba ya wachimbaji madini wadogo waliopata ruzuku kutoka Serikalini awamu ya pili.
Mambo mbalimbali yalijadiliwa na washiriki wa mafunzo hayo ambapo baadhi ya washiriki waliipongeza Serikali kwa kuwashirikisha wanawake kwa upana zaidi katika uwezeshaji wa shughuli za uchimbaji mdogo.
Kufuatia pongezi hizo, nilitamani pia kupata mtazamo wa washiriki wa semina ikiwa Sera ya Madini ni Mkombozi wa wanawake wachimbaji wa madini kwa kuwa kundi hili ni mhimili wa maendeleo ya jamii yoyote.
Katika kutafuta jibu la swali hilo, nilizungumza na wadau mbalimbali, na hususan wanawake wawili kutoka Merelani, waliojitambulisha kama Pili Hussein na Susie Kennedy.
Nilivutiwa kuzungumza kwa kirefu na Pili Hussein ambae ni mama wa
makamo, na alikuwa na historia ya pekee katika uchimbaji wa madini ya Tanzanite tokea mwaka 1988 katika eneo la Merelani, Mkoani Manyara.
Pili anasema wakati akianza shughuli za uchimbaji, jamii kwa wakati huo iliichukulia shughuli hiyo kuwa ya wanaume pekee hivyo yeye alilazimika kujificha kwa kivuli cha mwanaume akitumia jina la bandia la ‘Mjomba Hussein’.
“Nililazimika kuiaminisha jamii iliyonizunguka katika kazi zangu kuwa mimi ni mwanaume na siyo mwanamke ili niweze kukubalika kufanya kazi hiyo,” anasema mama huyo.
Anasema alilazimika kuchanganyika na wanaume katika mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuvaa mavazi ya kiume muda wote, kuvuta sigara, na mambo mengine kadhaa ambayo ni aghalabu kwa mwanamke kufanya. “Hata jina la Mjomba Hussein lilianza wakati huo,” anasema Pili.
Pili au ‘Mjomba Hussein’, anawakilisha wanawake katika jamii yetu ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakikatishwa tamaa kutokana na mitazamo hasi ya baadhi ya watu hivyo kushindwa kufanya shughuli za kimaendeleo kwa dhana kuwa kazi hizo zinafaa kufanywa na wanaume tu.
Aidha, kutokana na Sera za miaka ya nyuma, hasa wakati wa ukoloni kutotambua rasmi uchimbaji mdogo, suala la ubaguzi wa jinsia lilikuwa na nguvu zaidi kwa kuwa uchimbaji ambao ulionekana kuwa haramu ulihitaji wanaume wenye kuweza kupambana na Serikali ilipobidi.
Ni jambo la kutia faraja kuwa Serikali imekuwa ikipambana na mitazamo na dhana hizo potofu zilizojengeka kwa muda mrefu katika jamii yetu
kwa kuwajengea mazingira wezeshi wanawake ili waweze kufanya kazi mbalimbali za kujiletea maendeleo pasipo kuwa na hofu ya aina yoyote.
Wizara ya Nishati na Madini mathalani, imekuwa ikifanya jitihada za kuwawezesha wanawake kushiriki katika shughuli mbalimbali zinazohusu sekta husika ikiwa ni pamoja na uchimbaji mdogo wa madini.
Katika awamu hii ya pili ya utoaji ruzuku, Serikali imepanua zaidi wigo ambapo imetenga takribani Shilingi za Kitanzania bilioni 7.2 kwa vikundi 111 vya wachimbaji wadogo na watoa huduma mbalimbali katika sekta ya uchimbaji madini mdogo ukilinganisha na Dola za Marekani 500,000 sawa na takribani Shilingi za Kitanzania bilioni moja zilizotolewa kwa waombaji 11 katika awamu ya kwanza.
Kwa mujibu wa Kamishna Msaidizi wa Madini, Sehemu ya Leseni, Mhandisi John Nayopa, utoaji ruzuku katika awamu ya pili umehusisha wachimbaji wadogo pamoja na watoaji huduma
mbalimbali katika sekta husika tofauti na ilivyokuwa katika awamu ya kwanza iliyofanyika katika Mwaka wa Fedha 2013/14 ambapo Wizara iliwalenga wachimbaji madini wadogo pekee.
