9
Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya Nishati na Madini Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected] HABARI ZA NISHATI &MADINI Toleo No. 76 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Julai 17 - 23, 2015 Bulletin News http://www.mem.go.tz Mradi gesi asilia wafikia asilimia 98 Soma habari Uk. 2 Luoga aagiza miradi ya Umeme Dar ikamilike kwa wakati Kituo cha kupokelea gesi eneo la Somanga kikiwa kimekamilika Mitambo ya kupokelea gesi ya Kinyerezi iliyokamilika kufungwa Mitambo ya kusafisha gesi na nyumba za wafanyakazi Madimba, Mtwara Uk. 2

Jarida La Wiki La Nishati Na Madini Toleo La 76

Embed Size (px)

DESCRIPTION

JARIDA LA WIKI LA NISHATI NA MADINI TOLEO LA 76

Citation preview

  • Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya Nishati na Madini

    Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

    HABARI ZA NISHATI &MADINI

    Toleo No. 76 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Julai 17 - 23, 2015

    BulletinNews

    Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya Nishati na Madini

    Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

    http://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI &MADINI

    Toleo No. 51 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Tarehe - 23-29 Januari , 2015

    JWTZ wapongezwa kunusuru mtambo wa Msimbati-Uk4

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini, anayeshughulikia Madini Stephen Masele

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Charles Kitwanga

    Mkurugenzi Mtend-aji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba

    Mkurugenzi Mkuu wa REA, Dk. Lutengano Mwakahesya

    Wabunge Soma habari Uk. 2

    Waimwagia sifa MEM, TANESCO, REA

    WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AZINDUA RASMI BODI YA TANESCO -Uk2Mradi gesi asilia wafikia asilimia 98

    Soma habari

    Uk. 2

    Luoga aagiza miradi ya Umeme Dar ikamilike kwa wakati

    Kituo cha kupokelea gesi eneo la Somanga kikiwa kimekamilika

    Mitambo ya kupokelea gesi ya Kinyerezi iliyokamilika kufungwa

    Mitambo ya kusafisha gesi na nyumba za wafanyakazi

    Madimba, Mtwara

    Uk. 2

  • 2 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHABARI ZA NISHATI/MADINI

    Asteria Muhozya na Teresia Mhagama

    Imeelezwa kuwa, utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa mitambo ya kusafisha gesi asilia ya Madimba na Songongo, Kilwa, pamoja na bomba la kusafirisha gesi hiyo

    kutoka Mtwara na Songosongo hadi Dar es Salaam kupitia Somanga Fungu itakamilika hivi karibuni.

    Hayo yameelezwa katika taarifa ya mwezi Juni mwaka huu, iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Kusambaza Gesi (GASCO) ambayo ni Kampuni Tanzu ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mhandisi Kapuulya Musomba

    Akielezea hatua zilizofikiwa katika miradi hiyo, Musomba alieleza kuwa, kwa ujumla mradi huo umefikia asilimia

    98 za ujenzi na kukamilika kwake kutaunganisha maeneo yanayozalisha gesi asilia hususan Mnazi Bay- Mtwara, Songosongo, Kiliwani, Mkuranga, Ntorya na gesi iliyogunduliwa katika eneo la bahari ya kina kirefu.

    Akifafanua zaidi alisema kuwa, Bomba limekamilika kwa asilimia 99.6 kwa ujumla, mitambo ya kusafisha gesi asilimia 97.5. Manunuzi ya vifaa vya ujenzi wa mradi yamekamilika kwa asilimia 100, na mradi mzima umekamilika kwa asilimia 98.

    Musomba alisema kuwa, hatua

    hiyo itaiwezesha Serikali kupitia TPDC kuhakikisha kuwa, Tanzania inazalisha umeme wa kutosha kupitia rasilimali hiyo na wananchi wake wananufaika na rasilimali ya gesi asilia.

    Serikali imedhamiria kuhakikisha kuwa, gesi inatumika katika kuzalisha umeme ambao kwa sasa unazalishwa kwa kutumia nishati ya mafuta ambayo huagizwa kutoka nchi za nje na hivyo kuligharimu taifa kiasi kikubwa cha fedha za kigeni, alieleza Musomba.

    Kuhusu mitambo ya kuchakata gesi asilia, alisema kuwa, ujenzi wa eneo la

    kusimika mitambo, jengo la kuendesha mitambo pamoja na barabara za ndani katika eneo la Madimba Mtwara umekamilika kwa asilimia 98, wakati ule wa Songosongo umekamilika kwa asilimia 100 na usimikaji mitambo umekamilika kwa asilimia 98.

    Akizungumzia suala la ajira katika mradi huo, alisema kuwa, kumekuwepo na wafanyakazi wapatao 1,427 wenye mchanganyiko wa wageni pamoja na watanzania kwa ngazi zote hadi taarifa hii inatolewa.

    Aidha, kuhusu ajira kwa upande wa TPDC, alieleza kuwa, shirika hilo tayari limeajiri wafanyakazi wapya wapatao 92 kwa upande wa mitambo ya kusafisha gesi na 42 kwa upande wa bomba la kusafirisha gesi, ambao tayari wanashiriki katika usimamizi wa shughuli za ujenzi.

    Sehemu ya taarifa hiyo inaeleza kuwa, mradi unatekelezwa kwa kutumia fedha za mkopo wa masharti nafuu kutoka Serikali ya Jamhuri ya watu wa China. Jumla ya gharama za ujenzi wa mradi huo ni Dola za Marekani zipatazo bilioni 1.255, ambapo asilimia 95 ni mkopo na asilimia 5 ni mchango wa Serikali.

    Vilevile taarifa inaeleza kuwa gharama nyingine nyingi ambazo serikali imeendelea kuzibeba nje ya asilimia 5 zinazotajwa ni pamoja na gharama za upatikanaji wa mkuza wa Bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Somanga Fungu na kuongezeka kwa upana maeneo mengine mengi ya mkuza tokea Somanga Fungu kuja Dar es Salaam hadi Tegeta. Hadi sasa zimefikia kiasi cha pesa za ki-Tanzania zipatazo shilingi Bilioni 200.