Mhandisi Nayopa anafafanua zaidi kuwa, watoa huduma katika uchimbaji madini mdogo walionufaika na ruzuku awamu ya pili ni pamoja na vikundi vya wanawake wanaotoa huduma ya chakula, kushona nguo kwa wachimbaji madini na wale wanaojishughulisha na uongezaji thamani madini, hasa ukataji na uchongaji madini ya vito.
Aidha, Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene wakati akifunga mafunzo kwa wachimbaji wadogo mjini Dodoma hivi karibuni aliwapongeza wachimbaji madini wanawake waliopata ruzuku awamu ya kwanza na kueleza kuwa wameonesha mfano mzuri kwa kutumia vizuri fedha walizopatiwa na hivyo kuongeza tija kwenye kazi zao.
Alitoa mfano wa mmoja wa walionufaika na awamu hiyo kuwa ni kampuni ijulikanayo kama Precision Décor inayomilikiwa na mwanamke na inajishughulisha na uchimbaji wa madini ya ujenzi yanayoitwa, Tanga stone.
Simbachawene aliwaasa wanawake wachimbaji kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kuwa mfano wa kuigwa. “Natarajia pia katika awamu hii wanawake wataendelea kuwa mfano wa kuigwa. Dhana ya akina mama wakisaidiwa ni sawa na kusaidia jamii kubwa, inajitokeza hapa,” alisema Waziri.
Wakati huu ambapo Serikali imebainisha kwamba Wizara inaendelea kuweka mikakati mingi ili kuendeleza wachimbaji wadogo, ni fursa nzuri kwa wanawake kujitokeza kwa wingi na kufanya kazi za uchimbaji madini au utoaji huduma katika sekta husika ili waweze kunufaika ipasavyo.
Bila shaka Sera ya Madini ni mkombozi kwa wanawake hawa na wengine ambao watachangamkia fursa zilizopo kwenye sekta ya madini. Shime wanawake wachimbaji, tuendelee kuonyesha mfano kwa kuisaidia Serikali kutimiza azma ya kuhakikisha sekta ya madini inachangia kwa asilimia 10 katika Pato la Taifa ifikapo mwaka 2025.
Sera ya Madini ni Mkombozi wa Wanawake wachimbaji?>>> “Mjomba Hussein” atoa ushahidi
Mchimbaji madini mdogo, Pili Hussein maarufu kama Mjomba Husein akipokea mkataba kutoka kwa Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene wakati wa mafunzo kwa waliopata ruzuku awamu ya pili ya kuendeleza uchimbaji madini mdogo. Wengine pichani kutoka Kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Madini, Sehemu ya Leseni, Mhandisi John Nayopa, Mkurugenzi wa Usimamizi wa Fedha za Serikali kutoka Benki ya Maendeleo ya TIB, Prisca Chang’a na Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Madini Tanzania (FEMATA), John Bina. Mafunzo hayo ya siku mbili yalifanyika mjini Dodoma Oktoba 7 na 8, 2015.
Baadhi ya akina mama ambao ni wachimbaji wadogo wa madini mkoani Shinyanga wakiwa katika semina kuhusu mfumo mpya wa huduma za utoaji leseni za madini kwa njia ya mtandao (Online Mining Cadastre Transactional Portal – OMCTP). Kutoka Kushoto ni Amina Mtoro, Hafsa Issa, Halima Mohamed, Khadija Salum na Nusura Juma. Semina hiyo ilifanyika hivi karibuni mjini Shinyanga.
MAKALA
7BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini
MIRADI YA GESI ASILIA, 2015TUMEWEZA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Kituo cha Kuchakata Gesi Asilia cha Madimba. Kulia kwake ni Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu. Kushoto kwake ni Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete. Wengine ni Viongozi mbalimbali wa Kitaifa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete (katikati) akikagua Kituo cha Kuchakata Gesi Asilia cha Madimba wakati wa uzinduzi wa mradi wa miundombinu ya kusafirisha na kuchakata gesi asilia. Kushoto kwake ni Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene akifuatiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt James Mataragio. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu akifuatiwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Jakaya Kikwete akipewa maelezo na Meneja Mitambo ya Kuchakata Gesi Asilia, Mhandisi Sultan Pwaga (aliyenyoosha mikono) kuhusu Mradi wa Kuchakata Gesi Asilia wa Madimba. Wengine katika picha ni viongozi mbalimbali wa Kitaifa waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Mradi.
Mtambo wa Kuchakata Gesi Asilia wa Madimba, Mkoani Mtwara
8 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini
1. Bomba la gesi katika hatua za awali za ujenzi
2. Mafundi wakifanya kazi ya kuziba maeneo yaliyokuwa na hitilafu katika bomba la kusafirisha gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam.
3. Baadhi ya nyumba za Wafanyakazi wa Kituo cha Kuchataka Gesi Asilia Madimba, Mtwara.
4. Bomba la gesi likiwekwa chini ya ardhi.
5. Meli ya Discover Americas – 83 ikichoronga visima katika Kitalu N0.2 kwenye kina kirefu cha maji katika Bahari ya Hindi.
Tulipotoka … Tulipofika
1 4
52
3
Kituo cha Kuchakata Gesi cha Madimba, chenye uwezo wa kusafisha Gesi kiasi cha futi za ujazo Milioni 210 kwa siku, Gesi husafirishwa kwenda kituoni hapo kwa njia ya bomba.
9BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini
PICHA 1 na 2: Mitambo ya Kufua Umeme ya Kinyerezi I, kutokana na Gesi Asilia kutoka Madimba- Mtwara yenye uwezo wa kuzalisha Megawati 150 za umeme. Mradi wa Kinyerezi I unaomilikiwa na Serikali kwa asilimia 100 kupitia Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), umegharimu kiasi dola za Kimarekani milioni 183 sawa na shilingi za Tanzania Bilioni 400. Ujenzi wa Miundombinu ya kusafirisha, kusafisha na kuzalisha umeme wa Gesi Asilia ulizinduliwa mwaka 2012 na Rais Jakaya Kikwete
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete akiwa katika eneo lilipo lango la kuingia katika Mitambo ya Kufua umeme ya Kinyerezi I, wakati akikagua mitambo hiyo wakati wa uzinduzi wa mitambo hiyo uliofanyika Oktoba 13, 2015.
PICHA 3 na 4: Mitambo ya kufua umeme eneo la Kinyerezi I, ikiwa katika hatua mbalimbali wakati wa ujenzi wake.
3
4 AWALI
AWALI
MRADI MKUBWA UMEME WA GESI ASILIATUMEWEZA
1
2
10 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini
he G
over
nmen
t of
Tan
zani
a, in
cr
eatin
g an
en
ablin
g en
viro
nmen
t fo
r fo
reig
n an
d lo
cal
inve
stm
ents
, form
ulat
ed th
e M
iner
al P
olic
y of
199
7; e
nact
ed t
he M
inin
g Ac
t of
199
8 an
d m
ajor
ref
orm
s in
the
min
ing
�sca
l re
gim
e w
hich
co
ntai
ned
gene
rous
ta
x in
cent
ives
aim
ed a
t at
tract
ing
both
loca
l an
d fo
reig
n in
vest
ors
in
the
min
ing
sect
or.T
he
mea
sure
s re
sulte
d in
to
incr
ease
d la
rge
scal
e ex
plor
atio
n an
d m
inin
g ac
tiviti
es,
inclu
ding
th
e es
tabl
ishm
ent o
f 7 la
rge
scal
e go
ld m
ines
be
twee
n 19
98 an
d 20
09.
How
ever
, th
e Go
vern
men
t co
uld
not
e�ec
tivel
y re
alize
the
exp
ecte
d be
ne�t
s du
e to
in
adeq
uate
ex
perti
se
and
ine�
ectiv
e m
onito
ring
of
min
ing
oper
atio
ns.
In
orde
r to
ad
dres
s th
is sit
uatio
n, t
he G
over
nmen
t, am
ong
othe
r m
easu
res
it re
view
ed t
he m
iner
al p
olic
y, m
inin
g le
gisla
tion
and
stre
ngth
ened
inst
itutio
nal
adm
inist
ratio
n.
As
part
of
inst
itutio
nal
arra
ngem
ents
, th
e Ta
nzan
ia
Min
eral
s Au
dit
Agen
cy
(TM
AA)
was
es
tabl
ished
in
20
09.