    Katika hatua nyingine, akizungumza wakati akifunga rasmi Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwishoni mwa wiki, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alieleza kuwa, serikali imejipanga kuhakikisha kuwa, hadi ifikapo mwaka 2020 uzalishaji umeme unafikia kiasi cha megawati 3000 kutokana na matumizi ya gesi asilia.

    Akieleza kuhusu miswada ya Sheria za Petroli na TEITI iliyosomwa Bungeni hivi karibuni na Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene, Rais Kikwete alisema yuko tayari kuisaini miswada hiyo wakati wowote itakapomfikia.

    Mradi gesi asilia wafikia asilimia 98

    Wakandaras i wa miradi ya k u b o r e s h a miundombinu ya umeme

    kwenye vituo vya kupoozea umeme jijini Dar es Salaam wametakiwa kuhakikisha wanakamilisha miradi hiyo ndani ya muda uliopangwa.

    Wito huo umetolewa hivi karibuni na Kamishna Msaidizi wa Umeme, Mhandisi Innocent Luoga wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa

    Mradi wa Kusambaza Umeme ujulikanao kwa jina la Electricity V unaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) ambao unahusisha ujenzi na ukarabati wa vituo vya kupoozea umeme vya Sokoine, Ilala na Njiro.

    Aidha, ziara hiyo pia ilihusisha ukaguzi wa Mradi wa Ujenzi na Ukarabati wa Vituo vya Ilala na New City Centre pamoja na ujenzi wa vituo vipya vya Ilala na Muhimbili ambao unafadhiliwa na Serikali

    ya Japan kupitia Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) na vilevile Mradi wa Mfumo wa Kusimamia na Kudhibiti Usambazaji wa Umeme Dar es Salaam ujulikanao kama Distribution SCADA System uliopo Mikocheni unaofadhiliwa na Serikali ya Finland.

    Mhandisi Luoga alielezea lengo la ziara hiyo kuwa ni kujionea hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa miradi hiyo

    Hatua hiyo itaiwezesha Serikali kupitia TPDC kuhakikisha kuwa, Tanzania inazalisha umeme wa kutosha kupitia rasilimali hiyo na wananchi wake wananufaika na rasilimali ya gesi asilia

    Mitambo ya kusafisha gesi ya Madimba

    Luoga aagiza miradi ya Umeme Dar ikamilike kwa wakati

    >>Inaendelea Uk. 3

    Mradi wa Electricity V- Ilala: Transfoma mpya iliyofungwa kwenye kituo cha kupooza umeme cha Ilala mara baada ya majaribio ya awali.

  • 3BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHABARI ZA NISHATI/MADINI

    TahaririMEM

    Na Badra Masoud

    FIVE PILLARS OF REFORMS

    KWA HABARI PIGA SIMU KITENGO CHA MAWASILIANO

    BODI YA UHARIRI MHARIRI MKUU: Badra Masoud

    MSANIFU: Essy OgundeWAANDISHI: Veronica Simba, Asteria Muhozya, Greyson Mwase Teresia Mhagama, Mohamed Saif, Rhoda James

    na Nuru Mwasampeta

    INCREASE EFFICIENCYQUALITY DELIVERY

    OF GOODS/SERVICESATISFACTION OF

    THE CLIENTSATISFACTION OF

    BUSINESS PARTNERS

    SATISFACTION OF SHAREHOLDERS

    TEL-2110490FAX-2110389

    MOB-0732999263

    Hongera Simbachawene kwa mkakati wa kuisuka

    Upya TIPER

    TEL-2110490FAX-2110389

    MOB-0732999263

    Kamishna Msaidizi wa Umeme, Mhandisi Innocent Luoga (wa pili kushoto) akimsikiliza Meneja Mradi wa Electricity V, Mhandisi Florence Gwangombe (wa pili kulia) wakati wa ziara yake kwenye kituo cha kupoozea umeme cha Ilala.

    Luoga aagiza miradi ya Umeme Dar ikamilike kwa wakati

    ikiwa ni pamoja na kubaini changamoto zinazokabili utekelezaji wa miradi husika.

    Katika taarifa yake ya utekelezaji wa Mradi wa Electricity V, Meneja wa Mradi huo, Mhandisi Florence Gwangombe alisema kutokana na sababu mbalimbali huenda mradi huo ukachelewa kukamilika tofauti na makubaliano ya awali kitendo ambacho kilimkera Mhandisi Luoga na hivyo kumuagiza Meneja huyo kukaa na wakandarasi wa Mradi na kurejea makubaliano ya awali.

    Mhandisi Florence alisema moja ya sababu inayopelekea

    Mradi huo kuwa na kasi ndogo ni wakandarasi kushindwa kuajiri wafanyakazi wa kutosha.

    Mhandisi Luoga aliwaagiza wakandarasi hao ambao ni kampuni ya National Contracting Company Ltd (NCC) ya India na ELTEL Group kutoka Finland kuhakikisha wanaajiri wafanyakazi wa kutosha na pia kuandaa ratiba ya shughuli zinazotakiwa kufanywa ili kuepuka kuchelewa kukamilika kwa miradi husika.

    Aidha, Mhandisi Luoga aliwaagiza Mameneja Miradi wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) kuhakikisha kunakuwepo na usimamizi madhubuti wa miradi iliyo chini yao ili kuleta matokeo

    yanayotarajiwa.Alisema lengo la Serikali ni

    kuhakikisha taifa linakuwa na umeme wa uhakika kwa ajili ya kukuza uchumi hivyo aliwaasa mameneja hao kuhakikisha azma hiyo inatimia.

    Ninawasisitiza muhakikishe kunakuwepo na ufatiliaji makini wa miradi mnayoisimamia na sio kuwaachia wakandarasi wafanye kila kitu bila usimamizi wenu, aliagiza Mhandisi Luoga.

    Kwa upande wake Meneja wa kampuni ya NCC Ltd, Sadeesh John alimuahidi Mhandisi Luoga kuwa atahakikisha kasi ya utekelezaji inaongezeka na kutimiza maagizo husika ili kuhakikisha mradi unakamilika ndani ya muda uliopangwa.

    >>Inatoka Uk. 2

    Mapema wiki hii Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene alikutana na Uongozi wa Shirika la kuhifadhi mafuta ya TIPER ambayo serikali ni mbia kwa asilimia 50.

    Katika kikao hicho alisisitiza kuhusu dhamira ya Serikali kuboresha na kulisuka upya shirika hilo la kuhifadhi mafuta ili liweze kutoa huduma ya kupokea mafuta kwa kampuni zote kwa haki na usawa.

    Simbachawene alisema lengo la kulisuka upya Shirika hilo ni kuliboresha na kuhakikisha kuwa linatoa huduma ya kuhifadhi na kupitisha mafuta yote yanayoletwa nchini, na kuhakikisha gharama za kuhifadhi mafuta hapa nchini zinakuwa nafuu.

    Kwa mara nyingine tunapenda kupongeza jitihada zinazofanywa na Serikali katika kuhakikisha kwamba Sekta ya mafuta nchini inalinufaisha taifa ikiwemo kuleta unafuu wa nishati hiyo.

    Hakika katika hili la kuisuka upya TIPER ni mikakati madhubuti ambayo inatarajia kuleta mabadiliko makubwa katika Shirika hivyo, wadau wa TIPER na Watanzania tuunge mkono juhudi hizi za Serikali kwani kauli hii ya sasa inadhihirisha dhamira ya dhati ya Waziri Simbachawene juu ya kulisuka upya Shirika hilo ambapo alisisitiza umuhimu TIPER katika sekta ya mafuta nchini, na kuleza kwamba hivi sasa shirika hilo linahitajika kuliko wakati mwingine wowote.

  • 4 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHABARI ZA NISHATI/MADINI

    JK ajivunia mchango Sekta ya Madini

    Na Asteria Muhozya,

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amesifu jitihada zilizofanywa na Serikali ya Awamu ya Nne katika

    kuimarisha Sekta ya Madini nchini na kuitaja kuwa ni ya pili kwa kuingiza fedha za kigeni baada ya Sekta ya Maliasili.

    Rais Kikwete aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati akihutubia wananchi kupitia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mjini Dodoma na kuyataja mafanikio kadhaa katika Sekta hiyo, ikiwemo ya migodi ya madini kuanza kulipa ushuru wa huduma.

    Hotuba ya Rais Kikwete inarejea taarifa ya awali iliyotolewa na Wizara ya Nishati na Madini ikieleza kuwa, mgodi wa dhahabu wa Geita unaomilikiwa na kampuni ya AngloGold Ashanti; na migodi ya Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara inayomilikiwa na kampuni ya Acacia Mining, imeanza kulipa ushuru wa huduma kwa kiwango cha asilimia 0.3 (0.3%) ya mapato ghafi kwa Halmashauri husika.

    Tayari migodi inalipa kodi ambazo zinachangia katika pato la Taifa. Pia tuna Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 haya yote yamesaidi kuweza kunufaika zaidi kupitia rasilimali hii, alisisitiza Rais.

    Aidha, Rais Kikwete alieleza mafanikio

    yaliyopatikana baada ya serikali kulifufua upya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), ambapo alisema kuwa, mafanikio hayo yamechangia shirika hilo kumiliki mgodi wake wa dhahabu wa STAMIGOLD uliopo Biharamulo, ambao tayari umeanza kutoa mikuo ya dhahabu.

    Vilevile, katika hotuba yake, Rais Kikwete alieleza namna Serikali ilivyofanya jitihada za kuwawezesha wachimbaji wadogo kupewa ruzuku, lengo likiwa ni kuwawezesha kutoka katika uchimbaji mdogo kwenda katika uchimbaji wa kati.

    Katika taarifa yake wakati akizindua Kamati inayoshughulikia maombi ya ruzuku Awamu ya Pili hivi karibuni, Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Paul Masanja alisema kuwa, kiwango cha fedha katika awamu hii kimeongezwa kufikia Dola za Kimarekani milioni na tatu na shilingi za Kitanzania bilioni 1.7 kutoka Dola za Marekani Laki tano (500,000) zilizotolewa Awamu ya Kwanza.

    Lakini pia tumetenga maeneo 8 kwa ajili ya wachimbaji wadogo. Tumefanya hivi ili wasisumbuliwe na wachimbaji wakubwa, alisema Kikwete.

    Vilevile, Rais Kikwete alisema kuwa, mikataba imerekebishwa ili kulinda na kulinufaisha taifa ambapo pia baadhi ya mafanikio ya marekebisho hayo yamewezesha Kampuni za madini kuongeza huduma ya bidhaa zinatolewa nchini tofauti na ilivyokuwa awali.

    Katika hotuba yake pia aliitaja migodi mipya 3 ikiwemo ya Makaa ya Mawe ya Ngaka na Liganga na Chuma Mkuju, ambayo ilianzishwa katika kipindi cha miaka 10 na kueleza kuwa, sekta hiyo imeongeza kiwango cha ajira kutoka 3,500 hadi kufikia 15,000.

    >> Aitaja ya pili kuingiza fedha za Kigeni baada ya Maliasili>> Ajira zaongezeka kutoka 3,500 hadi 15,000.

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete

    Ujumbe kutoka Malawi watembelea Tanzania kujifunza sheria ya Madini, CADASTRE.Na Rhoda James

    Ujumbe kutoka Serikali ya Malawi umetembelea Wizara ya Nishati na Madini mwanzoni mwa wiki hii kwa lengo la kujifunza masuala mbali mbali ikiwemo Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 na Mfumo mpya wa kusajili leseni za madini kwa njia ya mtandao (Online mining Cadastre Transactional Portal)

    Ziara hiyo ya Malawi imekuja kufuatia nchi hiyo kuwa katika mchakato wa kutunga Sheria mpya ya Madini. Ujumbe huo pia umetembelea Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA),Ofisi ya Madini Kanda ya Mashariki, Kampuni ya Madini ya Acacia, pamoja na kitengo cha Leseni na TEHAMA katika Wizara ya Nishati na Madini.

    Ujumbe huo kutoka Malawi umeipongeza Serikali ya Tanzania kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kuendeleza sekta ya Madini na kuahidi kuendeleza ushirikiano uliopo kati ya Serikali hizo mbili.

    Ujumbe kutoka Malawi ukiwa katika Wizara ya Nishati na Madini wakati ulipofika Wizarani hapo kujifunza masuala ya Madini. Katikati ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Wizara ya Nishati, Mrimia Mchomvu na kushoto kwake ni Kamishna Msaidizi wa Madini kitengo cha Leseni, John Nayopa.

    Kulia ni kiongozi wa Msafara wa Ujumbe kutoka Malawi Katibu Mwandamizi, Ben Botolo akielezea jambo katika kikao hicho.

  • 5BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHABARI ZA NISHATI/MADINI

    Serikali kuisuka upya TIPERNa Mwandishi Wetu

    Serikali imedhamiria kuboresha na kulisuka upya shirika la kuhifadhi mafuta TIPER ili iweze kutoa huduma ya kupokea mafuta kwa kampuni zote kwa haki na usawa.

    Waziri mwenye dhama na Wizara ya Nishati na Madini George Simbachawene amebainisha hayo wiki hii alipozungumza na Uongozi wa shirika hilo huku akisisitiza kwamba lengo la Serikali kuboresha shirika hilo ni kuhakikisha inatoa huduma ya kuhifadhi na kupitisha mafuta yote yanayoletwa nchini.

    Simbachewene aliongeza kusema kwamba hadi ifikapo mwishoni mwa mwaka huu kampuni hiyo itakuwa na uwezo wa kuhifadhi mafuta kiasi cha lita 300,000.

    Kwa dhati kabisa tumeamua kuiboresha kampuni hiyo na tunapanga ifikapo Septemba mwaka huu uwezo wa TIPER wa kuhifadhi mafuta utaongezeka kutoka lita 147,000 hadi kufikia 210,000 na itakapofika Desemba watakuwa na uwezo wa kuhifadhi mafuta lita 300,000, alisisitiza George Simbachawene.

    Waziri Simbachawene aliongeza kwamba lengo la Serikali kuchukua hatua ya kuiboresha TIPER ni kuhakikisha gharama za kuhifadhi mafuta hapa nchini zinakuwa nafuu.

    Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la TIPER, Daniel Belair ( Wa kwanza kulia) akimwongoza Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (kushoto) na ujumbe wake walipotembelea shirika lake hivi karibuni.

    Mwenyekiti wa Bodi ya TIPER Prof. Abdulkarim Mruma akieleza jambo katika moja ya vikao na Waziri

    Wanafunzi waliopata ufadhili wa China waaswaNa Greyson Mwase, Dar es Salaam

    Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Wizara ya Nishati na Madini, Mrimia Mchomvu amewataka

    wanafunzi wanaosomea masuala ya gesi na mafuta nchini China kutumia utaalam na uzoefu wao katika kuleta mabadiliko kwenye sekta ya gesi na mafuta nchini.

    Mchomvu aliyasema hayo ofisini kwake, alipotembelewa na wanafunzi waliofadhiliwa na Wizara ya Nishati na Madini kwa ajili ya mafunzo ya Shahada ya Uzamili katika masuala ya gesi na mafuta katika Chuo Kikuu cha Jiosayansi Wuhan kilichopo nchini China.

    Wanafunzi hao ambao ni miongoni mwa wanafunzi nane waliofadhiliwa na Wizara kusomea masuala ya gesi na mafuta kwa mwaka 2013, walifanya ziara hiyo kwa lengo la kuishukuru Wizara pamoja na kuelezea mikakati yao katika kutumia elimu na uzoefu walioupata kuinua sekta za gesi na mafuta.

    Alisema lengo la Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini la kupeleka wanafunzi hao lilikuwa ni kuzalisha wataalam kwa ajili ya kufanya kazi katika Wizara, makampuni ya utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi

    nchini. Kutokana na kukua kwa shughuli za

    utafutaji wa gesi na mafuta nchini kama Serikali tulipanga mikakati mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwawezesha wazawa kushiriki katika shughuli hizo kwa kuwapeleka kusomea masuala ya gesi na mafuta ili waweze kufanya kazi na mashirika ya umma na makampuni yaliyowekeza katika shughuli za utafutaji na uchimbaji wa gesi na mafuta nchini, alisema Mchomvu.

    Mchomvu aliendelea kusema kuwa wataalam hao wanaweza kutumia elimu na uzoefu walioupata kutoka China kufanya kazi kwenye mashirika ya umma, taasisi na makampuni binafsi yanayojishughulisha na shughuli za uchimbaji na utafutaji wa gesi na mafuta.

    Alisisitiza kuwa serikali pekee, haiwezi kuajiri wahitimu wote wanaomaliza mafunzo ya gesi na mafuta bali kazi yake kuu ni kuwapatia elimu itakayowawezesha kushiriki katika fursa mbalimbali zinazojitokeza katika setka ya gesi na mafuta.

    Sekta ya gesi na mafuta inakua kwa kasi kwa sasa, fursa ni nyingi hivyo ni jukumu lenu kuchangamkia fursa mbalimbali za ajira zinazojitokeza katika makampuni ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi. Kuna Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) ambalo lina kampuni

    tanzu, makampuni ya utafutaji wa gesi na mafuta ya Statoil na BG ambayo yanahitaji wataalam, alisisitiza Mchomvu.

    Wakielezea uzoefu walioupata katika chuo hicho, wanafunzi hao walisema wamejifunza kwa kina hatua za utafutaji, uchimbaji na usafirishaji wa mafuta na gesi kwa kutumia vifaa vya kisasa hali iliyowapa uwezo wa kufanya kazi na kampuni za kimataifa.

    Bishanga Januarius ambaye ni mwanafunzi wa mwaka pili katika chuo hicho alisema kuwa utaalam na uzoefu alioupata katika chuo hicho utamwezesha kufanya kazi katika kampuni yoyote ya utafiti na uchimbaji wa madini na kuwa na mchango mkubwa kwa taifa.

    Alisema kuwa elimu ya vitendo waliyoipata katika makampuni ya mafuta na gesi nchini China imewapa mwanga mkubwa katika shughuli zote za utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi.

    Aliishauri Serikali kuendelea kutoa ufadhili katika fani za mafuta na gesi pamoja na masuala ya mazingira kwani shughuli za utafiti na uchimbaji wa gesi na mafuta ni lazima ziende sambamba na utunzaji wa mazingira.

    Naye Yazid Idd ambaye ni mhitimu katika chuo hicho aliishukuru Wizara kwa ufadhili huo na kuishauri Wizara kupeleka wanafunzi kwenye vyuo vingine vinavyotoa

    mafunzo ya mafuta na gesi katika nchi nyingine zilizopiga hatua katika sekta hizo.

    Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Wizara ya Nishati na Madini Mrimia Mchomvu, ( wa pili kutoka kushoto) Mkurugenzi Msaidizi Utumishi, Wizara ya Nishati na Madini Lucius Mwenda ( wa pili kutoka kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi waliowahi kufadhiliwa na Wizara kwa ajili ya kusomea Shahada ya Uzamili katika musuala ya gesi katika vyuo vya China.

  • 6 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHABARI ZA NISHATI/MADINI

    Na Jacqueline MattowoSTAMIGOLD

    Kampuni ya STAMIGOLD ambayo ni kampuni tanzu ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) imetimiza mwaka mmoja wa

    uchimbaji dhahabu katika mgodi wake wa Biharamulo uliopo wilayani Biharamulo Mkoa wa Kagera ambapo kiasi cha wakia 16,388 za dhahabu zimekwisha zalishwa tangu uchimbaji dhahabu ulipoanza rasmi mnamo mwezi Julai mwaka 2014 na jumla ya wakia 12,923 za dhahabu zenye thamani ya Dola za Kimarekani Milioni 15.6 zimeuzwa kwenye soko la kimataifa.

    Kiasi hicho cha dhahabu kilipatikana katika maeneo ya West Zone na Mojamoja takribani kilomita tatu na nusu kutoka uzio wa mgodi ambapo uchimbaji wa dhahabu bado unaendelea. Maeneo hayo mapya yalikabidhiwa STAMICO kutoka mgodi wa Tulawaka uliokuwa ukimilikiwa na kampuni ya African Barrick Gold sasa ACACIA mwishoni mwa mwaka 2013.

    Akizungumza katika hafla ya kusherehekea mwaka mmoja tangu kuanza kwa shughuli za uchimbaji wa dhahabu iliyofanyika mwishoni mwa juma katika mgodi wa Biharamulo, Meneja Mkuu wa mgodi wa Biharamulo, Mhandisi Dennis Sebugwao alieleza kuwa matarajio ya mgodi ni kutafuta namna

    ya kuhakikisha uzalishaji wa dhahabu unaendelea kwa kiwango kikubwa na gharama nafuu ili kusaidia kukuza uchumi wa nchi na kuongeza nafasi za ajira kwa Watanzania kwa ajili ya maslahi ya Taifa zima.

    Siwezi kuficha furaha yangu, siku ya leo ni siku ya muhimu kwetu sote katika historia ya Mgodi huu kwani tunathibitisha kwa Serikali na Watanzania

    wenzetu kuwa, Watanzania wasomi na wenye taaluma mbalimbali katika sekta ya uchimbaji na uzalishaji wa dhahabu wameendelea kuonyesha uwezo wao kwa kuhakikisha uzalishaji unaendelea kufanyika katika mgodi wa STAMIGOLD Biharamulo bila kuwepo wataalam wa kigeni kama ilivyokuwa ikiaminiwa. alieleza Sebugwao.

    Mhandisi Sebugwao pia alielezea mafanikio yaliyofikiwa na mgodi ndani ya mwaka mmoja ambayo ni pamoja na mgodi kuendeshwa kwa kufuata taratibu za usalama na afya kazini, ulinzi imara ndani na nje ya mgodi, kupunguza gharama za uendeshaji wa mgodi, kulipa ushuru wa huduma wa 0.3% ya mauzo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo kiasi cha Shillingi milioni 40.9 mpaka June 2015, kuajiri wafanyakazi wa Kitanzania 340 wa fani mbalimbali za kitaalamu, ajira za muda mfupi 43 kwa wakazi wa vijiji vilivyo jirani na mgodi na wakandarasi wa Kitanzania 281.

    Aliongeza kuwa mgodi umekuwa ukizisaidia jamii zilizo jirani na mgodi kupunguza changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwa ni pamoja na kugawa madawati 1500 kwa shule zenye upungufu katika Wilaya za Biharamulo, Muleba na Ngara, ujenzi wa choo cha wanafunzi Shule ya Msingi Mavota, ukamilishaji wa ujenzi wa madarasa manne Shule ya Msingi Mpago, ukarabati

    wa miundo mbinu pamoja kuwawezesha wananchi kiuchumi kupitia vikundi vitatu vya ujasiriamali kwa kununua vyakula vya asili, mbogamboga na matunda wanayozalisha.

    Kwa upande mwingine, katika kusherehekea siku hiyo shamrashamra mbalimbali zilifanyika ikiwemo mpira wa miguu na mpira wa kikapu ambapo timu ya mgodi ya mpira wa miguu ilicheza mechi ya kirafiki na timu iliyoundwa na wachezaji kutoka vijiji vya Mavota na Mkunkwa na timu ya mgodi kuibuka kidedea kwa bao 2-0. Baada ya michezo kumalizika timu zote za mpira wa miguu zilikabidhiwa zawadi na Meneja Mkuu wa mgodi.

    Katika kuhitimisha sherehe hizo zilitolewa zawadi na vyeti kwa wafanyakazi 10 ambao walifanya vizuri katika Idara zao kwa kipindi cha mwaka mmoja wa uzalishaji ambao pia walipatiwa heshima ya kushiriki na Meneja Mkuu wa mgodi kukata keki ya kutimiza mwaka mmoja wa uzalishaji.

    Wakati huo huo, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala kutoka STAMICO Deusdedith Magala, aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo Mhandisi Edwin Ngonyani, aliupongeza uongozi na wafanyakazi wa mgodi kwa kazi nzuri ambayo inaendelea kufanyika na kusema kuwa mafanikio yanayopatikana ni sifa kwa Shirika na Taifa kwa ujumla kwani tayari mgodi umethibitisha uwezo wa Watanzania kuzalisha dhahabu bila kuongozwa na wataalam wa kigeni.

    Nimefurahishwa sana na mafanikio mliyofikia pamoja na namna wafanyakazi wanavyojituma baada ya kutembelea maeneo mbalimbali hapa mgodini na kujionea kazi zinavyofanyika naomba muendelee na bidii hiyo na vile vile mjitahidi kuongeza zaidi njia za mawasiliano za kutangaza mafanikio ya mgodi huu mfano misaada inayotolewa katika jamii ili dunia na taifa kwa ujumla kufahamu kuwa ipo kampuni ya Kitanzania inayochimba dhahabu kwa manufaa ya Taifa zima la Tanzania alifafanua Magala.

    Mbali na mafanikio hayo mgodi wa STAMIGOLD Biharamulo bado unakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo ni pamoja na kuyumba kwa bei ya dhahabu katika soko la dunia, ufinyu wa mtaji wa kuendesha shughuli mbalimbali za mgodi pamoja na uhaba wa maji kutokana na vyanzo vilivyopo kutegemea msimu wa mvua.

    Kampuni ya STAMIGOLD Biharamulo ilizalisha dhahabu yake ya kwanza mnamo mwezi Agosti 2014 na mpaka sasa imeendelea kuweka historia kwa kuwa kampuni pekee hapa nchini inayozalisha dhahabu kwa kusimamiwa na kuendeshwa na wataalam wa Kitanzania pekee.

    Stamigold yatimiza mwaka mmoja wa uchimbaji dhahabu.

    Mratibu wa kitengo cha Tehama na Mawasiliano, Belatrix Kasuga akipokea cheti cha mfanyakazi bora kutoka kwa Meneja mkuu wa mgodi Mhandisi Dennis Sebugwao (kulia) wakati wa maadhimisho ya mgodi kutimiza mwaka mmoja wa uzalishaji. Pembeni ni Meneja Uchimbaji, Mhandisi Abdallah Kwassa aliyeshikilia zawadi tayari kwa kumkabidhi.

    Pichani Keki ya mfano wa mawe ya dhahabu iliyoandaliwa katika hafla ya mgodi wa STAMIGOLD Biharamulo kutimiza mwaka mmoja wa uzalishaji.

  • 7BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHABARI ZA NISHATI/MADINI

    Na Veronica Simba

    Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) imetoa taarifa yake ya utendaji kwa kipindi cha Serikali ya Awamu

    ya Nne (2005-2015), ambayo pamoja na mambo mengine imeainisha mafanikio yaliyopatikana katika nyanja mbalimbali.

    Taarifa hiyo iliyotolewa hivi karibuni, imeainisha mafanikio ya Wakala huo kwa kipindi husika katika makundi matatu ambayo ni utekelezaji wa kazi za jiosayansi, kuboresha rasilimali watu, vitendea kazi, miundombinu na mazingira yake pamoja na kazi na tafiti zilizokamilika na zinazoendelea kutekelezwa.

    Kwa upande wa utekelezaji wa kazi za jiosayansi, Taarifa ya GST imeeleza kuwa Ramani mpya 60 za jiolojia zimekamilika na kuchapishwa. Ramani hizi ni muhimu kwani huwezesha kubainisha uwepo wa madini katika eneo husika.

    Pia, taarifa ilibainisha kuwa ukusanyaji wa takwimu za jiofizikia kwa kutumia ndege umefanyika katika Wilaya 35 ambayo ni asilimia 15 ya eneo la nchi. Wilaya hizo ni Dodoma, Bahi, Kongwa, Mpwapwa, Nchemba, Kondoa, Chamwino, Iramba, Manyoni, Ikungi, Mkarama na Singida.

    Wilaya nyingine ni pamoja na Igunga, Babati, Kiteto, Hanang, Simanjiro, Mbulu, Moshi, Same, Monduli, Korogwe, Handeni, Kilindi, Bagamoyo, Mvomero, Kilosa, Gairo,

    Mbarali, Chunya, Bukombe, Kahama, Ushirombo, Biharamulo na Mpanda.

    Takwimu hizi zimeainisha maeneo yenye viashiria mbalimbali vya uwepo wa madini, kwa mfano eneo la Misaki, Mpambaa, Sambaru na Londoni ambapo ufahamu wa uwepo wa madini ya dhahabu umeongezeka, taarifa imeeleza na kuongeza kuwa, takwimu hizi zimeonesha ongezeko la uwepo wa madini ya graphite huko Merelani mkoani Manyara na katika wilaya za Kilindi na Handeni.

    Imeelezwa kuwa, pamoja na kubaini ongezeko la madini mbalimbali, pia taarifa hizi hubaini mipasuko kwenye ardhi hivyo kusaidia kuratibu matetemeko na majanga mengine ya asili.

    Vilevile, uchunguzi wa sampuli kwenye maabara umeongezeka kutoka sampuli 650 (mwaka 2005) kwa mwaka na kufikia jumla ya sampuli 4500 hadi 5600 kwa mwaka kwa hivi sasa. Imeelezwa kuwa ongezeko hili la sampuli limetokana na kuboreshwa kwa vitendea kazi, majibu sahihi ya uchunguzi na wafanyakazi kupatiwa elimu na motisha.

    Kuhusu kuboresha rasilimali watu, vitendea kazi, miundombinu na mazingira yake, taarifa ya GST inaonyesha kwamba watumishi wapya wapatao 100 wameajiriwa na mafunzo mbalimbali ya muda mfupi na mrefu yameendelea kutolewa ndani na nje ya nchi. Vilevile, Wakala umeboresha vitendea kazi vya maabara, ugani, jiofizikia, uchoraji ramani, ofisi na samani.

    Aidha, taarifa imeeleza kuwa kwa upande wa kazi zilizofanyika ni pamoja na kukamilika kwa jumla ya tafiti 27. Tafiti hizo zilihusu utafutaji wa madini ya metali/vito, madini ya viwanda, nishati

    ya jotoardhi, matetemeko ya ardhi, milipuko ya volkano, mmomonyoko wa ardhi, upatikanaji wa magadi, uchenjuaji wa madini, ushauri wa namna bora ya utafutaji na uchimbaji wa madini kwa wachimbaji wadogo na uhifadhi wa mazingira.

    Wakala wa Jiolojia Tanzania ulianzishwa kama Wakala wa Serikali chini ya Wizara ya Nishati na Madini mwaka 2005 na kupewa jukumu la kubainisha maeneo yenye kupatikana madini mbalimbali nchini ili kuhamasisha uwekezaji katika sekta ya madini kwa lengo la kukuza uchumi wa Taifa.

    Pia, GST imepewa jukumu la kuratibu majanga asili ya jiolojia (matetemeko ya ardhi, milipuko ya volkano, mionzi ya asili kutoka kwenye miamba, kemikali za sumu zitokazo kwenye miamba na udongo, maporomoko ya ardhi) na kutoa ushauri wa namna ya kujikinga na kupunguza athari za majanga hayo.

    Dhima ya GST ni kutoa takwimu na taarifa za jiosayansi za kiwango bora kwa gharama stahiki kwa wadau ili kuongeza ufahamu wa rasilimali za madini, hivyo kuchangia katika lengo la Taifa la kupunguza umaskini, kuongeza ufahamu wa majanga ya asili na jinsi ya kupunguza athari zake, utunzaji wa mazingira, kuboresha usalama wa watu na mali zao.

    GST yaeleza mafanikio katika Serikali ya Awamu ya Nne

    Takwimu hizi zimeainisha maeneo yenye viashiria mbalimbali vya uwepo wa madini, kwa mfano eneo la Misaki, Mpambaa, Sambaru na Londoni ambapo ufahamu wa uwepo wa madini ya dhahabu umeongezeka

    Watalaam wa Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) wakifanya utafiti wa Jiolojia katika ukanda wa Dhahabu wa Lupa(Lupa Gold Field), wilayani Chunya mkoani Mbeya

  • 8 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHABARI ZA NISHATI/MADINI

    Elimu ya OMCTP kuanza kutolewa kwa kutumia gari la matangazo

    Na Zuena Msuya

    Wizara ya Nishati na Madini imeanzisha mfumo mpya wa usajili wa wateja kwa kutumia

    njia ya mtandao ijulikanayo kama Online Mining Cadastre Transactinal Portal( OMCTP) utakaowawezesha waombaji na wamiliki wa leseni za madini kujisajili kwa njia ya mtandao ili kufahamu na kuhakiki taarifa zao kwa urahisi.

    Kamishna Msaidizi wa Madini anayeshughulikia leseni, John Nayopa amesema utaratibu huo umeanzishwa ili kutekeleza agizo la Serikali la kutaka Wizara na Taasisi za Serikali kurahisha upatikanaji wa huduma bora karibu na wananchi, kupokea malipo ya Serikali kwa njia za kielektroniki ili kudhibiti mapato tofauti na ilivyokuwa hapo

    awali.Mwaka 2000, kitengo cha utoaji

    leseni kilikuwa Dodoma Wakati huo mamlaka ya utoaji leseni ilikuwa Dar-es-Salaam hali iliyosababisha ucheleweshaji wa kutolewa leseni na pia mfumo wa utoaji na kuchambua

    leseni ilifanyika kwa mkono, alisema Nayopa.

    Aliongeza kuwa mfumo huo unafanana na ule unaotumiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika malipo ya leseni za magari au mfumo wa kununua luku ambao utawapunguzia wananchi ugumu wa kupata huduma.

    Nayopa alisema mfumo wa OMCTP utaongeza uwazi na kasi ya utoaji wa leseni za madini,wateja wataingiza maombi ya leseni wao wenyewe, hivyo kupunguza tatizo la mlundikano wa maombi katika ofisi za madini.

    Vile vile alisema kuwa wateja watapata taarifa za leseni zao kila wakati na kujua wanapotakiwa kufanya malipo ya leseni au watakapotakiwa kutuma taarifa za utendaji kazi pia kurahisisha mawasiliano kati ya Wizara na wamiliki wa leseni.

    Awali waombaji wa leseni walilazimika kwenda katika ofisi za madini kujaza fomu za maombi, kufyeka mipaka ya eneo wanaloomba na kuweka vibao; kisha kumleta Afisa madini ili kukagua eneo linaloombwa na hatimaye kwenda kufanya malipo ya maombi hayo kwenye ofisi ya Madini,alisema Nayopa

    Aliongeza kuwa wateja na Serikali watakuwa na uhakika na maombi yote yatakayowasilishwa (yakiwamo maombi ya sihia (transfer), kuhuisha leseni n.k.); na pia kuwa na uhakika na malipo yote yatakayofanywa kupitia mfumo wa OMCTP

    Aidha aliongeza kuwa ili kutoa elimu kwa wadau wote wa madini Wizara itatoa mafunzo kuanzia tarehe 19 Julai hadi pale itakapomaliza wadau wote kwa kuanzia mikoa ya Kanda ya Mashariki, Kanda ya Kati,Magharibi na Kanda ya Kusini.

  • 9BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHABARI ZA NISHATI/MADINI

    STAMIGOLD YATIMIZA MWAKA MMOJA WA UCHIMBAJI DHAHABU

    Kwa wadau wa sekta za Nishati na Madini, tembelea kurasa mpya za Wizara kwenye Mitandao ya Kijamii ya Twitter na Facebook kwa anuani ya Nishati na Madini Karibu tuhabarishane na

    tujadili kuhusu sekta za Nishati na Madini kwa maendeleo ya Watanzania wote.Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

    Kampuni ya STAMIGOLD ambayo ni kampuni tanzu ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) imetimiza mwaka mmoja wa uchimbaji dhahabu katika mgodi wake wa Biharamulo uliopo wilayani Biharamulo Mkoa wa Kagera ambapo uchimbaji ulianza rasmi mnamo mwezi Julai, 2014. Ndani ya kipindi cha mwaka mmoja wa uchimbaji (Julai 2014 Juni 2015), kiasi cha wakia 16,388 za dhahabu zimekwishazalishwa na jumla ya wakia 12,923 za dhahabu zenye thamani ya Dola za Kimarekani Milioni 15.6 zimekwishauzwa kwenye soko la kimataifa.

    Kiasi hicho cha dhahabu kilipatikana katika maeneo ya West Zone na Mojamoja takribani kilomita tatu na nusu kutoka uzio wa mgodi ambapo uchimbaji wa dhahabu bado unaendelea. Maeneo hayo mapya yalikabidhiwa STAMICO kutoka mgodi wa Tulawaka uliokuwa ukimilikiwa na kampuni ya African Barrick Gold sasa ACACIA mwishoni mwa mwaka 2013.

    Akizungumza katika hafla ya kusherehekea mwaka mmoja tangu kuanza kwa shughuli za uchimbaji wa dhahabu iliyofanyika katika mgodi wa Biharamulo, Meneja Mkuu wa mgodi wa Biharamulo, Mhandisi Dennis Sebugwao alieleza kuwa matarajio ya mgodi ni kutafuta namna ya kuhakikisha uzalishaji wa dhahabu unaendelea kwa kiwango kikubwa na gharama nafuu ili kusaidia kukuza uchumi wa nchi na kuongeza nafasi za ajira kwa Watanzania kwa ajili ya maslahi ya Taifa zima.

    Siwezi kuficha furaha yangu, siku ya leo ni siku ya muhimu kwetu sote katika historia ya Mgodi huu kwani tunathibitisha kwa Serikali na Watanzania wenzetu kuwa, Watanzania wasomi na wenye taaluma mbalimbali katika sekta ya uchimbaji na uzalishaji wa dhahabu wameendelea kuonyesha uwezo wao kwa kuhakikisha uzalishaji unaendelea kufanyika katika mgodi wa STAMIGOLD Biharamulo bila kuwepo wataalam wa kigeni kama ilivyokuwa ikiaminiwa. alieleza Sebugwao.

    Mhandisi Sebugwao pia alielezea mafanikio yaliyofikiwa na mgodi ndani ya mwaka mmoja ambayo ni pamoja na mgodi kuendeshwa kwa kufuata taratibu za usalama na afya kazini, ulinzi imara ndani na nje ya mgodi, kupunguza gharama za uendeshaji wa mgodi, kulipa ushuru wa huduma wa 0.3% ya mauzo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo kiasi cha Shillingi milioni 40.9 mpaka June 2015, kuajiri wafanyakazi wa Kitanzania 340 wa fani mbalimbali za kitaalamu, ajira za muda mfupi 43 kwa wakazi wa vijiji vilivyo jirani na mgodi na wakandarasi wa Kitanzania 281.

    Aliongeza kuwa mgodi umekuwa ukizisaidia jamii zilizo jirani na mgodi kupunguza changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwa ni pamoja na kugawa madawati 1500 kwa shule zenye upungufu katika Wilaya za Biharamulo, Muleba na Ngara, ujenzi wa choo cha wanafunzi Shule ya Msingi Mavota, ukamilishaji wa ujenzi wa madarasa manne Shule ya Msingi Mpago, ukarabati wa miundo mbinu pamoja kuwawezesha wananchi kiuchumi kupitia vikundi vitatu vya ujasiriamali kwa kununua vyakula vya asili, mbogamboga na matunda wanayozalisha.

    Kwa upande mwingine, katika kusherekea siku hiyo shamrashamra mbalimbali zilifanyika ikiwemo mechi ya mpira wa miguu ambapo timu ya mgodi ilicheza mechi ya kirafiki na timu iliyoundwa na wachezaji kutoka vijiji vya Mavota na Mkunkwa na timu ya mgodi kuibuka kidedea kwa bao 2-0. Baada ya michezo kumalizika timu zote za mpira wa miguu zilikabidhiwa zawadi na Meneja Mkuu wa mgodi.

    Katika kuhitimisha sherehe hizo zilitolewa zawadi na vyeti kwa wafanyakazi 10 ambao walifanya vizuri katika Idara zao kwa kipindi cha mwaka mmoja wa uzalishaji ambao pia walipatiwa heshima ya kushiriki na Meneja Mkuu wa mgodi kukata keki ya kutimiza mwaka mmoja wa uzalishaji.

    Wakati huo huo, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala kutoka STAMICO Deusdedith Magala, aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo Mhandisi Edwin Ngonyani, aliupongeza uongozi na wafanyakazi wa mgodi kwa kazi nzuri ambayo inaendelea kufanyika na kusema kuwa mafanikio yanayopatikana ni sifa kwa Shirika na Taifa kwa ujumla kwani tayari mgodi umethibitisha uwezo wa Watanzania kuzalisha dhahabu bila kuongozwa na wataalam wa kigeni.

    Nimefurahishwa sana na mafanikio mliyofikia pamoja na namna wafanyakazi wanavyojituma baada ya kutembelea maeneo mbalimbali hapa mgodini na kujionea kazi zinavyofanyika. Naomba muendelee na bidii hiyo na vile vile mjitahidi kuongeza zaidi njia za mawasiliano za kutangaza mafanikio ya mgodi huu mfano misaada inayotolewa katika jamii ili dunia na taifa kwa ujumla kufahamu kuwa ipo kampuni ya Kitanzania inayochimba dhahabu kwa manufaa ya Taifa zima la Tanzania alifafanua Magala.

    Mbali na mafanikio hayo mgodi wa STAMIGOLD Biharamulo bado unakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo ni pamoja na kuyumba kwa bei ya dhahabu katika soko la dunia, ufinyu wa mtaji wa kuendesha shughuli mbalimbali za mgodi pamoja na uhaba wa maji kutokana na vyanzo vilivyopo kutegemea msimu wa mvua.

    Kampuni ya STAMIGOLD Biharamulo ilizalisha dhahabu yake ya kwanza mnamo mwezi Agosti 2014 na mpaka sasa imeendelea kuweka historia kwa kuwa kampuni pekee hapa nchini inayozalisha dhahabu kwa kusimamiwa na kuendeshwa na wataalam wa Kitanzania pekee.

    Imetolewa na: Kitengo cha Mawasiliano

    STAMIGOLD Biharamulo Plot. No. 417/418

    UN Road S.L.P 78508

    Dar es Salaam. Email: [email protected] Website: www.staigold.co.tz

    KAMPUNI YA STAMIGOLDMGODI WA BIHARAMULO

    TAARIFA KWA UMMA