The
Agen
cy
is m
anda
ted
to m
onito
r an
d au
dit
larg
e,
med
ium
and
smal
l sca
le m
inin
g op
erat
ions
in
or
der
to
ensu
re
max
imiza
tion
of
Gove
rnm
ent
bene
�ts
from
the
min
ing
indu
stry
, th
ereb
y en
hanc
ing
socio
-eco
nom
ic de
velo
pmen
t.Ke
y fu
nctio
ns o
f th
e Ag
ency
inc
lude
m
onito
ring
and
audi
ting
of q
ualit
y an
d qu
antit
y of
m
iner
als
prod
uced
an
d ex
porte
d by
larg
e, m
ediu
m a
nd sm
all s
cale
m
iner
s in
ord
er t
o fa
cilita
te c
olle
ctio
n of
pa
yabl
e ro
yalty
; au
ditin
g of
re
venu
e ge
nera
ted,
ca
pita
l in
vest
men
t an
d op
erat
ing
expe
nditu
re o
f th
e la
rge
and
med
ium
sca
le m
ines
for
the
pur
pose
of
gath
erin
g ta
xabl
e in
form
atio
n an
d pr
ovid
ing
the
sam
e to
th
e Ta
nzan
ia
Reve
nue
Auth
ority
(T
RA)
and
othe
r
rele
vant
aut
horit
ies;
and
mon
itorin
g an
d au
ditin
g en
viro
nmen
tal
man
agem
ent,
envi
ronm
enta
l bud
get a
nd ex
pend
iture
for
prog
ress
ive
reha
bilit
atio
n an
d m
ine
closu
re.
Sinc
e its
est
ablis
hmen
t TM
AA h
as re
cord
ed
rem
arka
ble
achi
evem
ents
as
a re
sult
of
e�ec
tive
mon
itorin
g an
d au
ditin
g of
m
inin
g op
erat
ions
in
the
coun
try.
Key
achi
evem
ents
inclu
de:
• Pa
ymen
ts o
f Co
rpor
ate
Inco
me
Tax
(CIT
) am
ount
ing
to U
SD 4
19 m
illion
by
m
ajor
m
ines
fo
r th
e pe
riod
cove
ring
year
200
9 to
Sep
tem
ber
2015
. No
CIT
was
pai
d be
fore
TM
AA
esta
blish
men
t. •
Facil
itatio
n of
in
puts
to
di
stric
t co
uncil
s ho
stin
g m
inin
g co
mpa
nies
to
ena
ble
them
with
the
colle
ctio
n of
Lo
cal
Serv
ice
Levy
w
hich
ha
s am
ount
ed to
USD
5.4
milli
on fo
r the
pe
riod
cove
ring
year
20
09
to
Sept
embe
r 201
5.•
Roya
lty
paym
ents
on
bu
ildin
g m
ater
ials
and
indu
stria
l m
iner
als
whe
reby
st
rate
gic
audi
ts
of
such
m
iner
als c
ondu
cted
by t
he A
genc
y in
colla
bora
tion
with
Zo
nal/R
egio
nal
Min
es
O�
ces,
enab
led
the
Gove
rnm
ent t
o co
llect
a to
tal o
f TZS
11
.7 b
illion
from
med
ium
and
sm
all
scal
e m
iner
s fo
r the
per
iod
cove
ring
June
201
1 to
Sep
tem
ber 2
015.
Thes
e au
dits
whi
ch a
re c
ondu
cted
thro
ugh
the
use
of “M
iner
al S
ales
Vou
cher
s” co
ver v
ario
us re
gion
s in
the
coun
try
and
are
expe
cted
to
inclu
de a
lmos
t al
l re
gion
s. Cu
rrent
reg
ions
bei
ng
cove
red
inclu
de A
rush
a, Co
ast.
Dar e
s Sa
laam
, D
odom
a, Ge
ita,
Iring
a, Ka
gera
, Ka
tavi
, Ki
liman
jaro
, Li
ndi,
Man
yara
, M
beya
, M
orog
oro,
M
wan
za,
Mtw
ara,
Rukw
a, Ru
vum
a, Si
miy
u, S
ingi
da an
d Ta
nga.
• Ro
yalty
pay
men
ts o
n go
ld p
rodu
ced
by
min
eral
pr
oces
sors
us
ing
vat
leac
hing
tech
nolo
gy in
Gei
ta, M
beya
an
d M
wan
za re
gion
s. M
onito
ring
of
such
act
iviti
es w
hich
is c
ondu
cted
in
colla
bora
tion
with
Min
es O
�ce
s ha
s en
able
d th
e Go
vern
men
t to
colle
ct a
to
tal o
f TZS
5.9
billi
on fo
r the
per
iod
cove
ring
July
201
2 to
Sep
tem
ber
2015
. Fut
ure
mon
itorin
g w
ill in
volv
e ot
her
regi
ons
like
Shin
yang
a an
d Si
ngid
a w
here
suc
h ac
tiviti
es t
ake
plac
e.
• Th
e Ag
ency
’s sp
ecia
l des
ks a
t maj
or
airp
orts
(Jul
ius
Nyer
ere
Inte
rnat
iona
l Ai
rpor
t, Ki
liman
jaro
In
tern
atio
nal
Airp
ort a
nd M
wan
za A
irpor
t) th
roug
h co
llabo
ratio
n w
ith o
ther
Gov
ernm
ent
enfo
rcin
g in
stitu
tions
, inte
rcep
ted
78
incid
ents
of il
lega
l min
eral
smug
glin
g be
twee
n Ju
ly 2
012
and
Sept
embe
r 20
15.
Thes
e in
ciden
ts
invo
lved
m
iner
als w
orth
USD
10
milli
on. S
ome
of th
e min
eral
s wer
e con
�sca
ted
afte
r co
urt
hear
ings
and
con
vict
s w
ere
�ned
acc
ordi
ng t
o th
e pr
ovisi
ons
unde
r the
Min
ing
Act o
f 201
0.
• Re
gard
ing
envi
ronm
enta
l co
mpl
ianc
e at
m
inin
g sit
es,
envi
ronm
enta
l aud
its c
ondu
cted
by
TMAA
ha
ve
cont
ribut
ed
to
a tre
men
dous
im
prov
emen
t in
en
viro
nmen
tal c
ompl
ianc
e by
larg
e,
med
ium
an
d so
me
smal
l sc
ale
min
ers.
• Th
e Ag
ency
’s la
bora
tory
in
Dar
es
Sala
am, w
hich
is e
quip
ped
with
stat
e of
the
art
equi
pmen
t an
d hi
ghly
tra
ined
pe
rson
nel,
was
ac
cred
ited
with
ISO
/IEC
1702
5: 2
005
in M
arch
20
15
by
SADC
AS,
Bots
wan
a (a
n in
tern
atio
nal a
ccre
dita
tion
body
for
Ea
ster
n an
d So
uthe
rn A
frica
). TM
AA
Labo
rato
ry o
�ers
a w
ide
rang
e of
qu
ality
serv
ices o
f min
eral
anal
yses
at
com
petit
ive
price
s to
all s
take
hold
ers
in th
e m
iner
al se
ctor
.
Des
pite
th
e ab
ove
achi
evem
ents
, th
e Ag
ency
con
tinue
s to
wor
k tir
eles
sly i
n or
der t
o en
sure
that
the
min
ing
indu
stry
in
Tanz
ania
ben
e�ts
bot
h th
e Go
vern
men
t an
d th
e m
inin
g co
mpa
nies
in a
win
-win
sit
uatio
n. In
real
izing
this,
the
Agen
cy w
ill co
ntin
ue to
stre
ngth
en it
s mon
itorin
g an
d au
ditin
g of
min
ing
oper
atio
ns t
o m
eet
Gove
rnm
ent’s
exp
ecta
tions
and
the
publ
ic at
larg
e.
Min
eral
s Aud
iting
in Ta
nzan
ia a
t a G
lanc
e
TMAA
Chi
ef E
xecu
tive o
�ce
r En
gine
er D
omin
ic R
wek
aza
talk
ing
to re
port
ers
at o
ne o
f the
age
ncy'
s pub
lic a
war
enes
s sem
inar
s
Aeria
l vie
w o
f one
of
the
min
ing
area
s in
Tanz
ania
.
12 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHabari za nisHati/madini
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIAMINISTRY OF ENERGY AND MINERALS
Kwa wadau wa sekta za Nishati na Madini, tembelea kurasa mpya za Wizara kwenye Mitandao ya Kijamii ya Twitter na Facebook kwa anuani ya ‘Nishati na Madini’ Karibu tuhabarishane na
tujadili kuhusu sekta za Nishati na Madini kwa maendeleo ya Watanzania wote.Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini