204

Click here to load reader

31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

  • Upload
    vutruc

  • View
    1.609

  • Download
    360

Embed Size (px)

Citation preview

Page 1: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

1

BUNGE LA TANZANIA________________

MAJADILIANO YA BUNGE___________________

MKUTANO WA KUMI NA MOJA

Kikao cha Thelathini na Tisa - Tarehe 31 Mei, 2013

(Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi)

D U A

Naibu Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge leo ni Kikao chaThelathini na Tisa Mkutano wa Kumi na Moja. Katibu!

HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI

Hati Zifuatayo Ziliwasilishwa Mezani na:-

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO, SAYANSI NATEKNOLOJIA:

Randama ya Makadirio ya Mapato na Matumizi yaWizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kwa Mwakawa Fedha 2013/2014.

NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI:

Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi yaWizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi kwa Mwaka waFedha 2013/2014.

Page 2: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

2

MHE. AMINA N. MAKILAGI (K.n.y. MWENYEKITI WAKAMATI YA KILIMO, MIFUGO NA MAJI):

Taarifa ya Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji KuhusuUtekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Maendeleo ya Mifugona Uvuvi kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013, Pamoja na Maoniya Kamati Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi yaWizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014.

MHE. JOSEPH R. SELASINI MSEMAJI WA KAMBI YAUPINZANI KWA WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NAUVUVI):

Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani waWizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Kuhusu Makadirioya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha2013/2014.

MASWALI NA MAJIBU

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge kablahatujaendelea na maswali, naomba niwajulishe tu kwamba,Mheshimiwa Waziri Mkuu yuko safari, lakini kwenye kiti paleanayekaimu kwa shughuli za Serikali Bungeni ni MheshimiwaSamuel J. Sitta. (Makofi)

Na. 312

Kutenga Makazi kwa ajili ya Jamii ya Waadzabe

MHE. NEEMA M. HAMID aliuliza:-

Je, Serikali ina mikakati gani ya kutenga makazi kwaajili ya Wahadzabe ambao hujishughulisha na urinaji wa asalina kukusanya matunda ili jamii hii pamoja na mila zaoisipotee?

Page 3: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

3

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZAMIKOA NA SERIKALI ZA MITAA, (TAMISEMI) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya MheshimiwaWaziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimwa NeemaMgaya, Mbunge nwa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Jamii ya Wahadzabeambayo iko katika kundi Kihistoria la Khoisan inapatikanakatika Bonde la Ufa la Kaskazini mwa Tanzania hususan Wilayaya Mbulu, Karatu, Iramba na Meatu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imefanya jitihadambalimbali katika kuhakikisha kuwa Jamii hii haipotei na piainapata huduma muhimu za kijamii kama zilivyo jamii nyinginekatika nchi yetu. Nia ya Serikali ni kuibadilisha jamii hii kwakuiwezesha kupata mahitaji na huduma muhimu za kijamiibila kuathiri tamaduni zao.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imetenga maeneoya makazi ya Wahadzabe, na kupeleka huduma za jamiikama elimu, maji na afya. Kwa Halmashauri ya Wilaya yaMbulu, jamii ya Wahadzabe wametengewa maeneo katikaVijiji vya Dumanga na Mongo wa Mono, na kujenga shule zaMsingi katika vijiji vya Yaeda Chini (Shule za Bweni), naEndagulda na Sekondari moja katika kijiji cha Yaeda Chini.

Pia imechimba visima vya maji katika vitongoji vitatuvya vijiji hivyo na kwa kushirikiana na wadau wa maendeleona inakusudiwa kupeleka miradi mingine mikubwa, ikiwemoya maji ya bomba katika vijiji vya Yaeda na Mongo wa Mono.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kutambua Utamaduniwa jamii hii, katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu naHanang kwa kushirikiana na wadau wa maendeleowameweka mikakati ya kuhifadhi utamaduni wa jamii hizi zakihistoria katika kituo cha utamaduni cha Haydom-Mbulu.Aidha bila kuathiri utamaduni wa jamii hii, Serikali imelengakuwabadilisha kabila la Wahadzabe kuwa wakulima nawafugaji bora wa nyuki ili kujitosheleza kwa chakula.

Page 4: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

4

Kwa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba jamii hiiimepatiwa mafunzo ya kilimo cha Mhogo na ufugaji wa Nyukikwa kupatiwa Mizinga 123.

MHE. NEEMA M. HAMID: Mheshimiwa Naibu Spika,nashukuru kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri,nilikuwa n aswali moja tu dogo la nyongeza, nilikuwa ntatakakujua, pamoja na yote haya Serikali iliyofanya. Je, kunamkakati gani wa kuhakikisha kwamba vijana wa Kihadzabewanapata fursa ya kupata mikopo kama wanavyopatavijana wengine ili kuweza kuendeleza biashara zao zakurina asali?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZAMIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa NaibuSpika, naomba kujibu swali la nyongeza la MheshimwaNeema Mgaya, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza mimi nimpongezeMheshimiwa Neema Mgaya kwa jitihada zake hizi za kuionahii jamii kwamba nayo inaendelezwa kama viletunavyowaendeleza Watanzania wengine bila kuwabagua,lakini wakati huo huo tukiendelea kuhakikisha kwamba tunahifadhi tamaduni zao ili zisije zikapotea kama nilivyoelezahapa.

Sasa kuhusu hili suala la kwamba hao vijana waliokokatika hizi Halmashauri wanasaidiwa, hatuwaondoi katikamfumo mzima wa Halmashauri, katika Halmashauritiunatenga asilimi atano kwa ajili ya vijana, na tunatengaasilimia tano kwa ajili ya akina mama.

Kwa hiyo, hatuwaodoi katika huo mfumo, lakini piaanavyosema Mheshimiwa Mgaya hapa, ni kwamba upelekefocus maalum kwa sababu hili ni kundi ambalo kidogo kamavile limeachwa nyuma ya mfumo, ili tuweze kulisaidia.

Page 5: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

5

Kwa hiyo, tutakwenda kuangalia sasa kwa kiasi ganihao nao tunaweza tukawa-consider, lakini tukitumia mfumohuu hu wa Halmashauri, na ndiyo maana nimesema hapakwamba kumekuwa kuna taratibu za kuona kwambawanapata hata hiyo mizinga, wanapata shughuli nyingineza kilimo bora na cha kisasa ili waweze kuondoka katika haliile ya umasikini. (Makofi)

MHE. CHRISTOWAJA G. MTINDA: Mheshimiwa NaibuSpika, ahsante, nina swali dogo tu la nyongeza, kwanzanikubaliane na Serikali kabisa kwamba ilifanya kazi kubwasana ya kuwaandalia mazingira hawa ndugu zetuWahadazabe, pia kuna kabila lingine la Watindiga ambalolinafanana kabisa na la Wahadzabe, ambalo pia najuaSerikali ilifanya juhudi ya kuwajengea shule pamoja nahospitali, mfano mzuri ni katika Mkoa wa Singida, Iramba kulemaporini kule.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa habari ambazo ninazona kwa uhakika amabao ninao ni kwamba, zile shule ambazozilijengwa na Serikali pamoja na Kanisa, wale Wahadzabena Watindiga walizikimbia, na wameendelea kuingia porinikuishi porini. Kwa hiyo, watoto wale wa Wahdzabe hawananafasi tena ya kwenda shuleni.

Je, Serikali iko tayari sasa kwenda kufanya utafiti wakina, hususan Mkoa wa Singida kuangalia ni kwa namna ganiinaweza kushawishi hiyo jamii ya Watindiga na Wahadzabeili waweze kurudi katika maeneo ambayo walitengewa naSerikali na kuwasomesha watoto wao?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Christowaja, hivi kumbeWahadzabe na Watindiga ni kabila mbili tofauti.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZAMIKOA NA SERIKALI ZA MITAA, (TAMISEMI): Mheshimiwa NaibuSpika, naomba kujibu swali la nyongeza la MheshimwaChristowaja G. Mtinda, kama ifuatavyo:-

Page 6: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

6

Anachosema Mheshimiwa Christowaja ni kweli,wakati tulipokuwa tunatafuta haya majibu, ilionekana onceupon a time, wakati wa Mwalimu, kuna hata na nyumbaambazo zilikuwa zimeandaliwa kwa ajili ya haya makundiambayo yanazungumzwa hapa, na ambazo zinaonekanakwamba ziliachwa hivi hivi, haziendelei kutumika, na tunaionahii kama ni sehemu ya changamoto, lakini pia wakatiunapoangalai masuala ya udamaduni ni lazima uwemwangalifu sana, uweze kwenda nao kwa taratibu, graduallyili kutokuathiri sasa hizo tamaduni zao, lakini wakati huohuoukihakikisha kwamba wanaingizwa katika mfumo huo wakisasa wa teknoloji na high take. Tungekwenda kwa mwendohuu tunaokwenda tusingeweza kusafiri kwenda mpakaUchina, kwa sababu kusingekuweko na Ndege, tungekuwatuna kaa tu tunawinda na vitu vingine.

Mheshimiwa Naibu Spika, ambacho tutakifanya hapani kwamba, tutaziagiza hizi kwa maana ya haya mazungumzoyanayokuja hapa. Tutaziagiza Halmashauri zetu, tufuatilie kwakaribu, madarasa yael yamejengwa kule, n ashulezimejengwa kule, tumejenga nyumba kule, sasa tungetakakuona haya makundi kidogo kidogo tinawapeleka kwanamna ambayo wanaelimishwa, ili waweze kuiona a one toone function kati ya hiyo development na maisha yao.Otherwise watabaki tu wa kuokota matunda na kuwindahuko msituni, kitu ambacho nadhani si target yetu sisi kamataifa. (Makofi)

Na. 313

Kufufua Barabara ya Mjerumani

MHE. IGNAS A. MALOCHA (K.n.y. MHE. JOSEPHAT S.KANDEGE) aliuliza:-

Barabara ya zamani ya Mjerumani itokayo kijiji chaIsanga - Wilaya ya Mbozi–Kijiji cha Kisanga - Wilaya mpya yaKalambo ni fupi kuliko zote kuunganisha Mkoa wa Rukwa naMbeya, Kigoma, Katavi, Tabora na nchi jirani za Zambia,Burundi na Congo DRC.

Page 7: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

7

Je, Serikali haioni umuhimu wa kuifufua barabara hiyokulingana na umuhimu wake kiuchumi hasa ikizingatiwa kuwakukosekana kwa daraja la mto Kalambo ndiyo kikwazokikubwa cha kutokamilika kwa barabara hiyo?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZAMIKOA NA SERIKALI ZA MITAA, (TAMISEMI) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya MheshimiwaWaziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa JosephatS. Kandege, Mbunge wa Kalambo, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, barabara ya Mjerumaniinaanzia Mkao wa Mbeya katika kijiji cha Isanga hadi Kakosina Ilonga katika Wilaya mpya ya Momba na kuendeleakatika Mkoa wa Rukwa kupitia vijiji vya Mambwenkoswe,Kalepua, Mwimbi, Kamawe hadi Kasitu (kwenye eneo la MtoKalambo) katika Wilaya mpya ya Kalambo.

Mheshimiwa Naibu Spika, ili kukufua barabara hii, Timuya watalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawangakwa kushirikina na wataalamu kutoka ofisi ya TANROADSMkoa wa Rukwa mwezi Februari, 2013 ilitembelea barabarahiyo na kuikagua kwa lengo la kuifanyia matengenezo.

Aidha, ili kufufua barabara hii sehemu ya Kisatu hadiKasanga kutahitajika ujenzi wa daraja kubwa katika mtoKalambo ili kuunganisha kijiji cha Kisatu na Nondo kuelekeakuelekea katika eneo la Kasanga.

Tathimini ya awali inaonyesha kuwa zinahitajikashilingi milioni 217.5 kwa ajili ya kujenga daraja na shilingimilioni 858.0 kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwangocha changarawe. Hivyo, gharama za matengenezo yabarabara na daraja kwa makadirio ya awali zinafikia shilingibilioni 1.075.

Page 8: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

8

Mheshimiwa Naibu Spika, azima ya Serikali ni kuijengabarabara hiyo ili kuwaondolea kero ya usafiri wananchi wamaeneo hayo. Kwa mantiki hiyo, Mkurugenzi Mtendaji waHalmashauri ya Wilaya Kalambo anaagizwa kufanyaupembuzi yakinifu wa barabara hiyo ili kujua gharama halisina hivyo kutenga fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi wabarabara hiyo

MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Naibu Spika,nashukuru, kwanza nashukuru kwa ufafanuzi wa MheshimiwaNaibu Waziri, lakini ninayo maswali mawili ya nyongeza.

Kwa vile usanifu wa awali unaonyesha gharamakaribu ya bilioni 1.7 na Halmashauri ya Kalambo, katikamakusanyo yake, hayazidi milioni 500.

Je, Serikali ipo tayari kuisaidia Halmashauri yaKalambo ili kuwezesha matengenezo ya barabara hiyo?

Swali la pili, kutokana na shida iliyopo ambayoimeanza kukua kwa wananchi wa Halmashauri ya Kalambo,nini udharura wa Serikali kaytika kuwasaidia wananchi hao?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZAMIKOA NA SERIKALI ZA MITAA, (TAMISEMI): Mheshimiwa NaibuSpika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Ignas Malocha,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, yuko light, Halmshauri yaKalambo ile ni mpya, own source yake kama anavyosema,siyo milioni 500, ni milioni 700.5, ndiyo own source yake, hataukiwaambia waende wakajenge wenyewe hawatawezawale, na fedha za barabara zilizopelekwa katika Wilaya hiimpya ya Kalambo hapa ni shilingi milioni 500, ndizotumezipitisha hapa, kwa hiyo, unaweza ukaona tu kwambahaitawezekana.

Page 9: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

9

Kwa hiyo, tunachokisema hapa, hii barabarakutengenezwa kwa kiwango cha changarawe na hilo darajaliweze kujengwa pale la wakati wa Mjerumani, na bahati nzurimimi nimekwenda katika hilo daraja, nalifahamu, naombanimpongeze sana Mheshimiwa Kandege, ni Mbunge ambayeanapigania sana maendeleo ya watu wake, anahangaikanao kweli, hata kama hayupo hapa nadhani itakuwa nisababu hiyo hiyo, ya kwamba anaendelea.

Mimi nataka nimpongeze sana, hapa cha kufanyahapa, cha kwanza, kwanza kabisa tumeagiza Halmashauriifanye feasibility study ijue kiasi halisi kinachohitajika kwaajili ya hii barabara, hiyo ya kwanza.

Sasa anazungumza habari ya udharura, udharura nikupita kwenye barabara ya lami, kule ambapo tunajengasasa hihi, maana yake apoitie Sumbawanga, palewanatakiwa waende kilomita 112, kitu ambaho ni bugudha,lakini sasa hatuna jinsi kama mvua zitakuwa zimenyesha,lazima wapitie katika ile barabara. Otherwise hatuna namnaya kwenda kuweka magogo pale ni pagumu sana. Lakinimimi naomba tu wafanye haraka, watutengenezee hizotwakwimu, walete katika maombi maalum, halafututazungumza na Wizara ya Fedha tuone jinsi ya kuwasaidia.(Makofi)

Na. 314

Kima cha chini cha Mishahara

MHE. MENDRAD L. KIGOLA aliuliza:-

Serikali ilitangaza kima cha chini cha Mshahara kwamfanyakazi kuwa ni shilingi 170,000/= kwa mwaka wa 2012/2013.

(a) Je, kwa nini Serikali haijaweka na kutoa tamkola kima cha chini cha mishahara kwa Mashirika ya watubinafsi pamoja na Kampuni kubwa za wawekezaji?

Page 10: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

10

(b) Je, kwa nini Kampuni zenye uzalishaji mkubwalakini wanalipa mishahara midogo kuliko kima cha chini chaSerikali?

(c) Je, kwa nini Kampuni binafsi hazitoi mikatabamirefu ili mfanyakazi apate haki zake?

NAIBU WAZIRI WA KAZI NA AJIRA alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya MheshimwaWaziri wa Kazi na Ajira, naomba kujibu swali la MheshimiwaMendrad L. Kigola, lenye kipengele (a) (b) na (c) kamaifuatavyo:-

(a) Kima cha chini cha mshahara kwa sektabinafsi inasimamiwa na Bodi za Mishahara Kisekta. Bodi zaMishahara Kisekta zinaundwa kwa mujibu wa Sheria ya Taasisiza Kazi Na. 7 ya mwaka 2004. Kwa mujibu wa Sheria hiyo,mishahara katika Sekta binafsi inapangwa kulingana na ainaya uzalishaji, mazingira ya kazi na eneo kwa sekta husika.

Mheshimiwa Naibu Spika, Tarehe 29 Mei, 2013 wakatiwa Hotuba ya Bajeti ya Wizara Kazi na Ajira kwa mwaka waFedha 2013/2014, Serikali ilitoa tamko la kima cha chini chamshahara kwa sekta binafsi (Private Sector)

(b) Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu Kampunizenye uzalishaji mkubwa kulipa mishahara midogo, Serikaliinalipokea suala hili kama changamoto. Bodi zilizoundwakisekta na ambazo tayari zimeshaanza kazi ya utafitizitaendelea zitabaini uhalali wa ulipaji wa mishahara kwawatumishi wa kila sekta husika.

(c) Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibu waSheria ya Ajira na Mahusiano kazini Na. 6 ya mwaka 2004,Mikataba ya kazi ipo ya aina tatu ambayo ni; Mkataba usiona ukomo wa muda, Mkataba wa muda maalum kwaMameneja na kazi za taaluma, pamoja na Mkataba wa kazimaalum.

Page 11: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

11

Mheshimiwa Naibu Spika, Mwajiri yoyote hapaswikuajiri mfanyakazi kinyume na aina ya mikataba kamanilivyokwisha itaja hapo juu na kwamba aina zote tatu zamikataba ya kazi zinakubalika kisheria.

MHE. MENDRAD L. KIGOLA: Mheshimiwa Naibu Spika,nashukuru sana, napenda niulize maswali mawili yanyongeza. Kwa kuwa amekili kwamba kuna Mashirika yakemakubwa ambayo yanalipa kiwango cha chini chamishahara, na ameunda Tume kwa ajir i ya kubainichangamoto hiyo.

Je, ikigundulika kwamba kuna Mashirika yanafanyauzalishaji mkubwa na wamewalipa mishahara midogo walewafanyakazi, Serikali itachukua hatua gani?

Swali la pili, imetokea kwamba kuna mashirikawanaajiri wafanyakazi wa muda mfupi, wanaita SeasonLabour, na wale wanakwenda, miezi mitatu mitatu, nawanafanya kazi kwa muda wa miaka mingi bila kuajiriwa,kupewa mikataba ya kudumu.

Je, Serikali ikija kugundua, kwamba mtu amefanyakazi kwa muda mfupi mfupi, na hakupata haki zake, itawezakuchukua hatua gani? (Makofi)

NAIBU WAZIRI KAZI NA AJIRA: Mheshimiwa NaibuSpika, napenda kujibu Maswali mawili ya Nyongeza yaMheshimiwa Mendrad L. Kigola, kama hivi ifutavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kama ambavyotumetangaza kwenye wakati kuwasilisha Bajeti yetu hapa.Mishahara hii kwa kila sekta itatangazwa kwenye Gazeti laSerikali. Kwenye Gazeti tutaonyesha viwango kamiliambavyo vitalipwa, kwa sekta zote 12.

Page 12: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

12

Sasa kama kutakuwa na Kampuni ambayoitakwenda kinyume na malipo yatakayokuwayameonyeshwa kwa kila sekta. Au kuna zile sekta ambazozimewekwa kidaraja, kwa kila daraja, ni kwamba hatua kaliza Kisheria zitachukuliwa kwa sababu atakuwa amevunjaSheria. Lazima alipe hicho kama kiwango cha chini. Lakiniwaweze wakalipa kiwango cha juu zaidi kutegemea nauzlishaji.

Pili, kuhusu wanaoajiriwa kwa Mikataba isiyo ya mudamrefu. Nimesema, kuna mikataba aina tatu. Na lazimawafanyakazi waangalie katika mikataba ya aina tatu ile.Mikataba usiokuwa na ukomo. Mikataba ya waleProfessionals, ambayo inakuwa ni ya muda maalum auMameja, na Mikataba ya kazi maalum. Ni mikataba hiyomitatu tu. Hakuna Mkataba unaoitwa Mkataba labda waTemporary au wa muda.

Sasa akipewa Mkataba wa aina hiyo lazima alipwekutegemea na aina hiyo ya Mkataba na Mwajiri hawezikwenda kinyume na Mkataba huo. Kama akienda kinyumena Mkataba aliompa basi, sheria itachukua mkodo wake.

NAIBU SPIKA: Ahsante sana nilikuona MheshimiwaHamad Rashid Mohamed. Swali la mwisho la nyongeza.

MHE. HAMAD RASHID MOHAMED: Mheshimwia NaibuSpika, ahsante sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, wafanyakazi wetu wotenchini, hutegemea sana siku ya Mei Mosi hutangazwakiwango cha mshahara ama kupanda au kutokupanda.

Je, Serikali inafikiri ni utaratibu huu mzuri huu wawafanyakazi kungojea hali ya Kiongozi kutangaza kiwangocha chini au kikubwa cha mshahara. Haioni kwamba wakatiumefika sasa kuwa na utaratibu ambao kila mfanyakaziatajua kiwango chake cha kuongezewa mshahara kinakujani automatic, badala ya kungojea hii hali ya kutangazwatangazwa.

Page 13: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

13

Je, huu ni utaratibu mzuri? (Makofi)

NAIBU WAZIRI KAZI NA AJIRA: Mheshimiwa NaibuSpika, napenda kujibu swali la nyongeza la MheshimiwaHamad Rashid Mohamed, rafiki yangu kama hivi ifutavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, utaratibu wa kutangazamishahara kwa siku za karibuni, siyo kwenye majukwaa aukwenye Mei Mosi. Kwa watumishi wa Serikali, mishaharawanaikuta tayari kwenye pay slip zao. Lakini wakati wakusoma Bajeti yake, Waziri wa Utumishi anaweza kuonyeshatu viwango kulingana na ongezeko la Bajeti ya mishaharakwamba Bajeti ya mishahara imeongezeka na kwa maanahiyo mwaka huo wafanyakazi wategemee nyongeza yamishahara watakapopokea mishahara yao.

Kwa upande wa Sekta Binafsi, kama ambavyo Waziriwa Kazi na Ajira, amefanya. Mishahara hii hutaangazwakwenye Gazeti la Serikali. Ila anaweza kutoa mwelekeo,kwamba hali ni nzuri kwa maana mishahara itaongezekaama kwenye Bajeti ama Mei Mosi. Lakini kujua hasamshahara wa mfanyakazi ataona kama ni Sekta Binafsiataiona kwenye Tangazo la Gazeti la Serikali. (Makofi)

Na. 315

Ucheleweshaji wa Maamuzi ya Kesi Zilizokamilika

MHE. CLARA D. MWATUKA aliuliza:-

Je, ni sababu gani za msingi zinazosababisha, kesizisizohitaji uchunguzi au ambazo uchunguzi wakeumekamilika kutotolewa uamuzi kwa haraka?

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali laMheshimiwa Clara Mwatuka, Mbunge wa Viti Maalum, kamahivi ifuatavyo:-

Page 14: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

14

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa naombakuweka wazi kwamba kesi zote za jinai zinazopelekwa katikaMahakama zetu ni lazima zifanyiwe upelelezi wa kina kablahazijafunguliwa Mahamani. Kesi zikikisha funguliwaMahakamani, Sheria na Kanuni zilizopo za uendeshaji wa Kesizinataka Kesi isikilizwe na kutolewa uamuzi mapema ila kamakuna sababu ya msingi inayosababisha kucheleweshamaamuzi.

Mheshimiwa Naibu Spika, zipo sababu kadhaaambazo zinasababisha ucheleweshaji wa maamuzi kwa kesiambazo upelelezi wake umekamilika. Sababu hizo nipamoja:-

(i) Wingi wa kesi zinazofunguliwa ikilinganishwa na idadindogo ya watumishi waliopo.

(ii) Sababu za kiufundi za kisheria yaani (LegalTechnicalities) zinazosababisha mapingamizi ya kisheria nahivyo kukwamisha kwa muda ukamilishaji wa maamuzi/uamuzi mapema.

(iii) Bajeti finyu inayosababisha:-

• Vikao vya kusikiliza kesi za Mahakama Kuu kutofanyikamara kwa mara.

• Vile vile upungufu wa virtendea kazi kwa upande waMahama za chini na Wadau wake.

• Kutopatikana kwa fedha za kuwalipa mashahidi.

(iv) Kutopatikana kwa mashahidi kwa wakati nakunakosababisha kesi kluahirishwa mara kwa mara.

(v) Mahabusu kutofikishwa Mahakamani siku za kusikilizakesi zao.

Page 15: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

15

(vi) Dharua kwa watendaji/pande muhimu kwenye kesiMahakamani, kama vile Hakimu, Mwendesha, Mashtaka,Wakili wa Utetezi, Mshtakiwa na Wazee wa Baraza.

(vii) Lakini nyingine ni pamoja na uhamisho wa Mahakimu.Unaosababisha Kesi isiendelee, hadi atakapopatikanaHakimu mwingine wa kuendelea kusikiliza Kesi hiyo au kuanzakuisikiliza upya kwa kadri Sheria itakavyohitaji kwa Kesi husika.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Clara Mwatuka,ameridhika. Ninakushukuru sana, na Mheshimiwa Dkt.Augustine Mrema atauliza swali la nyongeza.

MHE. CLARA D. MWATUKA: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuriya Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, inaonyesha wazikwamba sababu inayosababisha au inayopelekea mamboyote haya kutokea ni ufinyu wa Bajeti.

Je, Serikali haioni kwamba upo umuhimu wakuiongezea Idara hii pesa il i isizidi kuwacheleweshaMahabusu Mahakamani na kuwanyima haki zao? (Makofi)

Swali la pili, Mheshimiwa Rais alipotemembeleaMagerezani, alishauri kwamba kesi ndogo ndogo zitozwefaini, ili kupunguza msongamano wa Mahabusu Magerezani,pia kupunguza idadi ya kesi Mahakamani. (Makofi)

Je, Mheshimiwa Waziri, utekelezaji wa suala hiliumefikia wapi? (Makofi)

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: MheshimiwaNaibu Spika, kwanza kabisa ametaka kujua endapo Serikaliinaona ni muhimu kuiongezea Mahakama fedha. Ni kweliSerikali inaona ni muhimu kuiongezea fedha, na kamautakumbuka tarehe 3 Mei, 2013 tulipopitisha Bajeti ya Wizaraya Katiba na Sheria. Idara ya Mahakama iliongeweza katikaMipango ya Maendeleo, Shilingi Bilioni 20 na kufanya hivi sasa

Page 16: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

16

kuwa na Shilngi Bilioni 42.7. Lakini pia kwa upande wa fedhaza Matumizi yaani (OC) mwaka huu tumetengewa ShilingiBilioni 86.6, tofauti ni mwaka 2012, ambapo tulikuwa natakriban Shilingi Bilioni 57.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pia siyo haya tu.Bunge lako Tukufu kupitia Kamati ya Bajeti na kupitia Wizaraya Fedha, imeiongezea Kurugenzi ya Mashtaka Shilingi Bilioni10 zaidi kwa ajili ya (O.C) ili kuweza kuhakikisha basi tunafanyaziara za mara kwa mara katika Magereza yetu na kuhakikishakwamba tunawatoa wale wote ambao wamebambikizwakesi. Lakini pia kufahamu ni kesi gani za muda mrefu, ili ziwezekusikilizwa haraka.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini endapo miaka ijayoikiruhusu, tutashukuru pia tukiongezewa zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika swali la pili, kuhusianani kwa nini sasa hatutumii utoaji wa faini au adhabu mbadalana utekelezaji wake umefikia wapi baada ya agizo laMheshimiwa Rais, alipotembelea Magereza. Ni kweli aliagizahivi, lakini pia ni kauli mbiu na niadhma ya Mahakamakutumia adhabu mbadala na ndiyo maana hivi sasa kwakushirikiana na Mratibu wa huduma za jamii, Hivi sasa katikaMahakama nyingi tayari tunao Waratibu wa Huduma zaJamii, na adhabu hizi mbadala tayari zimekwisha kuanzakutolewa katika mikoa mingi ikianzia na Dar es Salaam, natayari matunda tumeishaanza kuyaona.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, sasa tumsikilizemtu mwenye uzoefu mkubwa katika eneo hili MheshimiwaDkt. Augustine Lyatonga Mrema.

MHE. DKT. AUGUSTINE L. MREMA: Mheshimiwa NaibuSpika, ninakushukuru sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, siyo Kesi za JInai tuzinazochelewa Mahakamani. Hata kesi za madai. Mfanomzuri ni kule Himo. Serikali imetangaza mji wa Himo upimwe,watu wajenge. Barabara zitengenezwe, lakini kwa muda wa

Page 17: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

17

miaka 11 kuna kesi Mahakamani inayozuia ujenzi wa Mji ulena Mahakama inajua, Wizara ya Katiba na Sheria mnajua.Hata mimi nimekulalamikia, kwamba haiwezekani tuwe namji usiopimwa, usiojengwa watu wana kesi Mahakamani, kwakipindi cha miaka 11 hakuna upelelezi. Wanao dai wakopale pale na tunao daiwa tuko pale.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba MheshimiwaWaziri aniambie. Hatima ya mji wa Himo ni nini, na kesi iliyopoMahakamani kwa miaka 11?

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: MheshimiwaNaibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt.Augustine L. Mrema.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabsia ninapendakumhakikishia Mheshimiwa Mrema kwamba tayari janatarehe 30 Mei, 2013 Mheshimiwa Jaji Mziray, ameishafikakatika Mahakama hiyo na tayari ameishaanza kusikiliza naana wiki mbili atakuwa ana vikao vya Mahakama kwa ajiliya kusikiliza kesi tatu. Inaweza ikaonekana ni kesi chache.Lakini ni kesi ambazo zina wadai wengi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo nimuombeMheshimiwa Dkt. Augustine Mrema, kwa sababu ndani siku14 tunatarajia kesi hiyo ya kwako ya wadai 700 itakuwaimeshatolewa hukumu. Lakini nikuombe uwaambie wadaihao 700 wajaribu kufika Mahakamani. Kwa sababu kesi hiyoinaendelea na kila siku ushahidi unatolewa. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Kwa kweli Mheshimiwa Naibu Waziritunakushukuru kwa jibu hilo.

MHE. FREEMAN A. MBOWE: Mheshimiwa Naibu Spika,ninakushukuru sana. Swali langu ni jepesi tu lakini ni la msingisana.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kwamba kumekuwa naucheweshaji mkubwa sana wa kesi, ambao pamoja namambo mengi unachangiwa na kushindwa, kufikishwa

Page 18: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

18

Mahakamani kwa Watuhumiwa. Nikitoa mfano waMahakama ya Wilaya ya Hai. Mahabusu ambao wako katikaMagereza ya Karanga, ambayo iko katika eneo la Manispaaya Moshi, hupelkwa katika kesi zao katika Wilaya ya Hai, maramoja kwa wiki. Kama kwa bahati yoyote ile mbaya au nzuriHakimu akawa hayupo au sababu nyingine yoyote, inamaana watasubiri wiki nyingine tena ya Alhamisi nyinginekupelekwa Mahakamani. Kwa hiyo, watu wanakaaMagerezani bila sababu za msingi.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninamwomba MheshimiwaWaziri kwa niaba ya Serikali, atuambie, kuna utaratibu ganiwa kumaliza tatizo hili, kwa sababu wako watu wengi ambaowanateseka kukaa sana Magerezani kwa sababu tu yakushindwa kufikishwa Mahamani. Kwa nini tunawaadhibuwatu kwa kesi ambazo hazistahili? (Mkofi)

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: MheshimwiaNaibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa FreemanMbowe, kama ifuatavyo:-

Kwanza kabisa jukumu la kusafirisha Mahabusu niJukumu la Jeshi la Polisi. Lakini kwa upande wa Mkoa waDar es Salaam, hivi sasa jukumu la kusaifirisha Mahabusu likochini ya Magereza. Wote tunatambua kwamba Polisiwamekuwa wakifanya kazi nzuri, lakini wanakbailiwa naukosefu wa mafuta. Lakini pia wanakbiliwa na uhaba waMagari.

Hivi sasa tayari Mheshimiwa Waziri wa Mambo yaNdani, anajitahidi kuzungumza na Wafadhili mbali mbali, lakinipia kupitia Wizara ya Fedha kuona ni kwa namna gani basiwanaweza wakongeza Idadi ya Magari na Mafuta kwa ajiliya kuongezea magari haya kuwasafirisha Mahabusu.

Lakini siyo hiyo tu, kupitia Mradi wa Programme waMaboresho wa Sekta ya Sheria tumekuwa tukinunua Mabasimbali mbali na tumekuwa tukiyasambaza katika mikoa mbalimbali. (Makofi)

Page 19: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

19

Na. 316

Kuboresha Huduma ya Maji Makambako

MHE. SELEMANI S. JAFO (K.n.y. MHE. DEO KASENYENDASANGA) aliuliza:-

Mji wa Makambako unakua kwa haraka na idadi yawatu zaidi ya 50,000 wakati miundombinu ya maji iliyopoinatosha kuhudumia watu 15,000 tu:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kuboresha hudumahii ya maji ili kuwasaidia wakazi wa Makambako?

NAIBU WAZIRI , OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZAMIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) (K.n.y. WAZIRI WAMAJI) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali laMheshimiwa Deo Kasenyenda Sanga, Mbunge wa NjombeKaskazini, kama ifuatavyo:-

Mheshimwia Naibu Spika, ninakubaliana naMheshimiwa Mbunge kuwa Mji wa Makambko unakua kwakasi na idadi ya Watu inaongezekana kila mwaka. Ongezekohilo la watu linasababisha kuongezeka kwa mahitaji ya majikwa wakazi wa mji huo. Ili kuboresha huduma ya maji kwenyemji huo, mwaka 2008/2009, Serikali ilitumia Shilingi milioni 90,kwa ajili ya kuchimba visima virefu viwili (2) pamoja nakukarabati mfumo wa usambazaji wa maji.

Pia Serikali kwa kushirikiana na Shirika la AmericanCultural Resources Assossosion (ACRA). Imechimba jumla yavisima vinne (4) na kati ya visima hivyo vilivyochimbwa visimavitatu (3) vilipata maji. Visima hivyo vina uwezo wa kutoajumla ya lita 614,400 kwa siku ambazo zitaongeza hudumaya maji kufikia asilimia 62. Hadi sasa, ujenzi wa miundombinuya maji umekamilika kwa asilia 90 na visima viwili (2) vimeanzakutoa maji.

Page 20: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

20

Aidha, katika kuendelea juhudi za kuboreshaupatikanaji wa maji katika mji wa Makambako, wa mwakawa fedha wa 2013/2014, Serikali imetenga jumla ya shilingimilioni 150 zitakazotumika kwa ajili ya upanuzi wa chanzo chamaji pamoja na kuboresha mfumo wa usambazaji maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mipango ya mudamrefu, mwezi Machi, 2012, Serikali imekamilisha kazi yaupembuzi yakinifu, usanifu wa kina pamoja na uandaji wamakabrasha ya zabunni. Serikali inandelea kutafuta fedhaili kuanza ujenzi huo.

MHE. SELEMANI S. JAFO: Mheshimiwa Naibu Spika,pamoja na majibu mazuri ya Naibu Waziri, natambua juhudikubwa zinazofanywa katika mji wa Makambako. Lakini kwaajili ya kutafuta tatizo hili na mpaka hivi sasa katika mweziSeptemba, mpaka mwezi Desemba, mara nyingi sana mjihuu unakuwa na shida na kadhia kubwa kwa wananchi wamji wa Makambako.

(a) Je, Serikali ina mpango gani kutengeneza kikosi kazi,kuhakikisha kwamba hii pesa iliyotengwa na hii Miradiinakamilika ili mradi kuondoa tatizo kubwa la watu wa mjiwa Makambako?

(b) Kwa kuwa mji wa Makambako sambamba na ulemji wa Kisarawe shida zao za maji. Na kwa kuwa Serikali,kwa nia ya dhati imeona kwamba ni vema kuhakikishamiundombinu kutoka Mipera na Kimbiji inasaidia kuletwakatika ji j i la Kisarawe. Lakini kwa kuwa mradi huuunawezekana ukachelewa sana kukamilika.

Je, Serikali ina mpango gani kuhakikisha kwambakisima kilichochimbwa pale katika eneo Vigama katika mjiwa Kisarawe, ambacho kimefunikwa sasa hivi kina mikamitatu. Kikaweka miundombinu, ili maji yale yakaingia katikamfumo wa maji kuwasaidia Wana-Kisarawe? (Makofi)

Page 21: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

21

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZAMIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) (K.n.y. WAZIRI WAMAJI): Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswalimawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Jafo, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, hili analolisema Mheshimiwani kweli. Pale Makambako inavyokuwa idadi ya watuwamefika 100,000. Idadi ya watu waliopo pale ni kubwa kwasababu ya biashara zinazofanyika kati ya Zambia na nchiyetu ya Tanzania.

Kwa hiyo ninakubaliana naye. Na capacity iliyopopale tank tunalopeleka pale, tunalotegemea litafanya kaziile. Tanki lile lina uwezo la lita 100,025. Kwa maneno menginekila mwananci aliyeopo pale ni kama anapata lita 1.2 na1.3. Kwa hiyo Mheshimiwa Jafo pale ana point kubwa,ninakubaliana na yeye.

Ukiangalia hesabu inaonyesha kwamba ili kukamilishampango mzima wa wananchi wote waliopo paleMakambako wapate maji safi na salama, unahitaji ShilingiBilioni 57.7. Sasa unaweza ukaelewa kwamba hili tatizo nikubwa. Lakini mimi niadhani tumeleza hapa mambo ambayotunayafanya. Vile visima vyote nil ivyovitaja hapatutahakikisha kwamba vinatoa maji safi na salama kwa ajiliya kuwasaidia wananchi.

Kwa hiyo, nilitaka nitoe hizi takwimu tu kuonyeshamagnitude ya problem iliyopo pale na population iliyoko paleMakambaku ni kubwa inakuwa kwa hiyo kuna jambo lamsingi linalosemwa hapa ambalo tutaendelea kufuatilia.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini hili ni pamoja na lilela Kisarawe alilolizungumziwa Mheshimiwa Jafo, tumewekakatika utaratibu kama mmemsikiliza vizuri Waziri wa Majialipokuwa anawasilisha hapa hotuba yake. Mamlaka zoteza Maji, na Mamlaka zote za miji, zote zilizopo katika nchi hii,zimewekewa utaratibu maalum na ni nchi nzima.

Page 22: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

22

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiki anachokisemaMheshimiwa Jafo kwa maana ya kile kisima kilichopo pale,tutakachofanya hapa ni kujaribu kwenda kuangalia vizurianachokisema ili niweze kupata, kwa sababu sikujuakwamba atauliza Swali la namna hiyo ili tuweze kusaidianana yeye.

Habari ya kuunda kikosi maalum kwa ajili ya maji, hiziMamlaka zote tunazozitaja hapa zina Mamlaka za Maji labdakitu ambacho tunakifanya hapa ni kuboresha tu hizoMamlaka za Maji zilizopo kule ili tuweze kusaidiana nakuhakikisha kwamba tunaondoa hili tatizo. (Makofi)

Na. 317

Tatizo la Maji Katika Mji wa Shirati

MHE. ESTHER M. MATIKO aliuliza:-

Mji wa Shirati ulikuwa na Mamlaka ya Maji chini yaKanisa la Menonite Tanzania (KMT) ambapo usambazaji wamaji haukuwa tatizo lakini mwaka 2004 KMT ilikabidhiwaMamlaka ya Maji Serikalini na tangu wakati huo kumekuwana kero kubwa sana ya maji.

(a) Je, kwa nini Serikali imeshindwa kutengenezamashine iliyoharibika ili kurejesha huduma ya maji kwawananchi?

(b) Je, gharama ya kutengeneza mashine hiyo nikiasi gani na kama ni kununua msahine nyingine itakuwakiasi gani cha fedha ambacho Serikali haiwezi kumudu tangumwaka 2004?

(c) Je, ni kwa nini Serikali inaendelea kuwalipamishahara wafanyakazi wa Mamlaka ya Maji wakatihawafanyi kazi yoyote?

Page 23: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

23

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI NKUU, TAWALA ZAMIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) (K.n.y. WAZIRI WAMAJI) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya MheshimiwaWaziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa EstherNicholas Matiko, Mbunge wa Viti Maalum, lenye sehemu(a), (b) na (c) kama ifuatavyo.

(a) Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kuwakulikuwepo na tatizo la upatikanaji wa maji kwa wakazi waMji wa Shirati kutokana na kuharibika kwa mashine. Ilikukabiliana na tatizo hilo, Serikali imenunua na kufungapampu tatu pamoja na mota mbili kwa ajili ya kuboreshahuduma ya maji kwa wakazi wa Shirati na hospitali za Shiratina Rao. Kazi hizo zimeboresha huduma ya maji katika eneola Shirati na katika hospitali hizo.

(b) Mheshimiwa Naibu Spika, mashine zilizokuwazikihudumia mji wa Shirati ziliharibika kutokana na kuunguakwa mota zake. Hata hivyo, ilibainika pia kuwa mashine hizozilikuwa na uwezo mdogo kukidhi mahitaji ya maji ya sasakwa wakazi wa Mji wa Shirati. Aidha, kama nilivyoeleza katikasehemu (a) hapo juu, ununuzi wa pampu mpya tatu, motampya mbili na kurudishia umeme uliokatwa uligharimu jumlaya shilingi milioni 500.

(c) Mheshimiwa Naibu Spika, huduma ya majikatika mji wa Shirati inasimamiwa na Jumuiya ya WatumiajiMaji Shirati (Shirati COWSO). Watumishi waliopo kwenyeJumuiya hiyo hufanya kazi kwa mkataba na hulipwa paleinapotokea kazi ya kufanya. Watumishi hao hufanya kazi zaulinzi wa nyumba ya mashine, uendeshaji mashine, ukusanyajimaduhuli na matengenezo madogomadogo yamiundombinu ya mradi huo.

Page 24: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

24

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Naibu Spika,nashukuru. Ingawaje kuna rekebisho kidogo kwani kwakaratasi niliyopewa gharama halisi wameniambia ni shilingimilioni 100 lakini Mheshimiwa Naibu Waziri ananiambia nishilingi milioni 500. Sasa sijui lipi ni sahihi.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na kwamba Serikaliilinunua na kuweka mota kwenye Hospitali ya Shirati lakinikwa taarifa zilizopo ni kwamba baada ya miezi mitatu tu ilemashine ilikufa ambayo ilikuwa ni ML 91, sasa inawezekanakabisa hii mashine ambayo Serikali imenunua na kufungailikuwa haina kiwango na tukizingatia umuhimu wa hospitalikwamba tunahitaji maji. Nataka Serikali inihakikishie vipiitaboresha huduma ya maji katika Hospitali ya Shirati kwakwenda kununua pampu ambayo ni imara na ambayo ita-sustain matumizi.

Pili, kwa kuwa, matatizo ya maji na hasa kwa Mkoawa Mara wanawake tumekuwa tukiteseka sana na kwamwaka huu tu tumeshuhudia mama mjamzito ameamkaalfajiri kwenda kutafuta Mto Mara akakamatwa na Mambaikabidi apate pre-labour. Nataka Serikali inihakikishie kwambaitawezaje sasa kutoa kipaumbele katika Majimbo yote yaMkoa wa Mara kuhakikisha kwamba tatizo la maji kwa akinamama ambao tunatembea kilomita nyingi na tunaamkausiku kitu ambacho kinapekea hata wengine kupata talakalinatatulika?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri majibu,nilimwona Mheshimiwa Wassira anaangalia kwa umakini!

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI NKUU, TAWALA ZAMIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) (K.n.y. WAZIRI WAMAJI)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waMaji, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza yaMheshimiwa Esther Nicholas Matiko, kama ifuatavyo:-

Page 25: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

25

Kwanza naomba aniwie radhi kwamba ni kwelikwamba nimepitiwa tu hapa, ni shilingi milioni 100 kamaunavyosema, ukikaa hapa ni kitimoto wakati mwingineinakuwa ni shida, lakini ni shilingi milioni 100 na hii karatasiniliyonayo hapa imeandikwa hivyohivyo naomba Hansardisahihishe kwani she is right na ni sahihi anavyosemaMheshimiwa Mbunge.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu pampu, hii habariya pampu anayoisema hapa nilijua itaulizwa, kwa hiyo,nimeuliza Shirati karibu mara kumi wakaniambia pampu zamwanzo ni kweli zilikuwa na mushkeli na ndizo zilizoharibika.Hizi pampu tunazozigumza sasa ni pampu mpya. Miminasema kabisa kwamba hapa tunachozungumza sasa kamaMheshimiwa Matiko anakuwa Tomaso kwamba ana wasiwasina hizo sasa tusubiri tuzione kama zitaleta matatizo tutakujakueleza. lakini sasa nisemeje?

Niseme tunazing’oe tena na zile ambazo zimeletwampya pale au ambazo tumeweka mpya na zile mota?Ninachosema hapa ni kwamba tumecheki tumerudia natume-cross check na asubuhi hii tume-cross check tena naShirati ili kuhakikisha kwa sababu nilijua hili swali litakuja hapa.Kwa hiyo, mimi I stand to be corrected anaweza akaja ofisinitukacheki vizuri aipate from the horses mouth ili tuweze kuwavizuri. Nilijua hilo litakuja.

La pili, kuhusu Mama anayesema hapa ni jambo lakusikitisha kwamba Mama sasa kwa sababu ya matatizo yamaji yaliyopo pale amekwenda kule ameparamiwa nawanyama na kadhalika, hili ni jambo ambalo kama Taifatumelipokea na Serikali linatusikitisha kwamba linatokana natatizo la maji lililopo vijiji vyetu na unaona kwamba amepatamatatizo hayo na kwamba mbele kule inaweza ikasababishana talaka na kadhalika. Wanawake wakaachika kwasababu ya tatizo hilo la maji. Ni kweli inaweza ikatokea hivyokwa sababu Mama akienda kwenye maji huwezikupambanua kwamba ni maji tu au kuna mambo mengineyanayoendelea kule na kadhalika. Inaweza kuwa ni tatizo.(Makofi)

Page 26: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

26

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kifupi sisi tuseme hivi,hii Shirati inayosemwa hapa ungeweza ukaondokana natatizo lake kama ingekuwa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Shiratiyaani ungekuwa na mamlaka ungekuwa na authority, ndiyomaana hapa tunazungumza Association, na Associationinaanzishwa wakati unapokuwa na vikundi viwili vinaanzishwapale ndiyo inaanzishwa pale. Kwa hiyo, utaona kwamba hataukienda ule mpango wa maji ili kuona kama mradi wa majikatika huu mji wa Shirati upo unakuta kwamba haipo.

Sisi tutamshauri Mheshimiwa Waziri wa Maji kuonakwamba Shirati iangaliwe kwa jicho tofauti. Mimi nimefikaShirati na hao Kanisa la Menonite ambao wanatusaidiatunawashukuru sana kwa kazi nzuri ambayo wanaifanya pale.Tutakwenda kumshauri Waziri kwa sababu mpango uliopo niwa miji midogo ndio ulipo pale, sasa Shirati kwa sababu siyomamlaka ya Mji mdogo na hili nitoe changamoto piakwamba tuliwahi kuwashauri mwanzishe Mamlaka ya Mjimdogo pale ili muweze kupata huduma kwa mujibu wa hichokitu tunachokizungumza hapa. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Naibu Waziri,na mimi nikubaliane na wewe kwamba sababu za talakazipo nyingi.

Wizara ya Maliasili na Utalii, swali la Mheshimiwa KaikaSaning’o Telele!

Na. 318

Matumizi ya Nyuki Wadogo kwa Asali

MHE. KAIKA SANING’O TELELE aliuliza:-

Je, ni kwa nini watumiaji wengi wa Asali wanapendazaidi kutumia Asali ya Nyuki wadogo kwa matumizi yao?

Page 27: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

27

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waMaliasili na Utalii, naomba kujibu swali la Mheshimiwa KaikaSaning’o Telele, Mbunge wa Ngorongoro, kama ifuatavyo:-

Asali ya Nyuki wadogo hupendwa na watu wengikutokana na uwezo wake wa kutibu magonjwa mbalimbaliya wanadamu. Uwezo wa kutibu magonjwa mengiunasababishwa na Nyuki hawa wadogo kutembelea mimeamingi zaidi wakati wa kutengeneza Asali kuliko Nyukiwakubwa. Utafiti kutoka nchi za Amerika ya Kusini unaoneshaNyuki wadogo wanatembelea mimea yenye maua(Foraging) mara mbili zaidi ya idadi ya mimeainayotembelewa na Nyuki wakubwa. Kwa kuwa, dawa nyingizinatokana na mimea, Asali ya Nyuki wadogo ina uwezo wakimatibabu zaidi ya (Medicinal Value) kuliko ile ya Nyukiwakubwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, sababu nyingine inatokanana ladha na riha ya ukakasi au ugwadu ambao haikinaishi.Hapa nchini Tanzania utafiti kuhusu Nyuki wadogo na Asaliyake bado uko katika hatua za awali. Kwa hiyo, Wizara hainatakwimu sahihi ni magonjwa aina gani yanatibiwa na Asaliya Nyuki wadogo kuliko ile ya nyuki wakubwa. Utafitiuliofanyika katika nchi za Guatemala, Mexico na Venezuelaunaonyesha kuwa Asali ya Nyuki wadogo inasaidia akinaMama waliojifungua kupona upesi (post birth recovery),maradhi ya mfumo wa chakula, mfumo wa hewa, kuimarishamfumo wa uzazi kwa akina Mama (female fertilite), kutibumaradhi ya ngozi na kusaidia macho kuona vizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, Asali ya Nyuki wadogo(wasiouma) haipatikani kwa wingi ikilinganishwa na nyukiwakubwa (wanaouma), hii ni kutokana na maumbile yaokuwa madogo ambapo uzalishaji wao ni lita moja hadi tanokwa kundi la Nyuki. Wakati Nyuki wanaouma uzalishaji waoni lita tano hadi ishirini kwa kundi. Nichukue fursa hiikuwaomba wananchi watumie Asali za Nyuki wote kwa kuwaviini lishe na viini tiba katika Asali hizo ni sawa.

Page 28: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

28

Pia niwaombe wafuge Nyuki wasiouma karibu namakazi yao endapo hakuna shughuli zinazotumia viatilifu.(Makofi)

MHE. KAIKA SANING’O TELELE: Mheshimiwa NaibuSpika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ili niulize swali moja lanyongeza.

Kwa kuwa, maelezo ya Serikali yamekiri kwamba Asaliya Nyuki wadogo ina uwezo zaidi wa kimatatibabu kuliko kitukingine chochote. Je, kwa nini utafiti huu usiende sambambana ule wa mti wa Mrigariga uliotumiwa na Babu wa LoliondoMchungaji Ambilikile Mwaisapile, kwa nini utafiti huu usiendesambamba ili kubaini magonjwa ambayo Asali ya Nyukiwadogo wanaweza kutibu kwa binadamu?

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaNaibu Spika, naomba nijibu swali la nyongeza la MheshimiwaKaika Telele, kama ifuatavyo:-

Kwanza, nimhakikishie tena Mheshimiwa Telele nanilihakikishie Bunge lako Tukufu kwamba utafiti wa faidazinazopatikana kimatibabu na kilishe za Nyuki wadogo hapanchini zinaendelea na utafiti wa jumla katika tasnia ya Nyukiunaendelea. Pili, Serikali katika hatua mbalimbali imeendeleakuangalia na kufanya kufanya utafiti wa mti wa Mrigarigakwa sababu wote tunafahamu shughuli ambayo alikuwaanaifanya Babu wa Loliondo ilihamasisha watu wengi nchinina katika Bara la Afrika na tuliambiwa hata nje ya Afrika watuwamekwenda Loliondo na tunaamini kwamba tafiti hizozitakapokuwa zimekamilika hatutasita kuleta majibu hapaBungeni.

MHE. DIANA M. CHILOLO: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante. Kwa kuwa, siku ya uzinduzi wa ufugaji Nyuki kitaifaulifanyika Mkoani Singida Wilayani Manyoni na MheshimiwaWaziri Mkuu na akawaahidi wanawake wajasiriamali Singidakwamba atawapa mizinga 120 na mizinga 100 kwa kilaWilaya baada ya kuona juhudi za Mkoa wa Singida kwakutundika mizinga.

Page 29: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

29

Je, ni lini hiyo mizinga itafika Singida?

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaNaibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza laMheshimiwa Diana Mkumbo Chilolo, kama ifuatavyo:-

Ni kweli Mheshimiwa Waziri Mkuu alifika Singida katikauzinduzi wa siku ya ufugaji wa Nyuki hapa nchini naMheshimiwa Waziri Mkuu aliahidi mizinga hiyo 120 kwa ajiliya akina Mama na mizinga 100 kwa kila wilaya nanimhakikishie Mheshimiwa Chilolo kwamba ahadi hiyo yaMheshimiwa Waziri Mkuu inatekelezwa na Wizara ya Maliasilina Utali i na tunajiandaa na tutaitekeleza mapemaiwezekanavyo.

Na. 319

Kiwanda cha Kusindika Nyama – Mbeya

MHE. ALIKO N. KIBONA (K.n.y. MHE. MCH. LUCKSON N.MWANJALE) aliuliza:-

Mheshimiwa Waziri Mkuu atalipotembelea Kiwandacha Kusindika Nyama Mbeya aliuagiza Uongozi wa Kiwandahicho kwamba kama kiwanda bdo hakijapata mwekezajibasi kiwekwe katika mpango wa haraka wa kukifufua.

(a) Je, kiwanda kimeishapata mwekezaji?

(b) Kama bado hakijapata mwekezaji, je, ni liniSerikali itakifufua kiwanda hicho?

NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVIalijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waMaendeleo ya Mifugo na Uvuvi, napenda kujibu swali laMheshimiwa Mchungaji Luckson Ndaga Mwanjale Mbungewa Mbeya Vijijini lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-

Page 30: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

30

(a) Mheshimiwa Naibu Spika, Ujenzi wa Kiwandacha Nyama cha Mbeya ambao ulianza mwaka 1975,ulisimama mwaka 1978 kutokana na ukosefu wa fedha.Kutokana na mabadiliko ya kisera yaliyoelekeza kuwashughuli nyingi za kiuchumi zifanywe na sekta binafsi, mnamomwaka wa 2008 PSRC ilianza kutafuta mwekezaji makiniatakayekiendeleza, juhudi ambazo hazikuzaa matunda.

Mnamo mwezi Machi mwaka 2013, Shirika laConsolidated Holdings Cooperation (CHC) lilitoa tangazo lakutafuta mwekezaji kwenye magazeti. Kufuatia matangazohaya, hadi tarehe 24/4/2013 iliyokuwa siku ya mwisho yakupokea maombi, makampuni matatu ya Jovet TanzaniaLimited, Tanfroz Tanzania Limited na Tandam Farms yalikuwayamejitokeza na kamati ya wataalam imeanza kuyafanyiatathmini na mapendekezo yake yatapelekwa kwenye Bodiya CHC kwa maamuzi.

(b) Mheshimiwa Naibu Spika, namshauriMheshimiwa Mbunge kuvuta subura hadi hapo uamuziutkapotolewa. Aidha, napenda kumjulisha kuwa, iwapo CHChaitampata mwekezaji makini anayekidhi vigezo vilivywekwaWizara itatekeleza agizo la Mheshimiwa Waziri Mkuu la kufufuakiwanda hiki kwa kukiombea fedha kwenye Bajeti ijayo.

MHE. ALIKO N. KIBONA: Mheshimiwa Naibu Spika,nashukuru kwa kupata nafasi ili niweze kuuliza maswali mawiliya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, sote tunafahamu kwambawakulima wa Chai wa viwanda, Miwa wana viwanda,Kahawa wana viwanda, Pamba wana viwanda, Nyuki wanaviwanda, Zabibu wana viwanda na kadhalika. Kwa nini nani sababu gani zimesababisha taifa letu lenye mifugo mingiya kutosha mpaka sasa hivi tukose kiwanda cha Nyamaambacho kingewaongezea wakulima wetu thamani yamifugo yao?

Page 31: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

31

Mheshimiwa Naibu Spika, pili, majosho ya mifugo vijijinimengi yamekufa, operation ya chanjo kamatulivyozishuhudia siku za nyuma hazipo tena, MabwanaMifugo wengi wanaishi mijini, inaonyesha kabisa kwambahatuko makini na sekta hii ya mifugo. Ni nini sasa au ni liniSerikali itaweza kurekebisha jambo hili?

NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI:Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawilimawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Aliko Nikusuma Kibona,kama ifuatavyo:-

Nakubaliana na Mheshimiwa Mbunge kwambamazao mengi yana viwanda lakini Serikali ina mikakatiambayo tumeianza ya kufufua viwanda vilivyokuwepozamani na kujenga vipya na kwa taarifa tu ya MheshimiwaMbunge katika ukanda huo wa Kusini tayari kiwanda chanyama kimejengwa Iringa kilichogharimu jumla ya shilingimilioni 596 na hii imefanywa Serikali imechangia mfuko waASDP na UNIDO imechangia. Baada ya kiwanda hiki kuanzakazi mwezi Desemba kingine kitajengwa Mbeya kwa mtindohuohuo wa kuchangiwa na mifugo hiyo niliyoitaja ambayoimechangia machinjio ya Iringa.

Mheshimiwa Naibu Spika, pili, ni kweli miundombinumingi inahitajika na hasa ya maji na majosho na katikamkakati na mpango wa kuendeleza sekta ya mifugo,mapendekezo yapo na tutakapoleta Bajeti yetu leotunaomba mtuunge mkono ili angalau harakati hizi zakujenga miundombinu kwa ajili ya mifugo iweze kuanza.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la chanjo mwaka janatulipitisha sheria iliyobadilisha maabara kuu ya mifugo kuwawakala na kwa sasa wakala wana uwezo wa kutengenezachanjo kadhaa zikiwemo ya SBPP, Foot and Mouth namdondo kwa wafugaji wa kuku.

Page 32: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

32

Kwa hiyo, kwa hili la chanzo tuna uwezo sasakutengeneza lakini tunahitaji kuwezeshwa zaidi kifedha ilijitihada hizi ziweze kuwanufaisha wafugaji wetu kokote walikowaliko katika nchi yetu.

Na. 320

Ahadi ya Njia Mbili Kutoka Morocco – Kawe

MHE. RITA LOUISE MLAKI aliuliza:-

Tatizo la mafuriko na uharibikaji wa barabara ya OldBagamoyo eneo la TMJ Hospital na Mayfair limekuwa kubwana baya kwa muda mrefu kiasi cha kusababishamsongamano mkubwa wa magari na ajali wakati mwingine.

(a) Je, Serikali ina mpango gani wa kutatua tatizohilo?

(b) Je, ni lini Serikali itatekeleza ahadi yake yakuijenga barabara hiyo toka Morocco hadi njia Panda yaKawe, kwa kiwango cha njia mbili?

NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-

Kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi naomba kujibu swalila Meheshimiwa Rita Louse Mlaki, Mbunge wa Viti Maalum,lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Naibu Spika, tatizo la mafuriko nauharibifu wa barabara ya Old Bagamoyo eneo la TMJHospital husababishwa na kutozingatiwa kwa Kanuni Kanuniza ujenzi wa majengo katika eneo husika ikiwa ni pamojakujenga kuta za majengo, kuziba mifereji, kutupa takatakakatika mifereji inayopitisha maji na kadhalika. Hata hivo, ilikutatua tatizo la mafuriko katika barabara ya Old Bagamoyoeneo la TMJ Hospital na Mayfair linalojulikana kama Bondela Mpunga, Wizara kupitia TANROADS tayari usanifu wa kinawa mfumo wa maji ya mvua (storm Water Drainage System)umefanyika na kukamilika.

Page 33: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

33

Kazi ya ujenzi wa mfumo wa maji ya mvua katika eneola Bonde la Mpunga inatarajiwa kuanza na kukamilika katikamwaka wa fedha 2013/2014. Kwa sasa Mhandisi Mshaurianakamilisha makabrasha ya kuitisha zabuni.

(b) Mheshimiwa Naibu Spika, ahadi ya kujengabarabara kutoka Morocco hadi njia panda ya Kawe kuwanjia nne (4 lane dual carriageway) imeanza kwa kukamilishausanifu. Serikali inatafuta fedha ili ujenzi uweze kuanzamapema iwezekanavyo.

MHE. RITA LOUISE MLAKI: Mheshimiwa Naibu Spika,nashukuru sana kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa NaibuWaziri ambayo yanatupa matumaini wananchi wa Kata yaMikocheni, hususan Bonde la Mpunga katika jimbo la Kawe.Ningependa kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Swali la kwanza, kwa kuwa, katika juhudi za kujinusuruna mafuriko haya wananchi wanaoishi katika Kata yaMikocheni hususan eneo la Bonde la Mpunga na lililoponyuma ya Engene Petrol Station, wamejenga kuta holela ilikujinusuru kila mtu na nyumba yake, kwa maana hiyo hatatutakapojenga mifereji mikubwa bado kuna watuwataathirika na mafuriko ya wenyewe kwa wenyewe.

Je, Serikali itakuwa tayari kuniunganisha mimi na haowahandisi watakaoshughulikia mradi huo ili tuweze kupataushauri na maelezo ya kuwasaidia wananachi hawa?

Swali la pili, kwa kuwa, barabara ya kuanzia Moroccohadi Kawe ambayo imeishafanyiwa usanifu lakini badohaijatengewa fedha itachukua muda mrefu kabla yakujengwa, sasa foleni imehama au kupugua katika barabaraya Ali Hassan mwingi na sasa imeongezeka barabara ya chiniya Afrikana mpaka Morocco.

Je, Serikali itakuwa na mpango gani wa kutupatiamsaada wa dharura ikizingatia hali halisi ya foleni?.

Page 34: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

34

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika,kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mlaki kwa shukuraniambazo ametoa kwa Serikali. Pili niseme tu kwamba, masualaya kujenga kuta kiholela, Manispaa ya Kinondoni inabidiichukue hatua. Hili ndilo tatizo kubwa ambalo tunalipatakwenye barabara ile. Watu wanajenga zile kuta na hawawekimatoleo ambapo maji yanaweza kupita, hivyo mvuazikinyesha barabara nzima inakumbwa na mafuriko. Naombanitoe agizo kwa Manispaa ya Kinonondoni kuchukua hatuana kuwaelekeza hawa wenye nyumba ambao wamejengabila mpangilio, waweze kubomoa kuta zile ili maji yawezekupita kwa kufuata mkondo wake.

Kuhusu sehemu ya pili ya swali lake juu ya mpangowa dharura, nafikiri ili kupunguza msongamano ni lazimabarabara ile ijengwe kwa njia 4 kama nilivyosema kwenyejibu la msingi. Hata hivyo, tutaendelea kuitengenezabarabara ile iweze kutumika kwa kutumia fedha za mfukowa barabara. (Makofi)

Na. 321

Utoaji wa Mikopo ya Elimu ya Juu

MHE. ASHA MUHAMED OMAR aliuliza-

Je, kwa nini utaratibu wa utoaji wa Mikopo ya Elimuya Juu na Vyuo Vikuu usirudishwe kuwa kama wa zamanikwa Zanzibar kupewa nafasi zake kwa idadi maalum ilikuepusha vitendo vya upendeleo?

WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI:Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali laMheshimiwa Asha Muhamed Omar, Mbunge wa Viti Maalum,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kulitaarifu Bungelako Tukufu kwamba, tangu Serikali ilipoanza kutoa mikopokwa wanafunzi wa Elimu ya Juu mwaka 1994 hatujawahikuwa na utaratibu wa Tanzania Zanzibar kupewa nafasi zakekwa idadi maalum ya wanafunzi. Kuanzia wakati huo mikopo

Page 35: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

35

ilitolewa na iliyokuwa Wizara ya Sayansi, Teknolojia na Elimuya Juu, hadi ilipoanzishwa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi waElimu ya Juu mwaka 2004. Sheria ilyounda Bodi ya Mikopo yaWanafunzi wa ELimu ya Juu, imeelekeza mikopo kutolewakwa mtanzania yeyote mhitaji aliyepata udahili katika chuocha elimu ya juu chenye ithibati na mwenye kutimiza vigezovilivyowekwa bila kujali anatoka sehemu gani ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania, kabila lake, dini yake au itikadi yakeya kisiasa.

Mheshimiwa Naibu Spika, utaratibu wa utoaji mikopokwa wanafunzi wa elimu ya juu, huzingatia taratibu za kisheria,miongozo mbalimbali na vigezo ambavyo hutolewa kilamwaka bila kuwa na vitendo vya upendeleo. Vigezohuangalia zaidi uhitaji wa mwombaji, vipaumbele vya taifa,ukomo wa Bajeti ya Serikali pamoja na sifa za kitaaluma zamwombaji wa mkopo.

MHE. ASHA MUHAMED OMAR: Mheshimiwa NaibuSpika, nashukuru. Nakubaliana na majibu ya MheshimiwaWaziri, lakini kwa upande wa Zanzibar huwa ni kazi ngumukwa mwanafunzi mwenye sifa hizo kupata mikopo.

Je, ni kwanini sasa kusiwe na idadi maalum yawanafunzi wanaotoka Zanzibar ili kuondokana na usumbufuunajiotokeza?

WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI:Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyojibu katika swali lamsingi ni kwamba, mwongozo wa utoaji wa mikopounaangalia hasa uhitaji wa mwombaji. Je, huyu mwombajiana uhitaji?

Hilo ndilo kubwa zaidi na haliangalii anatoka upandegani katika nchi yetu. Vijana wa Zanzibar kama vile vijanawa Tanzania Bara wamekuwa na nafasi sawa ya kupatamikopo. Kila mwaka vijana wa Zanzibar wengi zaidi walikuwawanapata mikopo kufuatana na mahitaji yao.Watatofautiana chuo na chuo, mwaka fulani wanapatawanafunzi wengi zaidi, mwaka mwingine wanapata

Page 36: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

36

wanafunzi wengi zaidi wenye mikopo. Hata hivyo, kilamwaka idadi hiyo imekuwa ikiongezeka kama ambavyoidadi ya jumla ya wanafunzi wanaopata mikopoimeongezeka sana. Tangu ilipoanza mwaka 1994 ambapowanafunzi 6061 walipata mikopo, mpaka mwaka huu wamasomo ambapo ni wanafunzi elfu 98 na ushee ambaowamepata mikopo.

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Waheshimiwa Wabungekwa sababu ya muda kama mnavyoona naomba tuchukueswali la mwisho la Mheshimiwa Maria Ibeshi Hewa.

Na. 322

Vyuo vya Walimu wa Shule za Awali

MHE. MARIA I. HEWA aliuliza:-

Je, Serikali inajua idadi ya vyuo vilivyosajiliwakufundisha Walimu wa Elimu ya Awali (Chekechea) tu hapanchini na ni vingapi vya Serikali na ni vingapi ni vya watubinafsi?

WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali laMheshimiwa Maria Ibeshi Hewa, Mbunge wa Viti Maalum,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibu wa Sera ya Elimuna Mafunzo ya mwaka 1995, Elimu ya Awali ni elimuinayotolewa kwa watoto wenye umri wa miaka 5 hadi 6ambao wanaandaliwa kuingia Elimu ya Msingi (Darasa lakwanza). Elimu ya Chekechea (Nursery) ni elimu ya maleziinayotolewa kwa watoto wenye umri wa kati ya miaka 3 na4 chini ya Idara ya Ustawi wa Jamii.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara ya ELimu na Mafunzoya Ufundi, ndiyo yenye jukumu la kusajili shule za Awali, Msingina Sekondari na pia Vyuo vya Ualimu. Kutokana na Mtaala

Page 37: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

37

wa Mafunzo ya Ualimu Ngazi ya Cheti wa mwaka 2009,mafunzo ya Uallimu wa Elimu ya Awali ni mchepuommojawapo katika Mafunzo ya Ualimu Ngazi ya Cheti(Daraja A). Michepuo mingine ni Cheti cha Elimu ya Michezona Cheti cha Elimu ya Kawaida. Kwa mantiki hiyo sifa zakujiunga na mafunzo ya Ualimu wa Elimu ya Awali ni sawa nasifa za kujiunga katika mafunzo ya Cheti Michezo na ChetiKawaida.

Mheshimiwa Naibu Spika, kila chuo cha ualimukilichosajiliwa kutoa mafunzo ya ualimu ngazi ya Cheti nangazi ya Stashahada, kinaweza kutoa mafunzo ya Ualimuwa Elimu ya Awali kutegemeana na uwepo wa wakufunziwa Elimu ya Awali. Kwa sasa vyuo vya Ualimu vya Serikalivinavyoweza kutoa mafunzo ya ualimu wa Elimu ya AwaliNgazi ya Cheti ni 34 na visivyokuwa vya Serikali ni 89.

MHE. MARIA I. HEWA: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante. Niulize maswali mawili mafupi tu.

Swali la kwanza, kwa kuwa, hapa nchini tatizo kubwaambalo linajitokeza mara kwa mara ni kwa wanafunzi waDarasa la I – VII kumaliza shule bila kujua kusoma, kuandikana kuhesabu, ambapo nadhani ni kutokana na kukosa hayamadarasa ya awali.

Je, Waziri haoni kuwa sasa ni wakati mwafaka kwakila shule ya msingi kuwa na madarasa haya ya awali kwasababu Walimu wengi ambao wamefuzu madarasa hayowamo mitaani?

Swali la pili, katika jibu la msingi la Mheshimiwa Waziriamesema kuna idadi ya vyuo 123 (34 + 89). Kwa swalilangu ambalo linasema hapa kwamba, walimu wengiambao wamefuzu elimu hiyo ya kufundisha madarasa ya waliwamo mitaani. Je, Waziri anaweza akatamka sasa kwamba,walimu hao ninaosema wako mitaani huko wakiwa hawanashule za kufundisha, wajitokeze na kwa tamko lake wamuonenani ili shule hizi ziweze kupata walimu wa madarasa yaawali? Ahsante. (Makofi)

Page 38: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

38

WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI:Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza ni kuhusu hitaji lakuwa na darasa la elimu ya awali katika kila shule ya Msingi.Hiyo ndiyo sera yetu kwa sasa na ndiyo ahadi ya Chamacha Mapinduzi na tunaenda nayo kwa kasi sana.

Hivi karibuni tumemaliza zoezi maalum ambalolimeangalia namna ambavyo tunaweza tukaboresha elimuya msingi kwa kusisitizia elimu ya awali na elimu ya msingikatika ngazi za chini kwa maana ya darasa la I na II.

Kwa hiyo, tutaelekeza fedha na nguvu zetu zote katikaeneo hili ili tuweze kutekeleza kile ambacho Chama ChaMapinduzi kimeahidi katika Ilani yake.

Swali la pili, kuhusu walimu wa elimu ya awali. Kwanzanasikitika kama kuna walimu hao wako huko kwa sababutunawahitaji sana na tunaendelea kufungua nafasi nyingizaidi katika shule zetu kwa madarasa ya elimu ya awali.

Sekta binafsi pia imetuunga mkono kwa mazingirawezeshi ambayo tumeyaweka. Wao nao wamefunguamadarasa mengi sana katika shule zao za elimu ya awali.Tunawahitaji sana walimu hao wa elimu ya awali. Waandikebarua zao kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu na Mafunzo yaUfundi, nafasi hizo tunazo tutawapatia.

Wale walimu wa Chekechea siyo walimu wa Elimuya Awali na dhamana ya mafunzo ya Elimu ya Chekechea,Sheria Na. 21 ya Mtoto imetoa mamlaka ya mafunzo yachekechea kwa Kamishina wa Ustawi wa Jamii ambayeanasajili pia vyuo vya Ualimu wa Elimu ya Chekechea na Vituovya Chekechea.

Page 39: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

39

Kama wako walimu hao vituo viko vingi, jumla 670nchi nzima. Vyuo vya Elimu ya Awali navyo viko vingi, viko 17kimoja kikiwa cha Serikali. Tunawahitaji walimu hawawajitokeze mapema iwezekanavyo. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge maswaliyameisha na muda kwa kweli haupo upande wetu kabisa.Kwa haraka haraka naomba niwatambulishe wagenitulionao katika Ukumbi wa Bunge.

Tunaye Balozi wa India hapa nchini, Shri DebnathShaw, Indian Ambassador to Tanzania, karibu sana. Yupo piaAfisa kutoka Ubalozi wa India, Ndugu, G.K Pant, karibu sana.

Ninao wageni wangu maalum kutoka Kongwaambao ni machifu, wamekuja kutembelea hapa na kuletasalamu kwa niaba ya wenzao. Mzee Tumaini Ndumula, MzeeNgeke Nyamwanji na Mzee Jackson Sekwao. Karibuni sanawazee wangu, muwaambie Kongwa kijana wenu nikosalama. Ahsanteni sana, kaeni. (Makofi)

Pia nina wageni 22 kutoka Dayosisi ya CentralTanganyika kutoka kule District Designated Hospital ya Mvumipamoja na Diocese of Central Tanganyika, Makey HouseDodoma. Pale mlipo wale wageni 22 naomba msimame.Wako pale karibuni sana. Wanajishughulisha sana na masualaya afya na hasa matatizo ya macho kwa nchi nzima. Karibunisana leo mjifunze masuala ya Bunge. (Makofi)

Kwa ajili ya mafunzo kuna wanafunzi wa Vyuo vyaUDOM na Saint John, pale mlipo karibuni sana. Hivi ni vyuovikuu vilivyo po hapa mjini Dodoma na vyenye sifa kubwasana hapa nchini. Tunakaribisha vijana wetu mjifunze masualaya Bunge.

Page 40: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

40

Wanafunzi na walimu kutoka shule ya Sekondari yaChilonwa kule kwa Mzee Chibulunje. Ahsante sana, Walimuna wanafunzi wote kutoka kule Chilonwa. Naona MzeeChibulunje amefanikiwa kuleta mpaka na walimu kutoka njeya nchi. Karibuni sana na ahsanteni sana Wanafunzi naWalimu kutoka Chilonwa. (Makofi)

Wanafunzi kutoka Chuo cha Uandishi wa Habari chaDar es Salaam City College, pale mlipo. Ahsanteni sana hapomlipo. (Makofi)

Pia tuna madaktari wetu na timu nzima ya wauguzina kadhalika waliokuja kwa ajili ya kufanya vipimo mbalimbalina kuwashughulikia Waheshimiwa Wabunge kwa umahirimkubwa sana. Madaktari pale mlipo, karibuni sana.Waheshimiwa Wabunge wanashukuru sana kwa hudumaambayo mmeitoa kwa wiki nzima, wanaomba wakatimwingine mkipata nafasi mtutembelee tena hapa Dodoma.Karibuni sana. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, nawashukuruni sana kwamakofi hayo.

Mwenyekiti wa Bunge Sports Club, Mheshimiwa IddiAzan anaomba niwatangazie Waheshimiwa Wabungekwamba, kesho tarehe 1 Juni, 2013 kwenye Uwanja waJamhuri, kutakuwa na michezo ya mpira wa miguu na petena combine ya NSSF.

Kwa hiyo itakuwa NSSF na Bunge kwa maana yafootball na netball. Michezo hiyo itaanza Saa Kumi jioni naitaoneshwa live na Kituo cha Televisheni cha Star TV.

Page 41: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

40

Mpira wa kesho ni l ive, utaonyeshwa na Star TV,mnakaribishwa wote kushangilia timu yetu ya Bunge. Kwataarifa yenu Waheshimiwa Wabunge Kamati ya Ufundi chiniya Profesa Majimarefu imeshamaliza kazi yake. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Peter Serukamba, Mwenyekiti wa Kamatiya Bunge ya Miundombinu anaomba niwatangazie Wajumbewa Kamati hiyo wakutane saa 7.00, ukumbi Na. 227.

Katibu Msaidizi wa Wabunge Wanawake wa CCMBungeni, Mheshimiwa Kisangi anaomba leo tarehe 31 saasaba mchana pawe na kikao cha Wabunge wotewanawake wa CCM katika ukumbi wa Pius Msekwa,mnaombwa kuhudhuria. Narudia tena akinamama woteWabunge wa CCM mnaombwa saa saba ukumbi waMsekwa.

Pia naomba niwatangazie watendaji wa Wizara yaMaendeleo ya Mifugo na Uvuvi pale mlipo naombamsimame. Ahsante sana Katibu Mkuu, Wakurugenzi wotekaribuni sana tunawatakia kila la kheri kwenye shughuli yenuya leo hapo baadaye. (Makofi)

Pia kwa kumalizia naomba niendelee na masuala yautaratibu. Waheshimiwa Wabunge mnakumbuka jinsi sikuya jana ilivyokuwa haikwenda vizuri na wakati naahirishaBunge niliomba Kamati ya Maadili waende wakutane iliwatushauri namna gani tunaweza tukatoka pale tulipokuwatumekwama jana. Kwa hiyo, kwa fursa hii ninamwombaMheshimiwa Chiligati ambaye ni Makamu Mwenyekiti waKamati hiyo lakini aliyekuwa anaongoza kikao hicho janaalitaarifu Bunge nini kimejiri na ushauri wao kwetu ni jambogani.

Mheshimiwa Chilligati, kwa heshima nakuombatafadhali.

Page 42: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

41

MHE. JOHN Z. CHILLIGATI (MAKAMU MWENYEKITI WAKAMATI YA HAKI, MAADILI NA MADARAKA YA BUNGE):Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Kamati ya Haki,Maadili na Madaraka ya Bunge, napenda kuwasilisha taarifaya kikao cha jana ambacho kilihusu malalamiko yaMheshimiwa Masoud Abdallah Salim dhidi ya sehemu yataarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani MheshiwaWenje kuhusu bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikianowa Kimataifa.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kuahirisha kikaocha jana jioni, uliitaka Kamati yetu ikae na iendeleekushughulikia suala hili. Kamati ilikaa na tuliamua tushirikishemarafiki wa Kamati kutoka vyama ambavyo vilikuwavinahasimiana. Kwa hiyo, tulimwalika Mheshimiwa Mboweakiwa Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani kama rafiki waKamati. Vilevile tulimwalika Mheshimiwa Hamad Mbaroukambaye ni Kaimu Mwenyekiti wa Caucus ya CUF humu ndaniya Bunge. Vilevile tulimwalika Mheshimiwa Mary Naguambaye ni Kaimu Mnadhimu wa upande wa Serikali. Kwahiyo, kwa hivi vyama, CHADEMA tulikuwa na MheshimiwaMbowe na Mheshimiwa Arfi ambaye ni Makamu Mwenyekitiwa CHADEMA, lakini pia ni Mjumbe wa Kamati. Kwamadhumuni ya shauri hili tulimruhusu awe upande waCHADEMA. Vilevile tulikuwa na Mheshimiwa Rashid Abdallah,yeye ndiye Mnadhimu wa Wabunge wa CUF ndani ya Bunge,ni Mjumbe wetu lakini naye kwa madhumuni wa suala hilitulisema awe upande wa CUF.

Mheshimiwa Naibu Spika, tuliwapa notisi fupi lakiniwote walifika kwa muda mfupi kuonyesha kwamba nawenyewe jambo hili walilitilia maanani. Mazungumzo yetuyaliongozwa, kwanza tulisema hapa tutangulize maslahi yanchi badala ya vyama vyetu. Vilevile tuzingatie suala lakurejesha mshikamano na upendo ndani ya Bunge kwasababu katika zogo hili maneno yasiyofaa yalirushwarushwakila upande, kwa hiyo tulikuwa na jukumu la kurejesha amanina upendo na mshikamano ndani ya Bunge. Vileviletulizingatia suala la kukwamua bajeti ya Wizara hii ya Mambo

Page 43: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

42

ya Nje ambayo ni dhahiri kwamba ilikuwa imekwama sikuya jana. Haya ndiyo yaliyotuongoza.

Mheshimiwa Naibu Spika, mjadala ulivyoendelea,upande wa CHADEMA ukiongozwa na Mheshimiwa Mbowealisisitiza mambo makubwa mawili pale kwenye Kamati.Kwanza, alisema walichokiandika kwenye hotuba yaokwamba CUF ni wanachama wa Liberal International, ni sahihina kwamba hawa Waliberali moja ya mambo ya msingikatika sera zao ni uhuru wa mtu binafsi, hiyo ni pamoja namambo ya ushoga, usagaji na kadhalika. Kwa hiyo, akasemasera hii ndivyo ilivyo. Kwa hiyo, kwa msingi huu hawajafanyakosa na wao walikuwa wanazungumzia masuala ya U-liberalina sera za U-liberali hawakukusudia kabisa kuihusisha CUFkatika hili. Kwa hiyo, wakasema wenyewe wako sahihi nahawako tayari kuomba radhi.

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili kubwa alilolisisitizakwenye Kamati Mheshimiwa Mbowe kwamba katika zogohil i CUF na wenyewe wameidhalil isha CHADEMA.Wameidhalilisha kwanza kwa kumtukana Mheshimiwa Wenjematusi mazitomazito, lakini pili hotuba yao baadhi yaWabunge wa CUF waliichanachana na kuitupa, wakasemahili nalo lizungumzwe na wenyewe limewaumiza,limewakera, limewaudhi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile Mheshimiwa Mbowealisema kwa sababu ya vurugu za CUF kikao kiliahirishwa,hili nalo alisema si sawa, nalo vilevile ni kosa lizungumzwe.Kwa hiyo, hayo ndiyo makubwa mawili aliyoyasemaMheshimiwa Mbowe.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa CUF,Mheshimiwa Mbarouk alikiri kwamba ni kweli CUF niwanachama wa Liberal International, huo Umoja waWaliberali lakini alisema si sera zote za Liberal InternationalCUF wanazikubali, si zote, kuna zingine hawamo,hawazikubali, likiwemo hili la ushoga na mambo ya usagajikwamba wao halimo kwenye Katiba yao wala halimokwenye maandishi yao yoyote, kwani hawalikubali na isitoshe

Page 44: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

43

Tanzania kama nchi ilishalitolea msimamo suala hili paletulipoambiwa na Mheshimiwa Cameroon kwamba nchizinazoendelea zikitaka msaada basi ziunge mkono masualahaya; Tanzania ilitoa msimamo kwamba masuala hayahayakubaliki. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa ndio CUF wanasemakama nchi ilishatoa msimamo huo kwamba masuala hayahapa Tanzania hayakubaliki, inakuwaje tena yanaingizwakwenye hotuba ya CHADEMA, halafu na sisi tunahusishwa?Kwa hiyo, wakasema hapa sisi kama chama CUF, tumepakwamatope, tumedhalilishwa, kwa hiyo, maneno hayo yafutwena tuombwe radhi. Haya ndiyo yalikuwa makubwa ambayoCUF waliyasema kwenye kikao kile. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kikao kiliendelea kwa mudamrefu, tulikaa mpaka karibu saa 2.30 usiku kuanzia saa 11.00jioni lakini baadaye tukaja kupata maelewano. Muafakaambao tuliupata baada ya mazungumzo marefu sana nikama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, la kwanza kuhusuCHADEMA, tulikubaliana kwamba ili kujenga mshikamanondani ya Bunge na kuondoa uhasama ndani ya Bunge nakwa vile yale maneno ya kwenye hiyo hotuba yaliumizachama cha CUF, kwa hiyo, yale maneno ya sehemu ya tatuya hotuba yao yote yaondolewe. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tulikubaliana hivyo naKiongozi wa CHADEMA aliafiki hivyo kwamba yale manenoyanaondolewa, sehemu yote ya tatu, yanaanzia ukurasa wa7 – 9, yote yale yaondolewe ili kuleta mshikamano, kuondoauhasama na ili kuleta umoja ndani ya Bunge yaondolewekwa misingi hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, pili, kwamba CHADEMAwaiombe radhi CUF kwa sababu yale maneno, ingawayanafutwa lakini tayari yalishaleta maumivu makubwa nauhasama mkubwa kati ya CUF na CHADEMA. Kwa hiyo,anaomba radhi kwa yale maneno ambayo yaliwakwaza

Page 45: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

44

wenzetu wa CUF. Vilevile tulikubaliana kwambaMheshimiwa Mbowe aombe radhi kwa Naibu Spika kwasababu Naibu Spika jana alipotoa ruling kwamba sasaMheshimiwa Wenje aombe radhi, afute yale maneno nandipo aendelee na hotuba yake, Mheshimiwa Wenjehakufanya hivyo, nia ni kudhalilisha Kiti cha Spika, ni kosa.Kwa hiyo, kwa kosa ali lolifanya Mheshimiwa Wenje,Mheshimiwa Mbowe ataomba radhi ili vilevile kujenga tuheshima ya Bunge letu kwamba Kiti cha Spika lazima wakatiwowote kiheshimiwe. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile ataomba radhi kwaBunge lote kwa sababu jana Wabunge tumewasumbuasana. Kwa hiyo, nalo vilevile kiungwana tu kwamba jamanisamahani tuliwasumbueni lakini sasa limekwisha, tunasongambele. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa CUF,muafaka ambao tuliufikia jana usiku ni kwamba Mnadhimuwa CUF, awaombe radhi Wabunge wa CHADEMA kwasababu ya lugha za matusi zilizotoka upande wa CUF kwendakwa Mheshimiwa Wenje, nalo vilevile si jambo jema. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile awaombe radhiCHADEMA kwa kile kitendo tu cha kuchanachana ile hotubayao na kuitupa, si uungwana na iliwaudhi CHADEMA kuonakwamba hotuba yao inachanwachanwa na kutupwa, hilosio uungwana hivyo waombe radhi.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile Mnadhimu waWabunge wa CUF amwombe radhi Naibu Spika kwa zilevurugu walizozifanya mpaka Naibu Spika akaahirisha kikao.Hilo nalo si uungwana, hivyo tulisema basi na wao wawewaungwana wamwombe radhi Naibu Spika kwa zile fujoambazo zilipelekea Bunge likaahirishwa hapo jana.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile Mnadhimu waWabunge wa CUF naye aliombe radhi Bunge kwa uleusumbufu ambao Wabunge mliupata kwa siku ya jana.

Page 46: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

45

Mheshimiwa Naibu Spika, haya ndiyo tuliyoafikianana nina imani kwamba pande zote mbili, ule moyo wamaridhiano waliounyesha jana usiku, watakuwa waaminifuna waungwana watamke humuhumu ndani yaletuliyokubaliana na ni haya ambayo niliyoyasoma, nina imaniwatafanya hivyo. Siamini kwamba kuna mtu usiku huuatakuwa ameshageuka. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, siamini kwamba usiku huuatakuwa ameshageuka halafu ayakane yote haya ambayonimeyasema. Haya ndiyo tuliyokubaliana, naamini wenzanguwatakaposimama watakubali haya haya ndiyo tuliyoyasemana sisi Kamati tunaamini kama haya yakitekelezwa, ugomviutakuwa umekwisha, amani imerudi na tutasonga mbelekama timu moja, Bunge moja. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuwasilisha.(Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa KapteniMstaafu John Chilligati na Kamati yako kwa kazi nzuri nakwa kweli wamefanya kazi mpaka usiku kwelikweli namchana wote jana walikuwa kwenye kazi hii hii,tunawashukuru sana Kamati ya Maadili kwa hatua hiyo. Sasakama haya ni kweli tuyathibitishe katika utaratibu huuufuatao. Nitamwomba Mheshimiwa Rashid Ali Abdallahatakuwa wa kwanza halafu na wengine watafuata,Mheshimiwa Rashid Ali Abdallah kuhusu yaliyosemwa.

MHE. RASHID ALI ABDALLAH - MNADHIMU WA CUF:Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Kwanza, sina budinimshukuru Mwenyezi Mungu kunijalia leo hii kusimama hapa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Chama chaCUF, sina budi nikupe pole, lakini pia nikupongeze kwa hatuauliyochukua kuweza kulidhibiti Bunge kuendesha shughulizake. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nipende pia kuwapa pole,Mheshimiwa Waziri wa Mambo wa Nchi za Nje na Ushirikiano

Page 47: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

46

wa Kimataifa na Naibu Waziri pamoja na watendaji wakewote kwa usumbufu mkubwa walioupata tarehe 30 Mei,2013. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda pia niwape poleWabunge wenzangu wote waliokosa nafasi ya kujadilihotuba hii tarehe 30 Mei, 2013 kutokana na mzozo uliotokeahapa Bungeni. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, niipongezeKamati yangu ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bungeikiongozwa na Kapteni Mstaafu Chilligati kwa hekima kubwailiyofanya kufikia ufumbuzi wa suala hili. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimpongeze MheshimiwaRajab Mbarouk, Mbunge wa CUF ambaye alikuwepo katikaKamati yetu lakini pia nimpongeze Mheshimiwa Mboweambaye pia naye alikuwepo katika Kamati yetu.Nimpongeze Mheshimiwa Mary Nagu kwa kujumuika na sisikatika kufikia maamuzi haya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kitendo kilichodhahirikwamba chama cha CHADEMA, kwa makusudi au kwabahati mbaya au kwa kutokuelewa, kukidhalilisha chamacha CUF katika hotuba yake. Mheshimiwa Masoud AbdallahSalim, Mbunge wa Mtambile, napenda nimpongeze kwakusimama kwa niaba ya CUF kuomba utaratibu kwa mujibuwa Kanuni za Bunge. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, chama cha CUF katikakufikia maamuzi haya kiliweka mbele maslahi ya wananchiwake na maslahi ya Taifa kwa ujumla. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niwapongeze chama chaCHADEMA katika kikao chetu kwa mambo matatu. Jambola kwanza, kujua kosa lao katika hotuba yao. Jambo la pili,kukubali kuyafuta maneno yote yaliyoidhalilisha CUF katikahotuba yao. Tatu, kukubali kuomba radhi kwa chama chaCUF na wananchi wake. (Makofi)

Page 48: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

47

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa hotuba yaCHADEMA iliidhalilisha CUF, ni dhahiri Waheshimiwa Wabungewa CUF damu ilichemka na ikalazimika kutoa manenoambayo hayastahiki kutolewa Bungeni. Napenda kuchukuafursa hii kwa niaba ya Chama cha CUF, kuwaomba au kutoasamahani kwa wale wote walioguswa na maneno haya.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda niseme kuwaWabunge wote tufanye kazi kwa kulijenga Taifa letu. MunguIbariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Rashid AliAbdallah, Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya CUF. Sasa ninaombanimwite Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, MheshimiwaFreeman Mbowe.

MHE. FREEMAN A. MBOWE - KIONGOZI WA KAMBIRASMI YA UPINZANI BUNGENI: Mheshimiwa Naibu Spika, naminimshukuru sana Mwenyezi Mungu kwamba ametufikishahapa salama na alituongoza vizuri katika kikao chetu chajana.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninamshuru MheshimiwaMwenyekiti wa Kamati ya Maadili kwa taarifa aliyoiwasilishamahali hapa. Katika spirit ya reconciliation yaani katikadhamira ya usuluhisho na kurejesha amani ndani ya Bungeletu na mshikamano wetu kama Wabunge, sina sababu yakuhoji chochote katika mawasil isho aliyoyafanyaMheshimiwa Chiligati. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini la pili, niombe tukurekebisha jambo moja dogo sana katika mamboaliyozungumza Mheshimiwa Chiligati. Kwa kutambua kuwamiongoni mwa Wajumbe ambao walialikwa katika kikaokile tulikuwa vilevile na Mheshimiwa Dkt. Augustine LyatongaMrema ambaye naye mchango wake ulikuwa ni muhimu naushauri wake ulikuwa ni wa msingi sana. Kwa hiyo, kibinafsi,napenda kutambua uwepo wa Mheshimiwa Mrema kwenyekikao kile kama Kiongozi wa Upinzani, kama Kiongozi mzoefu

Page 49: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

48

katika Taifa ambaye naye mchango wake ulitusaidia kufikatulikofika. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimesikia kauli iliyotolewana Mheshimiwa Rashid Abdallah, Mnadhimu, Kiongozimwenzetu kutoka upande wa chama cha Wananchi CUF.Nil ipokwenda kwenye Kikao kile ambacho binafsininakiheshimu, nilitanguliza kusema jambo moja ambaloninaomba nilirudie mahali hapa. Mheshimiwa Ezekia DibogoWenje, Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani, kauli ile haikuwayake binafsi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ile ilikuwa ni kauli ya Kambi.Ndiyo sababu kama kauli ya Kambi ni lazima sisi wote tuwena collective responsibility kama ambavyo naamini hatawenzetu upande wa Serikali kauli inayotolewa na Waziri siyokauli binafsi ni Kauli ya Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, kumtukana,kumdhalilisha, kumtusi Mheshimiwa Wenje kama vile jambolile ni lake binafsi, ni dhahiri halikuwa jambo la kiungwanawala jambo la kistaarabu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini WaheshimiwaWabunge wenzetu wa Chama cha Wananchi CUF,walionekana kukwazika sana na sehemu ya ile hotubaambayo iliwasilishwa na Mheshimiwa Wenje. Kwa kweli niwajibu tu kwamba whether maneno yale yana ukweli auhayana ukweli, walikwazika. Kwa kukwazika huko niustaarabu kukubaliana kuombana radhi kwa sababuhaitakuwa na maana yoyote kama tutafanya vyama vyetuni vya muhimu kuliko Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vyama vya siasa hivi nivyombo vya wananchi. Ni vyema tukaelewa vilevile kuwatunapoparagana huku ndani ya Bunge, Taifa nalo linakuwakatika sintofahamu hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tunalazimikakukubali katika wakati mwingine kumeza fried zetu kama

Page 50: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

49

walivyofanya wenzangu wa CUF na sisi tutafanya hivyohivyokwa sababu wote tunajenga nyumba moja, tusigombanekwa sababu ya vito. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna mambo makubwakatika nchi hii ya kuzungumza na tukatofautiana katikamisimamo kuliko hili jambo. Jambo hili haliwezi kuwa linamsingi mzito kuliko ulazima wetu wa kujenga umoja waKitaifa na kujadili yale mambo ambayo tunafikiri yana maslahizaidi kwa nchi yetu. Vilevile katika mikakati yote ya harakati,wanazungumza kwa lugha ya kijeshi kwamba tu-withdraw,labda pengine nisiende mbali sana lakini niseme tu kwambaunaweza kujitoa katika mstari wa mbele katika jeshi nisehemu ya mkakati tu wa kazi na kwa maana hiyo, nisemekabisa kwa wenzangu wa CUF wala wasifikiri kuwa ninajaribukuyumbisha maneno mahali hapa hapana, sijaribu kutungamaneno wala kuyumbisha maneno, napenda niwaomberadhi sana Waheshimiwa wenzangu wa Chama ChaWananchi CUF na ninapenda vilevile kumwomba radhiMheshimiwa Naibu Spika, tumeairisha Bunge mara mbili bilasababu za msingi. Tukitafuta nani ni mshindi, walahaitausaidia sisi kama Bunge wala sisi kama Taifa.Nawaomba sana wakubali apology yetu, tuendelee kufanyakazi ndani ya Bunge na Waheshimiwa Wabunge wote vilevilepoleni sana kwa usumbufu wote ambao ulijitokeza katikasiku ya jana. Tumejikuta tunatafakari tulikoangukia penginetumepata wakeup call ya kutafakari tulikojikwaa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana,ninawashukuru Waheshimiwa Wabunge wenzangu naahsanteni sana. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Kwa niaba yenu WaheshimiwaWabunge, niwashukuru sana Kamati ya Maadili, niwashukurusana Wabunge wa Chama Cha CUF na hasa Msemaji waowa leo Mheshimiwa Rashid Ali Abdallah lakini vilevileniwashukuru Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na hasa kwa

Page 51: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

50

maneno mazuri sana ya kujenga yaliyosemwa na Kiongoziwa Upinzani Bungeni, Mheshimiwa Freeman Mbowe.Natumaini kazi waliyoifanya kutwa nzima ya jana inatuwekamahali pazuri sana. Mimi niseme tu kuwa sisi wote humu ndaniya Bunge, tunamwamini Mwenyezi Mungu na katika kufanyahivyo mara nyingi tunafanya toba kwa makosa mbalimbali,sisi Wakristo tunasema kwa makosa ambayo tumeyafanyakwa mawazo, kwa maneno, kwa matendo au kwakutotimiza wajibu. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, kwa hiyo, ninatumainikatika yote haya tumejifunza, tutulie, tujirekebishe, Taifa zimalinatutazama, sisi ni mfano wa jamii ya Tanzania, tuwe makinina yale ambayo tunayatamka Bungeni sote kabisa kamaambavyo Kiti kimekuwa kikisisitiza tangu tumeanza Bungehili la kumi. Katika eneo ambalo Bunge hili limelaumiwa sana,ni kauli zetu za humu Bungeni. Naendelea kuwaasaWaheshimiwa Wabunge wote kabisa, kujiepusha na kauliambazo kwa kweli hata unapoiweka unajua kabisa kuwanitawaudhi watu wengine, nyingine zimevumiliwa hukonyuma, huenda zisivumiliwe huko mbele lakini tujitahidikuzirekebisha, ziko nyingi sana za kirejareja, nyingi sana,tuzingatie makubaliano.

Kesho kama shughuli ya kutengua Kanuniitakayofuata muda mfupi ujao itakubalika, tutakutana kesho,matarajio yetu na mapendekezo ni kwamba kesho tumalizeWizara hii ya Mifugo na Wizara ya Mambo ya Nje. Kwa hiyo,ni matumaini yangu ni kwamba hiyo sehemu ya tatuhaitasomwa, hayatajitokeza yale ya siku zile ambapotunakubaliana kitu fulani kisifanyike halafu watu wanaendakufanya kitu kilekile na kama mambo mengine yoteyatakwenda kama tulivyokuwa tumekubaliana.

Baada ya maelezo hayo, sasa nimwite MheshimiwaMwanasheria Mkuu ili atupatie pendekezo alilo nalo.

Page 52: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

51

HOJA YA KUTENGUA KANUNI

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: MheshimiwaNaibu Spika, kabla sijaanza kusema na kwa sababuumesema lakini ninaomba pia kusoma utenzi wa 154 waKitabu cha Mfasihi Mkuu wa nchi hii Shaaban Robert, aliandikatarehe 5/4/1958, miaka 55 iliyopita alisema:-

“Chuki jambo la udhia,Siyo jema kutaradhiwa,

Na kama litadhiriwa,Tutamezwa na ushenzi,Siyo vyema kurudi tenaUshenzi wema haunaLakini dawa hapanaIla sera ya mapenzi ‘’

Mheshimiwa Naibu Spika, maneno haya yanatokakatika kitabu cha Mapenzi Mema. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunawashukuru sanaWaheshimiwa kwa hili ambalo limefanyika asubuhi hii.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya utangulizi huo,kwa mujibu wa Kanuni ya 153 (1) na kwa shabaha maalumu,naomba kutoa maelezo yafuatayo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa Mkutano waKumi na Moja wa Bunge wa kushughulikia bajeti ya Serikalipamoja na shughuli nyingine za Bunge zilizopangwa,umepangwa kumalizika tarehe 28/6/2013;

Na kwa kuwa ratiba ya shughuli zote zilizopangwakufanyika katika Mkutano huu wa Kumi na Moja, imepangwakwa kuzingatia Kanuni ya 99(1) ya Kanuni za Kudumu za BungeToleo la mwaka huu;

Na kwa kuwa awali uwasilishaji wa majadiliano yaWizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi ulipangwa uwe

Page 53: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

52

kwa siku moja jambo ambalo lingeruhusu wachangiajiwachache sana;

Na kwa kuwa ni ukweli usiopingika kuwa Wizara hiiinahusisha sekta mbili za Mifugo na Uvuvi ambazozinawalenga wananchi walio wengi moja kwa moja moja;

Na kwa kuwa katika Kikao cha Kamati ya Uongoziwa Bunge kilichofanyika katika Ukumbi wa Spika tarehe 30/5/2013, Wajumbe wa Kamati hiyo waliohudhuria waliazimiakuliomba Bunge likubali kuiongezea Wizara hii siku moja kwakufanya kazi siku ya Jumamosi tarehe 1/6/2013 yaani kesho;

Na kwa kuwa kwa mujibu wa Kanuni ya 28(15) yaKanuni za Bunge, Toleo la mwaka huu, Bunge haliwezikukutana na kufanya kazi siku za Jumamosi, Jumapili au sikuza mapumziko;

Na kwa kuwa ili kuliwezesha Bunge kuweza kukutanasiku ya Jumamosi yaani kesho tarehe 1/6/2013, ni lazima Bungelitengue Kanuni ya 28(15) ya Kanuni za Bunge, Toleo la mwakahuu kwa mujibu wa Kanuni ya 153(1).

Hivyo basi, Bunge linaazimia kwamba kwamadhumuni ya utekelezaji bora wa shughuli za Bunge katikaMkutano huu wa Kumi na Moja, Kanuni ya 28 (15) itenguliwekama ifuatavyo:-

Kanuni ya 28 (15) ambayo kwa ujumla wakeinaelekeza kuwa Bunge halitakutana siku za Jumamosi,Jumapili na siku za mapumziko, itenguliwe na badala yakeBunge lako Tukufu likutane siku ya Jumamosi, tarehe 1/6/2013yaani kesho kuanza saa tatu asubuhi hadi saa nane mchana,isipokuwa kwamba siku hiyo hakutakuwa na kipindi chamaswali.

Mheshimiwa Naibu wa Spika, naomba kutoa hoja.

Page 54: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

53

WAZIRI WA USHIRIKIANO WA AFRIKA YA MASHARIKI:Mheshimiwa Naibu Spika, naafiki.

(Hoja ilitolewa iamuliwe)(Hoja iliamuliwa na Kufikiwa)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, sote tumeafiki,nawaomba sana Waheshimiwa Wabunge, kesho siku yaJumamosi sote tufike, tujitahidi tufanye kazi zilizoko Mezanikwa siku ya kesho. Kama nilivyosema tunaweza kabisa kwauendeshaji bora hapa tukamalizika shughuli za Wizara yaMifugo saa tano kamili, tutawaomba tumalizie masaamatatu yatakayobakia kwa Wizara ya Mambo ya Nje ilipasiwe na kiporo tena ili Jumatatu tuendelee na ratiba zetukama kawaida.

Baada ya hatua hiyo, sasa nawaomba WaheshimiwaWabunge nimkaribishe Mheshimiwa Mwenyekiti JenistaMuhagama aweze kuendelea na shughuli zilizoko Mezani.

Hapa Mwenyekiti (Mhe. Jenista J. Muhagama) Alikalia Kiti

MWONGOZO WA SPIKA

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mwongozo wa Spika.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, hatuwezikuendelea kupoteza muda, hiyo Miongozo tutaisikilizabaadaye, Katibu!

HOJA ZA SERIKALI

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali - Waziri waMaendeleo ya Mifugo na Uvuvi

MWENYEKITI: Naomba nimwite Mheshimiwa Waziri!

WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI:Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kuzingatia taarifailiyowasilishwa mbele ya Bunge lako Tukufu na Mwenyekiti

Page 55: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

54

wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji,iliyochambua bajeti ya Wizara ya Maendeleo ya Mifugo naUvuvi, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufulikubali kujadili na kupitisha taarifa ya mapitio ya utekelezajiwa kazi za Wizara kwa mwaka 2012/2013 na mwelekeo wakazi za Wizara kwa mwaka 2013/2014. Aidha, naliombaBunge lako Tukufu likubali kupitisha Mpango wa Maendeleona Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Wizara yaMaendeleo ya Mifugo na Uvuvi kwa mwaka wa fedha 2013/2014.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kumpongezaMheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Mohamed GharibBilal, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniana Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda, Mbunge waKatavi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano waTanzania, kwa jitihada zao za kuongoza, kusimamia nakuendeleza amani, utulivu na uchumi wa nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara il ipokea kwamasikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mheshimiwa Mbungemwenzetu; Hayati Salim Hemed Khamis aliyekuwa Mbungewa Chambani. Naungana na Waheshimiwa Wabungewenzangu kutoa salamu za rambirambi kwa familia yamarehemu, ndugu na wananchi wa jimbo alilokuwaanaliwakilisha. Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemumahali pema peponi, Amina. Aidha, naomba nitumie fursahii kuwakumbuka wananchi wenzetu waliopoteza maishakutokana na sababu mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuchukua fursa hiikumshukuru Mheshimiwa Profesa Peter Mahamudu Msolla,Mbunge wa Kilolo na Mheshimiwa Said Juma Nkumba,Mbunge wa Sikonge pamoja na wajumbe wote wa Kamatiya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kwa ushauri,maoni na ushirikiano waliotupatia katika utekelezaji wamajukumu ya Wizara na maandalizi ya bajeti hii. Napendakulihakikishia Bunge lako Tukufu kwamba Wizara yanguitaendelea kuzingatia ushauri, mapendekezo na maoni ya

Page 56: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

55

Kamati na yale yatakayotolewa na Bunge lako Tukufu.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuchukua fursa hiikumpongeza Waziri Mkuu, Mheshimiwa Mizengo KayanzaPeter Pinda, Mbunge wa Katavi kwa hotuba yake nzuri yenyekutoa malengo ya Serikali na mwelekeo wa utendaji wa sektambalimbali pamoja na kazi za Serikali kwa mwaka 2013/2014.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hali ya sekta za mifugo nauvuvi na changamoto zilizopo. Sekta ya mifugo ni moja katiya sekta zilizopewa umuhimu katika kutekeleza Mkakati waKukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini Nchini (MKUKUTA II).Mifugo hutoa ajira, lishe, nishati, mbolea na hutumika kamawanyamakazi na benki hai. Baadhi ya mifugo ikiwemong’ombe, mbuzi, kondoo, kuku, nguruwe ni chanzo chamapato ya haraka wakati wa hali ya ukame na njaa, hususanmaeneo ya vijijini. Aidha, mifugo na bidhaa zake huokoafedha za kigeni ambazo zingetumika kuagiza mazao hayokutoka nje ya nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2012, sektaya mifugo ilikua kwa asilimia 3.1 ikilinganishwa na asilimia3.9 mwaka 2011 na kuchangia asilimia 4.6 katika pato laTaifa ikilinganishwa na asilimia 3.7 mwaka 2011. Kulinganana takwimu zilizopo, idadi ya mifugo nchini inafikia ng’ombemilioni 22.8, mbuzi milioni 15.6 na kondoo milioni 7.0. Pia,wapo kuku wa asili milioni 35.5, kuku wa kisasa milioni 24.5na nguruwe milioni 2.01. Ulaji wa mazao ya mifugo kulinganana viwango vya Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja waMataifa (FAO, 2011) ni kilo 50 za nyama, lita 200 za maziwana mayai 300 kwa mtu mmoja kwa mwaka. Kwa upandewa nchi yetu, viwango vya ulaji wa mazao hayo kwa sasa niwastani wa kilo 12 za nyama, lita 45 za maziwa na mayai 75kwa mtu mmoja kwa mwaka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, shughuli za uvuvi hufanyikakatika maeneo ya maji chumvi na maji baridi. Nchi yetu inaukanda wa pwani wa bahari wenye urefu wa kilometa 1,424ambao umegawanyika katika eneo la Maji ya Kitaifa

Page 57: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

56

(Territorial Sea) lenye ukubwa wa kilometa za mraba 64,000na eneo la Bahari Kuu lenye ukubwa wa kilometa za mraba223,000. Eneo la maji baridi linajumuisha maziwa makuumatatu ambayo ni; Ziwa Victoria (kilometa za mraba 35,088),Ziwa Tanganyika (kilometa za mraba 13,489) na Ziwa Nyasa(kilometa za mraba 5,700), maziwa ya kati na madogo 29,mito na maeneo oevu. Aidha, ukuzaji wa viumbe kwenyemaji unafanyika kwenye maeneo hayo na maeneo ya nchikavu yenye maji ya kutosha ambapo kuna mabwawa 20,134ya ufugaji samaki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sekta ya uvuvi huchangiakatika upatikanaji wa lishe bora, ajira, kipato kwa wananchi,pato la Taifa na hivyo kuchangia katika kuondoa umaskini.Sekta hii imekua kutoka asilimia 1.2 mwaka 2011 hadi asilimia2.9 mwaka 2012 na kuchangia katika pato la Taifa kwaasilimia 1.4. Vilevile idadi ya wavuvi wadogo imeongezekakutoka 177,527 mwaka 2011/2012 hadi wavuvi 182,741mwaka 2012/2013 na zaidi ya wananchi milioni 4.0wameendelea kutegemea shughuli za uvuvi katika kujipatiakipato kutokana na biashara ya samaki, uchakataji wamazao ya uvuvi, utengenezaji wa zana na vyombo vya uvuvina biashara nyingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2012/2013sekta za mifugo na uvuvi zimeendelea kukabiliwa nachangamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na:-

(i) Uwekezaji mdogo wa Serikali na sekta binafsikatika sekta za mifugo na uvuvi na hasa katika uzalishaji,uvunaji, usindikaji na masoko ya mazao ya mifugo na uvuvi;

(ii) Kutopatikana kwa mikopo ya kutosha nayenye masharti nafuu kwa ufugaji na uvuvi ikilinganishwa namahitaji yao;

(iii) Kasi ndogo katika kuainisha, kupima nakumilikisha wafugaji maeneo ya ufugaji endelevu ili kudhibitikuhamahama kwa mifugo na hivyo kupunguza migogoro

Page 58: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

57

baina ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi, uharibifuwa mazingira na ueneaji wa magonjwa ya mifugo;

(iv) Matumizi madogo ya mbegu bora za mifugo,pembejeo na huduma ya uhimilishaji pamoja na uhabawa mbegu bora za samaki;

(v) Ukosefu wa soko la uhakika la mazao yamifugo na uvuvi na hasa katika maeneo ya vijijini;

(vi) Kuenea kwa magonjwa mbalimbali yamifugo, hususan magonjwa ya mlipuko kutokana na uwezomdogo wa kuyakabili kutokana na uhaba wa wataalamna vitendea kazi;

(vii) Uhaba wa maafisa ugani wa mifugo na uvuviikilinganishwa na mahitaji ya wataalam hao pamoja namatumizi madogo ya elimu na teknolojia sahihi kwa ufugajina uvuvi endelevu; na

(viii) Ushiriki mdogo wa wadau katika kudhibitiuvuvi na biashara haramu ya samaki na mazao ya uvuvi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, i l i kukabiliana nachangamoto hizi, Serikali imeweka mikakati mbalimbali yakuzifanya sekta za mifugo na uvuvi kuwa endelevu zenyeuzalishaji bora, zinazoendeshwa kibiashara na kuzingatiahifadhi ya mazingira kupitia sera, mikakati na programuzifuatazo:-

(a) Sera ya Taifa ya Mifugo ya mwaka 2006,Mkakati wa Kuendeleza Sekta ya Mifugo (2011) na Programuya Kuendeleza Sekta ya Mifugo ya miaka mitano (2011/12 –2015/16) ambazo zinalenga kuongeza ukuaji wa sekta kutokaasilimia 3.1 mwaka 2012 hadi kufikia 4.5 kwa mwaka ifikapomwaka 2016.

(b) Sera ya Taifa ya Uvuvi na Mikakati yake ya mwaka1997 na Programu ya Kuendeleza Sekta ya Uvuvi ya miakamitano (2011/12 – 2015/16) ambazo zinalenga kuimarisha

Page 59: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

58

usimamizi na matumizi endelevu ya rasilimali za uvuvi nakuongeza ukuaji wa sekta kutoka asilimia 2.9 mwaka 2012hadi kufikia 5.3 kwa mwaka ifikapo mwaka 2016.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mapitio ya utekelezaji waMpango wa mwaka 2012/2013 na mwelekeo wa Bajeti yamwaka 2013/2014. Ukusanyaji wa Mapato. Katika kipindi chamwaka 2012/2013, Wizara ilitarajia kukusanya kiasi cha shilingi18,207,055,000.00. Kati ya hizo, shilingi 8,049,864,000.00 ni kutokasekta ya mifugo na shilingi 10,157,191,000.00 ni kutoka sektaya uvuvi. Hadi kufikia mwezi tarehe 21 Mei, 2013, kiasi chashilingi 11,935,010,942.71 kimekusanywa na Wizara ikiwa nisawa na asilimia 65.6 ya lengo. Sababu kubwa ya kupunguakwa maduhuli hayo ni kutokana na mtikisiko wa uchumikwenye soko la samaki na mazao ya uvuvi la kimataifapamoja na kupungua kwa maduhuli yatokanayo na mauzoya ngozi ghafi nje ya nchi na kuwezesha kiasi kikubwa changozi kusindikwa hapa nchini. Kati ya hizo, shil ingi4,721,898,802.72 zimekusanywa kutoka sekta ya mifugo(asil imia 58.6 ya lengo) na shil ingi 7,213,112,140.00zimekusanywa kutoka sekta ya uvuvi (sawa na asilimia 69.7ya lengo). Katika mwaka 2013/2014, Wizara inatarajiakukusanya kiasi cha shilingi 18,584,074,280.00. Kati ya hizo,shilingi 8,247,973,280.00 zitatoka kwenye sekta ya mifugo nashilingi 10,336,101,000.00 zitatoka kwenye sekta ya uvuvi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, matumizi ya fedha. Katikamwaka 2012/2013, Wizara ilitengewa jumla ya shilingi54,566,124,000.00. Kati ya hizo, shilingi 40,726,641,000.00 ni kwaajili ya Matumizi ya Kawaida na Shilingi 13,839,483,000.00 nikwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo. Kati ya fedhaza Matumizi ya Kawaida, shilingi 13,959,071,000.00 ni kwa ajiliya mishahara ya watumishi (PE) na shilingi 26,767,570,000.00 nikwa ajili ya matumizi mengine (OC). Vilevile, kati ya fedhazilizotengwa kwa ajili ya maendeleo, shilingi 4,000,000,000.00ni fedha za ndani na shilingi 9,839,483,000.00 ni fedha za nje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hadi kufikia tarehe 20 Mei,2013, jumla ya shilingi 34,428,187,941.05 (sawa na asilimia 63.09)zimetolewa. Kati ya hizo, shilingi 29,433,287,941.05 (sawa na

Page 60: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

59

asilimia 67.3) ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida, ambaposhilingi 27,773,854,092.68 (sawa na asilimia 94.4) zimetumikana shilingi 4,994,900,000.00 (sawa na asilimia 36.1) zimetolewakwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambaposhilingi 2,843,009,324.18 zimetumika (sawa na asilimia 56.9).Kati ya fedha za Matumizi ya Kawaida, shil ingi18,320,198,135.00 zilikuwa ni kwa ajili ya Mishahara na shilingi11,113,089,806.05 kwa ajili ya Matumizi Mengine (OC). Kati yafedha za maendeleo, fedha za ndani ni shilingi 944,989,300.00na shilingi 4,049,910,700.00 ni za nje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ubunifu na utekelezaji waSera na Sheria za Sekta. Wizara imeendelea kuratibu, kupitiana kusimamia utekelezaji wa sera, sheria, mikakati naprogramu mbalimbali za kuendeleza sekta za mifugo nauvuvi nchini. Katika mwaka 2012/2013, Wizara imeendeleakusambaza na kutoa elimu kwa wadau kuhusu Sera ya Taifaya Mifugo ya mwaka 2006 na Sera ya Taifa ya Uvuvi naMikakati yake (1997). Jumla ya nakala 1,000 za Sera ya Taifaya Mifugo (2006) na nakala 500 za Sera ya Taifa ya Uvuvi naMkakati (1997) zimesambazwa kwa wadau mbalimbali hapanchini. Pia, elimu kwa wadau imeendelea kutolewa kupitiamaadhimisho mbalimbali ya kitaifa ya wadau pamoja namikutano ya kitaaluma ikiwemo sikukuu ya NaneNane, Sikuya Uvuvi Duniani, Siku ya Chakula Duniani na Wiki yaUhamasishaji Unywaji Maziwa. Vilevile, Wizara imekamilishakutafsiri Mkakati wa Kuendeleza Sekta ya Mifugo (2011) kwalugha ya Kiswahili na kufanya mapitio ya Sera ya Taifa yaUvuvi na Mikakati yake (1997).

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2012/2013,Wizara kwa kushirikiana na wadau, imeendelea kupitia sheriaza sekta ya mifugo na uvuvi ili ziendane na Sera ya Ugatuajiwa Madaraka (D by D) na kuboresha mazingira ya kibiashara.Kazi zilizofanyika ni pamoja na:-

(i) Kuandaa mapendekezo ya marekebisho yaSheria za Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Sura 146, Sheriaya Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania Sura 280 na Sheria yaUvuvi Sura 279;

Page 61: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

60

(ii) Kuandaa mapendekezo ya kutunga Sheria yaMbari Bora za Wanyama (Animal Breeding Act);

(iii) Kuandaa marekebisho ya Kanuni ya Biasharaya Ngozi (Trading in Hides, Skins and Leather Regulations, 2010)chini ya Sheria ya Ngozi Sura 120;

(iv) Kuandaa Kanuni ya Viwango vya Tozo zaMaabara za Uvuvi chini ya Sheria ya Uvuvi Sura 279 yenye GN.Na. 237, Kanuni ya Uingizaji na Uuzaji wa Maziwa na Bidhaaza Maziwa nchini chini ya Sheria ya Maziwa Sura 262 yenyeGN Na. 329 na Kanuni tano (5) chini ya Sheria ya Maeneo yaMalisho na Rasilimali za Vyakula vya Wanyama Sura 180zenye GN. Na. 54, 55, 56, 57 na 58; na

(v) Kutafsiri kwa lugha ya Kiswahili Sheria yaMaeneo ya Malisho na Rasilimali ya Vyakula vya WanyamaSura 180 na Kanuni za Uvuvi za Mwaka 2009.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2013/2014,Wizara itaendelea kutoa elimu kuhusu sera, sheria na kanuniza sekta za mifugo na uvuvi. Aidha, itachapisha nakala 1,000za Mkakati wa Kuendeleza Sekta ya Mifugo (2011) nakuzisambaza kwa wadau kwa ajili ya utekelezaji. Pia,itakamilisha mapitio ya Sera ya Taifa ya Uvuvi na Mikakatiyake (1997) na kuandaa Mkakati wa utekelezaji. Vilevile,Wizara itaendelea kufanya tafsiri ya Sheria ya Ustawi waWanyama Sura 154, Sheria ya Magonjwa ya Mifugo Sura 156,Sheria ya Veterinari Sura 319, Sheria ya Biashara ya Ngozi Sura120, katika lugha ya Kiswahili. Aidha, Wizara itakamilishamapendekezo ya kutunga Sheria ya Mbari Bora za Wanyama(Animal Breeding Act) na kuandaa mapendekezo ya kutungaSheria ya Ukuzaji Viumbe kwenye Maji (Aquaculture Act).

Mheshimiwa Mwenyekiti, uendelezaji wa Sekta yaMifugo. Uzalishaji na Biashara ya Mifugo na Mazao yake.Maziwa, katika mwaka 2012/2013, uzalishaji wa maziwaumeongezeka kwa asilimia 3.6 kutoka lita bilioni 1.85 mwaka2011/2012 hadi lita bilioni 1.92. Aidha, maziwa yanayosindikwakwa siku yameongezeka kutoka lita 130,400 mwaka 2011/

Page 62: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

61

2012 hadi lita 135,300 mwaka 2012/2013. Katika mwaka 2013/2014, Wizara itaendelea kuhamasisha sekta binafsi kuimarishaukusanyaji na usindikaji wa maziwa ili kuongeza usindikajiwa maziwa kufikia lita 160,000 kwa siku.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mashamba ya UzalishajiMifugo ya Serikali yameendelea kuboreshwa kwa kupatiwavitendea kazi ili kuongeza uzalishaji ambapo katika mwaka2012/2013, Wizara imenunua ng’ombe wazazi 109 kwa ajiliya mashamba ya Ngerengere (61), Sao Hill (33) na Mabuki(madume bora 15). Aidha, jumla ya mitamba 1,306imezalishwa na kusambazwa kwa wafugaji wadogo katikamaeneo mbalimbali nchini kutoka katika mashamba yaMabuki (301), Sao Hill (198), Nangaramo (101), Kitulo (77),Ngerengere (125) na NARCO (504). Vilevile, Chama chaUshirika cha Wafugaji wa Ng’ombe wa Maziwa Tanga(TDCU), Umoja wa Wafugaji wa Nyanda za Juu Kusini (SHILDA)na mashirika ya Heifer Project Tanzania (HPT) na Farm Friendsyamesambaza jumla ya mitamba 9,741.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2013/2014,Wizara itaendelea kuimarisha mashamba ya uzalishaji mifugokwa kuboresha miundombinu na kuyapatia vitendea kazipamoja na kuendelea kuhamasisha sekta binafsi kuzalishana kusambaza mitamba bora kwa wafugaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kuongeza tija katikauzalishaji wa ng’ombe wa maziwa, Kituo cha Taifa chaUhimilishaji – NAIC Usa River pamoja na vituo vya uhimilishajivya Kibaha, Dodoma, Lindi, Mwanza na Mbeyavimeimarishwa. Jumla ya dozi 168,000 za mbegu borazimezalishwa na kusambazwa kwa wafugaji ambapong’ombe 98,340 walihimilishwa ikilinganishwa na ng’ombe81,300 mwaka 2011/2012. Aidha, Wizara imetoa mafunzo kwawataalam 115 wa uhimilishaji. Pia, Wizara imeanzamaandalizi ya ujenzi wa vituo vipya vya uhimilishaji vyaMpanda na Sao Hill.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2013/2014,Wizara itaendelea kuimarisha uhimilishaji nchini kwa kuzalisha

Page 63: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

62

dozi 190,000 za mbegu bora za uhimilishaji, kuendeleza ujenziwa Kituo cha Uhimilishaji cha Sao Hill na Mpanda na kuanzishakituo kingine cha Tabora.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nyama - ng’ombe, mbuzi,kondoo na nguruwe. Katika mwaka 2012/2013, uzalishaji wanyama umeongezeka kutoka tani 448,387 mwaka 2011/2012hadi tani 466,047 (ng’ombe tani 299,581, mbuzi na kondootani 115,652 na nguruwe tani 50,814) mwaka 2012/2013. Aidha,idadi ya ng’ombe walionenepeshwa imeongezeka kutoka132,246 mwaka 2011/2012 hadi ng’ombe 155,206 mwaka2012/2013 Pia, katika juhudi za kuongeza uzalishaji na uborawa nyama, Wizara kwa kushirikiana na Halmashauriimeandaa na kusambaza nakala 1,000 za Mwongozo waUnenepeshaji Ng’ombe kwa wadau il i kuhamasishaunenepeshaji wa mifugo. Aidha, Wizara imeendeleakuimarisha minada ya upili na ya mipakani ambapo minadaya upili ya Pugu na Kizota (Dodoma) imekarabatiwa na ujenziwa mnada wa Nyamatala (Misungwi) na mazizi katikamnada wa Kirumi umekamilika. Pia, Wizara imenunua mizaniminne kwa ajili ya kusimika katika minada ya Kizota na Pugukwa ajili ya kupima uzito wa mbuzi na kondoo na minadaya Lumecha (Songea) na Sekenke (Iramba) kwa ajili yakupima uzito wa ng’ombe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara kwa kushirikiana naWizara ya Viwanda na Biashara na Halmashauri imeendeleakuratibu biashara ya mifugo na mazao yake ndani na nje yanchi. Katika mwaka 2012/2013, ng’ombe 1,105,037, mbuzi872,908 na kondoo 190,265 wenye thamani ya shilingi bilioni951.2 waliuzwa minadani. Aidha, ng’ombe 1,705, mbuzi nakondoo 1,003 wenye thamani ya shilingi bilioni 2.16 waliuzwanje ya nchi na tani 126.2 za nyama ya ng’ombe, 667.8 zambuzi na 88.4 za kondoo ziliuzwa nje ya nchi zikiwa nathamani ya shilingi bilioni 28.8.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2013/2014,Wizara kwa kushirikiana na wadau wa nyama itaendeleakuhamasisha wafugaji, wafanyabiashara ya mifugo nawadau wengine kuwekeza kwenye ufugaji wa kisasa

Page 64: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

63

ukiwemo wa ranchi na unenepeshaji ili kunenepeshang’ombe 175,000. Aidha, Wizara itakarabati miundombinuya minada ya upili ya Igunga, Weruweru na Meserani nakuendeleza ujenzi wa minada ya Kirumi na Longido. Pia,Wizara itaendelea kuhamasisha matumizi bora ya mizani nautunzaji wa miundombinu ya minada ya mifugo na kutoamafunzo kwa wakusanyaji maduhuli 50 na wafanyabiasharawa mifugo 200.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uzalishaji wa nyama katikaKampuni ya Ranchi za Taifa (National Ranching Company -NARCO). Katika mwaka 2012/2013, NARCO kupitia ranchi 10za mfano za Kagoma, Kalambo, Kikulula, Kongwa, Mabale,Missenyi, Mkata, Mzeri, Ruvu na West Kilimanjaro imeendeleakuzalisha, kunenepesha na kuuza mifugo kwa ajili ya nyama.NARCO ina jumla ya hekta 230,384 zenye uwezo wa kuwekang’ombe kati ya 80,000 na 90,000. Kwa sasa, Kampuni inajumla ya ng’ombe 20,214, kondoo 1,650, mbuzi 744, farasi 45na punda 40. Katika mwaka 2012/2013, NARCO imezalishandama 5,718 kutoka ng’ombe wazazi 8,997; kununua nakunenepesha ng’ombe 8,076 kutoka kwa wafugaji na kuuzang’ombe 13,438 wenye thamani ya shilingi bilioni 3.6.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2012/2013,Kampuni imetoa hati miliki ndogo (sub-lease) kwa vitaluvinane (8) katika ranchi ya Usangu na kufikisha idadi ya hatimiliki ndogo 83 kati ya 104 zinazotakiwa kutolewa. Aidha,imetoa ushauri na mafunzo ya kusimamia ufugaji wa kisasakwa wawekezaji watanzania 70 ambao wamemilikishwavitalu ndani ya Ranchi za Taifa, ambapo ranchi hizozimewekeza ng’ombe 54,300, mbuzi 4,400 na kondoo 1,800.Katika mwaka 2013/2014, NARCO inatarajia kununua nakunenepesha ng’ombe 14,580 wenye thamani ya shilingibilioni 4.5. Aidha, Kampuni itaendeleza ujenzi wa machinjiokatika Ranchi ya Ruvu ambao ulisimama kwa muda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na migogoroiliyojitokeza kati ya wawekezaji na wananchi katika ranchiza NARCO Mkoani Kagera, Wizara yangu kwa kushirikianana Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, Wizara ya Ardhi Nyumba na

Page 65: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

64

Maendeleo ya Makazi na vijiji vinavyozunguka ranchi hizoitapima upya ranchi hizo ili kutafuta ufumbuzi wa kudumu.Kwa kuanzia ranchi ya Kagoma itapimwa upya katikamwaka huu wa fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara kwa kushirikiana nawadau mbalimbali imeendelea kuhamasisha ufugaji wakuku kibiashara. Kutokana na juhudi hizi, uzalishaji wa nyamaya kuku na mayai umeongezeka kutoka mayai bilioni 3.5mwaka 2011/2012 hadi mayai bilioni 3.7 na nyama ya kukukutoka tani 84,524 hadi tani 87,408 mwaka 2012/2013 Aidha,Wizara imeshirikiana na Heifer International Tanzaniakusambaza majogoo 1,520 kwa wafugaji 322 waliopatamafunzo katika Wilaya za Bagamoyo, Kilosa na Mvomero ilikuboresha kuku wa asili na kuongeza uzalishaji. Katikamwaka 2013/2014, Wizara itaendelea kuhamasisha wadaukuwekeza katika ufugaji wa kuku wa asili na wa kisasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kuvutia usindikaji wa ngozindani ya nchi, Serikali iliongeza ushuru wa ngozi ghafizinazouzwa nje ya nchi kutoka asilimia 40 hadi 90 au shilingi400 hadi 900 kwa kilo kutegemea ipi ni kubwa. Kutokana nahatua hiyo, usindikaji wa ngozi uliongezeka kutoka vipandevya ngozi ya ng’ombe 166,773 kati ya Januari na Juni 2012hadi vipande 343,860 kuanzia Julai hadi Desemba 2012. Aidha,usindikaji wa ngozi ya mbuzi na kondoo uliongezeka kutokavipande 778,023 hadi vipande 1,173,875. Idadi ya ngozizilizosindikwa na kuuzwa nje ya nchi ni vipande 969,060 vyangozi za ng’ombe na vipande 2,582,525 vya ngozi za mbuzina kondoo vyenye jumla ya thamani ya shilingi bilioni 50.9.Kutokana na mafanikio hayo, Serikali imedhamiria kuzuiauuzwaji wa ngozi ghafi nje ya nchi. Hatua hiyo inatarajiwakuongeza usindikaji katika viwanda vya ndani, kuongeza ajirana kuondoa utoroshaji wa ngozi ghafi nje ya nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2012/2013,Wizara kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI,Wizara ya Viwanda na Biashara, Halmashauri 65 na Chamacha Wadau wa Ngozi Tanzania imeendelea kusimamia nakutekeleza Mkakati wa Kufufua na Kuendeleza Sekta na

Page 66: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

65

Viwanda vya Ngozi Nchini kwa kufanya yafuatayo:-

(i) Kuhamasisha uzalishaji, uhifadhi na usindikajiwa ngozi unaozingatia hifadhi ya mazingira katikaHalmashauri 65 zinazotekeleza Mkakati wa Kufufua naKuendeleza Sekta na Viwanda vya Ngozi;

(ii) Kujenga vituo vinne vya kutolea mafunzo yauendelezaji wa zao la ngozi katika Halmashauri zaNgorongoro, Rombo, Sumbawanga na Bariadi;

(iii) Kutoa mafunzo kwa wagani 650 kuhusumnyororo wa thamani wa zao la ngozi na wadau wa ngozi20 kuhusu uzalishaji bora wa ngozi, uhifadhi na usindikaji;

(iv) Kutoa mafunzo kwa wadau 3,408 wakiwemowachinjaji/wachunaji 911, wawambaji na wachambuzi wamadaraja 561, wasindikaji 67, wafanyabiashara 325 nawafugaji 1,505 ili kuboresha zao la ngozi; na

(v) Kuhamasisha uanzishwaji wa Chama chaWazalishaji wa Ngozi nchini ambacho kitasimamia maslahiya wazalishaji wa ngozi wakiwemo wafugaji, wachinjaji nawakusanyaji wa ngozi katika Halmashauri zote nchini. Wadauwameandaa rasimu ya Katiba ya uendeshaji wa chamachao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2013/2014,Wizara itaendelea kutekeleza Mkakati wa Kufufua naKuendeleza Sekta na Viwanda vya Ngozi katika Halmashauri75 ikijumuisha 10 zilizoongezwa mwaka huu kwa kufanyayafuatayo:-

(i) Kuandaa na kusimamia taratibu zakuhakikisha kuwa ngozi zote zinazozalishwa machinjionizinafikishwa viwandani kwa ajili ya kusindikwa hapa nchini;

(ii) Kujenga vituo sita vya kutolea mafunzo yauendelezaji wa zao la ngozi katika Halmashauri za KahamaMji, Mpwapwa, Sengerema, Tarime, Urambo na Jiji la Mbeya;

Page 67: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

66

(iii) Kutoa mafunzo kwa wadau kuhusu uzalishaji,uhifadhi na usindikaji wa ngozi unaozingatia hifadhi yamazingira; na

(iv) Kuimarisha Chama cha Wazalishaji wa Ngozinchini kwa kukipatia utaalam ili kisimamie vyema maslahiya wazalishaji wa ngozi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, matumizi ya rasilimali za ardhi,maji na malisho kwa mifugo na utatuzi wa migogoro. Wizaraimeendelea kuzihimiza Halmashauri kutenga na kuendelezamaeneo ya malisho kwa ajili ya mifugo kwa lengo la kuipatiamifugo malisho na kuepusha migogoro ya mara kwa marakati ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi. Aidha,Wizara imeendelea kuzielekeza Halmashauri kufanya tathminiya uwezo wa ardhi katika maeneo yao kwa kuzingatia Sheriaya Maeneo ya Malisho na Rasilimali za Vyakula vya WanyamaSura180 ili kuwezesha kufuga kulingana na uwezo wa eneo.Hadi sasa, jumla ya vijiji 781 vimepimwa na kati ya hivyo, vijiji479 vimeainisha maeneo ya malisho katika Halmashauri zaWilaya 69 katika Mikoa 21 na hivyo kufanya jumla ya maeneoyaliyotengwa kwa ufugaji kufikia hekta milioni 1.28.

Mheshimiwa Mwenyekiti, matukio ya hivi karibuni yawafugaji kuingiza mifugo katika Pori la Akiba la Burigi, Msituwa Hifadhi wa Biharamulo, Msitu wa Hifadhi wa Geita naMsitu wa Hifadhi wa Bukombe na Hifadhi ya Wanyamaporiya Maswa na katika maeneo mengine ambao mifugo yaoiliathirika, yametokana na wafugaji kukosa malisho yakutosha hususan wakati wa kiangazi. Nachukua nafasi hiikutoa pole kwa wafugaji wote walioathirika kwa namnamoja au nyingine kutokana na matukio hayo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea kulifuatiliasuala hili na inaahidi kuwachukulia hatua za kisheriawatakaobainika kusababisha usumbufu na athari hizo.Aidha, Serikali inaendelea kuzihimiza Halmashauri kutengamaeneo ya malisho kwa ajil i ya ufugaji na wafugajiwanashauriwa kufuga kwa kuzingatia Sheria ya Maeneo yaMalisho na Vyakula vya Mifugo Sura 180 inayoelekeza kufuga

Page 68: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

67

idadi ya mifugo kulingana na uwezo wa malisho na hivyokupunguza tatizo la wafugaji kuhamahama linalosababishamigogoro kati ya wafugaji na watumiaji wengine warasilimali za ardhi na maji na uharibifu wa mazingira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara imeendelea kuimarishamiundombinu katika mashamba ya kuzalisha mbegu boraza malisho ya Vikuge (Kibaha), Sao Hill (Mufindi), Langwira(Mbeya), Mabuki (Misungwi) na Kizota (Dodoma) ili kuwezeshaupatikanaji wa mbegu bora za malisho. Katika mwaka 2012/2013, jumla ya tani 48 za mbegu bora za aina mbalimbali namarobota 497,611 ya hei yamezalishwa katika mashambahayo na taasisi nyingine za umma. Aidha, sekta binafsiimeendelea kuhamasishwa kuwekeza katika uzalishaji wa heiambapo jumla ya marobota 421,000 yamezalishwa. Pia,sekta binafsi imeendelea kuwekeza katika usindikaji wavyakula vya mifugo ambapo uzalishaji wa vyakula vyamifugo ulifikia tani 905,000 mwaka 2012/2013. Vilevile, Wizaraimefanya ukaguzi wa ubora wa vyakula vya mifugo katikaviwanda 15 vinavyosindika vyakula vya mifugo ili kuonakama vinakidhi viwango. Kaguzi hizo zilibaini upungufu waprotini na wanga na ushauri umetolewa ili kuondoa kasorohizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Mipango yaMaendeleo ya Kilimo ya Wilaya (DADPs) inayotekelezwa naHalmashauri iliwezesha ujenzi wa malambo mapya 25,ukarabati wa malambo tisa (9) na uchimbaji wa visima virefusaba (7). Aidha, elimu ya matumizi bora ya ardhi imetolewakwa watalaam 26 katika Halmashauri 12 za Igunga,Kalambo, Kaliua, Kakonko, Kasulu, Mlele, Mpanda, Nkasi,Sikonge, Sumbawanga, Urambo na Uyui.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2013/2014,Wizara itaendelea kuimarisha mashamba ya Langwira,Vikuge, Sao Hill, Mabuki, Kongwa, Kizota, Buhuri na Mivumonikwa kuyapatia vitendea kazi na kuhamasisha sekta binafsikuongeza uzalishaji wa mbegu bora za malisho. Aidha,Wizara itaendelea kusimamia uzalishaji na usindikaji wavyakula bora vya mifugo nchini katika viwanda 80 vilivyopo

Page 69: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

68

na vingine vitakavyojengwa na kuwajengea uwezowakaguzi 45 wa vyakula vya mifugo. Vilevile, Wizara itatoamafunzo kwa wataalam 30 kuhusu usimamizi na matumiziya maeneo ya malisho kutoka Halmashauri za Chunya, Ileje,Iringa, Kalambo, Kilolo, Mbarali, Mbozi, Momba, Nkasi naSumbawanga ikiwa ni baadhi ya maeneo ambayo wafugajiwanahamia na kufikisha idadi ya watalaam 51 kutoka jumlaya Halmashauri 23.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utoaji wa Kifuta Machozi kwawafugaji. Zoezi la kutoa kifuta machozi kwa wafugajiwaliopoteza mifugo yao yote katika Wilaya za Longido (kaya2,852), Monduli (kaya 1,484) na Ngorongoro (kaya 1,791)kutokana na ukame uliotokea mwaka 2008/2009 linaendeleakutekelezwa kulingana na upatikanaji wa fedha. Mpangohuu unatarajiwa kusambaza ng’ombe katika Wilaya zaLongido (14,260), Monduli (7,420) na Ngorongoro (8,508)zitakazogharimu jumla ya shilingi 12,109, 900,000. Hadi sasa,jumla ya ng’ombe 6,933 na mbuzi 1,740 wenye thamani yashilingi 2,945,916,000 wamegawiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti,, udhibiti wa magonjwa yamifugo. Maeneo huru ya magonjwa ya mifugo. Katikamwaka 2012/2013, Serikali imeendelea kujenga uwezo katikamaeneo yaliyoainishwa kuwa huru na magonjwa ya mlipukoya mifugo ya Sumbawanga na Nkasi kwa kutoa mafunzokwa wadau na kuanzisha Kituo cha Uchunguzi wa Magonjwaya Mifugo Sumbawanga. Pia, uchunguzi wa sampuli 93 zanyati katika Hifadhi za Ruaha, Mikumi, Mkomazi na 155 zang’ombe kwenye maeneo yanayozunguka hifadhi hizoulifanyika na uchunguzi wa kubaini aina ya virusi vya ugonjwawa Miguu na Midomo unaendelea. Katika mwaka 2013/2014,Wizara itaendelea kutekeleza Mkakati wa Kuzuia Ugonjwawa Miguu na Midomo (FMD) katika maeneo mbalimbalinchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, magonjwa ya mlipuko.Katika mwaka 2012/2013, Wizara kupitia Mradi wa KuimarishaUwezo wa Kudhibiti Magonjwa ya Mlipuko ya Mifugounaotekelezwa katika nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini

Page 70: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

69

mwa Afrika imewezesha mafunzo ya uzamili kwa wataalam25 na 90 wamepata mafunzo ya muda mfupi. Aidha, vifaambalimbali ikiwa ni pamoja na mashine za “Fume hood naLympholysing machine” kwa ajili ya maabara ya kisasa Bio-Security Level 3 ya mifugo Temeke vimenunuliwa. Kazi nyinginezilizofanyika ni pamoja na kuandaa Mpango Mkakati waKudhibiti Ugonjwa wa Miguu na Midomo nchini, kuunganishavituo sita vya uchunguzi wa magonjwa ya mifugo kwenyemdahalisi (internet) na kuvipatia kompyuta 11.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2013/2014,Wizara itaendelea kugharimia mafunzo ya wataalam,ununuzi wa vitenganishi (reagents and diagnostic kits) nakuendeleza uchunguzi wa Ugonjwa wa Miguu na Midomokwenye nyati na wanyama wafugwao nchini. Aidha,uchunguzi wa magonjwa ya mlipuko utaendelea kwenyeng’ombe, mbuzi, kondoo na nguruwe katika maeneombalimbali nchini ili kubaini aina ya virusi na chanjoitakayosaidia kudhibiti ugonjwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2012/2013,Wizara imeendelea kufuatilia mwenendo wa Ugonjwa waMafua Makali ya Ndege (HPAI), ambapo hadi sasa ugonjwahuo haujatokea nchini. Aidha, Wizara kwa kushirikiana naOfisi ya Waziri Mkuu imeandaa na kuchapisha nakala 1,000za Mpango wa Tahadhari ya Mafua Makali ya Ndege waMiaka Mitano (2012 – 2017) kwa ajili ya kusambazwa kwawadau. Vilevile, Wizara imesambaza dozi milioni 5.4 zachanjo ya Mdondo kwa lengo la kuendelea kudhibitiugonjwa hatari wa Mdondo wa kuku.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2013/2014,Wizara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali itaendeleakufuatilia mwenendo wa Ugonjwa wa Mafua Makali yaNdege na kudhibiti Mdondo na Homa ya Nguruwe pamojana kukamilisha mikakati ya udhibiti wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2012/2013,Wizara imeendelea kudhibiti Ugonjwa wa Homa ya Mapafuya ng’ombe nchini kwa kununua chanjo dozi 300,000

Page 71: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

70

ambazo zimewezesha kuchanja ng’ombe 285,000 katikaWilaya za Kiteto, Iringa, Kilindi, Nkasi na katika mashambaya Kampuni ya Ranchi za Taifa. Katika mwaka 2013/2014,Wizara itanunua chanjo dozi milioni tano (5) kupitia mradiwa “SADC–TADs” kwa ajili ya kuendeleza uchanjaji katikaMikoa ya Kagera na Shinyanga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ugonjwa wa Sotoka yambuzi na kondoo umeendelea kudhibitiwa kwa kutoa chanjokatika Mikoa ya Arusha, Mtwara, Morogoro, Singida, Tanga,Rukwa na Mara. Katika mwaka 2012/2013, Wizara kwakushirikiana na FAO imesambaza dozi 400,000 za chanjokatika Mikoa ya Arusha, Singida na Tanga. Aidha, Wizara kwakushirikiana na FAO - ECTAD Nairobi imeandaa na kutekelezaMkakati wa Kudhibiti Mlipuko wa Ugonjwa wa Sotoka yaMbuzi na Kondoo. Katika mwaka 2013/2014, Serikaliitaendelea kuratibu na kusimamia kampeni za chanjo katikaMikoa ya Arusha, Mara, Tanga na Tabora.

Mheshimiwa Mwenyekiti, magonjwa yanayoenezwana kupe. Katika mwaka 2012/2013, Wizara kwa kushirikianana Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI, imeendelea kudhibitimagonjwa yanayoenezwa na kupe kwa kukarabati majosho20 na kujenga majosho mapya 14 kupitia DADPs. Aidha,Wizara imeendelea kutoa ruzuku ya asilimia 40 kwa dawaza kuogesha mifugo ambapo lita 92,323 zenye thamani yashilingi bilioni 1.5 zilinunuliwa na kusambazwa katika Mikoayote nchini. Vilevile, Wizara kwa kushirikiana na sekta binafsiilichanja ng’ombe 140,438 dhidi ya Ndigana kali katika Mikoaya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Kagera, Katavi,Kigoma, Kilimanjaro, Manyara, Mbeya, Morogoro, Mtwara,Pwani, Rukwa, Singida na Tanga. Katika mwaka 2013/2014,Wizara itaendelea kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu -TAMISEMI na wadau mbalimbali katika kudhibiti kupe namagonjwa wayaenezayo kupitia ujenzi wa majosho mapya,ukarabati wa majosho, matumizi sahihi ya dawa za ruzukuna kuhamasisha matumizi ya chanjo dhidi ya Ndigana kali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mbung’o na nagana. Katikamwaka 2012/2013, Wizara imeendelea kutekeleza Mkakati

Page 72: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

71

wa Kudhibiti Mbung’o na Nagana kwa kutekeleza kazizifuatazo:-

(i) Kukamilisha uchunguzi wa mtawanyiko wambung’o nchini ambapo matokeo yameonesha eneolinalokaliwa na mbung’o ni hekta 30,931,957.6 sawa naasilimia 32.8 ya eneo la nchi nzima

(ii) Kutega vyambo 9,286 vyenye viuatilifu aina yapareto na kusambaza mitego 32, mabomba ya mkono 64,viuatilifu aina ya pareto lita 24, mabango 2,000 na vipeperushi7,500 katika Wilaya za Urambo, Uvinza, Bagamoyo, Handeni,Pangani, Kisarawe, Mpanda na Mbulu; na

(iii) Kujenga uwezo wa wataalam 18, watatu kwakila Wilaya za Kilombero, Kondoa, Manyoni, Mbulu,Nanyumbu na Ulanga walijengewa uwezo wa mbinu shirikishiza udhibiti wa mbung’o na Nagana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2013/2014,Wizara kwa kushirikiana na wadau itaendelea kudhibitiMbung’o na Nagana katika Halmashauri za Kibondo, Kasulu,Meatu, Maswa, Karatu, Kiteto, Ngorongoro na Serengeti.Aidha, itanunua na kusambaza vitambaa vya vyambo mita50,000, mitego 500 na viuatilifu vya pareto lita 110 katikaHalmashauri za Ngorongoro, Kiteto, Mpanda, Nkasi, Kaliuana Uvinza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, magonjwa ya mifugoyanayoambukiza binadamu, kichaa cha mbwa. Katikamwaka 2012/2013, Wizara kwa kushirikiana na Wizara ya Afyana Ustawi wa Jamii, Taasisi ya Bill & Melinda Gates Foundationchini ya Uratibu wa Shirika la Afya Duniani imeendeleakutekeleza Mradi wa Kutokomeza Kichaa cha Mbwa katikaMikoa ya Dar es Salaam, Lindi, Morogoro, Mtwara na Pwani.Kupitia mradi huo, dozi 200,000 za chanjo zimenunuliwa nakusambazwa ambapo jumla ya mbwa 189,890 na paka 9,160walichanjwa. Katika mwaka 2013/2014, Wizara kwakushirikiana na Halmashauri pamoja na sekta binafsi

Page 73: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

72

itaendelea kudhibiti Kichaa cha Mbwa kwa kununua dozi250,000 za chanjo dhidi ya ugonjwa huo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, homa ya Bonde la Ufa,katika mwaka 2012/2013, jumla ya dozi 400,000 zilinunuliwana kusambazwa katika Halmashauri za Longido,Ngorongoro, Babati, Handeni, Mkuranga, Karagwe, Ngara,Geita, Chamwino, Bahi na Mpwapwa. Aidha, Wizara kwakushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imeandaana kusambaza nakala 1,000 za Mkakati wa kudhibiti Ugonjwawa Homa ya Bonde la Ufa wa Miaka Mitano (2007/2008 –2012/2013). Katika mwaka 2013/2014, Wizara itaendeleakuhamasisha udhibiti wa ugonjwa huo ikiwa ni pamoja nakununua chanjo dozi 100,000.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ugonjwa wa kutupa mimbana kifua kikuu, katika mwaka 2012/2013, Wizara iliendeleakupima kiwango cha maambukizi ya Ugonjwa wa KutupaMimba (Brucellosis) ambapo sampuli 2,910 (ng’ombe 2,856na mbuzi 54) kutoka Wilaya za Kiteto, Manyoni, Singida,Iramba, Kondoa, Urambo, Mbeya, Iringa, Lushoto, Muheza,Mufindi na Nanyumbu zilipimwa. Jumla ya ng’ombe 69waligundulika kuwa na maambukizi na kuchinjwa chini yausimamizi. Vile vile, sampuli 1,403 za ng’ombe kutoka Wilayaza Iramba, Manyoni, Singida, Mbeya, Mufindi na Iringazilipimwa ambapo sampuli tano zilibainika kuwa na vimeleavya Kifua Kikuu cha ng’ombe na kuteketezwa. Pia, wataalam6 walipata mafunzo ya muda mfupi ya udhibiti wamagonjwa hayo. Katika mwaka 2013/2014, Wizara kwakushirikiana na wadau mbalimbali itaendelea kupimakiwango cha maambukizi ya magonjwa ya Kutupa Mimbana Kifua Kikuu cha ng’ombe nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukaguzi wa mifugo namazao yake, Wizara kwa kushirikiana na Halmashauriimeendelea kufanya ukaguzi wa mifugo na mazao yake ilikudhibiti kuenea kwa magonjwa na kulinda afya ya walaji.Katika mwaka 2012/2013 jumla ya ng’ombe milioni 1.85,mbuzi 870,150, kondoo 216,304, kuku milioni 4.2 na nguruwe144,260 walikaguliwa katika machinjio mbalimbali. Aidha,

Page 74: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

73

wakaguzi 60 walipata mafunzo ya matumizi ya teknonojiaya kalamu ya dijitali na udhibiti wa ubora wa ngozi na nyamakutoka Halmashauri 23 katika Mikoa ya Arusha, Kagera,Kigoma, Kilimanjaro, Mara, Mbeya, Mtwara na Rukwa. Katikamwaka 2013/2014, Wizara itaendelea kufanya ukaguzi wamifugo na mazao yake nchini ili kudhibiti kuenea kwamagonjwa, kulinda afya ya walaji na kukuza soko la mazaoya mifugo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utambuzi, usajili na ufuatiliajiwa mifugo. Katika mwaka 2012/2013, Wizara imeendeleakuimarisha Mfumo wa Utambuzi na Ufuatiliaji wa Mifugo kwakutoa mafunzo kuhusu Sheria ya Utambuzi, Usajili na Ufuatiliajiwa Mifugo Sura 184 na Kanuni zake kwa wataalam 20 kutokaHalmashauri za Bagamoyo, Handeni, Lushoto, Mbeya,Mvomero, Njombe na Rungwe. Aidha, kupitia ufadhili waFAO ujenzi wa mfumo wa kielektroniki wa Utambuzi naUfuatiliaji Mifugo unaendelea. Pia, Wizara imenunua vifaavya utambuzi ikiwa ni pamoja na tufe za tumboni 5,000 nahereni 5,000. Vilevile, wafugaji 2,428 walisajiliwa na ng’ombe50,534 walipigwa chapa ya moto kuwatambua katika Wilayaya Kilombero.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2013/2014,Wizara itaendelea kuratibu utekelezaji wa Mfumo waUtambuzi, Usajili na Ufuatiliaji wa mifugo katika Halmashauri.Pia, Wizara itatoa mafunzo kwa wataalam 100 nakuhamasisha umma kuhusu mfumo huu. Vilevile, Wizaraitakamilisha ujenzi wa mfumo wa utambuzi na kushirikianana Halmashauri kufanya utambuzi wa ng’ombe 50,000.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uendelezaji wa sekta yauvuvi. Uvuvi wa samaki na uuzaji wa mazao ya uvuvi. Wizarakwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeendelea kuratibuna kusimamia uvunaji na matumizi endelevu ya rasilimali zauvuvi nchini. Katika mwaka 2012/2013, idadi ya wavuvi ilikuwa182,741 na vyombo vya uvuvi 56,985. Nguvu hii ya uvuviimewezesha kuvunwa tani 365,023.38 za mazao ya uvuviyenye thamani ya shilingi trilioni 1.3. Aidha, Wizara imeendelea

Page 75: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

74

kuratibu na kusimamia uuzaji wa samaki na mazao ya uvuvinje ya nchi ambapo jumla ya leseni 97 za kuuza nje ya nchisamaki na mazao ya uvuvi zimetolewa na tani 41,394.3 zamazao ya uvuvi na samaki hai wa mapambo 45,550 wenyethamani ya shilingi bilioni 254.9 waliuzwa nje ya nchi nakuiingizia Serikali mapato ya shilingi bilioni 6.8. Vilevile, Wizarakwa kushirikiana na FAO imekamilisha kuandaa Mpango waUsimamizi wa Samaki wanaopatikana katika Tabaka la Juula Maji (Pelagic Fisheries Management Plan) ili kuwa na uvuviendelevu wa samaki wanaopatikana katika tabaka hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2013/2014,Wizara itaendelea kusimamia uvunaji na matumizi endelevuya rasilimali za uvuvi na kuhamasisha wadau kuwekezakatika maeneo mbalimbali ya uvuvi yakiwemo ujenzi wa botibora za uvuvi na viwanda vya uvuvi ili kuongeza uzalishajina thamani kwenye mazao ya uvuvi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uwezeshaji wavuvi wadogo.Wizara imeendelea kuwawezesha wavuvi wadogo kwakuboresha miundombinu ya uvuvi. Katika mwaka 2012/2013,ujenzi wa mialo ya Kibirizi (Kigoma Ujiji), Muyobozi (Uvinza),Ikola (Mpanda) na Kirango (Nkasi) katika Ukanda wa ZiwaTanganyika umeanza. Aidha, ujenzi wa boma la karakanaya kutengeneza boti ya Mbamba Bay umekamilika. Pia,Wizara imesambaza nakala 595 za kitabu cha Kanuni Boraza Uvuvi na Ufugaji wa Samaki na vipeperushi 700 nakuhamasisha uanzishaji wa Vyama 23 vya Msingi vya Ushirikawa Wavuvi katika Mkoa wa Mwanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara kupitia Mradi waMACEMP uliokamilika Mwezi Februari, 2013, inakamilisha ujenziwa ghala la mwani katika kijiji cha Jibondo Mafia; ujenzi wamialo ya Nyamisati (Rufiji), Kilwa-Masoko na Kilindoni (Mafia)na kuweka mitambo ya barafu na majokofu kwa ajili yakuhifadhi mazao ya uvuvi; imeandaa filamu ya tathmini yakazi zilizofanywa na Mradi wa MACEMP; kukamilisha ununuziwa maboya 63 ya kuweka mipaka ya Hifadhi za Bahari ya

Page 76: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

75

Mafia, Ghuba ya Mnazi na Maingilio ya Mto Ruvuma naMaeneo Tengefu ya Dar es Salaam na Maziwe (Pangani).Aidha, Wizara imepokea taarifa ya uchunguzi kuhusumtandao wa vyanzo, usambazaji na masoko ya mabomuyanayotumika katika uvuvi haramu na madhara yake katikamaeneo ya mradi na inaifanyia kazi kwa kushirikiana navyombo husika. Baada ya MACEMP kukamilika, mradi mpyaunaandaliwa wa Southwest Indian Ocean FisheriesGovernance and Shared Growth Programme -SWIOFish chiniya ufadhili wa Benki ya Dunia ambao utatekelezwa kuanziamwaka 2014/2015 katika nchi za Afrika zinazopakana naKusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2013/2014,Wizara itakamilisha ujenzi wa karakana ya kutengeneza botiya Mbamba Bay na itaendelea kuhamasisha wavuvi wadogokuanzisha vyama vya ushirika na SACCOS; na kutoa elimukuhusu fursa za uwekezaji na matumizi endelevu ya rasilimaliza uvuvi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukuzaji wa viumbe kwenyemaji. Wizara imeendelea kuratibu shughuli za ukuzaji waviumbe kwenye maji kwa lengo la kuongeza upatikanaji wasamaki, ajira na kipato kwa wananchi. Katika mwaka 2012/2013, vituo vya kuzalisha vifaranga vya samaki wa maji baridivya Kingolwira (Morogoro), Luhira (Songea), Mtama (Lindi),Nyamirembe (Chato) na Mwamapuli (Igunga) vimeimarishwakwa kupewa wataalam na vitendea kazi. Katika mwaka2013/2014, Wizara itaendelea kujenga na kuimarisha vituovya ukuzaji wa viumbe kwenye maji vya Chongoleani (Tanga),Nyamirembe (Chato), Mbegani, Kingolwira, Ruhila (Songea),Mtama, Bukoba, Mwanza, Musoma na Karanga (Moshi) nakuanzisha vituo vipya vya Chihiko (Mtwara), Mwamapuli(Igunga) na Kibirizi (Kigoma) kwa lengo la kuongezaupatikanaji wa vifaranga kwa wafugaji wa samaki nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2012/2013,katika kusambaza teknolojia ya kufuga viumbe kwenye maji,Wizara kwa kushirikiana na sekta binafsi imetoa mafunzo kwawadau 1,547 kuhusu ufugaji wa samaki na kuwezesha

Page 77: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

76

kuanzishwa kwa vikundi 64 vya ukuzaji viumbe kwenye maji.Aidha, vifaranga 2,066,620 aina ya perege vimezalishwa nakusambazwa kwa wadau. Pia, Kampuni ya Alphakrust iliyopoMafia imezalisha na kusambaza vifaranga 11,520,000 vyakambamiti na imevuna tani 270 za kambamiti zenye thamaniya shilingi bilioni 2.16. Tani 384.75 za mwani zenye thamani yashilingi 153,900,000/= zimevunwa na wakulima wa mwani nakuuzwa nje ya nchi. Vilevile, Kikundi cha Msichoke katikaWilaya ya Bagamoyo kimetengeneza na kuuza miche 4,500ya sabuni za mwani na kikundi cha Mngoji katika Wilaya yaMtwara kimekuza na kuvuna vipande 762 vya lulu nakutengeneza jozi 120 za hereni. Vilevile, jumla ya mabwawa696 ya kufugia samaki yamechimbwa na kupandikizwasamaki katika Halmashauri mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2013/2014,Wizara kwa kushirikiana na Halmashauri itaendeleakuhamasisha wananchi kuhusu ukuzaji viumbe kwenye majikwa kutoa elimu, kuzalisha na kusambaza vifaranga vyasamaki milioni 10 pamoja na uongezaji thamani ya mazaoyakuzwayo kwenye maji. Baadhi ya vifaranga hivyovitapandikizwa kwenye mabwawa ya asili ya Bulenya(Igunga), Nara (Kilosa) na Msenda (Namtumbo). Aidha,maafisa ugani 40 watapatiwa mafunzo ya ukuzaji wa viumbekwenye maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utafiti, mafunzo na ugani wamifugo na uvuvi. Wizara imeendelea kusimamia nakuwezesha Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) naTaasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI); Wakala wa Elimuna Mafunzo ya Uvuvi (FETA), Wakala wa Vyuo vya Mafunzoya Mifugo (LITA) na Wakala wa Maabara ya Mifugo Tanzania(TVLA) ili ziweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Taasisi ya Utafiti wa MifugoTanzania (TALIRI). Naomba kuliarifu Bunge lako Tukufukwamba uanzishwaji wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzaniaumekamilika chini ya Sheria Na. 4 ya mwaka 2012 na Taasisi

Page 78: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

77

imeanza kutekeleza majukumu yake. Katika mwaka 2012/2013, Wizara imeendelea kuimarisha vituo vya utafiti vyaTALIRI vya Kongwa, Mabuki, Mpwapwa, Naliendele, Tanga,Uyole na West Kilimanjaro kwa kuvipatia vitendea kazi nakukarabati miundombinu. Aidha, Taasisi imeendeleakutekeleza miradi ya utafiti wa mifugo ya kuboresha uzalishajiwa ng’ombe wa nyama na maziwa, nguruwe; kuku, malishona masoko ya mazao ya mifugo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa lengo la kuhifadhikoosafu za asili, katika mwaka 2012/2013, Taasisi imetathminina kusambaza mifugo yenye tija vijijini ambapo ng’ombe1,353 wa aina ya Mpwapwa na 339 aina ya Friesian na chotarawa ng’ombe hao waliendelea kufanyiwa utafiti nakusambazwa kwa wafugaji walioomba na kuuziwa katikaMikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Mbeya, Mwanza, Pwani,Singida na Tanga. Aidha, Taasisi imetathmini ng’ombe 20aina ya Maasai, mbuzi wa asili 1,136 aina za Buha, RedMaasai, Pare White, Red Sonjo, Newala na Gogo White; ainatatu za kondoo za Red Maasai, Dorper na Black Head Persian(BHP); nguruwe 48; kuku wa asili 1,278 aina za Kuchi,Sasamala, Kawaida, Mtewa, Kishingo, Bukini, Kisunzu, Kuza,Sukuma, Msumbiji, Katewa, Mandendenga na Njachama; navinasaba 200 vya malisho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tafiti kuhusu malisho yamifugo zimeendelea ambapo ekari 543 za majaribiozimepandwa malisho aina ya Rhodes na Nyakachimbu(Cenchrus ciliaris) na kuzalisha marobota 78,600 ya hei. Aidha,kilo 1,100 za mbegu za nyasi zimevunwa na kusambazwakwa wafugaji katika Mikoa ya Dodoma, Kagera, Mtwara naPwani na kilo 40 ziligawiwa kwa watafiti wa mifugo waSerikali ya Mapinduzi Zanzibar. Vilevile, jumla ya kilo 37 zambegu za mikunde na 65 za mabingobingo zilisambazwakwa wafugaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baadhi ya matokeo ya tafitihizo yameonesha ng’ombe jike chotara anayetokana nang’ombe dume aina ya Mpwapwa na jike aina ya Zebuameongeza uzalishaji wa maziwa kufikia lita sita (6)

Page 79: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

78

ikilinganishwa na uzalishaji wa lita moja (1) hadi mbili (2) kwasiku. Aidha, chotara jike anayetokana na kupandisha dumela Fresian na ng’ombe wa asili ameonesha uwezo wa kuzaamara ya kwanza katika umri mdogo wa miaka 2 -3ikilinganishwa na miaka 4 - 5 kwa Zebu. Matokeo hayoyamesambazwa kwa wafugaji 764 kupitia mafunzombalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2013/2014,Wizara itakamilisha kuandaa miundo ya utumishi, kanuni zafedha na utumishi na miongozo mbalimbali ya uendeshajiwa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania. Aidha, Taasisiitaendelea kutekeleza miradi ya utafiti wa mifugo yakuboresha uzalishaji wa ng’ombe wa nyama na maziwa;mbuzi, kondoo, nguruwe; kuku wa asili na malisho pamojana utafiti wa masoko ya mifugo na mazao ya mifugo. Vilevile,Taasisi itatathmini kosaafu ya ng’ombe wa asili aina yaSukuma; itasambaza madume 150 ya ng’ombe aina yaMpwapwa na mbuzi 120 aina ya Malya kwa wafugaji kwalengo la kuboresha mifugo ya asili; na kusambaza kilo 1,000za mbegu za nyasi na kilo 500 za mikunde. Pia, Taasisiitaendelea na ujenzi wa maabara za sayansi ya nyama(Mabuki), uhawilishaji kiinitete (embryo transfer) - Mpwapwa,teknolojia ya maziwa (Uyole), lishe ya mifugo (Mpwapwa,Tanga na West Kilimanjaro) pamoja na ujenzi na ukarabatiwa nyumba za watumishi na ofisi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Taasisi ya Utafiti UvuviTanzania (TAFIRI). Wizara imeendelea kujenga uwezo waTaasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) ili kuongeza tijakatika utafiti wa uvuvi. Katika mwaka 2012/2013, Taasisiimekarabati maabara na jengo la utawala la kituo chaKigoma; imefunga vifaa vya uvuvi na utafiti katika meli yaRV Kiboko inayotumika kwa utafiti katika Bahari ya Hindi;imejenga matenki ya kufanyia majaribio ya vyakula vyasamaki katika kituo cha TAFIRI Dar es Salaam; imesimika windmill ya kuvuta maji kutoka ziwani na kukarabati mabwawaya kufanyia utafiti katika kituo cha Mwanza. Pia, Taasisi

Page 80: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

79

imenunua vitendea kazi vikiwemo gari, kompyuta, Printerna vifaa vya utafiti kwa ajili ya kuboresha utafiti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2012/2013,Taasisi imeendelea kufanya tafiti i l i kubaini wingi namtawanyiko wa Potwe (whale shark) katika Bahari ya Hindina kutathmini uchumi-jamii wa samaki aina ya Jodari (Tuna)katika pwani ya Bahari ya Hindi kwa kushirikiana na WorldWide Fund for Nature (WWF). Aidha, Taasisi imefanya utafitikuhusu bioanuwai ya uvuvi katika Mto Ruvu, Mto Ruvumana Ziwa Rukwa na matokeo ya awali yanaonesha uwepowa bioanuwai kubwa. Pia, imefanya utafiti wa kutengenezavyakula vya samaki kwa kutumia malighafi zipatikanazokaribu na wafugaji katika vituo vya Kunduchi na Mwanza;kuzalisha mbegu bora za samaki kituo cha Kunduchi naMwanza; kufuga samaki kwa mfumo unaojumuisha samaki,kil imo cha mbogamboga na kuku huko Kingolwira-Morogoro; kupunguza uharibifu wa mazao ya samaki baadaya uvunaji kwa kutumia kifaa cha kukaushia samakikinachotumia mionzi ya jua kwenye Kituo cha Kyela.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2013/2014,TAFIRI kwa kushirikiana na wadau wengine itaendelea nautafiti wa samaki na mazingira katika maziwa makuu(Victoria, Tanganyika na Nyasa), maziwa madogo, mito naBahari ya Hindi; kufanya utafiti wa ufugaji samaki; kuimarishamiundombinu ya Taasisi kwa kujenga na kukarabati ofisi namaabara na kununua vitendea kazi kwa vituo vya Dar esSalaam, Sota (Rorya), Kyela na Mwanza. Aidha, Taasisiitasambaza taarifa za kitafiti kwa wadau mbalimbali wauvuvi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wakala wa Maabara yaVeterinari Tanzania (Tanzania Veterinary Laboratory Agency-TVLA). Wakala wa Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA)imeendelea na majukumu yake ya kufanya tafiti, uchunguzina utambuzi wa magonjwa ya mifugo. Katika mwaka 2012/2013, Wakala imezalisha na kusambaza dozi milioni 5.4 zachanjo ya Mdondo, dozi 77,500 za Kimeta na dozi 36,900 zaChambavu; imefanya uchunguzi wa sampuli 416 za vyakula

Page 81: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

80

vya mifugo ambapo sampuli 333 zilibainika kuwa naupungufu wa nguvu na protini; kuendelea kufuga mbung’o10,760 kwa ajili ya tafiti za teknolojia za kudhibiti mbung’ona ugonjwa wa Nagana katika Kituo cha Utafiti wa Mbung’ona Ndorobo Tanga; kufanya utambuzi wa magonjwa yawanyama kwa sampuli 10,800 kutoka kwa wafugaji na vituovya uchunguzi wa magonjwa ya mifugo ambapo sampuli8,600 zil ibainika kuwa na magonjwa mbalimbali; nakuanzisha kitengo cha cell culture katika maabara. Aidha,Wakala inaendelea kufanya tafiti za kudhibiti mbung’o nandorobo katika maeneo ya Mikoa ya Lindi, Pwani na Mtwaraambapo mbung’o aina ya Glossina morsitans morsitans naGlossina pallidipes wamepungua. Pia, Wakala imeendeleakutafiti chanjo ya I-2 ya kuzuia Mdondo katika maeneo yaRorya, Rufiji, Same na Singida; na kufanya tathmini zakimaabara kwa chanjo za Homa ya Bonde la Ufa, Homa yaMapafu ya Ng’ombe, Kimeta, Ugonjwa wa Kutupa Mimbana Ndui ya Kuku.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2013/2014,Wakala itaimarisha kitengo cha Cell culture kwa kuwekavifaa katika maabara; itaendeleza tathmini ya aina tatu zachanjo za magonjwa ya mifugo ya Homa ya Bonde la Ufa,Homa ya Mapafu ya Ng’ombe na Ndui ya Kuku ili ziwezekutumika. Aidha, Wakala itazalisha, kuuza na kusambazachanjo za Mdondo dozi milioni 100, Kimeta dozi 500,000,Chambavu dozi 500,000 na dozi 250,000 za Ugonjwa waKutupa Mimba. Pia, itafanya tafiti na kusambaza teknolojiambalimbali kwa ajili ya kutambua na kudhibiti magonjwaya Ndigana Kali, Nagana na Malale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wakala wa Elimu naMafunzo ya Uvuvi (Fisheries Education and Training Agency -FETA). Wizara imeendelea kuimarisha Wakala wa Elimu naMafunzo ya Uvuvi ili kukidhi mahitaji ya wataalam katika fanihiyo. Katika mwaka 2012/2013, Wakala imeongeza udahiliwa wanafunzi katika Kampasi za Nyegezi na Mbegani kufikia943 ikilinganishwa na 714 mwaka 2011/2012. Pia, imetoamafunzo ya muda mfupi kwa wanafunzi 272 wakiwemo 56kutoka nchi za SADC. Aidha, vyuo hivi vimeimarishwa kwa

Page 82: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

81

kupatiwa wataalam na vitendea kazi. Pia, ukarabati waKampasi ya Kigoma umekamilika na mafunzo tarajali kwawataalam wa ugani 20 kutoka kanda ya Ziwa Tanganyikayametolewa na maandalizi ya kuanzisha kozi zaastashahada katika Kampasi hiyo yanaendelea. Vilevile, Meliya MV Mafunzo imefanyiwa ukarabati mkubwa katikaChelezo cha Zanzibar na taratibu za kuanzisha Kampasi yaMikindani na Kituo cha Kurasini zinaendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2013/2014,Wizara itaendelea kuimarisha Wakala kwa kukarabatiKampasi za Mikindani na Kigoma; na Vituo vya MwanzaSouth na Kurasini na kuvipatia vifaa ili kuwezesha Wakalakudahili jumla ya wanachuo 1,500. Aidha, Wakala itaanzishavituo vipya vya Mbamba Bay na Gabimori (Rorya), kufanyatafiti tumika na kutoa huduma za ushauri zinazohusu uvuvina ufugaji wa viumbe majini. Pia, kuendelea kuzalisha chakulana vifaranga bora vya samaki wa aina mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wakala wa Vyuo vyaMafunzo ya Mifugo (Livestock Training Agency - LITA). Wizaraimeendelea kuimarisha Wakala wa Vyuo vya Mafunzo yaMifugo ili kutoa mafunzo katika ngazi ya Stashahada naAstashahada katika Kampasi zake za Tengeru, Mpwapwa,Morogoro, Madaba, Buhuri na Temeke. Katika mwaka 2012/2013 jumla ya wanafunzi 1,720 walidahiliwa na kati ya hao,689 wa mwaka wa pili watamaliza mafunzo yao mwezi Juni2013. Aidha, Wakala kwa kushirikiana na wadau imetoamafunzo ya ufugaji bora kwa wafugaji 118, watengenezajimitambo ya biogesi 22 na kilimo biashara kwa maafisa ugani30.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2012/2013,Wakala imeendelea kujiimarisha kwa kuongeza wataalamna vitendea kazi; kujenga, kukarabati majengo namiundombinu katika Kampasi zake na kuanzisha kituo chaMabuki. Aidha, Wakala imenunua ng’ombe bora 50 wamaziwa na kuboresha hekta 120 za malisho kwa ajili yamafunzo na kuongeza mapato.

Page 83: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

82

31 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2013/2014,Wakala itatoa mafunzo kwa wanafunzi 2,000 katika ngazi yaAstashahada na Stashahada na mafunzo ya muda mfupi kwawafugaji na wakulima; kujenga, kukarabati na kuzipatia vifaaKampasi na Makao Makuu ya LITA. Aidha, itaboreshauzalishaji wa mifugo na mazao ya kilimo katika Kampasi zake,kufanya tafiti na kutoa huduma za ushauri zinazohusu afyana uzalishaji wa mifugo. Aidha, Wakala itaanzisha kituo kipyacha Kikulula (Karagwe).

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2012/2013,Wizara kwa kushirikiana na Halmashauri iliendelea kupelekateknolojia za kisasa kwa kutoa mafunzo maalum kwa wafugaji2,140, wavuvi 1,789 na wagani 20. Pia, wafugaji 10 kutokaHalmashauri za Bagamoyo, Mvomero na Njombewalikwenda Naivasha - Kenya kwa ziara ya mafunzo ya wikimoja kupitia Programu ya Eastern Africa AgriculturalProductivity Programme (EAAPP). Wizara ilitayarisha nakurusha hewani vipindi 52 vya redio na 12 vya runingavilivyohusu ufugaji na uvuvi. Aidha, vipeperushi 7,000 kuhusuufugaji bora wa ng’ombe wa maziwa vimesambazwa kwawadau. Vilevile, Wizara imeendelea kukarabati vituo vyamafunzo ya wafugaji na wavuvi vya Gabimori na Kikulula.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2013/2014,Wizara itatayarisha na kurusha hewani vipindi 52 vya rediona 12 vya runinga. Aidha, itatoa mafunzo elekezi kwawataalam wa Halmashauri 25 kuhusu ushirikishwaji wa sektabinafsi katika ufugaji wa samaki na kuwezesha wataalam waugani 30 kuhudhuria mafunzo ya muda mfupi na mrefu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara imeendeleakusimamia ubora wa mazao ya mifugo na uvuvi pamoja nahuduma za kitaalam kupitia Bodi ya Nyama, Bodi ya Maziwana Baraza la Veterinari Tanzania, Kitengo cha Udhibiti waUbora na Usalama wa Mazao ya Uvuvi na Maabara ya Taifaya Udhibiti wa Ubora wa Mazao ya Uvuvi-Nyegezi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2012/2013,Wizara imeendelea kuimarisha Bodi ya Nyama Tanzania kwa

Page 84: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

83

31 MEI, 2013

kuipatia wataalam na vitendea kazi. Aidha, Bodi imeendeleakutoa elimu kwa wadau kuhusu Sheria ya Nyama, Sura ya421 na kusambaza nakala 1,200 za vipeperushi vya tafsiri yasheria hiyo. Pia, Bodi imetekeleza mfumo wa ubia wakiushindani ambapo wadau 297 wa mnyororo wa thamaniwa nyama ya kuku katika Mkoa wa Dar es Salaamwametambuliwa. Vilevile, Bodi imeandaa mwongozo wausajili wa wadau wa tasnia ya nyama, imeandaa MpangoMkakati wa Bodi wa miaka mitano (2013/14 – 2017/18) nakuwawezesha Wajumbe wa Bodi kupata mafunzo kuhusuUtawala Bora. Aidha, Bodi kwa kushirikiana na Mamlaka zaSerikali za Mitaa za Kanda ya Ziwa imewezesha kuanzishwana kusajiliwa kwa Chama cha Wafugaji Kanda ya Ziwa(CHAWAKAZI).

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2013/2014,Wizara itaendelea kuiimarisha na kuiwezesha Bodi ya Nyamakwa kuipatia wataalam na vitendea kazi ili iweze kutekelezamajukumu yake. Aidha, Bodi itasajili wadau 200 wa tasnia yanyama na vyama vyao; kuendelea kuhamasisha utekelezajiwa Sheria ya Nyama, Sura ya 421 na kusimamia ubora wanyama na bidhaa zake. Pia, itahamasisha na kuwezeshauundaji wa Chama cha Wafugaji Kitaifa na kuimarishaVyama vya Wadau vya Wafanyabiashara wa Mifugo naNyama Tanzania (TALIMETA) na Chama cha Wasindikaji waNyama Tanzania (TAMEPA).

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara imeendeleakuimarisha Bodi ya Maziwa kwa kuipatia wataalam navitendea kazi ili iweze kutekeleza majukumu yake. Katikamwaka 2012/2013, Bodi imetoa elimu kwa wadau 400 ilikutekeleza Sheria ya Maziwa Sura 262 na Kanuni zake katikamikoa ya Iringa, Mbeya, Morogoro, Rukwa na Ruvuma. Aidha,Bodi imeratibu Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Unywaji waMaziwa Shuleni Duniani yaliyofanyika Njombe Mjini na Wikiya Maziwa iliyofanyika katika Manispaa ya Moshi. Vilevile, Bodiimeandaa Taratibu za Ukaguzi wa Maziwa (Code of MilkHygiene); na kuwezesha mafunzo kwa watumishi tisa wa Bodikuhusu taratibu na kanuni za utumishi wa umma. Pia, Bodiimeendelea kuratibu Programu ya Unywaji wa Maziwa Shuleni

Page 85: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

84

31 MEI, 2013

ambapo wanafunzi 66,528 kutoka shule 144 wamenufaikana mpango huo .

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2013/2014,Wizara itaendelea kuiimarisha Bodi ya Maziwa kwa kuipatiawataalam na vitendea kazi ili iweze kutekeleza majukumuyake. Aidha, itaimarisha ukaguzi wa maziwa kwa kuteua nakuwajengea uwezo wakaguzi wa maziwa; kuanzisha mfumowa takwimu; kuendelea kuhamasisha Mamlaka za Serikali zaMitaa kutekeleza Mpango wa Unywaji wa Maziwa Shuleni;na kuratibu Maadhimisho ya Wiki ya Maziwa yatakayofanyikakitaifa katika Manispaa ya Musoma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Baraza la Veterinarilimeendelea kusimamia viwango na kuandaa miongozo juuya utoaji huduma za mifugo nchini. Katika mwaka 2012/2013,Baraza limesajili Madaktari wa Mifugo 21; vituo vya huduma62; kuorodhesha na kuandikisha wataalam wasaidizi 227;kutoa leseni kwa wakaguzi wa nyama 27, wahimilishaji 18 nafundi sanifu wa maabara 13. Aidha, Baraza limetoa mafunzokwa wataalam 198 na wadau 124 na limekagua vituo vyahuduma za mifugo 201 katika Halmashauri za Mikoa yaArusha, Dar es Salaam, Geita, Iringa, Kagera, Kilimanjaro,Mbeya, Mwanza, Njombe, Ruvuma, Shinyanga na Simiyuambapo vituo 51 vilifungwa na kuelekezwa maboresho. Pia,Baraza kwa kushirikiana na NACTE limehakiki matumizi yamitaala ya Astashahada na Stashahada ya Afya na UzalishajiMifugo katika vyuo 11 vikiwemo 4 vya sekta binafsi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2013/2014,Baraza litasajili madaktari wa mifugo 30, kuandikisha,kuorodhesha na kuwapatia miongozo wataalam 700 nakusajili vituo vya huduma za mifugo 350. Vilevile, Baraza litatoaleseni kwa wakaguzi wa nyama 50, wahimilishaji 40 namafundi sanifu wa maabara 20; kuhakiki viwango vyataaluma ya veterinari katika vyuo 10 na makampuni 30yanayotoa huduma za mifugo. Aidha, Baraza litaratibu Sikuya Veterinari Duniani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara imeendelea kuhakiki

Page 86: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

85

31 MEI, 2013

viwango vya ubora na usalama wa mazao ya uvuvi kwenyeviwanda vya kuchakata mazao ya uvuvi na maghala yakuhifadhi mazao ya uvuvi. Katika mwaka 2012/2013, wadau40 walioteuliwa na Halmashauri kutoka Mikoa ya Dar esSalaam, Kagera, Kigoma, Mbeya, Mwanza, Pwani na Tanga,wamehamasishwa kuwekeza kwenye viwanda vya uvuviambapo viwanda vya kuchakata mazao ya uvuvivimeongezeka kutoka 34 mwaka 2011/2012 hadi 43 mwaka2012/2013. Aidha, kaguzi 618 za viwanda na maghala yakuhifadhi mazao ya uvuvi na 1,979 za kuhakiki ubora nausalama wa samaki na mazao yake kabla ya kusafirishwakwenye masoko ya nje ya nchi zilifanyika. Matokeo ya kaguzihizo yalionesha kukidhi viwango vya ubora. Pia, Wizara imetoamafunzo kuhusu matumizi ya teknolojia sahihi ya uandaaji,uchakataji na uhifadhi wa samaki na mazao yake kwawadau wa uvuvi 331 na wakaguzi 34 katika ukanda wa ZiwaVictoria, Ziwa Tanganyika na Ukanda wa Pwani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2013/2014,Wizara itafanya kaguzi 3,600 za kuhakiki ubora na viwangokwenye viwanda vya kuchakata na maghala ya kuhifadhimazao ya uvuvi. Aidha, itaendelea kuhamasisha sekta binafsikuwekeza kwenye ujenzi wa viwanda vya kuchakata nakuhifadhi mazao ya uvuvi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara kwa kushirikiana naHalmashauri imeendelea kuratibu miundombinu ya masokoya uvuvi kwa kufanya kaguzi 195 kwenye masoko makubwaya Samaki ya Magogoni - Dar es Salaam, Kirumba - Mwanzana masoko madogo katika maeneo ya mijini na katika mialoya Ziwa Victoria, Tanganyika, Rukwa na Nyasa, maziwamadogo na mito. Aidha, masoko matatu ya samakiyamejengwa katika Halmashauri za Babati, Iringa na Kyelakupitia DADPs.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2013/2014,Wizara itaendelea kuratibu usafi wa masoko na mialo nakuhimiza uhifadhi bora wa mazao ya uvuvi ili kukidhi mahitajiya soko la ndani na nje ya nchi.

Page 87: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

86

31 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2012/2013,Wizara imeendelea kuimarisha Maabara ya Taifa ya Udhibitiwa Ubora wa Mazao ya Uvuvi - Nyegezi kwa kuipatiavitenganishi (reagents) na kutoa mafunzo kwa wataalam wamaabara na kukamilisha uandaaji wa miongozo yauendeshaji. Aidha, Wizara imeandaa taratibu za awali zakupata ithibati ya uchunguzi wa kemikali, imechunguzasampuli 1,474 ili kuhakiki ubora na usalama wa mazao ya uvuvina imechunguza sampuli 1,135 za samaki, maji, vyakula vyasamaki na udongo. Pia, Maabara ya Viuatilifu ya Dar esSalaam imeimarishwa kwa kuipatia vitenganishi na vituo vyaukaguzi wa ubora na usalama wa mazao ya uvuvi vyaBukoba, Dar es Salaam, Kigoma, Kilwa, Mafia, Musoma,Mwanza na Tanga vimeimarishwa kwa kuvipatia wataalamna vitendea kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2013/2014,Wizara itaendelea kuimarisha na kuwezesha Maabara yaSamaki – Nyegezi, Maabara ya Viuatilifu ya Dar es Salaamna vituo vya ukaguzi pamoja na kufanya chunguzi zakimaabara kwa sampuli 800 za minofu ya samaki na majitaka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara kwa kushirikiana naOfisi ya Makamu wa Rais - Mazingira, Ofisi ya Waziri Mkuu -TAMISEMI, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara yaUlinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Wizara ya Maliasili na Utalii,Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Halmashauriimeendelea kusimamia rasilimali za uvuvi, hususan udhibiti wauvuvi haramu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2012/2013,Wizara imeimarisha vituo vya doria katika Ziwa Victoria (7),Ziwa Tanganyika (4), Ziwa Nyasa (3) na Bahari ya Hindi (6)kwa kuvikarabati na kuvipatia wataalam na vitendea kazi.Pia, doria zenye siku - kazi 2,999 zimefanyika na kuwezeshakukamatwa kwa nyavu za aina mbalimbali 58,191, mabomu866, tambi za kulipua mabomu 269, vifaa vya kuzamia jozi164, mikuki 69, bunduki za kienyeji 49, kasia 2,543, katuli 314,ndoano 94, miwani ya kuogelea 129, mitumbwi 505, injini zaboti 15, magari 18, pikipiki 7 na baiskeli 9. Pia, kilo 37,112 za

Page 88: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

87

31 MEI, 2013

samaki wachanga, 2,613 za samaki wabichi, 1,752 za samakiwakavu, 4,768 za dagaa wakavu, 1,997 za samaki waliovuliwakwa mabomu, 312 za jongoo bahari na 264 za makombezilikamatwa. Vilevile, watuhumiwa 294 walikamatwa kwakujihusisha na uvuvi na biashara haramu ya mazao ya uvuviambapo kesi 27 zilifunguliwa mahakamani. Aidha, Wizaraimekagua maduka ya nyavu 44 katika maeneo mbalimbalinchini ambapo maduka manne yalikutwa na nyavu haramuna wamiliki walifikishwa mahakamani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2013/2014,Wizara itaendelea kuimarisha vituo 21 vya doria, kushirikianana Halmashauri pamoja na wadau wengine kufanya doriazenye siku - kazi 24,000 na kuendelea kutoa elimu kwa wadaukuhusu athari za uvuvi haramu. Aidha, Wizara itapendekezakuanzisha mamlaka maalum ya kudhibiti uvuvi haramu chiniya Sheria ya Uvuvi Sura 279 inayofanyiwa marekebisho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara kwa kushirikiana naHalmashauri imewezesha kuanzisha Vikundi vya UsimamiziShirikishi wa Rasilimali za Uvuvi (Beach Management Units -BMUs) 20 na kufanya idadi ya BMUs kote nchini kufikia 739.Pia, BMUs 16 zimesajiliwa na nane kuwezeshwa kutunga sheriandogo. Aidha, wadau 754 wameelimishwa kuhusu athari zauvuvi haramu na usimamizi wa rasilimali za uvuvi unaozingatiaikolojia na mazingira. Pia, Wizara imeendelea kuzielekezaHalmashauri kuimarisha ulinzi shirikishi wa rasilimali za uvuvikatika maeneo yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2013/2014,Wizara kwa kushirikiana na Mamlaka za Serikali za Mitaaitawezesha uanzishwaji na uimarishaji wa BMUs na kuendelezautekelezaji wa mtandao wa vikundi hivyo. Pia, itaendeleakuhamasisha wadau kuhusu usimamizi wa rasilimali za uvuviunaozingatia ikolojia na mazingira nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara imeendeleakusimamia rasilimali za uvuvi kwenye maeneo ya uvuvi, kupitiaKitengo cha Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU).Katika mwaka 2012/2013, Kitengo kimefanya doria zenye siku

Page 89: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

88

31 MEI, 2013

- kazi 213 ili kudhibiti wavuvi haramu ambapo nyavu haramu140, mbao za mikoko 200, mabomu 18, mitumbwi 14, michinji43 na maboya 44 yalikamatwa. Aidha, Kitengo kimetangazavivutio vya utalii vilivyomo katika Hifadhi za Bahari na MaeneoTengefu kupitia maonesho ya Karibu (Arusha), Indaba (AfrikaKusini), Sabasaba na Nanenane; na kuchapisha nakusambaza nakala 10,000 za vipeperushi kwa wadau. Pia,Kitengo kimeimarishwa kwa kupatiwa wataalam na vitendeakazi vikiwemo magari matatu, pikipiki sita, boti la kioo nakujenga nyumba tatu za kuishi watumishi katika Hifadhi yaGhuba ya Mnazi - Mtwara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2013/2014,Kitengo kitaandaa kanuni za usimamizi wa maeneo nakuanzisha mchakato wa kutangaza maeneo mapya yauhifadhi, kufanya doria za siku kazi 400 kudhibiti uvuvi haramukwenye maeneo ya hifadhi na kuendelea kutangaza vivutiovya utalii vilivyomo katika Hifadhi za Bahari na MaeneoTengefu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, usimamizi wa uvuvi katikabahari kuu. Wizara yangu kwa kushirikiana na Wizara yaMifugo na Uvuvi ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inasimamiauvuvi katika Bahari Kuu kupitia Mamlaka ya Kusimamia UvuviBahari Kuu (Deep Sea Fishing Authority – DSFA). Katika kipindicha Julai, 2012 hadi Mei, 2013, Mamlaka imetoa leseni zauvuvi 38 ambazo ziliingiza Dola za Kimarekani 1,335.810.Wavuvi wakubwa hao wameanza kutekeleza Sheria ya DeepSea Fishing Authority, Sura ya 388 na Kanuni zake kwa kuletameli zao ili zikaguliwe kwenye bandari zetu na kuchukuawataalam wa uvuvi kama waangalizi wa shughuli za uvuvikwenye meli. Pia, ilifanya doria za saa 180 za anga na majikwa kushirikiana na Jeshi la Wanamaji, Polisi na Kikosi Maalumcha Kuzuia Magendo (KMKM) ili kudhibiti uvuvi haramu.Vilevile, Mamlaka imesasisha (update) mfumo wa kudhibitinyendo za meli Bahari Kuu kwa kuweka kifaa cha kuangaliamienendo ya vyombo vya uvuvi katika Bahari Kuu (VesselMonitoring System - VMS) na kuwezesha kufuatilia meli 51zilizopata leseni. Mamlaka kwa kushirikiana na Mpango waFISH-i Africa chini ya NEPAD ilibaini meli mbili zikiendesha uvuvi

Page 90: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

89

31 MEI, 2013

haramu na taarifa kuhusu suala hili imetolewa Indian OceanTuna Commission (IOTC) ili ifanye uhakiki ili tuweze kuchukuahatua stahiki. Aidha, Wizara inaendelea kufuatilia taarifa yakuwepo kwa meli kumi za uvuvi ambazo zimevua katika majiyetu kwa kutumia leseni za kughushi. Pia, Mamlaka kwakushirikiana na TAFIRI, IOTC na South West Indian OceanFisheries Project (SWIOFP), imefanya tathmini ya uvuvi wakibiashara kwa kutumia vifaa sita vya kuvutia samaki (FishAggregating Devices - FADs) na kuonesha ongezeko la ainambalimbali za samaki katika maeneo hayo. Vilevile, Wizaraimeanza kupitia Sheria ya Mamlaka ya Kusimamia UvuviBahari Kuu, Sura ya 388 na Kanuni zake il i kuandaamapendekezo ya kuiwezesha Sheria hiyo kutekelezwaipasavyo katika mazingira ya sasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2013/2014,Wizara itakamilisha mapendekezo ya kurekebisha Sheria yaMamlaka ya Kusimamia Uvuvi Bahari Kuu, Sura ya 388 naKanuni zake. Aidha, Mamlaka itanunua meli moja ya doriana kuongeza vifaa vya kuvutia samaki (FADs) baharini.Vilevile, itaendelea kuhamasisha wavuvi Watanzaniakuwekeza katika uvuvi wa Bahari Kuu, kushirikiana na nchiwanachama wa IOTC kufanya doria ya pamoja nakushirikiana na World Wide Fund for Nature (WWF) kufanyatathmini ya mnyororo wa thamani ya samaki aina ya Jodarina jamii zake. Pia, Mamlaka itatoa mafunzo kwa wavuvi 50na watumishi wake wanne.

Mheshimiwa Mwenyekiti, il i watumishi wawezekutekeleza majukumu yao ipasavyo, wanahitaji kujengewauwezo wa kiutendaji pamoja na kuendelea kukua katikataaluma zao. Katika mwaka 2012/2013, Wizara na Taasisi zakeimeajiri watumishi 20, kupandisha vyeo watumishi 234 na 50kuthibitishwa kazini. Aidha, Wizara kwa kushirikiana na wadauimewezesha mafunzo ya muda mrefu kwa watumishi 61,muda mfupi 143 na 166 wanaendelea na masomo ya mudamrefu. Pia, Wizara imewezesha kikao cha Baraza laWafanyakazi, kuelimisha watumishi 601 kuhusu Mfumo waUpimaji wa Utendaji Kazi wa Wazi (OPRAS), kuwezeshawatumishi 52 kushiriki katika michezo ya SHIMIWI na kuendelea

Page 91: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

90

31 MEI, 2013

kufanya mapitio ya miundo ya utumishi wa kada za mifugona uvuvi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2013/2014,Wizara kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais - Menejimenti yaUtumishi wa Umma itawezesha ajira ya maafisa ugani wamifugo na uvuvi 2,500 watakaoajiriwa katika Halmashauri.Halmashauri zinahimizwa zijiandae kuwapokea, kuwapangiakazi na kuwapatia vitendea kazi watumishi hao. Aidha,itapandisha vyeo watumishi 191, kuthibitisha kazini 54, kuajiri432 wa kada mbalimbali, kuwezesha mafunzo kwa watumishi176 na kuwezesha watumishi 50 kushiriki katika michezombalimbali inayoratibiwa na SHIMIWI. Pia, Wizara itaendeleakuwezesha majukumu ya matawi ya vyama vya wafanyakazi(TUGHE na RAAWU) Wizarani na Baraza la Wafanyakazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2012/2013,Wizara imeendelea kusimamia masuala ya utawala bora,jinsia na UKIMWI kwa kutekeleza yafuatayo:-

(i) Kuratibu na kuwaelimisha watumishi juu yauadilifu, maadili, wajibu na haki zao;

(ii) Kutoa mafunzo kwa watumishi kuhusu namnaya kuferejisha masuala ya jinsia katika mipango ya Wizara;

(iii) Kuelimisha watumishi kuhusu kutekelezaMkakati wa Kuzuia na Kuziba Mianya ya Rushwa;

(iv) Kufanya mapitio, kuchapisha na kutekelezaMkataba wa Huduma kwa Mteja;

(v) Kuendelea kutoa elimu kuhusu UKIMWI nahuduma kwa watumishi wanaoishi na VVU na wanaouguaUKIMWI; na

(vi) Kuanzisha dawati la malalamiko na kufanyiakazi malalamiko yanayotolewa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2013/2014,

Page 92: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

91

31 MEI, 2013

Wizara itaendelea kuhimiza watumishi kuzingatia sheria,kanuni na taratibu za kazi, kutekeleza Mkakati wa Kuzuia naKuziba Mianya ya Rushwa na kutekeleza Mkataba waHuduma kwa Mteja. Aidha, Wizara itaimarisha Dawati la Jinsiana Dawati la Malalamiko, kuhamasisha watumishi kuhusuumuhimu wa kupima afya zao kwa hiari na kutoa hudumakwa watumishi wanaoishi na VVU na wanaougua UKIMWI.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara imeendeleakutayarisha na kusambaza taarifa za matukio mbalimbalikuhusu sekta za mifugo na uvuvi kupitia vyombo vya habari.Katika mwaka 2012/2013, Wizara imeandaa na kurushahewani vipindi vya runinga 5 na redio 20 kuhusu sera, mikakatina mipango ya kuendeleza sekta za mifugo na uvuvi. Pia,Wizara imendaa na kusambaza nakala 1,000 za kalenda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2013/2014,Wizara itaimarisha maktaba ya Wizara na kuipatia vifaamuhimu; kukamilisha na kuchapisha Mkakati wa Mawasilianowa Wizara; kuandaa na kurusha hewani vipindi vinne vyaruninga na kumi vya redio kutangaza mafanikio ya sekta yamifugo na uvuvi; na kuandaa na kusambaza nakala 1,000 zakalenda ya mwaka 2014 na 1,000 za vipeperushi juu yautekelezaji ya majukumu ya Wizara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2012/2013,Wizara imeandaa Mkakati wa kutekeleza Sera ya Teknolojiaya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ya Wizara na kuimarishamfumo wa TEHAMA. Pia, imeboresha tovuti ya Wizara nakuiunganisha na mitandao ya vituo vya Mpwapwa, TAFIRIna Nyegezi, kwa lengo la kuweka msingi wa kutumia simu zamdahalisi (internet) na kuwezesha kutumia mfumo wamikutano ya masafa (video and teleconferencing). Aidha,Wizara imeimarisha Kitengo cha TEHAMA kwa kukipatiawatumishi na vitendea kazi. Katika mwaka 2013/2014, Wizaraitajenga mfumo wa kompyuta wa kuhifadhi kumbukumbuna kufuatil ia mzunguko wa majalada na kuendeleakuboresha tovuti ya Wizara kwa lengo la kuwawezeshawadau kupata taarifa mbalimbali za sekta za mifugo nauvuvi.

Page 93: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

92

31 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2012/2013,Wizara kwa kushirikiana na Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA),imeendelea kutoa taarifa kwa wafugaji na wavuvi kuhusuupatikanaji wa maji na malisho na hali ya bahari na maziwana kutoa maelekezo stahiki. Pia, Wizara kwa kushirikiana naMradi wa Taifa wa Biogesi, imebainisha maeneoyatakayojengwa mitambo ya mfano ya biogesi inayozingatiahali ya ukame katika mazingira ya ufugaji wa asili katikaWilaya za Arusha, Babati, Longido, Monduli, Hanang, Mbulu,Korogwe, Handeni, Dodoma, Kongwa, Bahi, Kondoa, Singida,Manyoni, Mwanga, Same na Arumeru. Vilevile, wadau 126kutoka kwenye vikundi vya wavuvi wa Wilaya za Muheza,Bagamoyo, Mkinga na Rufiji wamehamasishwa kutumiateknolojia ya kukausha samaki kwa nishati ya jua. Aidha,Wizara imeendelea kuhimiza sekta binafsi kuwekeza katikamatumizi ya boti za fibre glass ili kupunguza ukataji wa mitikwa ajili ya kutengeneza mitumbwi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2013/2014,Wizara itaendelea kutekeleza mfumo wa utoaji tahadharikuhusu mabadiliko ya tabianchi kwa wafugaji na wavuvi nakuhamasisha matumizi ya teknolojia zinazozingatia hifadhi yamazingira na matumizi ya nishati mbadala.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maadhimisho namakongamano muhimu katika sekta za mifugo na uvuvi.Katika mwaka 2012/2013, Wizara imeendelea kuandaa nakushiriki katika maadhimisho na makongamano mbalimbaliya Kitaifa na Kimataifa yakiwemo:-

(i) Siku ya Chakula Duniani ambayohuadhimishwa tarehe 16 Oktoba kila mwaka. Katika mwaka2012 maadhimisho na sherehe hizo zilifanyika katika Wilayaya Kigoma yakiwa na “kaulimbiu ya Ushirika katika Kilimo;”

(ii) Siku ya Mvuvi Duniani ambayo huadhimishwatarehe 21 Novemba kila mwaka. Katika mwaka 2012maadhimisho na sherehe hizo zilifanyika katika Wilaya ya Lindiyakiwa na kaulimbiu ya “Matumizi ya teknolojia sahihi katika

Page 94: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

93

31 MEI, 2013

uvuvi na ukuzaji wa viumbe kwenye maji, kuongeza uzalishaji,lishe, kipato na kupunguza kasi ya uvuvi kwenye maji ya asili;”

(iii) Maadhimisho ya Nanenane hufanyika tarehe8 Agosti kila mwaka. Katika mwaka 2012 maadhimisho hayoyalifanyika Dodoma yakiwa na kaulimbiu ya “KILIMOKWANZA - Zalisha Kisayansi na Kiteknolojia Kukidhi Mahitajiya Ongezeko la Idadi ya Watu;”

(iv) Siku ya Kichaa cha Mbwa Duniani ambayoiliadhimishwa kitaifa katika Manispaa ya Temeke tarehe 28Septemba, 2012. Kaulimbiu ilikuwa ni Tushirikiane KufanyaUgonjwa wa Kichaa cha Mbwa kuwa Historia;

(v) Siku ya Wanyama Duniani ambayoiliadhimishwa tarehe 4 Oktoba, 2012 Kitunda, Dar es Salaamna kaulimbiu ilikuwa Tuwapende na Kuwathamini WanyamaWetu;

(vi) Siku ya Veterinari Duniani iliyoadhimishwatarehe 27 Aprili, 2013 ilikuwa na kaulimbiu “Chanja ili kulindana kuzuia;”

(vii) Siku ya Maziwa Shuleni Duniani ilifanyikaMkoani Njombe tarehe 26 Septemba, 2012 ikiwa na kaulimbiu“Maziwa kwa Mtoto ni Afya na Chachu ya Mahudhurio;”

(viii) Wiki ya Uhamasishaji Unywaji wa MaziwaDuniani iliyoadhimishwa tarehe 29 Mei - 1 Juni, 2013 katikaManispaa ya Songea ambapo kaulimbiu ilikuwa ni ‘FugaNg’ombe wa Maziwa Boresha Kipato na Lishe’;

(ix) Mkutano wa mwaka wa Wataalam waUzalishaji Mifugo (Tanzania Society of Animal Production)uliofanyika tarehe 23 - 26 Oktoba, 2012 katika Jiji la Arusha.Maudhui ya mkutano huo yalikuwa “Teknolojia Mpya zaKuongeza Tija Uzalishaji wa Mifugo na Uvuvi ili Kufikia Malengoya Milenia;” na

(x) Mkutano wa mwaka wa Madaktari wa Mifugo

Page 95: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

94

31 MEI, 2013

(Tanzania Veterinary Association Scientific Conference)uliofanyika tarehe 11 - 13 Desemba, 2012 katika Jiji la Arusha.Maudhui ya mkutano yalikuwa ni “Mchango wa Taaluma yaVeterinari katika Kuboresha Afya ya Jamii”.

Katika mwaka 2013/2014, Wizara kwa kushirikiana nawadau mbalimbali itaendelea kuandaa na kushiriki katikamaadhimisho na makongamano hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla ya kuhitimisha hotubayangu, napenda kuchukua fursa hii, kuwashukuru wale wotewaliochangia kwa namna moja au nyingine katikakuiwezesha Wizara yangu kufanikisha majukumu yake.Napenda kuzitambua na kuzishukuru nchi za Jumuiya yaAfrika Mashariki (EAC), Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi zaKusini mwa Afrika (SADC), Umoja wa Nchi za Ulaya (EU),Serikali za Australia, Austria, Brazil, Canada, Jamhuri ya Czech,Hispania, Iceland, Ireland, Japan, Jamhuri ya Watu wa China,Israel, Korea Kusini, Marekani, Misri, Norway, Poland, Sweden,Ubelgiji, Ufaransa, Uholanzi, Uingereza, Ujerumani na Uswisipamoja na Mashirika ya Umoja wa Mataifa ya FAO, IAEA,UNICEF, UNDP, UNIDO na WHO na Mifuko ya Kimataifa yaGEF na IFAD kwa kuchangia katika maendeleo ya sekta zamifugo na uvuvi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile, nazishukuru Taasisiza Kimataifa ambazo ni pamoja na Benki ya Dunia, Benki yaMaendeleo ya Afrika; Shirika la Kimataifa la Ushirikiano laJapan (JICA), Shirika la Kimataifa la Ushirikiano la Jamhuri yaKorea (KOICA), Shirika la Misaada la Ireland (Irish Aid), Shirikala Misaada la Marekani (USAID), Shirika la Misaada la Australia(AUSAID), Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza(DfID), Taasisi ya Rasilimali za Wanyama ya Umoja wa Afrika(AU/IBAR), Shirika la Afya ya Wanyama Duniani (OIE), Shirikala Maendeleo la Uswisi (SDC), Shirika la Ushirikiano la Ujerumani(GTZ), United Nations University (UNU), Shirika la Maendeleola Denmark (DANIDA) na Shirika la Kimataifa la Maendeleola Sweden (SIDA), kwa michango yao katika kuendelezasekta za mifugo na uvuvi. Pia, nayashukuru Mashirika na Taasisiza hiari za Bill and Melinda Gates Foundation, Association for

Page 96: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

95

31 MEI, 2013

Agricultural Research in East and Central Africa (ASARECA),The New Partnership for African’s Development (NEPAD),International Livestock Research Institute (ILRI), World WideFund for Nature (WWF), Indian Ocean Commission (IOC),South West Indian Ocean Fisheries Commission (SWIOFC),Heifer Project Tanzania (HPT), Overseas Fisheries Co-operationFoundation of Japan (OFCF), Vetaid, Care International,OXFAM, Welcome Trust, World Vision, FARM Africa, Land O’Lakes, Building Resources Across Communities (BRAC), WorldSociety for Protection of Animals (WSPA), Global Alliance forLivestock and Veterinary Medicine (GALVmed), Institute forSecurity Studies (ISS-Africa), International Land Coalition (ILC),British Gas International, Sea Sense, Indian Ocean TunaCommission (IOTC), International Whaling Commission (IWC),SmartFish na Marine Stewardship Council (MSC).

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kutoa shukuranizangu za pekee kwa Wananchi wote, hususan wafugaji,wavuvi na wadau wengine kwa michango yao katikakuendeleza sekta za mifugo na uvuvi nchini. Nachukua nafasihii kuwaomba waendelee kushirikiana nasi katika kuendelezasekta za mifugo na uvuvi nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimaliziekuwashukuru kwa dhati Mheshimiwa Benedict Ole-Nangoro,Mbunge wa Jimbo la Kiteto na Naibu Waziri wa Maendeleoya Mifugo na Uvuvi, kwa msaada wake wa karibu katikakusimamia kazi za Wizara. Aidha, napenda pia nitoe shukuranizangu kwa Katibu Mkuu - Dokta Charles Nyamrunda, NaibuKatibu Mkuu - Dokta Yohana Budeba, Wakuu wa Idara naVitengo, Taasisi na Watumishi wote wa Wizara, kwa ushirikianowao katika kutekeleza majukumu tuliyopewa na Taifa nakufanikisha maandalizi ya bajeti hii. Vilevile, napendakuwashukuru Wananchi wa Jimbo la Same Magharibi kwaushirikiano wao wanaoendelea kunipa na kuniwezeshakutekeleza majukumu yangu. Pia, naishukuru familia yangukwa kuendelea kunitia moyo ninapotekeleza majukumu yakitaifa.

Page 97: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

96

31 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Mwaka wa Fedha wa2013/2014, Wizara inaomba Bunge lako Tukufu likubalikupitisha Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Maendeleo yaMifugo na Uvuvi ya jumla ya shilingi 47,180,225,000.00 kamaifuatavyo:-

(i) Shilingi 38,206,909,000.00 ni kwa ajil i yaMatumizi ya Kawaida. Kati ya hizo, shilingi 16,339,267,000.00ni kwa ajili ya mishahara ya watumishi (PE); na shilingi21,867,642,000.00 ni kwa ajili ya Matumizi Mengine (OC); na

(ii) Shilingi 8,973,316,000.00 ni kwa ajil i yakutekeleza Miradi ya Maendeleo. Kati ya hizo, shilingi3,488,270,000.00 ni fedha za ndani na shilingi 5,485,046,000.00ni fedha za nje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba tena nitoeshukurani zangu za dhati kwako na kwa WaheshimiwaWabunge kwa kunisikiliza. Hotuba hii pia inapatikana katikaTovuti ya Wizara kwa anuani: www.mifugouvuvi.go.tz.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hotuba hii,nimeambatanisha Randama ya Mpango na Bajeti ya Wizarakwa mwaka 2013/2014.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kutoa hoja.(Makofi)

WAZIRI WA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI:Mheshimiwa Mwenyekiti, naafiki

(Hoja ilitolewa iamuliwe)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Waziri.

Waheshimiwa Wabunge, hoja imetolewa naimekwisha kuungwa mkono, tunaingia sasa hatua inayofuata.Nitaomba sasa nimwite Mwenyekiti wa Kamati iliyochambuamakadirio haya, lakini kwa niaba yake ninamwonaMheshimiwa Amina Makilagi, Mbunge wa Viti Maalum,

Page 98: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

97

31 MEI, 2013

Mjumbe wa Kamati na anakwenda kusoma Taarifa ya Kamatikwa niaba ya Mwenyekiti na kwa niaba ya Kamati hiyo.

MHE. AMINA N. MAKILAGI (K.n.y. MWENYEKITI WAKAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KILIMO, MIFUGO NA MAJI):Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa Kanuni ya 99 (9) yaKanuni za Bunge, Toleo la 2013, naomba kuwasilisha Taarifaya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Majikuhusu utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Maendeleoya Mifugo na Uvuvi kwa Mwaka wa Fedha wa 2012/2013 naMakadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedhawa 2013/2014.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati ilikutana na Wizaraya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi katika Ofisi Ndogo yaBunge ya Dar es Salaam tarehe 28 Machi na 2 Aprili, 2013.Katika vikao hivyo, Waziri alitoa maelezo kuhusu utekelezajiwa maoni na ushauri wa Kamati kwa Mwaka wa Fedha wa2012/2013, changamoto za utekelezaji, malengo na maeneoya kipaumbele pamoja na makadirio ya mapato na matumizikwa Mwaka wa Fedha wa 2013/2014.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati wa kuchambuataarifa ya utekelezaji wa bajeti ya Wizara kwa Mwaka waFedha wa 2012/2013, Kamati ilitoa maoni na ushaurimbalimbali. Napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa,Kamati imeridhika kuwa, kwa kiasi kikubwa Serikaliimeyafanyia kazi maoni ya Kamati, isipokuwa kwa maeneoambayo utekelezaji wake ulikwamishwa na bajeti ndogo naucheleweshaji wa fedha pamoja na sababu mbalimbali zakiutendaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na jitihada kubwazinazofanywa na Wizara katika kutekeleza majukumu yake,kwa Mwaka wa Fedha wa 2012/2013, Wizara inakabiliwa nachangamoto mbalimbali ambazo zimekuwa ni kikwazo katikakufikia malengo iliyojiwekea. Baadhi ya changamoto hizo ni:-

Moja, kushindwa kufikia malengo yaliyotarajiwakutokana na kuchelewa kupata fedha zikiwemo fedha za

Page 99: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

98

31 MEI, 2013

maendeleo za ndani na nje kama zilivyoidhinishwa na Bungelako Tukufu. Aidha, fedha hutolewa kidogo kidogo kiasikwamba, haziendani na mpango kazi. Kwa mfano, hadikufikia tarehe 15 Machi, 2013 jumla ya Shil ingi22,422,553,000.95 tu zimetolewa, sawa na asilimia 56.04 kwaajili ya matumizi ya kawaida. Kwa upande wa fedha zamaendeleo ni Shilingi 4,609,833,000 tu, sawa na asilimia 33.3zimetolewa.

Mbili, uwekezaji mdogo wa Sekta za Mifugo na Uvuvihasa katika usindikaji wa mazao ya mifugo na uvuvi na katikaBahari Kuu kunaathiri mchango wa sekta katika Pato la Taifa.Katika mwaka 2012, sekta za mifugo na uvuvi zilikua kwaasilimia 3.1 na 2.9 sawia na kuchangia asilimia 4.6 na 1.4 sawiakatika Pato la Taifa.

Tatu, kasi ndogo ya Halmashauri katika kuainisha,kupima na kumilikisha maeneo ya ufugaji ili yawe endelevu,jambo ambalo limesababisha kwa kiwango kikubwakuhamahama kwa mifugo na hivyo kusababisha migogoromingi baina ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi nahasa wakulima.

Nne, kuenea kwa magonjwa mbalimbali ya mifugo,hususan magonjwa ya milipuko kutokana na ufugaji wakuhamahama na usiozingatia uwezo wa malisho kuhimili wingiwa mifugo. Magonjwa hayo ni pamoja na homa ya mapafu,mdondo, mapele ya ngozi, kichaa cha mbwa, mafua makaliya ndege na kadhalika.

Tano, kutopatikana kwa mikopo ya kutosha na yenyemasharti nafuu kwa shughuli za ufugaji na uvuvi ikilinganishwana mahitaji yao. Aidha, gharama za pembejeo na zana kwaajili ya ufugaji na uvuvi ni kubwa na kufanya wafugaji nawavuvi kushindwa kuzinunua.

Sita, uhaba wa Maafisa Ugani wa Mifugo na Uvuviiki l inganishwa na mahitaji ya wataalam hao katikaHalmashauri. Kwa mfano, mahitaji ya wagani wa mifugo na

Page 100: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

99

31 MEI, 2013

uvuvi kwa nchi nzima ni 17,525 na 16,000 sawia, ikilinganishwana wagani wa mifugo na uvuvi waliopo 5,197 na 436 sawia.

Saba, ukosefu wa mbegu bora za mifugo na samaki,pembejeo na huduma hafifu ya uhamilishaji (Artificialinsemination).

Nane, ukosefu wa soko la uhakika la mazao ya mifugona uvuvi na hasa katika maeneo ya vijijini.

Tisa, ushiriki mdogo wa wadau katika kudhibiti uvuvina biashara haramu ya samaki na mazao ya uvuvi. Hali hiiimesababisha kupungua kwa samaki katika bahari, maziwana mito, uharibifu wa mazalia ya samaki na uharibifu wamazingira kwa ujumla.

Kumi, elimu duni ya ufugaji bora, ufugaji usio wakibiashara na matumizi duni ya teknolojia za kisasa kwawafugaji na wavuvi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Mwaka wa Fedhawa 2013/2014, ili kutekeleza majukumu yake, Wizara chini yaFungu 99, inaomba jumla ya Shilingi 47,180,225,000. Kati yafedha hizo, Shilingi 38,206,909,000 ni kwa ajili ya matumizi yakawaida na Shilingi 8,973,316,000 ni kwa ajili ya Miradi yaMaendeleo. Kati ya fedha hizo za maendeleo, Shilingi3,488,270,000 ni fedha za ndani na Shilingi 5,485,046,000 nifedha za nje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kiasi hiki kilichotengwa nikidogo na hakiwezi kukidhi mahitaji ya utekelezaji wamajukumu muhimu ya Wizara ili kuwezesha kufikia malengoya utoaji wa huduma kwa wafugaji na wavuvi kamailivyoainishwa katika Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2010 yaChama cha Mapinduzi na maelekezo mbalimbali ya ViongoziWakuu wa Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati imebaini kuwa,Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi imekuwa ikipatabajeti ndogo na bajeti hiyo imekuwa ikipungua mwaka hadi

Page 101: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

100

31 MEI, 2013

mwaka na hivyo kushindwa kutekeleza majukumu yakekikamilifu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa fedha zaMiradi ya Maendeleo, Kamati imebaini kuwa mchango waWashiriki wa Maendeleo (DPs) kwa mwaka 2013/2014,umepungua kutoka Shilingi 9,439,483,000 mwaka 2012/2013hadi Shilingi 5,485,046,000. Hii imetokana na kukamilika kwaMradi wa MACEMP na Programu ya Kuendeleza Sekta yaKilimo (ASDP). Hata hivyo, Kamati imeridhika na hatuazinazochukuliwa na Serikali katika kuandaa miradi naprogramu mbadala kufuatia kukamilika kwa miradi naprogramu tajwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa fedha zandani za Maendeleo, Kamati imebaini kuwa, bajetiiliyotengwa kwa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvikwa mwaka 2013/2014 ni Shilingi 3,484,270,000, ikilinganishwana Shilingi 4,000,000,000 mwaka 2012/2013. Aidha, Kamatiimebaini kuwa fedha za Maendeleo kwa mwaka 2013/2014ni tegemezi kwa asilimia 61, yaani Shilingi 5,485,046,000. Kiasihiki kilichotengwa ni kidogo na hakiwezi kukidhi mahitaji yautekelezaji wa majukumu muhimu ya Wizara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati imebaini kuwa,pamoja na fedha ndogo zinazotengwa, fedha hizo hazitolewikama ilivyopangwa na kwamba zimekuwa zikipunguamwaka hadi mwaka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na ushauri waKamati uliotolewa mwaka jana kuhusu umuhimu wa Wizarahii kuongezewa fedha, Kamati imesikitishwa kuona kwamba,Bajeti ya Wizara imeshuka zaidi kutoka Shilingi 54,566,124,000mwaka 2012/2013 hadi Shilingi 47,180,225,000 kwa Mwaka waFedha wa 2013/2014. Ili kutekeleza majukumu yake ipasavyo,Wizara iliomba Shilingi bilioni 163 ili kuweka mazingira wezeshikwa ajili ya maendeleo endelevu ya Sekta ya Mifugo na Uvuvi,kwa kasi inayoendana na Kaulimbiu ya KILIMO KWANZA.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na upungufu wa

Page 102: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

101

31 MEI, 2013

Bajeti ya Wizara hii, Kamati inaishauri Serikali iongeze Bajetiya Wizara kiasi cha Shilingi 40,000,000,000 na kufikia Shilingi87,180,225,000 kwa mwaka 2013/2014 kwa ajili ya kutekelezavipaumbele muhimu kama vilivyoainishwa katika Mwongozowa Kitaifa wa Uandaaji wa Mpango wa Bajeti ya Serikali.Maeneo yanayoombewa fedha ni yale ambayo Kamatiinaona yatakuwa na matokeo ya haraka katika kuboreshamaisha ya wafugaji na wavuvi na hivyo kuongeza Pato laTaifa kwa ujumla. Vipaumbele hivyo ni kama vifuatavyo:-

Moja, kuwezesha Kampuni ya Ranchi za Taifa(NARCO), kuongeza idadi ya mifugo, kupanua programu yaunenepeshaji, kupanua machinjio ya Dodoma na kukamilishaujenzi wa machinjio ya Ruvu. Shilingi 5,000,000,000.

Mbili, kuendeleza kuboresha miundombinu ya mifugona uvuvi kwa kufanya upembuzi yakinifu wa ujenzi wa Bandariya Uvuvi Mbegani - Bagamoyo. Hii itawezesha kujengabandari ambayo itakuza mchango wa Sekta ya Uvuvi katikaPato la Taifa, kuvutia wawekezaji, kukuza ajira na kipato chawavuvi kwa ujumla. Shilingi 11,000,000,000.

Tatu, kuanzisha mfumo wa ruzuku kwa wavuvi nawafugaji. Kwa upande wa mifugo, ruzuku hii itatumika kwaununuzi wa madawa ya kuogeshea na chanjo za mifugo nahivyo kupunguza vifo vya mifugo vitokanavyo na magojwayaenezwayo na kupe hususan Ndigana Kali (ECF). Kwaupande wa uvuvi, ruzuku itatumika kwa ununuzi wa zana zauvuvi ikiwa ni pamoja na ununuzi wa boti, injini za boti, nyavuna mishipi na ruzuku ya uzalishaji wa chakula bora cha samakina vifaranga. Aidha, Mfumo huu utawawezesha wavuviwadogo wadogo kuvua kwenye maji ya kina kirefu naExclusive Economic Zone (EEZ) na kutoa ajira kwa vijana nakuboresha maisha ya jamii za wavuvi. Shilingi 4,000,000,000.

Nne, katika eneo la Utafiti na Mafunzo yafutayoyatatekelezwa: Kuimarisha utafiti wa mifugo na uvuvi kwakuboresha miundombinu ya TAFIRI, TALIRI na maabara zaTVLA; Kufanya utafiti wa magonjwa ya mifugo na

Page 103: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

102

31 MEI, 2013

kutengeneza chanjo zake na Kusomesha watafiti wa kutoshakwa ajili ya Taasisi za utafiti. Shilingi 9,500,000,000.

Tano, kudhibiti uvuvi haramu na utoroshaji wa mazaoya uvuvi, kwa kuimarisha mifumo ya ufuatiliaji wa melibaharini na katika maziwa (Vessel Monitoring) na kudhibitimeli za kimataifa zinazoiba samaki kwenye eneo letu la BahariKuu (EEZ). Shilingi 5,505,000,000.

Sita, kuimarisha usimamizi, ukaguzi na udhibiti wahuduma za mazao ya mifugo na uvuvi kwa kuimarisha Bodiza Mazao ya Mifugo na Uvuvi, Baraza la Veterinari Tanzaniana wakaguzi wa mazao ya mifugo na uvuvi. Shilingi5,000,000,000.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati inaishauri Serikalikutafuta kiasi cha Shilingi 40,000,000,000 kinachoombwa ilikuboresha huduma za sekta za mifugo na uvuvi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, miundombinu ya kuzalishavifaranga wa samaki na kununua mitambo ya kuzalishavyakula bora vya samaki. Kamati inaishauri Serikali kujengana kuboresha miundombinu ya kuzalisha vifaranga vyasamaki kwa kuanzia na vituo vitano vya Ruhila (SongeaManispaa), Mwamapuli (Igunga), Mtama (Lindi), Kibirizi(Kigoma) na Nyamirembe (Chato). Hii itasaidia kupunguzatatizo la upatikanaji wa vifaranga na kuongeza uzalishajikutoka vifaranga 5,000,000 (2012/2013) hadi 16,000,000 (2014/2015).

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati inashauri Serikalikujenga malambo makubwa ya maji kwenye maeneo yawafugaji yakiwemo maeneo ya Mbangala (Chunya), Miteja(Kilwa), Mji Mwema (Lindi), Mbondo (Nachingwea) naKwamaliga (Kilindi). Aidha, Wizara ianzishe vituo vipya vyakuzalisha mbegu bora za malisho. Hatua hizi zitasaidiakupunguza migogoro baina ya wafugaji na watumiajiwengine wa ardhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati inashauri Serikali

Page 104: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

103

31 MEI, 2013

kuimarisha huduma za uhamilishaji wa mifugo kwakuendeleza ujenzi wa Kituo cha uhamilishaji cha Sao Hill -Iringa na vituo vipya vitano vya uhamilishaji vya Tabora,Kagera, Tanga, Manyara na Katavi na kuimarisha NationalArtificial Insemination Centre (NAIC), kilichoko Arusha namashamba matano ya kuzalisha mitamba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, migogoro ya ardhi kati yawakulima na wafugaji imekuwa sugu na kila siku migogoromipya inaibuka na kusababisha maafa makubwa. Kamatiinashauri yafuatayo:-

Serikali ipeleke huduma muhimu katika maeneo yawafugaji; Serikali iharakishe zoezi la upimaji vijiji na kutengamaeneo ya ufugaji; na Kwa kuwa suala hili ni mtambuka,Wizara ishirikiane na Wizara nyingine kama Ardhi, Kilimo,Maliasili, Maji na TAMISEMI ili washirikiane kutatua migogoroinayojitokeza kila wakati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na ufinyu wabajeti ya Wizara hii, Sekta ya Mifugo na Uvuvi haijawezakuchangia kikamilifu katika Pato la Taifa na kuboresha maishaya Wafugaji na Wavuvi licha ya kuwa na rasilimali kubwakatika eneo hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kukushukuru kwakunipa nafasi kuwasilisha Taarifa ya Kamati. Aidha, napendakuwashukuru Wajumbe wa Kamati kwa ushirikiano namichango yao mizuri wakati wa kupitia na kuchambua Bajetiya Wizara hii. Naomba kuwatambua kwa kuwataja majinakama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Prof. Peter Mahamudu Msolla -Mwenyekiti, Mheshimiwa Said J. Nkumba - MakamuMwenyekiti, Mheshimiwa Prof. David Homeli Mwakyusa,Mheshimiwa Asaa Othman Hamad, MheshimiwaAbdusalaam Selemani Amer, Mheshimiwa Haji JumaSereweji, Mheshimiwa Mch. Peter Simon Msigwa,Mheshimiwa Namelok E. M. Sokoine, Mheshimiwa Dkt.Christine G. Ishengoma, Mhesheshimiwa Moshi Selemani

Page 105: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

104

31 MEI, 2013

Kakoso, Mheshimiwa Kheri Khatib Ameir, Mheshimiwa LolesiaJeremiah Bukwimba, Mheshimiwa Sadifa Juma Khamis,Mheshimiwa Donald Kelvin Max, Mheshimiwa Subira KhamisMgalu, Mheshimiwa Philemon Kiwelu Ndesamburo,Mheshimiwa Meshack Jeremiah Opulukwa, MheshimiwaMagdalena Hamis Sakaya, Mheshimiwa Jitu Vrajlal Soni,Mheshimiwa Dkt. Lucy Sawere Nkya, Mheshimiwa AbdallaHaji Ali, Mheshimiwa Sylvestry Francis Koka na MheshimiwaAmina Nassoro Makilagi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya maelezo hayo,sasa naliomba Bunge lako Tukufu lijadili na kuidhinishaMakadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maendeleoya Mifugo na Uvuvi kwa Mwaka wa Fedha wa 2013/2014 yaShil ingi 47,180,225,000. Kati ya fedha hizo, Shil ingi38,206,909,000 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Shilingi8,973,316,000 ni kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo. Kati yafedha hizo za maendeleo, Shilingi 3,484,270,000 ni fedha zandani na Shilingi 5,485,046,000 ni fedha za nje, ikiwa ni pamojana nyongeza iliyoombwa ya Shilingi 40,000,000,000 ili Wizaraiweze kutekeleza majukumu yake kikamilifu na kuleta tija kwaTaifa letu la Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsanteni kwa kunisikiliza.Naomba kuwasilisha na naunga mkono hoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Nakushukuru sana Mheshimiwa AminaMakilagi, kwa kuwasilisha taarifa kwa niaba ya Kamati.

Waheshimiwa Wabunge, hatua inayofuata sasanitamwita Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani kuhusu Wizarahiyo na ninamwona Mheshimiwa Rose Kamili, atatoa maoniya Kambi ya Upinzani.

MHE. ROSE K. SUKUM (K.n.y. MSEMAJI MKUU WAUPINZANI KWA WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI):Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Hotuba hii iingie kwenyeHansard kama nilivyowasilisha leo asubuhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Hotuba hii inatolewa chini

Page 106: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

105

31 MEI, 2013

ya Kanuni ya 99(9) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo laMwaka 2013.

Mheshimiwa Mwenyekiti, dira ya Wizara yaMaendeleo ya Mifugo na Uvuvi ni kuhakikisha kuwa, rasilimaliza mifugo na uvuvi zinaendelezwa na kutunzwa katikamazingira endelevu kwa ajili ya ukuaji wa uchumi nakuboresha maisha ya Wananchi. Aidha, dira inalengakuhamasisha ufugaji wa kisasa na uvuvi endelevu ili kujengauchumi endelevu kwa jamii nzima ya wafugaji na wavuvi nataifa kwa jumla.

Mheshimiwa Mwenyekiti, licha ya ukweli kwamba,wafugaji na wavuvi wana mchango mkubwa katika uchumiwetu, Serikali hii ya CCM imeshindwa kuwapatia maeneomaalum kwa ajili ya malisho kwa maendeleo ya mifugo yao.Wafugaji wamekuwa wakihamishwa na au wakifukuzwakutoka eneo moja la nchi hadi eneo lingine kama vilehawana haki ya kufanya shughuli za kiuchumi kama ufugajikatika nchi yao. Ni aibu kwa Serikali kushindwa kuwapatiawafugaji mahitaji muhimu ambayo yangepelekea ufugajiwao kuwa wa kisasa, kibiashara na endelevu kamailivyobainisha katika dira ya Wizara hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi Rasmi ya UpinzaniBungeni inayoongozwa na CHADEMA, haioni sababu yaSerikali kutowapatia wafugaji maeneo ya kufugia kwa kuwawafugaji wangeweza kuingia ubia na mashamba makubwaya mifugo ambayo yalikuwa yanamilikiwa na Ranchi za Taifa;lakini kutokana na ubinafsi na ufisadi uliofichwa kwenye kivulicha cha sera ya ubinafsishaji, Serikali ya CCM imesimamiazoezi la Viongozi wa Serikali na Chama cha Mapinduziwakigawiana ranchi hizo na kuwaacha wafugajiwakifukuzwa ovyo na kupewa jina la wachungaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa wavuvi, halini hiyo hiyo, kwani mapato mengi ya Serikali yanayokusanywakutoka katika Sekta ya Uvuvi yanatokana na wavuvi wadogoambao mara zote wao ndiyo waathirika wa mfumokandamizi wa Serikali. Zana za uvuvi zinapokamatwa, wao

Page 107: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

106

31 MEI, 2013

ndiyo wanapata hasara, lakini wauzaji wa zana hizo za uvuviwala hawaulizwi na wala hakuna hatua zinazochukuliwadhidi yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, changamoto kubwainayozikabili sekta hizi za ufugaji na uvuvi ni kwamba, sektazote mbili hazina bima dhidi ya majanga ambayo yanawezakutokea. Katika mazingira kama haya, dhana ya kuwa sektaza kisasa au kibiashara na endelevu inakuwa ngumu sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Hotuba ya MsemajiMkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwa Mwaka waFedha wa 2012/2013, iliainisha upungufu mkubwa wakiutendaji na kiuwajibikaji kwa Wizara hii na kuitaka Serikalikufanya mambo yafuatayo:-

Moja, kuwajibika kwa uzembe wa kuitelekeza meli yauvuvi ya Tawariq iliyokamatwa ikifanya uvuvi haramu katikaukanda wa bahari ya hindi hadi meli hiyo kuharibika kabisana kuanza kuzama bila faida yoyote?

Mbili, kuchukua hatua dhidi ya mwekazaji wa KageraSugar kwa kushindwa kuendeleza shamba la ukubwa wahekta 45,000 (sawa na ekari 112,500) kinyume na mkataba.

Tatu, kueleza sababu za kuwapa mashambamakubwa wawekezaji wa kigeni na kuwanyanyapaawafugaji wa asili kinyume cha sheria.

Nne, kutatua migogoro ya ardhi baina ya wakulimana wafugaji ambayo mara kadhaa imesababisha uvunjifuwa amani na umwagaji damu miongoni mwa Wananchi.

Tano, kujenga viwanda vya kusindika nyama katikamikoa ya wafugaji ili kuongeza thamani ya bidhaa ya nyamana hivyo kukuza uchumi.

Sita, kuweka wazi kiasi cha fedha kinachopatikakama mrabaha kutokana na uvuvi katika Bahari Kuu, pamoja

Page 108: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

107

31 MEI, 2013

na fedha za leseni kwa meli zinazofanya uvuvi katika Ukandawa Bahari Kuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sekta ya Mifugo ina nafasikubwa katika kujenga uchumi imara wa Taifa, kuongezakipato kwa Watanzania wanaotegemea mifugo na kutoafursa za ajira sanjari na kuhifadhi rasilimali za Taifa. Sera yaMifugo inaeleza nia ya Serikali na wadau wengine katikakukabiliana na changamoto zinazokabili Sekta ya Mifugo.Lengo kubwa ni kujenga mazingira mazuri yatakayotoa fursaza kuongeza kipato na ajira kwa wafugaji wadogo, kufugakibiashara na kuongeza ajira. Ili kufikia haya, Kambi Rasmi yaUpinzani inaitaka Serikali kutekeleza malengo makuu matatuya kisera kama ifuatavyo:-

Moja, kuendeleza Sekta ya Mifugo itakayokuwa namwelekeo wa kibiashara, yenye ufanisi na itakayohimiliushindani wa kimataifa;

Mbili, kuibua mifumo bora ya uzalishaji itakayoongezatija miongoni mwa wafugaji wadogo na wa asili; na

Tatu, kuhifadhi rasilimali za mifugo na kuunda sera nataasisi zitakazosimamia maendeleo na matumizi endelevu yarasilimali hizo na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sera hiyo ya Mifugoimeweka wazi azma ya Serikali ya kuboresha Sekta hii yaMifugo, lakini kutokuwepo na mkakati madhubuti wakufanikisha yale yote yanayohitajika kufanyika na Sera hii yaMifugo ya mwaka 2006, kunaendeleza matatizo katika Sektahii mpaka sasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sekta ya Mifugo hapa nchiniina nafasi kubwa katika ujenzi wa uchumi wa Taifa. Kwanza,kwa kuthamanisha kiwango cha nyama kinachotumika kilasiku hapa nchini ikiwa kiwango hicho kingekuwa kinaagizwatoka nje ya nchi. Pili ni kuongeza kipato kwa Watanzaniawanaotegemea mifugo na kutoa fursa za ajira sanjari nakuhifadhi rasilimali za Taifa.

Page 109: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

108

31 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, mashamba makubwa yamifugo yana uwezo wa kuongeza viwango vya uzalishaji nauuzaji wa mifugo na mazao yake nje ya nchi, ajira nakuboresha maisha ya wafanyakazi wake. Mkakati umetumikawa kugawa mashamba makubwa ya Kampuni ya Ranchi zaTaifa KARATA (NARCO) na yale yaliyokuwa chini ya Kampuniya Ng’ombe wa Maziwa (DAFCO) kuwa mashamba yenyeukubwa wa kati kwa ajili ya ufugaji wa kibiashara unaolengakutekeleza dhana hii. Mkakati huu umeongeza upeo waumilikaji mashamba na pia kuwawezesha Watanzaniakuingia katika ufugaji wa kibiashara. Maeneo ya Ranchi zaKARATA (NARCO) yaliyobaki, yataendelea kutumika kamaranchi za mfano na maeneo yasiyo na magonjwa ya mifugokwa ajili ya soko la nje ya nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ilani ya CCM ya mwaka 2005– 2010, aya ya 32 inasema kwamba: “Pamoja na kwamba,Tanzania ina mifugo mingi sana, mchango wa mifugo kwenyeUchumi wa Taifa ni mdogo. Kwa lengo la kuendeleza Sektaya Mifugo ili ichangie zaidi ukuaji wa Uchumi wa Taifa nakuwaongezea kipato wafugaji, Serikali za CCM zitaendelezakwa msisitizo zaidi lengo la kuzingatia zaidi ubora kuliko wingipekee katika ufugaji. Ili kufikia lengo hilo, hatua zifuatazozitachukuliwa katika kipindi cha 2005 - 2010:-

- Kujenga mazingira ya kuvutia uwekezaji katikaviwanda vya kuongezea thamani mazao ya mifugo kamavile ukataji nyama, usindikaji wa maziwa, utengenezaji wabidhaa za ngozi na kadhalika. Huu ni usemi wa Sera ya CCM.

- Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Ilani ya CCMya mwaka 2010 – 2015, aya ya 38 inasema kwamba: “Katikakipindi cha Ilani hii ya miaka 2010 - 2015, Chama chaMapinduzi kitazielekeza Serikali kuiendeleza Sekta ya Mifugokwa ari zaidi, nguvu zaidi na kasi zaidi ili kuiwezesha kutoamchango mkubwa kwenye Pato la Taifa kwa kuchukua hatuazifuatazo:-

- Serikali iandae Programu Kabambe yaKuendeleza Sekta ya Mifugo na Ufugaji. Programu hiyo

Page 110: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

109

31 MEI, 2013

ijumuishe pamoja na mambo mengine, masuala yauendelezaji wa maeneo ya malisho, kuchimba na kujengamalambo, mabwawa, majosho na huduma za ugani ilihatimaye wafugaji waondokane na ufugaji wakuhamahama.

- Benki ya Kilimo itakayoanzishwa iwe pia Benkiya Mifugo ili iweze pia kutoa mikopo kwa wasomi wenye niaya kufuga na kuwawezesha kuingia kwa wingi katika ufugajiwa kisasa.

- Kuelimisha wafugaji uwiano kati ya idadi yamifugo na eneo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuonesha kuwa CCMyale wanayoyaandika siyo wanayosimamia, katika kuinuaSekta ya Ufugaji hasa wa asilia ambao unachangia zaidi yaasilimia 85 ya ufugaji wote. Kambi Rasmi ya Upinzani inaulizakwa mkakati huo wa CCM dhidi ya wafugaji na ufugaji nikwa vipi ufugaji unaweza kuwa endelevu na wa kisasa wakatiwafugaji wanaporwa maeneo ya kulishia mifugo yao,hawapewi maeneo ya malisho, hawapati huduma za ugani,hawapati mikopo na hawana soko la uhakika wa bidhaazinazotokana na mifugo.

Kambi Rasmi ya Upinzani, inauliza kwa makati huo waCCM dhidi ya wafugaji na ufugaji ni kwa vipi ufugaji unawezakuwa endelevu na wa kisasa wakati wafugaji wanaporwamaeneo ya kulishia mifugo yao, hawapewi maeneo yamalisho, hawapati huduma za ugani, hawapati mikopo nahawana soko la uhakika? Kambi Rasmi ya Upinzani inaitakaSerikali kutoa kauli juu ya ni wapi wafugaji wa asili watafugiamifugo yao ili kuwa endelevu na ya kisasa?

Kwa mfano, wafugaji na wakulima wa vijiji vinne vyaMakuyuni, Loikisale, Naiti na Mswakini katika Wilaya yaMonduli, wanatishiwa kuhamishwa kutokana na mkakatimahususi ulioasisiwa na Mheshimiwa Waziri Kagasheki wakutangaza maeneo hayo kuwa ni Wildlife Management Area(WMA). Uhakika ni kwamba, WMA hiyo ni hewa haipo na

Page 111: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

110

31 MEI, 2013

ukweli ni kwamba, eneo hilo linapewa kikundi kinachoitwaELEWANA AFRIKA.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi Rasmi ya Upinzaniinaitaka Serikali kuwaeleza Wafugaji hao ni wapiwanakokwenda na mifugo yao. Aidha, kwa kuwa utaratibuwa kuanzisha WMA huwa inaanzishwa kwa kupata ridhaaza wanavijiji ambao kwa hiari yao wanatoa maeneo ya vijijivyao kuwa WMA na ndipo kazi ya Waziri husika inafuata yakutoa idhini ya uanzishwaji wa hiyo WMA. Kwa kuwa huondiyo utaratibu wa kuanzisha WMA; je, ni kwa nini vijiji hivyohavikupewa fursa hiyo ambapo ni sawa na Loliondo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, mgogoro wa ardhi katikaeneo la Loliondo ni taswira nyingine ya jinsi ambavyo Serikaliya CCM imekiuka haki za Wafugaji wa Kimaasai kwamanufaa ya wawekezaji wa kigeni katika Sekta ya Uwindajiwa Kitalii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mgogoro wa Loliondo badohaujapatiwa ufumbuzi na sasa umeanzishwa mgogoromwingine Wilaya ya Monduli. Hii ni kwa makusudi kuhakikishawafugaji wa asili wanakwisha kabisa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapo kabla ya uhuru Serikaliilitenga eneo la zaidi ya hekta 18,000, sawa na ekari 45,000,Wilayani Maswa, lililojulikana kama SHISHIYU Holding Groundkwa ajili ya kunenepesha mifugo kabla ya kusafirishwakwenye kiwanda cha Nyama cha Tanganyika Packers,ambacho kimekufa. Cha ajabu ni kwamba, katika eneo hilobado hadi sasa Wafanyakazi wa Idara ya Mifugo wapo palelakini mifugo hainenepeshwi. Je, hii siyo hujuma kwa Sektaya Mifugo na Wafugaji hasa wa Wilaya ya Maswa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, siyo hilo tu, bali pale IpalaWilaya ya Nzega, Mkoa wa Tabora, kuna kituo cha trenikilichokuwa kikitumika kupakia ng’ombe kwenda Dar esSalaam. Eneo hilo lilikuwa limetengwa rasmi kwa ajili yamifugo na kuna miundombinu ya kupakia mifugo kwenyetreni. Jambo la ajabu ni kwamba, Serikali imeligeuza eneo

Page 112: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

111

31 MEI, 2013

lile kuwa hifadhi ya misitu. Kambi Rasmi ya Upinzani inaitakaSerikali kuwa wafugaji wanaoishi eneo hilo waachiwe eneolitumike kwa malisho na miundombinu iliyopo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, kitendokinachofanywa na Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi waHalmashauri kuwahamisha wafugaji kwa nguvu katikamaeneo mbalimbali hapa nchini kwa kuwalipisha mamilioniya fedha wafugaji hao. Kwa mfano, mfugaji mmoja waMikumi alitozwa faini ya shilingi milioni 42.78 kwa kukamatwang’ombe wake na mwingine ni mfugaji wa Chunya zaidi yashilingi milioni 19 na kadhalika, nao ni ushahidi wa dhahirikwamba, Serikali hii ya CCM haina dhamira ya dhati katikakuhakikisha wafugaji na ufugaji unakuwa na tija katika nchiyetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wafugaji wa asil i yaKisukuma, Kimasai, Wairaq na Wabarbaig katika Wilaya zaKilombero, Ulanga, Kilosa, Mbarali, Chunya, Kilindi, Handeni,Mpanda, Rufiji na kadhalika, wamepata matatizo makubwasana na wengine wameuawa na Vyombo vya Dola. Kosalao kubwa ni kuwa na mifugo mingi iliyosababisha wahametoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa na Kanda ya Kaskazini kwasababu za malisho. Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikalikulieleza Bunge, je, kosa la ndugu zetu hao ni kuwa na utajiriwa mifugo mingi au nini hadi wanadharauliwa nakunyanyaswa na kufanywa kuwa Watanzania wa daraja lanne katika nchi yao?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na ukwelikwamba, Wizara imeshindwa kuwatetea na kuwalindawafugaji wa asili; hivyo basi, Kambi Rasmi ya Upinzani inaitakaSerikali iwaeleze wafugaji ni Wizara gani itakayosikiliza nakutatua matatizo yao?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ambavyo imekuwaikitokea katika maeneo ya Ranchi zilizokuwa za Mkoa waKagera, Rukwa, Morogoro, Tanga na Pwani, watu waliopewaekari 4,000 au ekari 10,000 za maeneo ya Ranchi za Taifakama wawekezaji, watu hao wameshindwa kuziendeleza

Page 113: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

112

31 MEI, 2013

ranchi hizo kwa vile wengine hawana hata mifugo ya kuwekakatika maeneo hayo. Kukosa mifugo ya kuendeleza eneohilo, kwa makusudi watu hao huona kuwa mbadalaunaobakia ni kupangisha maeneo hayo kwa wawekezajikutoka nchi jirani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi Rasmi ya Upinzaniinaona lingekuwa ni jambo la busara kama ushirika wawafugaji au mwekezaji mmoja mmoja kupewa ekari 1,000ikiwa eneo lote la ekari 10,000 lingegawanywa ili kurahisishauwekezaji wake na kufanya kuwa endelelevu. Kwa eneodogo uwezekano wa kupata mkopo toshelezo kwa uwekezajitoka benki zetu na asasi zingine za fedha ni rahisi kwani hatainvestment risk inakuwa ni ndogo na inakuwa imesambaakwa wawekezaji wengi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati Waziri akijibu swalinamba 26 kuhusu maeneo ya Ranchi za Mkoa wa Kagera;je, kwa nini Serikali isiyarudishe maeneo hayo kwaniwaliopewa wanayakodisha kwa wafugaji toka nchi jirani?Je, ni Watanzania gani kwa majina waliogawiwa maeneokwenye ranchi hizo? Orodha ya majina ya WawekezajiWatanzania waliogawiwa maeneo hayo ya Ranchi ipo,nitaomba kukutana na Mheshimiwa Mbunge baada ya hapaili nimkabidhi orodha hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hadi sasa hivi majina hayoya wamiliki, Waziri ameshindwa kuyatoa kama alivyoahidindani ya Bunge. Hoja ni kwamba, kama kweli wamiliki niWatanzania; kwa nini wanashindwa kuweka majinahadharani? Hivyo basi, Kambi Rasmi ya Upinzani inamtakaWaziri kutoa kwa Wabunge majina hayo ya wamiliki na uraiawao hadharani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kuiwezesha Sekta yaMifugo kutoa mchango stahiki kwa Taifa hili ni lazimauboreshaji katika Sekta ya Mifugo ufanyike kwaniwanachokosa wafugaji wetu ni ardhi na elimu ya ufugajiyenye mafanikio kutokana na kutumia mbinu za zamani zakuzalisha mifugo.

Page 114: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

113

31 MEI, 2013

Changamoto kubwa katika Sekta hii ni kukosekanakwa mbinu za kisasa, vifaa na madawa ya uhakikakuhudumia wanyama. Aidha, mifugo mingi inatunzwa kienyejina matokeo yake kukosa soko la kimataifa kama zilivyo nchinyingine. Kama elimu ya kutosha itatolewa na kuruhusuwawekezaji wa ndani katika Sekta ya Mifugo, changamotohizo zitapungua kwa kiasi kikubwa na hivyo kutoa nafasi yaongezeko la bidhaa zitokanazo na mifugo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi Rasmi ya Upinzaniinasema wawekezaji wa ndani, kwa maana kwamba,wafugaji wa asili wao mtaji wao mkubwa ni mifugo na NARCOwao mtaji wao ni utaalam na miundombinu iliyopo tayari.Hivyo basi, ni rahisi ubia huo kati ya wafugaji wa asili naNARCO kuleta tija zaidi kuliko mwekezaji toka nje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na kuongezekakwa idadi ya watu, kipato na ukuaji wa miji kwa nchizinazoendelea Duniani, Tanzania ikiwa ni mojawapo, mahitajiya bidhaa za mifugo nayo yamekuwa yakiongezeka pia.Takwimu zinaonesha kuwa, Tanzania pekee itaongezamahitaji mara nne kwa mwaka 2030. Hivyo, ni jukumu laSerikali sasa kulieleza Bunge hili ni kwa vipi Wizara imejipangakukabiliana na changamoto ya ongezeko hilo la mahitaji yanyama kwa muda huo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi sasa ni asilimia mbili tuya mifugo yote inayozalishwa na kufugwa kibiashara, hivi sasaTanzania ina machinjio ya kisasa manne ambayohayatoshelezi kwani mahitaji ya nyama safi na salamayanaongezeka kila siku. Aidha, inaonesha kuwa, chini yaasilimia moja ya nyama yote iliyosindikwa ndiyo inazalishwahapa nchini na sehemu yote iliyobaki inaagizwa na kuingizwanchini kutoka Kenya. Vilevile taarifa hiyo inaonesha kuwa zaidiya tani 700 ya nyama safi inaaagizwa toka nje ya nchi kilamwaka wakati mahitaji ya nyama ndani ya nchi na Kandayetu ya ushirikiano yanazidi kuongezeka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanzania ni nchi ya pilinyuma ya Ethiopia kwa kuwa na mifugo mingi katika Bara la

Page 115: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

114

31 MEI, 2013

Afrika. Sasa kwa hali ya kawaida tu; inakuwaje nchi yetuinaagiza nyama kutoka nje ya nchi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanzania ina rasilimali kubwaya maliasili ikiwemo ardhi, malisho na idadi kubwa ya mifugo.Kati ya jumla ya hekta milioni 94 za rasilimali ya ardhi, hektamilioni 60 ni nyanda za malisho zinazofaa kwa ufugaji. Kwasasa kuna ng’ombe milioni 21.3, mbuzi milioni 15.2 na kondoomilioni 6.4. Mifugo mingine ni pamoja na nguruwe milioni 1.9na kuku wa asili milioni 58.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa taarifa yautekelezaji wa mpango na bajeti ya mwaka 2012/2013 namakadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2013/2014,Kiambatanisho Na. 3 kinaonesha kuwa, kwa mikoa 21, wilaya69 na vijiji vilivyopimwa 479, eneo la malisho ambalolinasadikiwa kuwa limetengwa kwa ajili ya wafugaji kuwa nihekta milioni 1.28. Hii ni sawa na asilimia 2.13 ya hekta milioni60 za nyanda za malisho katika nchi hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi Rasmi ya Upinzaniinamtaka Mheshimiwa Waziri awaeleze wafugaji kwang’ombe milioni 21.3 na mbuzi na kondoo milioni 21.5wanatakiwa wachungwe kwenye eneo la ukubwa gani?

Mheshimiwa Mwenyekiti, uzalishaji wa mifugoumegawanyika katika mifumo mikuu miwili ambayo ni ufugajihuria na ufugaji shadidi. Mfumo wa ufugaji shadidi japo siyomkubwa nchini, unatiliwa mkazo zaidi katika kuendelezaufugaji na uwekezaji kwani unachangia zaidi kwenye uchumiwa soko.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande mwingine,mfumo wa ufugaji huria ambao hufanywa na wakulima-wachungaji na wachungaji-wahamaji, ni mfumounaotegemea upatikanaji wa malisho na maji kwa msimuna matokeo yake husababisha wafugaji kuhamahama.Mfumo huu unakabiliwa na matatizo ya utunzaji duni wamifugo, matumizi duni ya teknolojia za kisasa, kuhodhi mifugo

Page 116: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

115

31 MEI, 2013

wengi zaidi ya uwezo wa ardhi na ukosefu wa mazingiramazuri ya masoko.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa utafitiuliofanywa na Asasi ya Kiraia ya Tanzania Pastoralists, Huntersand Gatherers Organization (TAPHGO), kuhusu mfumo wabiashara ya mifugo Tanzania, inaonesha kwamba, Sekta yaUfugaji Tanzania inachangia asilimia 18 ya Pato la Taifa,uzalishaji wa nyama kwa mwaka unakadiriwa kuwa ni tani259,800, kwa mifugo inayofugwa kwa ajili ya nyama pekeehuchangia tani 181,800.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, mchango wawafugaji ambao pia ni wakulima huchangia asilimia 98 yauhitaji wote wa nyama hapa nchini, huku asilimia mbili hutokakwenye Ranchi za Taifa. Wakati mbuzi na kondoo huchangiatani 75,800. Thamani ya nyama inayozalishwa inakadiriwakuwa ni shilingi bilioni 727.44, kati ya hizo shilingi bilioni 537.94zinachangiwa na nyama ya ng’ombe na zilizobaki shilingibilioni 189.5 ni kwa mbuzi na kondoo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Hotuba yaMheshimiwa Rais wakati wa kufungua mkutano wa uwekezajikwa shabaha ya kuibua maendeleo ya Mkoa wa Mara, kwakutumia rasilimali na utajiri uliopo mkoani Mara, lazima tuanzekutekeleza misingi ya ufugaji wa kisasa na tujipange vizuri kwauwekezaji kwenye sekta hii.

Naomba tutenge maeneo maalum ya ufugaji wakisasa. Kwa mfano, tukigawa maeneo ya ukubwa wa hekta2,000 kila moja na tukawagawia watu kwa ajili ya kufugakisasa, watakaopewa maeneo hayo wahimizwe nakusaidiwa wayaendeleze kwa malisho na huduma muhimuza maji, majosho, pamoja na za matibabu kwa mifugo.Maeneo hayo yakitumiwa kunenepesha ng’ombe wanyama, tunawezesha kuwepo kiwanda cha nyamakitakachonunua toka kwao mifugo ya kuchinja. Kiwandahicho kitatengeneza soko la uhakika kwa wafugaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kauli hiyo ya Mheshimiwa

Page 117: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

116

31 MEI, 2013

Rais imekuja muda ambao tayari maeneo mengi mazuriyaliyokuwa yanamilikiwa na Serikali yamekwishachukuliwa.Kama utaratibu ambao tumejaribu kuutolea maelezo kwakuangalia Ranchi za Mkoa wa Kagera jinsi gani migogoroiliyopo haimaliziki kutokana na ukweli kwamba wahusikawakuu katika migogoro hiyo ni Watendaji wa Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, changamoto kubwainayoikabili tasnia ya mifugo ni namna ya kufikia viwangovya ubora wa mifugo na mazao yake vitakavyokidhi mahitajiya soko la kikanda na kimataifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuonesha kuwawatendaji wanashindwa kutenganisha kati ya machinjio yakisasa na viwanda vya kusindika ni pale Waziri alipokuwaanajibu swali namba 27 kwa mujibu wa Hansard; “Je, hivisasa kuna viwanda vingapi vya nyama na vinasindika kiasigani cha nyama?” Jibu la Waziri lilikuwa: “MheshimiwaMwenyekiti, Tanzania inahitaji viwanda ama machinjiomakubwa takribani 16, yenye uwezo wa kuzalisha nyama tani133 kwa siku kwa kila kiwanda au kila machinjio.”

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi Rasmi ya Upinzaniinasisitiza tena ni kwa njia zipi utekelezaji wa Ilani unawezakufikiwa kama tafsiri ya kiwanda cha kusindika nyama namachinjio inaonekana kuwa ni kitu kimoja?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hali ya kawaida,ng’ombe wa asili hutoa maziwa lita 0.5 kwa siku wakati yulewa kisasa anatoa kati ya lita 7 – 30 kwa siku kutegemeanana matunzo na elimu ya ufugaji aliyonayo mfugaji. Hivyo basi,ili mfugaji wa ng’ombe wa asili aweze kupata lita 30 zamaziwa kwa siku, atahitaji kuwa na ng’ombe 15. Mbali namambo hayo yote ambayo yataenda na uwiano huo, lakinijambo la muhimu kwa mfugaji wa asili ni kwamba, madawayanayohitajika kwa chanjo, kuosha na kutibu magonjwa nizile zile kwa ng’ombe wote wa asili na wa kisasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili sekta hii ya mifugo iwezekuleta tija inayokusudiwa, huduma ya ugani ni muhimu sana,

Page 118: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

117

31 MEI, 2013

lakini kwa mtindo wa utendaji kazi kwa watoa huduma hiyoulivyo ni dhahiri tija inayotegemewa ni vigumu kupatikana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na watoa hudumakutokuwa na idadi maalum ya wafugaji wanaowahudumia,eneo maalum na hivyo kuweza kuwajibika kwa matokeoyatakayopatikana katika eneo husika ni tatizo kubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi Rasmi ya Upinzaniinaona itakuwa ni vyema kama kila afisa ugani atakuwa naorodha kamili ya wafugaji anaofanya nao kazi katika eneomaalum, kwani utaratibu huo utarahisisha upatikanaji wakumbukumbu sahihi na pia kuweza kupima utendaji wa afisahuyo.

Kwa mfano, kwa maafisa ugani wanaofanya kaziMkoa wa Kagera, ambao ni Watumishi wa Serikali (Ndg.Patrick, Ndg. Kashankoro, Ndg. Kanyambo na Ndg.Mutabazi), hawa wote wanamiliki Vitalu vya Ranchi. Hoja nije, utaratibu wa watendaji wa Serikali kujimilikisha mali zaWananchi unaendelea hata kwenye ngazi ya chini? Je,mgongano wa masilahi katika suala hili unashughulikiwa vipi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati Waziri Kivuli wa Fedhaakiwasilisha maoni ya Kambi ya Upinzani kwenye Muswadawa Fedha, tarehe 16 Agosti, 2012 alisema yafuatayo:“Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kifungu cha 12 chaMuswada, Serikali inatoa pendekezo la kufanyia marekebishoSheria ya Kodi ya Mauzo ya Nje ya Nchi, Sura ya 196, kwakuweka jedwali jipya ambalo linaongeza viwango vya tozokwenye ngozi ghafi inayosafirishwa kwenda nje ya nchi. KamaSerikali ina mpango madhubuti wa kuendeleza Sekta yaViwanda nchini na kuleta tija kiuchumi ni dhahiri kuwainatakiwa kusitisha uamuzi huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye hotuba yetu yabajeti tulipendekeza kuwa, Serikali izuie kabisa ngozi ghafikusafirishwa nje ya nchi na badala yake, ijikite kutafutauwezekano wa kuitumia ngozi hiyo hapa nchini na kuanzishaviwanda vya kutengeneza bidhaa zitokanazo na ngozi hiyo.

Page 119: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

118

31 MEI, 2013

Hata Kamati ya Fedha na Uchumi ilikuwa na mapendekezohayahaya. Hii ni kutokana na manufaa makubwa yakiuchumi wanayopata wenzetu hasa nchi ya Ethiopia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata katika Jumuiya yaAfrika ya Mashariki, wenzetu wa Uganda na Rwanda naowamezuia ngozi ghafi kuuzwa nje ya nchi. Mapendekezohaya ya Serikali yakibaki kama yalivyo, hayataifanya Serikalikupata mapato yanayostahili kwa sababu wafanyabiasharawengi wanatoa takwimu zisizo sahihi kuhusu mauzo halisiwatakayokuwa wanauza nje ya nchi (under invoicing).

Mapato ambayo Serikali inahofia kuyapoteza kwakupiga marufuku uuzaji wa ngozi ghafi nje ya nchi,yatapatikana tena kwa kiasi kikubwa kutokana na ajirazitakazopatikana katika viwanda vya kusindika ngozi, kodiya mapato kama vile PAYE na kadhalika. Sasa ni wakatimwafaka tuchukue hatua hii kwani hata nchi ya Pakistaniambao ndiyo wanunuzi wa ngozi yetu, wamepiga marufukukabisa uuzaji wa ngozi ghafi nje ya nchi yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nizungumzie Sektaya Maziwa. Taarifa ya uwezo wa viwanda na hali halisi ilivyosasa hivi inayonesha kuwa hadi sasa kuna viwanda 35 vyenyeuwezo wa kusindika zaidi ya lita 1,000 kwa siku kwa kila kimoja.Kati ya hivyo, ni viwanda 28 tu ambavyo vinazalisha hadi sasana vingine saba ama vimefungwa au kusimamisha uzalishaji.Kuna baadhi ya viwanda vinatumia hadi zaidi ya asilimia 80ya uwezo wake na vingine chini ya asilimia 16. Kwa vile kunaviwanda visivyozalisha kabisa, wastani wa matumizi ya uwezowa kusindika ni asilimia 12 tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uwezo wa jumla waviwanda vyote ni kusindika lita 428,500 kwa siku, lakini halihalisi ni kusindika lita 52,330 kwa siku. Hali hii inaonesha kuwa,juhudi kubwa zinahitajika ili kuwezesha Sekta ya Viwanda vyaMaziwa kuwa na uwezo wa ushindani na kutoa mchangomkubwa kwenye uchumi wa taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, matatizo yanayovikabili

Page 120: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

119

31 MEI, 2013

viwanda vya maziwa ni mengi na yanahitaji uchunguzi wakina katika kila kiwanda ili kutoa ushauri kwa kila kiwandahusika, lakini matatizo yaliyotajwa na viwanda vyote ni kamayafuatayo:-

- Ukosefu wa maziwa ya kutosha. IngawaTanzania inakadiriwa kuzalisha lita 1,400 milioni za maziwakila mwaka, kiasi cha maziwa yanayopatikana kwa ajili yakusindika ni kidogo sana. Hali hii inatokana na maziwa mengikuzalishwa na wafugaji wa jadi, ambayo kiasi kikubwakinatumika na wafugaji wenyewe, uzalishaji ni wa msimu naukusanyaji ni mgumu. Wafugaji hawa ndiyo huzalisha asilimia70 ya maziwa yote nchini.

- Upungufu wa maziwa ya kusindika ambaohuwa zaidi wakati wa kiangazi unachangiwa na sababunyingi ambazo ni gharama kubwa na ugumu wa kukusanyamaziwa ya wafugaji waliosambaa maeneo ya mbali;ushindani na wachuuzi wadogo wadogo; faida ndogokutokana na matumizi kidogo ya uwezo wa viwanda; nauzalishaji wa msimu ambapo maziwa mengi hupatikanamsimu wa mvua na kidogo sana wakati wa kiangazi na hivyokushindwa kutosheleza

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuhakikisha kuwaviwanda vya maziwa vilivyopo vinapata maziwa ya kutosha,Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kuhakikishakwamba, maziwa yanayozalishwa na wafugaji wadogo auwa asili yanauzwa kwenye vituo maalum vya kukusanyiamaziwa na pia maziwa yasiuzwe kwa wanunuzi bila yakuyasindika. Kufanya hivyo kutaondoa kwanza matatizoambayo yanaweza kutokana na magonjwa ya kuambukizwakati ya mifugo na binadamu (zoonotic deseases).

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia liwe ni jukumu laHalmashauri kulinda soko la maziwa yaliyosindikwa na kwanjia hiyo wafugaji wadogo na wale wa asili, maziwa yaoyatakuwa na uhakika wa soko badala ya sasa ambapowakati wa msimu wa mvua maziwa yanakosa soko na hivyokumwagwa.

Page 121: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

120

31 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa maziwa kuuzwamoja kwa moja na wafugaji wadogo na wakubwa ni upotevuwa mapato; hivyo basi, Kambi Rasmi ya Upinzani inaitakaSerikali kuwa, liwe ni jukumu la Halmashauri kutunga kanunindogo za kuhakikisha viwanda vya maziwa vinalindwa kwakupata maziwa muda wote ili kiwanda kiweze kulipa kodikwa Halmashauri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mbali na matatizo yakimfumo na sera, pia katika kundi hili kuna matatizo ya urasimukatika vyombo vya kudhibiti ubora kama TBS, kuwa navyombo vingi vya udhibiti, wadau kutoshirikishwa katikamaandalizi ya sera na migogoro kati ya wafugaji nawasindikaji na vyama vya wadau visivyo imara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi Rasmi ya Upinzaniinaitaka Serikali kuwepo uwajibikaji kwenye vyombo vyaudhibiti na vyombo hivi madhumuni yake yawe ni kuwezeshana siyo kukwamisha. Inapendekezwa kuwa, shughuli zote zaudhibiti wa Sekta ya Maziwa zifanywe na Bodi ya Maziwa,tofauti na sasa ambapo vyombo vingi hufanya hivyo. Aidha,Bodi ya Maziwa iliyoanzishwa kisheria, iwezeshwe kufunyashughuli zake kwa kupewa rasilimali zinazotakiwa tofauti nasasa ambapo Bodi ipo kwa jina tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, wadau washirikishwekatika utayarishaji wa Sera zinazohusu Sekta ya Maziwa, kwanisasa wanaohusishwa ni wale wenye viwanda vya maziwa.Je, wafugaji wa asili wanahusishwa vipi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, matatizo mengine ni kamakipato kidogo cha Wananchi, wawekezaji kuwa na miradimingi kwa pamoja, Sekta ya Maziwa kutokuwa na mvuto kwawawekezaji, ukosefu wa vyombo vya mikopo ya muda mrefuna riba ndogo na kutokuwa na maeneo maalum, yenyemiundombinu ya kutosha ya kujenga viwanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi Rasmi Upinzaniinaitaka pia Serikali itafute njia ya kuimarisha Vyama vyaKitaifa vya Wadau (TAMPA, TAMPRODA), ili viwe kweli vya

Page 122: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

121

31 MEI, 2013

Kitaifa na vyenye uwezo wa kushirkiana na Serikali kundelezasekta.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nguzo ya 7 aya ya 7.2.3 yaKILIMO KWANZA inayosema kwamba; “Kuainisha nakuimarisha uwezo unaohitajika kwa kuendeleza Sekta yaMifugo, kwa mwaka 2010 Serikali pamoja na TPSF, ilitakiwakukarabati viwanda vyote vya maziwa vilivyopo nchini nakuanzisha vituo vya kukusanyia maziwa.” Kambi Rasmi yaUpinzani inaitaka Serikali kulieleza Bunge na wadau kwenyeSekta hii ya Maziwa utekelezaji wa nguzo hii ya KILIMOKWANZA imetimizwa kwa kiasi gani?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa Mpango waMaendeleo wa Miaka Mitano inaonesha ili Sekta ya Mifugoiweze kuleta tija tarajiwa, ilitakiwa kwa Mwaka wa Fedhawa 2013/2014 ipewe shilingi bilioni 275.98 kama fedha zamaendeleo. Kwa masikitiko makubwa, mwaka huu wa fedhaWizara imetengewa jumla ya shilingi bilioni 8.97.

Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kulielezaBunge ni kwa nini imeshindwa kutekeleza matakwa yaMpango wa Maendeleo ambao ulipitishwa na Bunge?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanzania inamiliki maeneomakubwa ya maji ambapo rasilimali za uvuvi hupatikana kwawingi. Maeneo hayo ni pamoja na Ziwa Victoria, ZiwaTanganyika, Ziwa Nyasa, Mabwawa (Nyumba ya Mungu,Mtera na mengine mengi ya asili), Mito (Rufiji, Ruvu, Kilomberona kadhalika), malambo na maeneo oevu ambayo yanafursa kubwa ya uvuvi hapa nchini. Aidha, kuna Bahari ya Hindiambayo ina maeneo mawili ya Bahari ya Taifa (Territory Sea)na Ukanda wa Uchumi wa Bahari (Exclusive Economic Zone- EEZ).

Sekta ya Uvuvi inatoa mchango mkubwa katikakuwapatia Wananchi ajira, lishe, kipato na kuiingizia nchifedha za kigeni. Uvuvi nchini huendeshwa na wavuvi wadogotakriban 200,000 ambao huvua asilimia zaidi ya 90 ya samakiwote wanaovuliwa nchini. Zaidi ya Wananchi 4,000,000

Page 123: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

122

31 MEI, 2013

hujishughulisha na kujikimu kutokana na shughulizinazoendana na uvuvi hapa nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na uharibifu uliopokatika uvuvi umesababisha kuwepo kwa upungufu mkubwawa rasilimali ya uvuvi, hususan katika Ziwa Victoria, ambalohuongoza kwa upatikanaji wa samaki aina ya Sangaraambao wamepungua kutoka tani 676,000 mwaka 2006 haditani 331,000 mwaka 2009. Hali hii imetokana na sababuzifuatazo:-

- Ongezeko la kasi ya matumizi ya zana haramupamoja na ongezeko la idadi ya wavuvi kutoka 92,529mwaka 2000 hadi 105,016 mwaka 2008;

- Ongezeko la vyombo vya kuvulia samakikutoka vyombo 30,171 (2000) hadi vyombo 52,174 (2008);

- Ongezeko kubwa la mahitaji ya samaki namazao yake katika soko la samaki ndani na nje ya nchi nahivyo kuwa kichocheo kikubwa cha samaki wachangakuvuliwa. Kwa upande wa Bahari ya Hindi, mathalani rasilimaliya kambamiti imepungua kiasi cha kusababisha uvuvi wakekwa meli kubwa kufungwa hadi sasa. Aidha, rasilimali yaKambamiti (Prawns) imepungua kutoka tani 1,320 kwamwaka 2003 hadi kufikia tani 205 mwaka 2007.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na uwepo waongezeko la mahitaji ya samaki na mazao yake katika soko,wavuvi wamekuwa wakiilalamikia Serikali kuwa inakwamishaau kuwahujumu kwa uchomaji wa nyavu za wavuvi ambaohata hawaelewi ni kwa nini wanauziwa nyavu zisizostahili kwamujibu wa Watendaji.

Ukweli ni kuwa, nyavu zote kustahili au kutostahiliinategemea unavua samaki wa aina gani na nyavu hizozinatumika namna gani; hivyo basi, kitendo cha kuchomanyavu za wavuvi (zana za uvuvi) bila ya kuhakiki matumiziyake na bila ya kutoa nyavu (zana mbadala) ni hujuma kwasekta hii ya uvuvi na wavuvi wenyewe. Kumekuwepo na tabia

Page 124: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

123

31 MEI, 2013

ya kufunga ziwa au kusitisha shughuli za uvuvi kiholela, bilataarifa au sababu za kisayansi zinazotolewa kwa wavuvi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano wa tabia hii yenyekujenga hisia ya chuki za Wananchi kwa Serikali yao ni ZiwaBasotu. Hili Ziwa limeingizwa kwenye mitego, chambo nachuki au ulipizaji visasi vya kisiasa tu. Kumewekupo na shinikizola ulipazaji kisasi wa kisiasa kwa kufungiwa Ziwa mara kwamara ili wataabike, wasipate kitoweo na kipato na kuvurugamfumo wao wa maisha ya kila siku, lakini siyo ukweli wa halihalisi kuwa kuna uvuvi usiofaa.

Je, haya ndiyo maendeleo ya Sekta ya Uvuvi? Hivijambo la kisayansi linaendeshwaje kisiasa? Nadhani haya siyomaendeleo tuliyotarajia kwa mujibu wa Ilani za CCM zamwaka 2005 - 2010 na 2010 - 2015 bali ni hujuma naupandikizwaji wa mbegu mbaya za chuki za kisiasa tu.

Kambi Rasmi ya Upinzani inamtaka Waziri awaelezeWananchi wa Basotu kwanza ni nani mwenye mamlaka yakusitisha uvuvi katika Ziwa na hatua zipi ambazo piazinashirikisha wadau zinapaswa kufuatwa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, shughuli za ufugaji wasamaki hufanywa na wafugaji wadogo. Hata hivyo, ufugajiwa samaki lazima ushindane na shughuli zingine za vijijini kwaeneo la ardhi, maji, nguvu kazi na vyakula. Hali hii hupelekeaumuhimu wa kutathmini gharama na faida ya ufugaji samakina mchango wake kwa maisha ya wakazi wa vijijini kulinganana shughuli zao zingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, zaidi ya hayo, ufugaji wasamaki hukabiliwa na matatizo na changamoto zingine kamaukosefu wa sera thabiti ya ufugaji samaki; mabadiliko katikasera za uchumi; ukosefu wa teknolojia bora; upungufu wavifaranga bora; miundombinu duni ya usafiri; utafiti usiokidhimahitaji; ukosefu wa takwimu za uzalishaji; na upungufu wataarifa sahihi za utunzaji wa bwawa la samaki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kuwa na uwezo wa

Page 125: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

124

31 MEI, 2013

kufanya shughuli kwa mafanikio, ni muhimu kuwa na takwimuya utendaji na shughuli husika. Vivyo hivyo, ili kuendeshashughuli za ufugaji samaki kibiashara, mfugaji analazimikakuchukua na kutunza takwimu kwa hatua zote au shughuliyoyote anayoifanya ikiwemo ya kutunza matumizi na mapatoya fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa Mpango waMaendeleo wa Miaka Mitano, Sekta ya Uvuvi kwa Mwakawa Fedha wa 2013/2014 ilitakiwa itengewe jumla ya shilingibilioni 60.896 ili sekta nzima ya uvuvi iweze kuleta tija stahili.Pamoja na faida zingine ni kwamba, kama uwekezaji kwamujibu wa mpango hadi 2015, makusanyo ya Serikali kwamwaka katika sekta hii yalifanikiwa kukua kutoka shilingi bilioni6.58 hadi shilingi bilioni 12.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi Rasmi ya UpinzaniBungeni inaitaka Serikali iwaeleze Watanzania ni kwa niniSerikali imekinzana na Mpango wa Maendeleo uliopitishwana Bunge?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia mwenendo waBajeti ya Wizara kwa miaka minne inayoonesha kuwa Bajetiambayo imekuwa ikitolewa kwa Wizara hii imekuwa ikishuka,Mwaka wa Fedha wa 2010/2011 zilitengwa shilingi bilioni 58.8,mwaka 2011/2012 zilitengwa shilingi bilioni 57.2, mwaka 2012/2013 zilitengwa shilingi bilioni 54.6 na kwa mwaka huu wafedha zimetengwa shilingi bilioni 47.18.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi Rasmi ya Upinzaniinatoa tafsiri ya kupungua huko kwamba ni fundisho kwawatendaji wa Wizara, kuangalia fursa za mapato ambazozipo katika Wizara hiyo, zifanyiwe kazi na ziweze kuwekezwakwa maendeleo ya sekta hizi mbili (Mifugo na Uvuvi); nakwamba, kutokana na ukweli uliopo wa fursa hizo, Wizaraimelala na hata kusimamia sheria na kanuni zilizopo zakuhakisha mirabaha ya uvuvi inalipwa au imeshindwa nawajanja wanaovuna rasilimali yetu bila nguvu yoyote yaziada.

Page 126: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

125

31 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi Rasmi ya UpinzaniBungeni inayoongozwa na CHADEMA, inasema kwamba,Wizara hii kwa kipindi kirefu imekuwa kama nyumba isiyokuwana msimamizi, kiasi kwamba, rasilimali za nchi hii zimekuwazikigawiwa, zikivunwa na kutumiwa bila kufuatwa kwa sheriana kanuni. Mfano mmojawapo ni ugawaji wa mashambaya Ranchi za Taifa na kilichofuata ni nchi kuingia kwenyemigogoro mikubwa kati ya wafugaji na wakulima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuonesha kuwaSerikali imeshindwa kuthamini Sekta ya Mifugo kwa ujumla,mwaka 1981, Mwasisi wa nchi hii, Marehemu Mwalimu J. K.Nyerere, akiwa Morogoro alisema: “Tumetenga kwa mfano,maeneo maalum kwa ajili ya mazao kama pamba, kahawa,tumbaku na katani, lakini hatujatenga maeneo kama hayokwa ajili ya mifugo. Tumetenga maeneo maalum kwa ajiliya pundamilia (Hifadhi za Taifa), lakini wafugaji wananing’iniahewani tu.”

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi Rasmi ya Upinzaniinaona kama kungekuwa na umakini katika Serikali hii yaCCM ni dhahiri kuwa, makosa ambayo yalikuwayanatendeka huko nyuma, ulikuwa ni muda mwafaka wakurekebisha makosa katika Sekta hii ya Mifugo na hivyoyanapelekea wafugaji kuwa wahamiaji au watu wasiohitajikakatika nchi yao kama ilivyo sasa.

Mheshimiwa Menyekiti, mwisho lakini kwa umuhimumkubwa ni shukurani kwa wanachama na wapenzi wote waCHADEMA nchi nzima na hasa Wilaya ya Hanang, kwakushirikiana na mimi, kwa kazi zote tunazozifanya bega kwabega kwa ajili ya maendeleo ya Wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo,naomba kuwasilisha. (Makofi)

MWENYEKITI: Ninakushukuru. WaheshimiwaWabunge, bila kupoteza muda, ninaomba nimwitemchangiaji wetu wa kwanza, ambaye ni Mheshimiwa CharlesMwijage, atafuatiwa na Mheshimiwa Dkt. Festus Limbu, kama

Page 127: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

126

31 MEI, 2013

muda wetu utatosha, lakini ninaomba hawa wawili angalauwapate nafasi.

MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: MheshimiwaMwenyekiti, ninakushukuru sana kwa kunipatia fursa.Nimelazimika kurudi, nilikuwa kwenye majukumu mazito yakitaifa, lakini na hili la Wizara ya Mifugo na Uvuvi linanihusu.Nisije nikafanana na mtu aliyelisha watoto wa kwale, watotowa kuku wakafa njaa. Nimelazimika kurudi ili nizungumziesuala la mgogoro wa NARCO na Serikali kwa upande mmojana Wananchi wangu wa Kata ya Lutoro. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwaeleze binafsi miminakula nyama. Napenda ng’ombe na ninafuga; ninafugaDar es Salaam na ninafuga kijijini kwangu Ilogero. Sinauhasama na mtu anayefuga. Jitihada za ufugaji katikaRanchi ya NARCO, zilipelekea maafa ya unyama dhidi yautu. Ninaishauri Serikali yangu na ndiyo maana ninasemasijui niseme namna gani; ninaishauri Serikali yangu, kiasi chapesa kilichotengwa cha shilingi bilioni 47, kwa kazi niliyonayohakitoshi. Mimi nina kazi kubwa, shughui za mifugo zimeletamatendo mabovu dhidi ya ubinadamu.

Nakwenda zaidi; katika taarifa ya Mheshimiwa Wazirisijaona kitu. Mimi ninafikiria maridhiano, ninaishukuru Serikali,ninaishukuru Wizara na hasa hasa Naibu Waziri na KatibuMkuu wa Wizara ya Mifugo, wamekuwa mstari wa mbelekufuatilia ule mgogoro wa Lutoro wanautatua. Serikali naWizara hii wako mstari wa mbele sina matatizo nao. Tatizolangu ni wale watekelezaji wa chini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, umefanyika unyama. Wazirihakufanya unyama kule. Waziri hajambambika mtu kesi.Waliobambika kesi baada ya kumaliza mgogoro wenu huuinabidi mfanye maridhiano. Mfanye maridhiano kama watuwa South Africa. Katika Kata yangu ya Lutoro akionekanaPolisi watu wanakimbia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ninakuja hapamahususi kuomba pesa zaidi ziongezwe ili zielekezwe katika

Page 128: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

127

31 MEI, 2013

kutatua migogoro hiyo ambayo Wananchi na Wabungemnaisikia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa ProfesaMwakyusa, Mheshmiwa Waride, Mheshimiwa Dkt. Kamani,kwa kutaja baadhi, ni watu ambao walifika Kashenambonikatika Kata yangu ya Lutoro. Mheshimiwa Waride alilia namimi nillia. Kwa hiyo, mtu yeyote anayezunguka nchi hiiakisema Mheshimiwa Mwijage anachochea, hajui uchunguwa mwana. Niko Bungeni kwa sababu nilichaguliwa naWananchi, full stop. Kwa hiyo, mtu anayeingilia mchezo huu,jitihada zangu kwa kubeba Ilani ya Chama ni kwamba, sisitunatetea Wananchi na suala hili nimelipeleka juu mpakaofisi ya juu kabisa na Mwenyekiti wa Chama changualinihakikikishia, Naibu Waziri alikuwepo kwamba, maslahi yaChama cha Mapinduzi ni Wananchi na siyo ng’ombe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba pesa ziongezwe,migogoro ya Lutoro iishe, migogoro iliyoko Misenyi iishe, tuanzeukurasa mpya. Zaidi ambacho ninakielekeza kwa Serikali nahasa Waziri wa Mambo ya Ndani, kuna haja ya maridhiano.

Mtoto wa Lutoro, ukimwambia Polisi anakuja hataangelikuwa ana miezi mitatu utamlaza kwenye umande nahawezi kulia. Kwa hiyo, Wananchi wamejenga hofu kwaWatendaji wa Serikali hasa Jeshi la Polisi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika nchi ya Marekani,kuzungumza suala lililoko Mahakamani siyo tatizo, Tanzanianinasikia inazuiwa. Ndugu zangu mlioko ndani kwa kesi zakubambikizwa, mnakufa, mnateswa, lakini mateso yenuyatawakomboa ndugu zenu wa Lutoro na mimi niko nao.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kumaliza suala laLutoro, ninaomba niishauri Serikali yangu kamailivyozungumzwa katika bajeti zenu, mwombe pesa zaidituwekeze kwenye Pasture Management. TuwahimizeWananchi wetu kuwa na Pasture. Sisi tunazo hifadhi nyingi,asilimia 28 ya nchi yetu ni Hifadhi, wakati umefika sasa wa

Page 129: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

128

31 MEI, 2013

kupunguza Hifadhi na kutengeneza Ranching Association iliWananchi wetu hao ambao mnasema wanatangatanga,hawatangitangi, wanatafuta malisho; mtengeneze RanchingAssociation ili tuwaweke. Ningelipenda Wananchi wapewemaeneo waweze kufuga katika maeneo ambayowanaangaliwa.

Mheshimiwa Mwneyekiti, ninarudia, sitafuni maneno;nisingelipenda kulisha watoto wa kwale, wakati watoto wakuku wanakufa. Wako ndugu zangu Wasukuma wamekujakwangu, lakini wameburuzwa, wamepigwa risasi; lakinianapotokea mtu kutoka atokako kule nje ya nchi yangu,anapoguswa Polisi nywele zinawasimama na Viongozi wotewanaanza kusema Mwijage anachochea migogoro.Sichochei migogoro, ninataka kulisha watoto wa kukuwanenepe, mimi Msukuma ni ndugu yangu, kwanza,tutosheke sisi kabla ya kuwakaribisha wengine.Anayewakaribisha kama ana masilahi yake atajijuamwenyewe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie suala la samaki.Samaki katika Ziwa Victoria wamekuwa wana mahitajimakubwa. Kuna uvuvi kupita kiasi. Sisi watu wa Kerebe,Gospa, Makibo, Kinagi na Bumbile, maisha yetu ni samaki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumezungumza naMheshimiwa Waziri na ndiyo maana ninamwombea pesa.Kwamba, Wananchi wale mwangalie namna yakuwawezesha, muwape zana za kisasa na muwaelekezenamna ya kuvua kitaalam na ndiyo maana ninaomba pesazaidi kwa ajili ya watu hawa. Ninaomba pesa kwa ajili yaWizara hii ili waweze kupata pesa zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, majilio ya mahitaji makubwaya samaki, yamepelekea Wananchi kwenda kufuga. Kwetusisi tumekwenda mbele zaidi, Wizara inajua, Mheshimiwa Dkt.Charles anajua, J & B, Kituo cha Ufugaji Samaki cha Ruanda,kimeshakwenda mbele na ninaishukuru Serikali imewapelekawatu wangu, wapambanaji wangu Vietnam. Tunachoomba,

Page 130: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

129

31 MEI, 2013

Taasisi za pesa ziende kasi, panapoonekana kwamba mtuanakopesheka, urasimu upungue.

Mheshimiwa Mwenyeiti, ninaomba niwaeleze kitukimoja; kuna jambo huwa ninalisema kila siku la allocationadvantage. Nchi za Magharibi mwa Tanzania hasa Congo,nchi ambazo zinajengwa sana, wanahitaji samaki. Huwezikuamini, samaki wanapita kwenye makontena wakitokakatika nchi za Uajemi, wakitoka Mashariki ya Mbali,wanasafirishwa kwenda katika nchi za Congo ambakouchumi unakua kwa kasi. Sisi tunayo mito, hata nisipoitajamnaijua; mito yetu sisi ikiandaliwa vizuri, tukapewa mitambohiyo ya kisasa kama waliyoomba watu wa J & B, watu wotewakafuga, tutaondoa umaskini, tutapata lishe na tutawezakuongeza Pato la Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa muhtasari, ninasimamahapa kuiomba Serikali angalieni, wanasema jungu kuu halikosiukoko, siridhiki mimi; mipangilio ninaiunga mkono, hasa lile lakumaliza migogoro, lakini pesa shilingi bilioni 47 zilizotengwa,ninaomba chondechonde tuangalie. Unaweza ukawawewe unashabikia kutafuta umeme katika nyumba yako,lakini wenzako Urutoro na wapi, wanateketea kwa matesokwa sababu ya migogoro. Ninaomba pesa ziongezwe iliWizara ya Mifugo waweze kwenda vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachoomba zaidi,Wananchi wengi wako kwenye ufugaji. Wizara ya Mifugona Uvuvi iwezeshwe, kusudi vyuo vyao vya Mifugo viwezekufundisha wanafunzi wa miaka miwili, wa mwaka mmojana hata wa miezi mitatu. Wafundisheni wafugaji wetuwaweze kujua ku-handle mambo haya. Itawezekana kwakuwa na Vituo vidogo vidogo vya kuwawezesha Wananchikwenda Kisasa. Pasture Management itafundishwa kwavipindi vifupi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kuyasema hayo,ninaomba niseme ninaishawishi Serikali yangu, Serikali Kuu,kwenye Fuko Kuu, mwongeze pesa kwenye Wizara hii, iliWizara hii iende kutekeleza majukumu hayo.

Page 131: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

130

31 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru naninaendelea na majukumu yenu mliyonipa. Ahsante sana.(Makofi)

MWENYEKITI: Ninakushukuru sana MheshimiwaMwijage, ninafikiri kule Lutoro wamekusikia. Sasa ninaombanimwite Mheshimiwa Dkt. Festus Limbu.

MHE. DKT. FESTUS B. LIMBU: Mheshimiwa Mwenyekiti,ninakushukuru kwa kunipa fursa niwe mchangiaji wa mwishomchana huu. Kwanza, naipongeza safu ya Wizara, mmekaavizuri mmetulia, tatizo lenu hamna Bajeti ya kutoshakutekeleza majukumu. (Makofi)

Mna Sera ya Mifugo nzuri ya mwaka 2006. MnaProgramu ya Kuendeleza Mifugo ya 2001, imekaa vizuri kabisana Programu ya Kuendeleza Uvuvi. Mnafanya kazi nzuri,endeleeni na mimi niungane mkono na Wabunge wenzangu,akiwemo Mheshimiwa Charles Mwijage, aliyemaliza kuongeasasa, Wizara iongezewe fedha. Kamati ya Kilimo, Maji naMifugo, imeomba Serikali iongeze shilingi bilioni 40; mimininaunga mkono hilo lifanyike. (Makofi)

Kwa sababu unapoweka shilingi bilioni nne kwa sektakama hii, kwa ajili ya Maendeleo ya Sekta, shilingi bilioni nnefedha za ndani, huitendei haki Sekta hii. Sekta muhimuambayo ni mboga na kitoweo. Nchi yetu ni ya pili katikaAfrika kwa wingi wa mifugo, baada ya Sudan kugawanyikatulikuwa wa tatu, sasa tumekuwa wa pili, baada ya Ethiopia.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara ilikuwa imeombashilingi bilioni 163 wamepewa 47. Ninarudia, fedha hizi chondechonde ziongezwe. La pili, Wananchi wa kutoka Jimbo laMagu, Wafugaji ambao sasa wanaitwa Wachungaji,wameenea maeneo mengi na Mheshimiwa Mwijageamenisaidia kusema katika Jimbo lake la Muleba Kaskaziniwapo Wasukuma; Wasukuma wale wengi wanatokaMwanza, wanatoka Magu. Mkoa wa Mwanza ni wa pili kwaidadi kubwa ya watu katika nchi hii baada ya Dar es Salaam;

Page 132: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

131

31 MEI, 2013

kwa hiyo, hakuna mahali pa kulisha mifugo, hakuna mahalipa kuchungia na ndiyo maana sasa inabidi waende mahalipengine wanaitwa wahamiaji; na hawako Kagera tu; wapoMpanda, wapo Morogoro, wapo Kigoma, wapo Lindi nasehemu mbalimbali. Wengine walikwenda mpaka Ihefu nawamepoteza mali nyingi wakati wanahama kwenda Lindi,mpaka Zambia wengine wanajaribu kufika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ninaombanipendekeze; hatuwezi kukaa tunalialia kama vile sisi nimaskini. Tanzania siyo maskini hata kidogo. Tanzania eneolake, ujumlishe Kenya, ujumlishe Uganda, ujumlishe Rwanda,ujumlishe Burundi, ujumlishe Comoro, ujumlishe Shelisheli, zote.(Makofi)

Tunalo eneo kubwa la kutosha, kufanya mambo yetuna kupanga mambo yetu vizuri. Tumefanya uamuzi mzuri,lakini siyo wa busara sana; asilimia 25 ya eneo letu tumewekaHifadhi za Taifa ambazo ziko 13. Mapori ya Akiba ambayoyako 29 na maeneo yaliyodhibitiwa (Controlled andProtected Areas 40). Jumla haya yote yanakula asilimia 25ya eneo letu. Asilimia 25 unaweka kwa ajili ya wanyamapori,lakini usawa wa wanyama uko wapi; unapendeleawanyama wa porini, hawa wanyama wanaofugwa nabinadamu huwapi stahili yao, hiyo siyo sawa sawa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lililotengwa kwa ajiliya Hifadhi, ni sawa sawa linakaribia na eneo na Uganda yote.Uganda nzima imetengwa kwa aji l i ya Hifadhi yaWanyamapori; hiyo siyo sawa sawa. (Makofi)

Ninaomba hili eneo lililohifadhiwa limegwe asilimia 25,libaki asilimia 75 ili asilimia 25 ambayo ni kilometa za mraba60,000, ambayo ni karibia hekta milioni sita, wagagiwewafugaji. Lengo la kutenga haya mapori lilikuwa ni zuri nasipingani na uhifadhi, naomba nieleweke. Unapokuwa unamatatizo ya idadi ya watu, migogoro ya wafugaji nawakulima na Serikali, huwezi kuendelea kushikilia eneo hili kwaHifadhi ya Wanyama.

Page 133: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

132

31 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba tuvunje angalauHifadhi mbili. Ninapendekeza kwa Serikali, iangalie Hifadhimbili au tatu zivunjwe tubaki na Hifadhi kumi ama tumegemaeneo katika Hifadhi zetu ili turuhusu wafugaji. KuleSerengeti yatafutwe maeneo ili wapewe wakulima. KuleMaswa Game Reserve nako yatafutwe maeneo wapewewakulima na kwenye maeneo mengine kwenye Ranchi zetuzote, kwenye Hifadhi zetu zote, hili lifanyike, asilimia 25 naeneo hili likitengwa asilimia 25 ni sawa sawa na Mikoa yaDodoma na Mkoa wa Kilimanjaro kwa pamoja. Kwa hiyo,tuwatengee wafugaji wa Mkoa wa Dodoma, eneolinalolingana na Mkoa wa Dodoma, ujumlishe na Mkoa waKilimanjaro ili tuwatengenezee utaratibu mzuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitatoa mfano wa jinsi watuwanavyohangaika. Bangladesh, nimesoma kule mwakammoja; ina eneo asilimia 16 ya eneo la Tanzania. Asilimia 16nchi hiyo ya Bangladesh. Tanzania, idadi ya watu ni asilimia28 peke yake, lakini wamejitosheleza kwa chakula naumaskini umepungua kwa asilimia 25 toka miaka ya 90. Wanashida na wamejibana. Tusione tu kama sisi haya matatizohayatugusi. Migogoro hii lazima majibu yake tuyapate naninapendekeza hilo lifanyike. Tuweke vichwa vyetu pamoja,siyo matumbo yetu pamoja, tuthubutu, tufanye maamuzimagumu. (Makofi)

Tuangalie maeneo ambayo tutaongeza il iwakafundishwe kule kufuga kisasa na kufanya kamawanavyofanya nchi nyingine. Wote hapa tunatembea,tunafanya ziara kwenda Botswana, tunakwenda Argentina,kote ambako wameendelea, tunaona jinsi wanavyofanya;kwa nini sisi hatufanyi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni matumaini yangukwamba, Serikali itasikia kilio cha wafugaji na kilichotokeaIfakara kwa wafugaji, kwenye lile Bonde ambako tunahifadhimnyama anayeitwa Sheshe, lakini watu wamepata maumivumakubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mambo mengine tuyafanye

Page 134: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

133

31 MEI, 2013

lakini tuwe na moyo wa kibinadamu. Ninashukuru angalaubaadhi ya wakulima wamerudishiwa mashamba. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema haya,ninaomba nikushukuru sana. Ninaamini Serikali itasikia kiliocha Wabunge, kwamba Bajeti ya Wizara hii iongezwe iliwakachape kazi na kuleta maendeleo ya nchi hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Ninakushukuru sana Mheshimiwa Dkt.Limbu.

Waheshimiwa Wabunge, uwiano wa kuchangia leoni Wabunge 15 ambao wanatoka Kambi ya Chama Tawala,Wabunge watatu kutoka CHADEMA na Wabunge wawilikutoka CUF. Ninawashukuru sana Ma-Chieef Whip;Mheshimiwa Halima Mdee, ameshanipa orodha na utaratibuwa kuchangia kwa Wabunge wa CHADEMA; na Chief Whipwa Chama cha CUF, naye ameshanipa utaratibu kutokaChama cha CUF; na Chama cha Mapinduzi pia orodha tayariiko hapa mezani. Kwa hiyo, ninaomba WaheshimiwaWabunge wote, wawasiliane na Ma-Chief Whip wao, wajueutaratibu wa kwao wa kuchangia leo.

Niwataje wale watakaoanza mara tutakapoingiahapa saa 11.00 jioni. Tutamsikiliza Mbunge wa tatu wa Kambiya Chama Tawala, Mheshimiwa Lekule Laizer, halafu tutampanafasi Mbunge wa CHADEMA, Mheshimiwa Shibuda nabaadaye tutaendelea kama nilivyosema, uwiano wote wavyama kadiri ya Ma-Whip walivyowasilisha majina hapaMezani, tuweze kukamilisha uchangiaji wetu ndani ya Bungekwa siku hii ya leo.

Waheshimiwa Wabunge, baada ya kusema utaratibuhuo, ninaomba nisitishe shughuli hizi za Bunge na tutaonanatena ndani ya Ukumbi wa Bunge saa kumi na moja jioni.

(Saa 7.00 mchana Bunge lilifungwa mpaka saa 11.00 jioni)

Page 135: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

134

31 MEI, 2013

(Saa 11.00 jioni Bunge lilirudia)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, naombatuendelee na shughuli za leo na Mkutano wetu ni wa Kumina Moja, Kikao cha Thelathini na Tisa na Wizara iliyo mbeleyetu ni Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, hoja iliyo mbeleyetu kama ilivyotamkwa na Katibu na kama nilivyosemamajadiliano yanaendelea. Wakati nasitisha kikao saa sabamchana nilisema tutakaporejea tena Bungeni jioni hii,msemaji wetu wa kwanza atakuwa ni Mheshimiwa LekuleLaizer atafuatiwa na Mheshimiwa Magalle Shibuda. Kwa hiyo,naomba nimwite Mheshimiwa Laizer na Mheshimiwa Shibudaajiandae. Mheshimiwa Laizer!

MHE. MICHAEL L. LEKULE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi ili nichangie hotuba ya Waziriwa Mifugo na Uvuvi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza niishukuru sanaSerikali kwa kuona kwamba mwaka 2009 mifugo ilikufa sanakatika Majimbo yetu katika Wilaya ya Longido, Ngorongorona Monduli na wakatupa mifugo kwa ajili ya kifuta machozi.Nawashukuru sana kwani hali ilikuwa mbaya sana, kulikuwana watu ambao hawakubakiwa na ng’ombe hata mmoja,lakini Waswahili wao wakimwona Mmasai wanadhanikwamba, kila Mmasai ana ng’ombe lakini wakati huohawakuwa na ng’ombe kabisa.

Kwa hiyo, walipaswa kupewa ng’ombe kamawalivyopewa na Serikali. Namshukuru sana Rais kwa kuonahilo na kutupa mifugo na mifugo bado inaendeleakugawanywa kulingana na fedha zinavyopatikana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningependa kuzungumziabajeti ya Wizara hii, Wizara hii ndiyo wafugaji wote Tanzaniawanaitegemea, na nadhani wafugaji ni wengi kweli, nadhanikwa sensa hii, sikujua wafugaji watakuwa wangapi, lakininadhani wako zaidi ya 30% na wanategemea bajeti hii, lakini

Page 136: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

135

31 MEI, 2013

Wizara hii imepewa fedha kidogo sana na inapunguzwa kilamwaka. Kila bajeti wanapunguza na wanapopunguza ndiyowanadidimiza kabisa mifugo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara hii ndiyo tulitegemeawatuchimbie mabwawa, miaka yote iliyopita hatunamabwawa yaliyochimbwa kutokana na ufinyu wa bajeti.Wizara hii ndiyo tulitegemea itupatie majosho kwa vijijiambavyo havina majosho, lakini bado kila siku ni kilio. Wizarahii ndiyo tunategemea itupatie madawa, kama alivyosemaWaziri katika bajeti yake foot and mouth disease, ECF hayoni magonjwa sugu ambayo yanamaliza mifugo na kufanyawafugaji kuwa maskini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, dawa kwa sasa ya ECF doziya ndama mmoja ni sh. 8,000/= na mkubwa ni sh. 12,000/=,sasa kama ni wafugaji ndiyo wananunua na kutafutamadawa haya wengine wanashindwa kuchanja. Kwa hiyo,naona hali hii, sijui kwa nini Wizara imeundwa ambayo inajina la mifugo, lakini hakuna huduma ya mifugo. Hilo kwakweli ni jambo la mshangao, nataka Serikali iangalie kwabajeti hii na hatukubali fedha kidogo kama hizi, tunatakafedha za kutosha kwa ajili ya hayo niliyoyataja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni kuhusuminada. Wilaya yangu iko mpakani nadhani nategemeakatika idadi ya ng’ombe waliouzwa ambao Waziri alitajakwenye bajeti yake ng’ombe wa Longido hawapo na sisitunauza ng’ombe, lakini hatuuzi Tanzania tunauza Kenya nang’ombe wa Longido ndiyo ng’ombe bora Tanzania lakinihatuna masoko wala hatuna viwanda kuanzia Tarime,Ngorongoro, Longido na hata Monduli.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ng’ombe wote wanauzwaKenya na kwa sababu hakuna masoko ya kutoshelezamifugo, tunaomba Serikali hii na narudia kila bajeti kuombafedha kwa ajili ya kujenga soko mpakani kwa sababuwenzetu wanafaidi sana mapato ya mifugo kutoka maeneoyetu.

Page 137: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

136

31 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kenya hawana ng’ombebali wapo Tanzania, lakini wanajivunia kwamba wao ndiyowanauza nyama nyingi nchi za nje, wao ndiyo wanauza ngozilakini ni za ng’ombe wa Tanzania na nyama ni ng’ombe waTanzania, lakini pia wanarudisha nyama za ng’ombe waTanzania kuleta Dar es Salaam. Napenda Serikali isikilize kiliochetu kwa sababu kila siku tunalia kwamba hali ni mbaya.Kwa wiki ng’ombe wanaouzwa Bisi ni 3,000 kutoka Tanzania,sasa utapiga hesabu kwa mwaka watakuwa wameuzang’ombe wangapi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hali ni mbaya,pamoja na soko la ngozi, ngozi zinakwenda huko huko.Napenda Serikali iangalie sasa hali hii kwa sababu ni mbaya,kule ndiyo wanapata ruzuku na kodi ya mifugo na Tanzaniahawapati kodi ya mifugo kwa ajili ya ng’ombe wao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni migogoroya wakulima na wafugaji. Kwanza nawapongeza wafugajina wakulima wa Wilaya yangu ya Longido kwa sababu waohawana mgogoro, pamoja na kwamba wapo wakulima nawafugaji, lakini hawapigani. Nawashukuru sana na hawawafugaji na wakulima waige mfano wa maeneo yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mgogoro uliopo huku niunyanyasaji wa wafugaji kuvamiwa katika maeneo yao,popote pale ambapo wafugaji wapo, wakulimawanakwenda na kuweka maboma na kuanza kuwavamia.Kwa hiyo, naomba hali hiyo iangaliwe, pamoja na masualaya maeneo ya wanyamapori. Maeneo ya wanyamaporiyaangaliwe kwa sababu eneo lote la wanyamapori katikaLongido, Ngorongoro na Loliondo ni eneo la vijiji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2009 hakuna gamecontrol area itakayokuwa ndani ya vijij i, lakini badowanang’ang’aniza. Naomba ionekane kwamba, hayomaeneo ni maeneo ya vijiji na ni eneo la malisho ya vijiji.Hatuchukii wanyama wakiwa ndani ya maeneo hayo yamalisho, lakini l isi je likaonekana kwamba ni eneo lawanyamapori na siyo eneo la wafugaji.

Page 138: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

137

31 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalonapenda kusema ni kwamba, Serikali iangalie kuboreshamashamba ya NARCO. Serikali iipe NARCO fedha kwa ajiliya kuboresha mashamba hayo ili Tanzania ianze nayo kuuzanyama nje. Tuna mashamba makubwa tumeanza sasakuyabinafsisha, ni afadhali tuanze kuyafufua kulikokuyabinafsisha kwa sababu bado Serikali ina uwezo wakusimamia na Tanzania kuwa na soko la nyama katika nchinyingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, narudia kusema kwamba,kuna mgogoro mkubwa wa wakulima na wafugaji.Ukiangalia katika maeneo ya wafugaji yanavamiwa kila siku,ukienda Kiteto wakulima ambao hawapo katika maeneoyale wametoka Dar es Salaam na kila mahali na kwendakwenye maeneo ya wafugaji au malisho na kwendakufungua mashamba makubwa na bado inasemekana etiwenye haki ni wale wakulima walioacha maeneo yao nakuja kufungua mashamba. Bado hilo ni tatizo na ndivyo ilivyokatika maeneo yote. Naomba Serikali imalize mgogoro wawafugaji na wakulima kwa sababu inawezekana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru na naungamkono hoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Nakushukuru sana Mheshimiwa Laizer,lakini kabla sijamwita Mheshimiwa Shibuda ningeombawahudumu wa Ukumbi wa Bunge mahali popote walipo,warejee ndani ya ukumbi haraka kwani hatuna mtu wakutuhudumia humu ndani. Kwa hiyo, naomba sanawahudumu wetu wa Ukumbi wa Bunge mahali popotewalipo, nadhani wananisikia warejee ndani ya ukumbi waBunge.

Mheshimiwa Shibuda!

MHE. JOHN S. MAGALLE: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana kwa kunipatia fursa hii ili niweze kuchangiamawazo katika Wizara hii ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi.

Page 139: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

138

31 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa masikitiko makubwasana naomba kuwasilisha mawazo na maono ya wafugajiambao wako katika hali ngumu na ya matatizo makubwasana baada ya kuwa wafugaji wengi wanauawa na mifugoinauawa, dhuluma zilizopo, rushwa iliyopo na yote hayahayana mahali pa kimbilio.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuihimiza Wizarahii na napenda kuwapa tu chemsha bongo ya kwamba, bilaninyi muelewe wazi ya kwamba maslahi ya wafugaj hayanamtetezi na hayana msemaji. Kwa hiyo, naomba Serikali piaitambue ya kwamba, mwisho wa ubaya wowote wadhuluma ambao unatendwa na watumishi ni aibu kwaChama cha Mapinduzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, narudia tena, mwisho waubaya wowote unaofanywa na watumishi wa Serikali ni aibuna itarejea kwenye Chama cha Mapinduzi. Kwa hiyo,naomba Chama cha Mapinduzi ambacho ndiyo ChamaTawala mwamke na mzinduke, muwe macho na muwemasikio na muwe midomo ya sauti ya wokovu na wokovukwa wafugaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara ina deni kubwa sanana napenda kupongeza juhudi za Bunge hili. NapongezaBunge kwa juhudi zake za kuandaa Kamati ya kwendakufuatilia matatizo ya gesi Mtwara pamoja na matatizoyanayowakabili wananchi wote wa Kusini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa, naomba, mtazamohuo huo ambao umetumika na ukafikia kufanyiwa uamuzikwamba tukatazame matatizo, vifo na mauaji yaliyotokeakule, vivyo hivyo napenda kutambulisha Bunge hili nakuomba umwambie Mheshimwa Spika kwamba na sisiwafugaji tunahitaji Kamati iende ikachunguze mauaji yawafugaji yanayotendwa na Askari wa Wanyamapori.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vivyo hivyo tunatakatutambue mauaji ya mifugo yetu, rushwa na dhulumaambazo zinatendeka kule. Vivyo hivyo, naomba kueleza

Page 140: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

139

31 MEI, 2013

kwamba, damu ya wafugaji iliyomwagika katika Mikoambalimbali ni zaidi ya wananchi wengi ambao wamepatamadhara Rukwa pamoja na Mtwara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba kusisitizakwamba, Kamati ya Bunge ambayo imekwenda Mtwara,basi na mfumo huohuo ufanyike kuwa ni sauti ya ukombozina Bunge lisitafsirike kwamba lina tabia za ubaguzi kwambakuna maeneo bora zaidi ya kwenda kuchunguzwa na kunamaeneo bora zaidi ya kwenda kusikilizwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wafugaji wanalia nanaomba ieleweke wazi kwamba, wafugaji ni kabila kubwasana, ambao ni Wasukuma. Sasa upole wa Wasukumausichukuliwe kwamba ni malighafi ya uhondo wa viongoziwa kisiasa pamoja na Serikali. Naomba kusema kwamba,upole wetu utambuliwe na upewe heshima ya ustaarabu,lakini naomba kusema kwamba mdai chake kwa mdaiwahuambiwa kwamba ni mtu mbaya. Sisi itafikia pahalitutakachodai mwaka 2015 asiyejua maana haambiwimaana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba hilo uliweke nawewe ni Mjumbe wa Kamati Kuu, naomba salamu hiziwapelekee pia na Kamati kuu. Ukimya wa CCM, mifugoinauawa, wafugaji wanauawa, dhuluma na rushwa, hakunakikosikazi kinachokwenda kutafsiri na kuangalia matatizo yawafugaji, hili ni tatizo ambalo linaleta taarifa kwamba, kunaubaguzi na matabaka ya kuhudumia matatizo yaWatanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu suala la gesi Mtwara,viwanda vinamiminika kwenda kule, lakini sisi wafugajiViwanda vya Kusindika Nyama hakuna, Viwanda vya Maziwahakuna, ukiangalia Viwanda vya Ngozi vilibinafsishwa, hivimnataka Wasukuma na sisi tufanye nini? Naomba majibutoka kwa Mheshimiwa Waziri na naomba ushauri wa Bungeuzingatie masuala haya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kukumbusha

Page 141: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

140

31 MEI, 2013

historia ya Tanganyika, bila wafugaji kuunga mkono kura zamaoni za kudai uhuru wa Tanganyika wakulima na wafugaji,Gavana asingeruhusu na asingemwambia Watanganyikatupo tayari kujitawala. Lakini baada ya kujitawala wafugajileo tunaambiwa ni wafugaji haramuna wahamiaji haramu,je na wale wafanyabiashara waliotoka mikoa asilia ya kwaowakaenda mikoa mingine na wenyewe ni wafanyabiasharawahamiaji haramu? Je, kwa nini nchi hii kama mnaona ardhini ndogo, wakimbizi mnawapa ardhi wakati wafugajihamuwapi ardhi yao? Naomba suala hilo mlitazame naSerikali mlifanyie kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati mwaka 1978,wendawazimu wa Iddi Amini ulipomega eneo la Kagera,wafugaji walitoa kitoweo kwa majeshi yetu yote, hapowakaambiwa ni wazalendo na waaminifu. Baada ya vitaleo mnawaambia wafugaji ni haramu, wahamiaji haramu,Wakuu wa Mikoa wanawatesa na Ma-DC wanawatesa,tuliondoa ukaburu, tuliondoa ubeberu na ukoloni, huu sasani ubeberu na ukoloni mamboleo wa Kiafrika, lakini CCMimekaa kimya, naomba mje mtueleze mwaka 2015. (Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo naomba kusema hayokwa sababu nina masikitiko makubwa sana. Wakati wa Babawa Taifa alizungumza na Marehemu Bomani na HayatiMnanka, akawaambia waambieni wafugaji na Wasukumawote na wakulima wote muunge mkono kura ya maoni.Gavana akasema kweli sasa mnadai uhuru, mmeungwa naKanda ya Ziwa, lakini leo heshima ya wafugaji iko wapi? Leoheshima hata ya wakulima wafugaji na yenyewe iko wapi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, jiko la dhuluma ni Wizara yaMaliasili. Mheshimiwa Kaimu Waziri Mkuu, Wizara ya Maliasilindiyo dhulumati wakubwa kupitia kikosikazi chawanyamapori. Kikosi cha Wanyamapori wanadhulumu,wanaua ndiyo kitengo cha rushwa. Wizara ya Mifugo nayenyewe mmekaa kimya, hivi ukimya huu tuuelewe vipi?(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba mwende huko

Page 142: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

141

31 MEI, 2013

mkazungumze na hao watu, kama kuna sheria hatarishiambazo zimevamia maeneo ya wakulima na wafugaji,wakati umefika Wizara ya Wafugaji, hakikisheni viongozi waWizara hii mnakwenda kudai sheria ambazo ni hatarishoambazo haziboreshi utulivu wa fikra za wafugaji na wakulima,tunaomba tuelewe kwamba sasa tunatengewa maeneo yahifadhi maalum.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ikiwa wanyamaporiwanapozaliana mnasema ni kuongezeka kwa uchumi, lakinimifugo ikiongezeka mnasema ni uharibifu wa mazingira, kwanini viwanda vinapoongeza uzalishaji mnavipongeza, lakinimifugo ikiongezeka tusipongezane? Kwa kweli nasikitika sanana kama mnaona kwamba wanyamapori wanaendeleakuzaliana wataleta fujo, basi anzisheni uzazi wa mpango kwawanyamapori. (Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba viwandaambavyo vitakwenda sambamba na mahitaji ya mifugo zaidiya milioni 20 na mbuzi zaidi ya milioni 15. Serikali imeserereka,haisemi ni nini wanafanya kuhusiana na kwenda sambamba,lakini ajira kwenye Viwanda vya Kusindika Nyama ingekuwani kubwa sana na tungepunguza tatizo hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wafugaji Tanzania ni yatimana wanaishi maisha ya ghadhabu kwa sababu hawana mtuwa kuwasaidia. Leo mtambo wa kuzalisha fitina na hila hizi niWizara ya Maliasili. Wizara ya Maliasili wanazungumza kilasiku kwamba sheria, sheria, sasa kama sheria haina uhai kwamaslahi ya utulivu wa Watanzania ni sheria gani hiyo?Tulikataa ukaburu na ubeberu, lakini leo mnaurudishakinyumenyume na kusema kwamba, wafugaji ni wavamizi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kusema kwamba,mporomoko wa viwanda uliotendeka Tanzania nakubinafsishwa, kwa kweli ni janga kwa maslahi ya Watanzaniawote. Naomba kusema kwamba, viwanda viongezweharaka sana na viende sawasawa, wanyamapori

Page 143: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

142

31 MEI, 2013

kuongezeka ni neema, lakini mifugo mnailaani, kwa hiyonaomba na wafugaji pia mhakikishe kwamba, wanapewaneema ya uhuru wa Tanganyika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukidadisi maisha ya wafugajiutakuta kwamba ni kamali ya rushwa, hakuna kikosikazi chakuwasikiliza, hakuna sikio sikivu, Wizara hii na yenyewe siyosikio sikivu, kwa hiyo wafugaji wanaishi maisha taabani sana.Nawaomba wafugaji wote mkae macho, kura zenu ndiyoukombozi wenu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, huduma ya Wizara hii najuaimedumaa, imedorora, naomba Wizara hii sasa muamke namhakikishe kwamba, mnakuwa watu ambao mnahakikishautiifu bila shurti wala rushwa unaondoka kwa wafugaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwanzo wa moto ni chehe,cheche za Mtwara ni cheche zinazowaka hovyo hovyo, lakininapenda kuwaambia cheche za wafugaji ni za kimya kimya.Amkeni, zindukeni, la sivyo majuto ni mjukuu. Hitilafu yakukosekana imani na amani kwa wafugaji inasababishwa naSerikali. Dhahama ya Serikali mjue ndiyo mchwa unaoitafunaCCM, wala msigombane na Vyama vya Upinzani, ninyi ndiyomnaozalisha agenda kwa sababu ya uwajibikaji wenuambao hamtaki kuwa sikio la wanyonge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kusema kwamba,CCM na Serikali yake hivi sasa mmepokonya haki za wafugaji.TANU ilikuwa tulizo la wafugaji, lakini leo hatuna utulivu. TANUilikuwa ngao na usalama wa wafugaji, leo hakuna chamaambacho ni ngao na usalama wa wafugaji. Nawaomba,ukombozi dhidi ya wafugaji na mtambue kwamba nyiewafugaji ndiyo ngome kubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kuyasema hayo,nasema kwamba, CCM na Serikali yake kaeni… (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

Page 144: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

143

31 MEI, 2013

MWENYEKITI: Kengele ya pil i. TunakushukuruMheshimiwa Shibuda kwa mchango wako, ingawa leoumetunyima raha yetu Wabunge ya nahau za Kiswahili, lakinitunakushukuru sana.

Waheshimiwa Wabunge sasa tunaendelea na naruditena kwenye Kambi ya Chama Tawala. NitamwitaMheshimiwa Kakoso atafuatiwa na Mheshimiwa Abuu Jumaana atafuatiwa na Mheshimiwa Ole – Telele.

MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi hii. Awali ya yote sitaungamkono hoja hii mpaka pale tutakapokuwa tumeongezewazile fedha zilizoombwa na Kamati, shilingi bilioni 40. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara hii ni muhimu sanakwani inahudumia wananchi ambao ni wengi kwa maanaya wakulima na wafugaji. Bajeti ya Serikali kwa Wizara hiiimekuwa ikishuka mara kwa mara. Asilimia kubwa ya bajetihii ni ya mishahara tu ya wafanyakazi, fedha za maendeleohakuna. Wizara nzima imetengewa shilingi bilioni nane tu, sijuiWizara hii inafanya kazi gani?

Mheshimiwa Mwenyekiti, naiomba Serikali kama kwelitumedhamiria kutatua matatizo ya wafugaji na wavuvi, nivyema basi, ikatenga fedha tulizoomba ambazo Kamatiimependekeza ili tuweze kufanya kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna matatizo makubwasana kwenye sekta hii; tatizo la kwanza, wakulima au wafugajiwalio wengi wanahamahama kwa sababu hawajapatahuduma iliyo nzuri katika maeneo yao. Hatuwezi kutatuamigogoro ya wakulima na wafugaji kama Serikalihaijawajengea mabwawa, majosho ya mifugo na kutengamaeneo ya malisho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni vizuri Serikali ikaangaliaupya, kuna maeneo mengi sana ambayo imeyaacha kwaajili ya matumizi, either ni hifadhi za misitu au ni hifadhi zaTaifa. (Makofi)

Page 145: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

144

31 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni vizuri sasa wakaangaliaumuhimu wa wananchi ambao wanatangatanga katika nchiyao na wanaonekana kama wakimbizi kwa sababuhakujawa na miundombinu ya kuwasaidia wafugaji hawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimboni kwangu kunawafugaji wengi sana ambao wametoka Mikoa ya Shinyangana Mwanza. Sababu kubwa ni kwamba, kule hakunamiundombinu. Kama wangekuwa wamejengewamabwawa, majosho na huduma nyingine kama vile maeneoya kulishia mifugo, hawa wananchi wa kutoka mikoa hiyowasingefika kwenye maeneo ya kwetu. Sasa ni lazima Serikaliijipange kuhakikisha inaandaa miundombinu ili kuwasaidiawafugaji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, miundombinu inayohitajikakatika maeneo ya wafugaji. Wafugaji wajengewe Viwandavya Kusindika Nyama. Kama viwanda vitajengwa katikamaeneo hayo, ni vigumu sana kuwaona wafugajiwanatangatanga na kupeleka mifugo katika maeneomengine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile, kama kutakuwa naujengaji wa Viwanda vya Ngozi tutakuwa tumezalisha ajiranyingi ambazo zitatoka kwenye sekta hii. Niiombe Serikaliwatilie mkazo na umuhimu katika maeneo haya ili kuwezakuondoa migogoro isiyokuwa na ulazima. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sekta ya uvuvi. Sekta hii nieneo ambalo halijafanyiwa kazi na Serikali, kwani imeshindwakuwekeza kwenye sekta hii ambayo ingekuza uchumi waTaifa hili. Tuna maeneo makubwa sana katika nchi hii;mwambao wa bahari ambao ni mrefu kuzidi maeneomengine katika nchi za Afrika hasa katika Bahari hii ya Hindi,ukianzia maeneo ya Mtwara mpaka kule Tanga. Eneo hili nila uvuvi ambalo kama lingewekezwa lingeweza kutoa ajiranyingi kwa Watanzania, lakini kwa bahati mbaya hakuna kituambacho kimewekezwa katika sekta hii. (Makofi)

Page 146: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

145

31 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeshuhudia meli nyingi zanje zikija kuvua katika ukanda wa bahari yetu kama vile wakonyumbani kwao. Inasikitisha sana na nitaomba maelezo yaWaziri atakapokuja kuhitimisha atueleze. Wenzetu wa nchiya Msumbiji walipokamata meli iliyokuwa inaiba katikamwambao wa Bahari ya Hindi ambapo na sisi tulikamata meli,ile meli wenzetu waliitumia vizuri. Mara walipoikamatawaliitaifisha na ikaanza kufanya doria kwa ajili ya kusimamiawale wavuvi haramu katika maeneo husika ya nchi yaMsumbiji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi ile meli tuliichukua nakuiweka kama kielelezo cha Mahakama. Leo hii ile meli haipona iliishazama. Tunaomba maelezo ya Serikali ni kwa ninitusingeitumia ile meli ikafanya shughuli za doria kwa ajili yakutafuta wale ambao wanafanya uharibifu kwenyemwambao wa bahari yetu ya Hindi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine la uvuvi likoZiwa Victoria. Eneo hili limekuwa likivuliwa samaki nawanaonufaika sana ni nchi za Uganda na Kenya. Ukiangaliakatika ramani mmiliki wa Ziwa Victoria kwa asilimia kubwa ninchi yetu ya Tanzania. Bahati mbaya hakuna kitu chochoteambacho tumekiwekeza kwa ajili ya kusimamia uvuvi wamaeneo haya. Hatuna mafuta ya kufanya doria ya kutosha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, matokeo yake Waganda naWakenya, wanavua kwa wingi katika maeneo ya kwetu nahata wale wafanyakazi ambao wapo na wangewezawakalinda zile rasilimali tulizonazo wanashindwa kwa sababuhawana vitendea kazi. Naomba Serikali iangalie na ihakikisheinawatengea Wizara fedha zile zilizoombwa, wapewe iliwaweze kwenda kufanya kazi na hatimaye tutaona matundaya Wizara hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ni ZiwaTanganyika. Ziwa Tanganyika hakuna uwekezaji wa ainayoyote uliofanywa na Serikali. Wenzetu wa Zambia wana

Page 147: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

146

31 MEI, 2013

eneo dogo sana la Ziwa Tanganyika, lakini samaki wotewanaovuliwa upande wa Tanzania wanakwenda kuuzwaZambia kwa sababu wenzetu wana miundombinu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, inasikitisha sana kuona kilamahali ambapo sisi tuna eneo la ziwa kama vile Tanganyikana Nyasa, wanaonufaika ni nchi jirani ambazo tumepakananazo. Sisi Watanzania tuna ugonjwa gani ambao hauna tiba?Ni vizuri tukaangalia na tukaona jinsi ya kuwasaidia wananchiwa maeneo haya wanaoishi kando kando na maziwa haya.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu uwezeshaji. Hakunamaeneo ambayo wamewasaidia wavuvi wadogo wadogo.Katika eneo hili, ili tuweze kuwasaidia wananchi, ni lazimaSerikali iandae mpango kazi maalum wa kuwasaidia wavuviwadogo wadogo ambao wakisaidiwa watatoa mchangomkubwa kwenye pato la Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tusipofanya hivyo, tutakuwatukizishuhudia kwa macho rasilimali zote zikibebwa nawajanja wachache ambao wanatumia fursa tulizonazo. Nilazima tupeleke viwanda kwenye maeneo ya ZiwaTanganyika ili kuhakikisha mazao yanayozalishwa katikamaeneo hayo yanaweza kusindikwa na hatimaye kuuzwanje na kusaidia jamii zinazozunguka katika maeneo haya.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ziwa Nyasa ni Ziwa ambalolina samaki wengi, lakini wanaonufaika ni Wamalawi na ndiyomaana Serikali ya Malawi inathubutu kusema lile ziwa lote nimali yao kwa sababu Serikali ya Tanzania haijaweka mpangomzuri wa kuwasaidia wavuvi katika maeneo hayo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niiombe Serikali na bahatimbaya Waziri wa Fedha hatujamwona leo hapa, angekujana tamko la kuisaidia Wizara hii ili iweze kufanya kazi. Wizarahii wapatiwe fedha ambazo zitawasaidia kutekelezamajukumu yao, vinginevyo kila siku tutakuwa tunapiga keleleisiyokuwa na faida ya aina yoyote kwa sababu bajeti

Page 148: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

147

31 MEI, 2013

inakuwa ndogo. Hii ni Wizara yenye migogoro mingi, lakinibahati mbaya ndiyo Wizara ambayo bajeti yake inashukakila mwaka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitaunga mkono palenitakapokuwa nimepata maelezo thabiti ya ongezeko.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Mheshimiwa kengele ya pili.

MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru sana. (Makofi)

MHE. ABUU H. JUMAA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa fursa hii ili niweze kuchangia bajetiya Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukue fursa hiikumpongeza Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri pamoja nawataalam wake wote kwa kazi kubwa ambayo wanaifanyana jitihada ambazo wanaendeleza katika Wizara hii ilikuhakikisha sekta hizi za mifugo na uvuvi zinaendelea. Kwakweli, jitihada wanazo, lakini tatizo kubwa ni fedha. Kila sikutunazungumzia masuala ya fedha hapa, mmeainishamambo mengi mazuri, lakini tatizo kubwa ni fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukue fursa hii tu kuiombaSerikali iisaidie Wizara hii ili iweze kukidhi mahitaji ya wananchiwetu wafugaji na wavuvi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, takribani miaka miwili aumitatu iliyopita, Mheshimiwa Rais alizindua ujenzi wa Kiwandacha Machinjio pale Ruvu. Kiwanda hiki kimechukua mudamrefu na wakati ule Mheshimiwa Rais anazindua ujenzi wake,wananchi wengi walihamasishwa na wakahamasika kufugang’ombe wa kisasa kwa kuwanenepesha.

Page 149: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

148

31 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, hilo halikutosha, wananchiwakahamasishwa na wakahamasika kutenga maeneo yaufugaji na walifanya hivyo. Jambo la kusikitisha ni kwamba,licha ya fedha za wananchi kutumika pale mpaka sasahakuna uendelezaji wowote uliofanyika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi ukipita paleunakuta gofu, vifaa na vitu vingine vinaibiwa na limekuwa nitatizo kubwa. Vijana takribani zaidi ya 1,000 waliahidiwakupata ajira kutokana na kiwanda kile. Vijana wamezagaatu pale Mlandizi, Jimboni kwangu, hawana kazi za kufanyakutokana na matumaini makubwa ambayo wameyapatakutokana na kujengwa kwa kiwanda kile.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwombe MheshimiwaWaziri wakati anakuja hapa, basi atupatie majibu kuhusianana kiwanda kile kwani kimechukua muda mrefu, jamboambalo ni sawa na kumtia aibu Mheshimiwa Rais, maanaMheshimiwa Rais alikwenda akafungua mradi ule,umechukua muda mrefu na hauna mategemeo yoyote. Kwabahati mbaya katika kitabu hiki cha hotuba ya MheshimiwaWaziri, sijaona hata sehemu moja ambayo inazungumziasuala zima la kiwanda kile. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa ndiyo mahali husikapa kuomba. Nichukue fursa hii kumwomba tena MheshimiwaWaziri, pamoja na matatizo ya kifedha, naamini Serikali itasikiakil io cha Wabunge, upo uwezekano mkubwa wakuongezewa fedha. Naomba Mheshimiwa Waziri atambuekwamba, Jimbo la Kibaha Vijijini vilevile ni la wafugaji kamamaeneo mengine, tuna wafugaji wengi tu pale ambaowanafuga ng’ombe, mbuzi na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka Mheshimiwa Waziriatambue suala hili kwa sababu wananchi wangu wakatimwingine hata ukiwaambia kuna Wizara ya Maendeleo yaMifugo na Uvuvi, hawaitambui. Inawezekana kutokuitambuahuko ni kwa sababu Waziri hajapata muda wa kutembeleakule ili wananchi wajue kuna Wizara hii. Namwomba tu

Page 150: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

149

31 MEI, 2013

Mheshimiwa Waziri, akipata muda wakati mwingine apitiekatika Jimbo la Kibaha Vijijini ili aweze kuona kwamba, kunawafugaji wengi tu pale. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuishauri Serikalikwamba, kwa sababu tuna wafugaji wengi na kiwanda kilekikikamilika maana yake tutaongeza pato kubwa la Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi tunalalamikahatuna fedha, kwa sababu kiwanda kile kimekaa kwa mudamrefu. Kama tungeweza kujenga kiwanda kile na kukimalizatungeweza kupata mapato na Taifa lingeweza kuongezamapato.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, ningependakumwambia Mheshimiwa Waziri kwamba, kwa sababu tunawafugaji na mifugo mingi pale, tuna maziwa mengi sana yakutosha, lakini wafugaji wetu pale wanashindwa kupata sokola kuuzia maziwa. Nashauri kwamba, kwa sababu Dar esSalaam ilipo Wizara ni karibu sana na Kibaha Mjini, Waziriangejaribu kufikiria Jimbo la Kibaha Vijijini liwe mfano kwakujenga kiwanda cha maziwa pale. Pia angehakikishaanatembelea pale mara kwa mara na kwa kuwa ndiyo njiakubwa ya Wabunge, basi wakipita wataona kwamba, Wizarayake inaanza kufanya kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namshauri tu MheshimiwaWaziri kama upo uwezekano na akiongezewa fedha, afikiriesuala la kujenga Kiwanda cha Maziwa pale. Pia nimwombeMheshimiwa Waziri kwamba, tatizo kubwa linalowakabiliwafugaji wangu ni elimu. Tumetenga maeneo ya wafugaji,lakini tatizo kubwa ni elimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, namwombaMheshimiwa Waziri aweke utaratibu wa kuhakikisha wafugajiwetu hawa wanapata elimu ya kufuga kisasa ili kuondokanana migogoro mingi ya wakulima na wafugaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunatenga maeneo, lakinitatizo kubwa ni kwamba, yale maeneo ambayo tunayatenga

Page 151: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

150

31 MEI, 2013

yanakabiliwa na ukosefu wa huduma muhimu. Kwa mfano,tumetenga maeneo, lakini hakuna malambo, majosho, hiloni tatizo kubwa. Kwa hiyo, wakati tunatenga maeneo nivyema kuhakikisha huduma muhimu zinafika kule. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile dawa za ruzuku nitatizo kubwa na wananchi kule wanashindwa kupata dawana haijulikani dawa zile zinaweza kufika kule kwa muda gani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumezungumzia suala lauvuvi na Wabunge wengi wamezungumzia kwamba, tunamito, bahari, lakini mkumbuke tuna Mto Ruvu pale. Kamatunaweza kuutumia mto huu ni vizuri na tuna vijana wengi,tukiweka pale miundombinu, tukijenga mabwawa menginetukaanza kufuga samaki, wakati huo huo tunawezatukapunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la ajira. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo,naunga mkono hoja, ahsante sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana kwa mchango wako.Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea na mchangiaji wetuanayefuata ni Mheshimiwa Telele atafuatiwa na MheshimiwaSanya.

MHE. KAIKA S. TELELE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ili nichangie hotuba yabajeti ya Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi. NaombaWaheshimiwa Wabunge watakaopata nafasi ya kuchangiabajeti hii waendelee kama walivyoanza wengine kupigiakelele na kutetea sana bajeti hii ndogo ambayo kwa kwelihairuhusu kutekeleza miradi ya wafugaji na wavuvi. Tupigiekelele kama ambavyo tumepigia kelele bajeti ya Wizara yaMaji na baadaye Serikali ikaenda kutafuta shilingi bilioni 184na ushehe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naona kwamba, kutokanana kushuka kwa bajeti hii mwaka hadi mwaka ndani ya miakamitano bajeti hii imeshuka kwa kiasi cha sh. 163,000,000,000;tangu mwaka 2009 hadi bajeti hii tunayoizungumzia leo. Kwa

Page 152: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

151

31 MEI, 2013

hiyo, hiyo graph inakwenda chini tu, mwisho itafika sifuri naikifika sifuri basi na mifugo kwa kweli itapotea kabisa, kwasababu kuna maradhi mengi sana ya mifugo, tunatakakukabiliana nayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo naomba kwamba,badala ya shilingi bilioni 40 ambayo Wizara hii imeomba kamanyongeza ili iweze kufanikisha shughuli zake kwa kweliwaongezewe sh. 163,000,000,000 waliyopoteza ndani yamiaka mitano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naamini hili linawezekanakwa sababu hata juzi hapa, Wizara hii imeongezewa siku mbili.Hii ni kwa sababu imeonekana kama alivyosema MheshimiwaLekule Laizer hapa Wizara hii inabeba Watanzania wengisana sio chini ya asilimia 30 kama alivyosema na inawezaikawa ni zaidi. Sasa kama wameweza kuongeza kwa sikumbili kwa nini washindwe kuongeza bajeti. Kama sio yotehiyo waliyopoteza kwa miaka mitano, basi wongezewe hiyowaliyoomba sh. 40,000,000,000/=.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wabunge wengiwamezungumzia kutenga maeneo ya wafugaji na siokutenga tu Serikali itenge na isajili maeneo yale ipatikanehati ili wafugaji hawa waendelee kutulia katika maeneo yao.Wakishafanya hivyo lazima miundombinu ya uhakika iwekwekatika maeneo ya wafugaji kama vile kuchimba mabwawakama walivyosema wenzangu wengi, majosho, wajengeviwanda, watafute masoko kwa ajili ya mazao ya mifugo,wakifanya hivyo angalau hii Wizara sasa inaweza ikavutiakwa kiasi fulani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, viongozi mbalimbaliwamekwenda ziara kule Botswana, wamekwenda Ugandawametembelea hata mashamba ya mifugo ya MheshimiwaRais, maana ni mfugaji yule. Sasa viongozi mbalimbaliwanakwenda, lakini wakirudi hawapeleki walichokiona kwawafugaji wa kawaida.

Page 153: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

152

31 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, nafikiri ni wakati muafakasasa na wafugaji wa kawaida nao watembelee, wapelekwemaana wanasema hasa ndugu zangu jamii yanguninayotoka, wanasema jicho lililotoka nje likaona, likirudilinaweza kufanya na kuleta mabadiliko. Sasa badala yakuwaacha tu katika hali yao ya kawaida na wenyewewatoke nje waone wenzetu wanafanya nini ili kuweza kujakuanzisha mambo ambayo yataboresha mifugo yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ni uwekezajimdogo katika sekta hii. Ni uwekezaji mdogo kwa upandewa Serikali na uwekezaji mdogo kwa upande wa sekta binafsi.Hakuna masoko, hakuna mikopo kwa ajili ya kuendeleza hiisekta ya mifugo. Watu wengine wanasema lazima tufugekulingana na uwezo wa eneo ambalo tunakusudia kufuga,wanaita carrying capacity, lakini ukifuga katika eneo dogona hakuna miundombinu kama nilivyoeleza, kwa kweliitakuwa ni balaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia nina matumainikwa sababu sekta hii imepigiwa kelele muda mrefu nahakuna mabadiliko yoyote. Naamini katika mchakato waKatiba mpya, wafugaji watakuwa wametoa maoni yaokuhusu mifugo yao itakuwaje ili Katiba mpya itamke kwamba,mifugo ni zao ambalo ni muhimu kama kilimo na kamatunasema Kilimo Kwanza isifanye sasa hali ya mifugo nayoikapotea katika mipango ya Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, yako magonjwa mengi sanaambayo yanasumbua mifugo. Magonjwa mengiyanasababishwa na kupe zaidi, kwa hiyo tukiweza kudhibitikupe magonjwa mengi ya mifugo yanaweza kupungua.Lakini yako magonjwa mengine kama foot and mouth aumiguu na midomo ambayo inahitaji chanjo tu, magonjwakama na ndigana kali yanahitaji chanjo, magonjwayanayoenezwa na mbung’o, tulielezwa katika hotuba yaWaziri kwamba hekta karibu 30,000 ambayo ni sawasawana asilimia karibu 30 ya eneo la Tanzania limekabiliwa nambung’o. Nimeona huko Serengeti wameweka vitambaa

Page 154: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

153

31 MEI, 2013

vyeusi ambavyo mbu akipita pale, anavutwa, ananasa palena kwa hiyo anafia palepale. Naomba utaalam huouenezwe katika maeneo yote ya wafugaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Brucellosis nao ni ugonjwaambao unapunguza sana idadi ya mifugo kwa sababumitamba inatupa mimba kwa wingi kutokana na ugonjwahuu. Mabadiliko ya tabianchi yataathiri pia sana wafugajikama ambavyo yataathiri wakulima. Kwa hiyo, ni lazimatutafute namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchiili kuweza kuwanusuru wafugaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili suala la migogoro yawakulima na wafugaji limedumu kwa muda mrefu, lakinivilevile kuna mgogoro unaozuka kati ya wafugaji nawawekezaji na wale wapiga picha ambao wako katikamaeneo ya wafugaji. Tunaomba migogoro hii ishughulikiweharaka na hao wawekezaji nao watambue wafugajikwamba ni good neighbours katika suala zima la uwekezaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo,napenda nikushukuru. (Makofi)

MWENYEKITI: Nakushukuru sana Mheshimiwa Telele.Kama nilivyosema, sasa nitamwita Mheshimiwa Sanya nabaada ya kumsikiliza Mheshimiwa Sanya tutampa nafasiMheshimiwa Mangungu.

MHE. MUHAMMAD IBRAHIM SANYA: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii ili kuchangiakidogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mara ya kwanzanasema, nitakuwepo kesho kuondoa shilingi katika mshaharawa Waziri, kwa sababu hii bajeti inaonekana kwamba weare not committed, we are not serious, hii ni Wizara ambayoina sekta mbili muhimu sana kwa nchi yetu, sekta ya mifugona sekta ya uvuvi. Lakini sekta zote mbili hizo hazijafanyiwakazi zikazalisha na zikasaidia nchi kiuchumi na zikawasaidiaWatanzania. Kwa nini nasema hivyo?

Page 155: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

154

31 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi kweli hatuoni kwamba,sisi Tanzania kama ingekuwa hatuna mifugo katika nchi hiitungetumia kiasi gani cha fedha kuagizia nyama kutoka nchiza nje. Hicho ni kigezo tosha kwamba, Mungu ametunusuru;tuna wanyama wa kutosha wa kuweza kula, lakini akatupana ziada ya kuweza kuwasafirisha ama nchi za jirani amanchi za nje, tunafanya hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kelele zimekuwa nyingibaina ya wafugaji na wakulima, lakini huwezi ukambadilishamkulima akageuka akawa mfugaji na mfugaji akawamkulima, ni two different subjects hizo. Kilichobaki nikujengewa mazingira mazuri, wakulima wakawa na maeneoyao na wafugaji wakawa na maeneo yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo wafugajiwanatangatanga tu na ng’ombe nchi nzima, lakinitumewajengea miundombinu gani ya kuwasaidia. Wafugajihawana majosho, vituo vya utafiti ni kidogo, maji kwa ajili yawanyama wao hakuna, matokeo yake tunakuja na datahapa kwamba kila Mtanzania anakula kilo 12 kwa mwaka.Ina maana kwa mwezi Mtanzania ambaye anahesabiwaana nyama nchi ya pili katika Afrika anakula kilo moja kwamwezi, ina maana kila mtu anakula mshikaki mmoja kwa siku,ndiyo hesabu hii ilivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utasemaje wewe ni mtu wapili Afrika, una ng’ombe wengi halafu Mtanzania anakula kilo12 kwa mwaka, ina maana kwa mwezi ni kilo moja, inamaana hata huo mshikaki mmoja anagawana baina ya yeyena mama nyumbani, kila mmoja anapata vipande viwili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukija kwenye mayai hivyohivyo na hawa wafugaji kama hatukuwaangalia,tukawatengenezea mazingira mazuri siku watakayogomakuchinja ng’ombe, basi tutamaliza mbuzi, sungura, kuku,mayai na mwisho tutakula kunguru nchi hii. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni hawa wanaolisha nchinyama. Kama wewe unapumzika baada ya kutoka hapa,

Page 156: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

155

31 MEI, 2013

kutoka kazini ukahitaji nyama choma, ni hawa wafugaji. Nihawa wanatoa maziwa, ni hawa wanatoa ngozi, ni hawawanaweza wakazalisha maziwa zikatoa products nyinginesiagi, jibini na mambo mengine chungu zima, matokeo yakemaziwa hakuna. Mashule yetu tunawapikia uji watoto bilamaziwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni ajabu na haya ni maajabumakubwa duniani kwamba Tanzania ni nchi ya pili kuwa namifugo lakini hatunywi maziwa. Kenya hawana mifugo kulikosisi, lakini wana maziwa mpaka wanasafirisha wanatuleteaTanzania. Kwa nini tusitengeneze viwanda vikazalisha virobavya maziwa badala ya viroba vya ulevi, tukawapa nafuuwananchi wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini tusifanyeinsemination baada ya kutoa kilo 200, ngombe akatoa kilo500 na 600. Siku zote itakuwa hapa tunakuja tunazungumzamasuala ya matatizo baina ya wakulima na wafugaji.(Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kijijini pako Peramiho, kunaKijiji kinaitwa Ngadinda, kama yeye hakielewei kuna matatizokimevamiwa na wafugaji, kwa nini? Kwa sababu hatujatengamaeneo, hatuna plan survey ya land ya kuwafanyia watuwetu, hawa wafugaji huku simba na faru, huku mkulima nahii reserve ya investment hatuna, wenzetu wanazo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nendeni Bostwana mkaonewanavyofanya, nendeni Malawi, Afrika ya Kusini, hadi hii leotunaagizia maziwa, hadi hii leo tuvae viatu vya plastiki kutokaThailand, hadi hii leo siagi itoke Kenya, is quiet ridiculous.Wamasai, Wasukuma, Wabarbaig wasaidiwe sasa wajisikiekwamba huu ndio uhuru wa Mtanzania katika kilimo chakisasa na ufugaji wa kisasa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, twende kwenye uvuvi; anzaTanga njoo zako Dar es Salaam teremka chini, Lindi mpakaMtwara tunafanya nini na samaki. Lake Victoria dominatedby three states Kenya, Uganda na Tanzania ile portion ndogo

Page 157: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

156

31 MEI, 2013

ya Tanzania, tunazalisha samaki wengi wakati katika LakeVictoria kuna species kidogo za samaki kuliko za bahari kuuna tunasafirisha in billions kupeleka Ulaya, ndege zinakujazinachukua, lakini hakuna ndege hata moja inayokujakuchukua hata dagaa Dar es Salaam. It’s quiet shame navijana wapo hawana kazi, wako Kilwa, Mtwara, Lindi, Tanga,Dar es Salaam, Pemba na Unguja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mashine za boti wala sioghali. Karibu nakwenda kuzindua mradi wangu kule Jimbonikwangu, nimeagizia hizi mashine za Japan, they are so cheapna hakuna ushuru nchi hii. Haya mabilioni ya MheshimiwaKikwete kama yangetumika katika suala la uvuvi, basi vijanawengi wangepata ajira. Matokeo yake fedha zile ukiendaukizichunguza, hujui zimechukuliwa na nani zimefanyiwamiradi gani zimezalisha nini. (Makofi)

Mheshimiwa Waziri watume wataalam waendeMauritania, Senegal, Namibia wakaone namna gani nchi zilezilivyojikita katika uvuvi wa kisasa. Wana fishing ports, sisihatuna hata fishing ports, tumekamata meli moja la Magufuliitabakia historia na litakuwa kwenye archieves mpaka kiamandio hilo hilo moja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumekwenda kudai ukubwawa bahari mpaka kilo 1,200 wakati maji ya futi tunashindwakuzoa hata chaza na chiwale. Kwa nini tusiwape watuwakaenda wakavua. Hii deep sea fishing kuna mameliyanavuna kule. Je, Serikali yetu inazo taarifa kwamba kunameli ngapi zinavua tani ngapi? Ndiyo Namibiawanavyofanya, meli inaripoti bandarini inakwenda kuvua,baadaye inarudi i le trawler kuja kuonesha kwambanimepakia kiasi gani cha samaki ili nchi ipate mapatokutokana na uwezo wa kile chombo na samaki iliyowabeba,sisi tunao mpango huo? Hatuna!

Mheshimiwa Mwenyekiti, siku hizi survey ya baharinizinakwenda na ndege za kisasa, zinazochukua njia za GPSza satellites kuweza kujua meli ziko wapi. Halafu hii Wizaraiwe na ndege yake au ndege zake, wanapo-trace kitu

Page 158: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

157

31 MEI, 2013

kwenye hiyo satellite, wawe wanachukua ndege yaowanakwenda kuikamata ile meli na kwenda kuizunguka leo,hamna hata helikopta.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwende mkakodi ndegeAirport ya kibiashara hata wale wenyewe wakiiona ile ndegeiwapo ni Coaster, ZanAir wataona this is a commercial flightshawatashtuka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi tulikwenda mpakaJordan tukaambiwa ndege zipo ambazo zina camera zakisasa, zinachukua radius kiasi gani ya bahari na bei yake ni1.5 dollar million. Hivyo kila mwaka kununua angalau ndegemoja kwa miaka miwili tukawa na ndege mbili inashindikana,mnakuja kutuletea bajeti ya shilingi bilioni 47! Kamamngekuwa serious katika hil i hata sisi Wabungetungekuchukulieni mkopo CRBD mkafanya kazi. Yes what is47 billions.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hizi sio fedha za kujinadikwamba nyie mnaweza kufanya kitu, hamuwezi kwa sababumna sekta mbili katika nchi. Lakini sisi tuna tatizo mojaTanzania nimeligundua hilo, ukipata kipya kikuukuu kinakuwakinyemi. Tumepata gesi tena mawazo yetu ohoo, gesi wee,utajiri huo unakuja, utakuja for how long wakati tunao kukuwanataga kila siku, wataka kumchinja kuku upate mayai yotesiku moja huwezi. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lazima tujikite na hayamambo ambayo tunayo mkononi, ukulima yaani kilimo,ufugaji na uvuvi. Nakwambia unaweza ukachangia asilimiampaka asilimia 65 ya bajeti ya Serikali ya Tanzania ukiachiliambali utalii. Hizi uranium, gold sijui gesi acha ziende katikamfumo wake, lakini tukijikita huku kwenye uchumi halali,uchumi utakaotoa ajira, vijana sisi tunawafanya kama kofiaya Msikitini ukiingia unavaa ukisha kusali unaitupa.Tunawahitaji wakati wa kura tu, wakishapiga kura, basi miakamitano tunangojea tena. (Makofi)

Page 159: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

158

31 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuwajengee mazingirawaipende nchi yao wafanye kazi, wazalishe. Mimi kwa hilibwana nitalisimamia mpaka dakika ya mwisho. Shilingi bilioni47 kuletwa hapa Bungeni, bora mngekaa kwenye Kamatimkapanga matumizi yenu, hii ni mishahara tu. Kuna excessgani pale, kuna fedha kidogo ambazo zimetoka nje na fedhaza ndani kidogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa kesho tupo tunatoashilingi, utarudi Dar es Salaam kwa miguu. (Makofi)

MWENYEKITI: Nakushukuru sana Mheshimiwa Sanyakwa mchango wako na nafikiri Mheshimiwa Waziri amesikiana kile kilio cha wananchi wangu wa Jimbo la Peramiho kuleNgadinda wanavyopata shida ya kuingiliwa na wafugaji.Kwa hiyo, atatuwekea mambo sawa huko.

Waheshimiwa Wabunge nil isema nitamwitaMheshimiwa Mangungu, atafutiwa na Mheshimiwa Kitandulana atafuatiwa na Mheshimiwa Richard Ndassa.

MHE. MURTAZA A. MANGUNGU: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru sana kunipa fursa ya kuchangiakatika hotuba ya bajeti ya Wizara hii muhimu na moja katikamihimili ya ustawi wa nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa kwa mujibuwa kanuni ya 61(1) naomba ku-declare interest kwamba,yapo mengine ambayo nitayazungumzia naweza kwamaana moja au nyingine nina maslahi nayo binafsi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hotuba ya bajeti hiiimedhihirisha ni jinsi gani ambavyo inakwenda ikishuka kilamwaka. Nimepiga hesabu za haraka haraka inaoneshakwamba kuna wastani wa shilingi zisizopungua bilioni 15 kilamwaka zinashuka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kwa trend hi itunayokwenda nayo, baada ya miaka mitatu inayokuja

Page 160: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

159

31 MEI, 2013

Wizara hii itakuwa haina bajeti na inawezekana Waziriatalipwa mshahara kupitia Wizara nyingine, huko ndikotunakoelekea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ipo haja ya kuongeza bajetihii kwa sababu hata ukienda kwenye cha bajeti yadevelopment upande wa fisheries hakuna senti hata mojaambayo imepangwa na Waziri anakuja hapa kwenye Bungekuja kuomba apitishiwe bajeti sijui kwa kazi ipi anayoifanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hakuna mpango wowotewa kuendeleza maeneo ya uvuvi na katika sekta ya uvuviliko tatizo kubwa sana na Wizara imeamua kukaa kimya bilakutoa majibu yanayoeleweka. Kwa kipindi cha zaidi ya miakasita wamezuia uvuvi wa Kamba katika maeneo ya Delta namaeneo ya ukanda wa Kilwa bila sababu za msingi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sababu yao wanasemakwamba, wazaliane umri wa kamba tangu anazaliwa mpakaanazeeka hadi anakufa ni miezi tisa, hii miaka sita mnatakakamba hao wafanye kitu gani? Tunaomba tupate majibu.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, liko tatizo katika uvuvi;wavuvi wadogo wadogo wananyanyaswa, wanateswa namara nyingine hata jeshi huwa linatumika kwendakuwakamata, kama vile katika eneo la ukanda wa Tanga,lakini vilevile katika maeneo mengine. Sasa najiuliza Wizaraimewahi kufanya utafiti wa kujua sababu zinazopelekea watuwakafanya uvuvi wa haramu? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sababu kubwa wananchiau wavuvi hawa hawajawezeshwa kuwa na vifaa kuwezakuvua vizuri. Ni jambo la kustaajabisha makampuni ya kigeniyanakuja yanapewa leseni na tumeambiwa only 1.3 milioniDollars ndiyo iliyopatikana katika leseni zilizotolewa katikaleseni za uvuvi ule wa bahari kuu. Samaki wanazaliwa mpakawanakufa au mara nyingine kwa sababu ni immigrated

Page 161: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

160

31 MEI, 2013

species wanakwenda kuvuliwa katika maeneo mengine, sisihuku tunawazalisha, wanazaliwa katika ukanda wetuwanakwenda kuvuliwa mahali pengine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tunataka kuanzia hivisasa licha ya leseni ambayo inachajiwa kwa mvuvi, tunahitajituwe tunalipwa royalty kama watu wa madini ambavyowanalipwa, maeneo yote ya Ukanda wa Pwani na maeneoyote ya uvuvi ili pesa zile ziweze kusaidia sekta ya uvuvi kwawavuvi wadogo. Sisi tunaotoka maeneo ya ukanda waPwani samaki ndiyo madini yetu, kwa hiyo na sisi tunatakatulipwe royalty. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ambalo natakanizungumzie ni mbolea za kemikali katika kil imo.Tunahamasisha sana utumiaji wa mbolea za kemikali katikakilimo, lakini mbolea hizi baada ya kutumika zinakusanywana mvua zinaingia kwenye mito, zinapelekwa baharini,samaki wanakufa, sasa tunataka nini? Tunataka kilimo sanaau tunataka kufuga sana?

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili ni jambo ambalo inabidituliangalie kwa sababu unapotumia mbolea za kemikaliunatengeneza green algae ambao wana–suck ile oxygenyote kwenye maji, matokeo yake yanakuwa ni dead water,samaki hawawezi ku- survive. Sasa hili tuliangalie na lazimatuweke namna ambayo tunaweza kusaidia wavuvi wetutusilaumu tu kuwa tunavua bila kuwa na uvuvi endelevu lakinimatatizo kama haya yapo pia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikija katika eneo la mifugo,tumekuwa na migogoro mingi katika maeneo mengi nchini,lakini kwa nini Wizara zinazohusika Wizara ya Utalii, Wizara yaKilimo, Wizara ya Mifugo, Wizara ya TAMISEMI pamoja naWizara ya Ardhi, msiweke mpango mkakati ili kuwezakuainisha maeneo ambayo yanafaa ufugaji na kuwapa skillswale wafugaji, jinsi ya kuweza kukuza nyasi, kuzalisha chakulakwa ajili ya mifugo yao na kuondokana na haya matatizo,maeneo yote bora wanapewa wawekezaji.

Page 162: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

161

31 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilitegemea kwa kuwawawekezaji wanao uwezo mkubwa ndiyo wapewe maeneoyasiyofaa ili waweke miundombinu wafuge mifugo yao nayale maeneo ambayo hayana miundombinu wapewewafugaji wetu ambao hawana uwezo il i wawezekujiendesha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, huu msamiati wa watuwanaohama, watu wanaofuga, sisi tumewapokeaWasukuma wengi sana sababu kubwa ni wanetu, lakini wapowengine ambao wanakuja hapa wanahamasisha ukanda,hawa wakae Kanda hii na hawa wakae Kanda hii. Je, haowatu ambao wanahama leo kwenda mahali pengine,tukishaweka ukanda watu hawa wata-move vipi kwendakatika kila eneo? Tusilete kilio cha mamba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ambalo natakanilizungumzie ni masuala ya genes Bank, Tanzania badohatujawa nazo, leo itafikia wakati hawa kuku ambaotunawatumia watakuja kupotea na tutagemea kuagizakutoka nje, utaratibu huu Mheshimiwa Waziri unauelewa vizuri,tuweze kuhifadhi genes zetu hasa kwa kuku wale wa kienyejispecies zingine hata za ng’ombe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ambalo natakanilizungumzie ni katika hizi Ranch zetu za Taifa. Yametokeamatatizo Mheshimiwa Laizer amezungumza hapa, ng’ombewalikufa katika maeneo mengi, lakini utakuta katika baadhiya maeneo hata Kongwa na maeneo yale ya Ruvu kwenyezile Ranch za NARCO walikataliwa wafugaji wasiingie palekwenda kulisha mifugo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii ni mali ya umma, sasapale umma unakuwa na maslahi kwa nini tusiruhusu kwakushirikiana na wale wananchi, wakaenda kulisha mifugoyao, mara nyingine tungeweza kuokoa fedha nyingi ambazoMheshimiwa Rais aliidhinisha ili wananchi waweze kulipwafidia ile.

Page 163: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

162

31 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho kabisa, natakanizungumzie suala la artificial insemination, sijui kwa ninimpaka leo tunakwenda kusomesha watu kule kwenye chuochetu cha LITI, lakini wakitoka pale vifaa hakuna, hawaMaofisa mifugo na kada nyingine katka sekta ya mifugohawapewi ujuzi wa kutosha, wakishapewa ujuzi hawapewivifaa vya kazi. Kwa hiyo, ni sawasawa na tunachota majikwa uma tunatia kwenye tenga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bado sijakubali kuungamkono hoja mpaka pale nitakapoona fedha imeongezwa.Ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Nakushukuru sana MheshimiwaMangungu. Waheshimiwa Wabunge tunaendelea, sasatutamsikiliza Mheshimiwa Kitandula na baada yake atafuatiaMheshimiwa Richard Ndassa.

MHE. DUNSTAN L. KITANDULA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru sana kwa kunipa fursa hii ili niweze kutoamchango wangu kwa bajeti hii. Nianze kwa kumshukuruMwenyezi Mungu ambaye amenipa uzima mpaka siku yaleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kusema kuwasiungi mkono hata kidogo hotuba hii. Siungi mkono katu,nasema hivi kwa sababu bajeti hii haituhakikishii watu waUkanda wa Pwani kupata maisha bora, nasema hivyo kwasababu bajeti hii haiwahakikishii wananchi wangukuondokana na umaskini. Naikataa bajeti hii kwa sababu nimwendelezo wa ahadi hewa ambazo tumekuwa tukipewawatu tunaotoka kwenye ukanda wa uvuvi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuikubali bajeti hii nikuwaambia watu wangu wa Mayomboni, Moa, Doga,Kichalikani, Kwale, Manza, Boma kwamba, waendeleekuhangaika na umaskini wao. Siko tayari katika hilo, nitakuwatayari kuunga mkono bajeti hii pale tu kilio cha kila Mbungealiyesimama hapa kusema Wizara hii iongezewe fedhakitakapotekelezwa. (Makofi)

Page 164: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

163

31 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, sera zetu na mipango yetuimewaangusha watu wanaotoka kwenye ukanda wa uvuvi.Leo nitajikita katika sekta ya uvuvi peke yake, sitagusia mifugokwa sababu Mzee wangu Ole-Telele na Mzee wangu Laizerwamezungumza sana kuhusu sekta ya mifugo, walichosemakama hatusikii, basi hatutasikia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kukubali bajeti hii ni kukubalikuendelea kwa migogoro ya ardhi kati ya wafugaji nawakulima. Tusikubali, nawashawishi Wabunge wenzanguambao tumepewa dhamana ya kuisimamia Serikali,tusimame kwa sauti moja, kuwaambia this is unacceptable,lazima tuongeze bajeti kwenye Wizara hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ripoti ya Shirika la ChakulaDuniani, State of the World Fisheries and Agriculture kwamwaka 2012, inatuambia hivi, kwa mwaka 2012 jumla ya tanimilioni 154 zilivuliwa katika ukanda wa bahari na kwenyemaeneo ya ufugaji wa samaki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kati ya hizo tani milioni 131zilitumika kwa chakula, lakini samaki waliopatikana kwakufugwa ni tani milioni 79. Ripoti hii inatuambia kuwa, katikasekta ya uzalishaji wa chakula hakuna sekta inayokua kwakasi ulimwenguni kwa sasa kama ufugaji wa samaki. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika miongo mitatumfululizo, sekta ya ufugaji wa samaki imekuwa kwa 12%mfululizo. Hii inatakiwa kutufanya tufungue masikio, Wachinaambao tunawapigia mfano kwa mafanikio yao ya kiuchumi,wamelichukua hili, wameichukulia sekta ya ufugaji wa samakikwa umuhimu mkubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ripoti hii pia inaoneshakwamba, kwa mwaka jana ufugaji wao wa samakiwameweza ku-export kwenda soko la Marekani tani milioni1.1 ambayo hii ni sawasawa na Dola za Kimarekani bilioni5.9.

Page 165: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

164

31 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama Taifa kubwa lakiuchumi kama Uchina linaona umuhimu wa kuwekeza katikasekta ya ufugaji wa samaki, sisi Tanzania si zaidi, lazimamipango yetu ijielekeze sasa kwenye kuhakikisha kuwatunaipa kipaumbele sekta ya uvuvi hasa tukizingatia kuwa5.7% ya eneo letu ni maji yanayofaa kwa uvuvi, kwa maanaya maziwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tuna ukanda wa baharisquare kilometer 64,000, maeneo yote haya hayatumikiipasavyo, hii haikubaliki hata kidogo. Miaka mitatu iliyopitawenzetu Wakenya baada ya kugundua kuwa upatikanaji wasamaki kwenye Ziwa Victoria unapungua kwa kasi,walianzisha mpango maalum wa kujielekeza kwenye kufugasamaki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mpango ule,walihakikisha kwamba, kila Jimbo walijenga mabwawa 200.Kwa hiyo, mwisho wa siku walikuwa na mabwawa 30,000katika nchi nzima ya Kenya. Target yao walikuwa wanatakakuwa rural direct investment na revenue ya bilioni 20, jamboambalo wamefikia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hii wana samaki wengikiasi kwamba wanapata shida ya kupata soko wana-targetkuja Tanzania maana wameshashika soko la Kongo, Sudan,na Uganda, kwa hiyo, sasa wanataka kuingia Tanzania. Hivisisi mpaka lini tutaendelea kuwa soko la watu wengine?(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna fursa hizi, lakinihatuzitumii. Nilikuwa nasoma ripoti moja inaniambia kuwa,hata hawa tilapia ambao Wachina wanaongoza sasa,walichukua mbegu kwenye Ziwa Victoria, hadithi ni ile ile yamafuta ya Mawese, hii haikubaliki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. (Makofi)

Page 166: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

165

31 MEI, 2013

MWENYEKITI: Nakushukuru sana MheshimiwaKitandula. Naomba sasa nimwite Mheshimiwa RichardNdassa na Mheshimiwa Rose Sukum ajiandae.

MHE. RICHARD N. NDASSA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru sana kwa nafasi hii ya kuchangia katika Hotubaya Waziri wa Mifugo, lakini kwa leo usinishangae sana kwamara yangu ya kwanza mtambue kabisa kuwa siungi mkonobajeti hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suing mkono kwa sababunitaulizwa kule ninakotoka kwenye Jimbo langu, kwenyeWilaya yangu, kwenye Mkoa wangu, lakini ni pamoja nawafugaji wa ng’ombe Tanzania, umeunga mkono Hotubaile kwa sababu gani? Niungane na mapendekezo ya Kamatiya kuiomba Serikali nyongeza ya shilingi bilioni 40 ipatikane.Bila nyongeza ya hiyo hela, sitaunga mkono, nitakwendakulala na shilingi kesho. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, zikiongezwa hizo hela,tutapata madawa kwa ajili ya mifugo, malambo kwa ajili yamifugo, utafiti kwa ajili ya mifugo, majosho na kadhalika. Lakiniili Waziri aende kutekeleza majukumu ambayo yamo kwenyekitabu chake kwa pesa hii, Waziri tutakuwa tunamwonea.Tunataka tumpe pesa za kutosha ili kwenye bajeti ijayo, tujetumbane na nina uhakika Serikali tasikia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaitaka Serikali bilioni 40itafute kwa njia yoyote ile ili kusudi Wizara iongezewe pesa.Wamesema wenzangu hapa hivi unapotoa bilioni 47,zikafanye nini kwenye Wizara hii? Ni pesa kidogo sana hizi,naishauri Serikali na nafikiri imenisikia na imesikia kilio chaWaheshimiwa Wabunge wengine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nizungumzie sektaya mifugo na wenzangu wamesema na mimi naombaniseme. Ng’ombe wanadhalilishwa sana Tanzania, wafugajiwa ng’ombe wanadhalilishwa sana sijui wameikosea niniTanzania, kila wanakopita wanazomewa, wanasumbuliwa,hawa wafugaji wa ng’ombe wamekuwa kama vile wahalifu.

Page 167: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

166

Mheshimiwa Mwenyekiti, wapo wananchi wangu wapale Sumve, Malya na Nyambiti, Shimbamatoranya naMponeja, wana mifugo yao. Wamesumbuliwa huwezikuamini, utafikiri ni wakimbizi kwenye nchi yao. Ng’ombewamekuwa kama vile paka, wakati tukitoka hapa tukiendaKantini tunakumbana na nyama za ng’ombe. Lakinitunaposikia ng’ombe, tunasikia kichefuchefu. Mimi sielewi nikwanini?

Hivi Mheshimiwa Waziri wa Fedha pamoja nawachumi wako wote ulionao, hivi hamjui kwamba ng’ombeni mali? Kwanini msiwekeze kwenye ufugaji wa ng’ombe namwenzangu Mheshimiwa Kitandula bahati nzuriamezungumza sana hapa. Ukiwekeza kwenye mifugo, uvuvi,hizi nakisi za bajeti za Serikali zitapungua. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali utafikiri haina masikio,haisikii, haioni! Hivi wenzetu Botswana wao wamewezaje, sisitusiweze? Hivi Watalaam tunao au hatunao? NaiombaSerikali kupitia Wizara hii, tusingependa tena mwakanikwenye bajeti ijayo, pamoja na maneno mazuri yaliyomohumu ndani, tusisikie huo upungufu.

Mheshimiwa Waziri wewe ni mtalaam, kijanauliyebobea kwenye fani hiyo, Naibu wako, Watalaam wako,Madokta, Maprofesa wa mifugo na uvuvi. Hivi inapofikatarehe 30 unakwenda dirishani kuchukua mshahara kwa kazigani uliyofanya? Maana yake ni lazima ujiulize, huu mshaharaninaoupata ni kwa kazi gani kama yale ambayo umeambiwautekeleze hutekelezi? Huku ni kuwanyonya na kuwaibiaWatanzania na Serikali. Tunaomba kila mtu kwenye sehemuyake awajibike. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili uwajibike vizuri, Serikali nilazima itoe pesa Shilingi bilioni 40 ziwe Shilingi bilioni 87 nasiyo vinginevyo. (Makofi)

Mheshimiwa mwenyekiti, naomba niende kwenyesekta ya ngozi. Tulipitisha sheria hapa, tukatoa kwenye asilimia40 kwenda kwenye asilimia 90. Hii ina tatizo. Pamoja na

Page 168: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

167

kwamba mnasema kuna mfanikio, lakini mafanikio hayo nimadogo mno. Naomba tufanye utaratibu wa kubadilisha.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa Mzungumzaji)

MHE. RICHARD M. NDASSA: Kengele ya kwanza au yapili?

MWENYEKITI: Kengele ya kwanza, endelea.

MHE. RICHARD M. NDASSA: Mheshimiwa Mwenyekiti,tubadilishe utaratibu. ile ngozi ghafi na yenyewe ikiwezekanaitozwe ushuru kuliko ilivyo hivi sasa. Tatu, naomba MheshimiwaWaziri katika hizi ranchi zako kumi, nenda ufanye sensa tena.Hizi ng’ombe ulizotaja kwenye kitabu chako, mimi nasemasiyo sahihi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama Watanzania haowanaosimamia vyombo vilevile wanaweza wakajilimbikiziamagari ya Serikali, sembuse ng’ombe! Anahamisha gari laSerikali linakuwa ni la kwake, lakini ni gari la Serikali. Sembuseng’ombe! Naomba Mheshimiwa Waziri uende ufanye sensaupya. Hizi zinazotajwa kwenye ranchi kumi siyo halisia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri yangu yaWilaya ya Kwimba inaomba gari kwa ajili ya Idara ya Mifugona barua ipo ofisini kwako. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, namalizia kwa kusemakwamba siungi mkono hoja mpaka Shilingi bilioni arobainizipatikane.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. (Makofi)

MWENYEKITI: Haya. Ahsante Mheshimiwa Ndassa. Sasatutamsikiliza Mheshimiwa Rose Kamili Sukum, atafuatiwa naMheshimiwa Mfutakamba na Mheshimiwa Malochaajiandaye.

Page 169: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

168

MHE. ROSE K. SUKUM: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana kwa kunipa na mimi fursa niweze kuwamchangiaji mmojawapo. Lakini ninaanza kwa kusema, sisemikushika Shilingi kwa sababu Waziri mmoja alisema ukishikaShilingi ya Uwaziri, napokea ya Ubunge. Sasa sisi tunasematutakutoa ndani ya Uwaziri na sababu zipo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara ya Maendeleo yaMifugo na Uvuvi maana yake ni kuendelea kutoka kwenyekitu kidogo au kibovu kwenda kizuri. Lakini Wizara hii yaMaendeleo kutenga fedha Shilingi bilioni 47, eti kwa sababuni kwa ajili ya Wizara yote ikiwa ni mishahara pamoja na fedhaya Maendeleo, hii siyo kweli. Hii ni kudhalilishana au nikuidharau Wizara ya Mifugo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naanza kusema Wizara yaMifugo inadharauliwa wapi, ni kwenye suala la maendeleo.Mimi suala la mishahara yenu, masuala ya OC shauri lenu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la kutengwa Sh.8,973,316,000/= kwa ajili ya maendeleo ni ndogo sana kwaWizara hii ya Mifugo na Uvuvi. Tena matokeo yake kwenyerandama mliyoandaa, mambo mengi yanayohusishwa humuni makaratasi, sijui ku-supply kompyuta, sijui kitu gani, walahaihusiani na ng’ombe wenyewe, wala haihusiani na samakiwenyewe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sasa Wizara hiiikipewa pesa, siyo bilioni 40, nadhani iwe ni Shilingi bilioni 200.Kwa sababu Mheshimiwa Waziri mwenyewe tarehe 8 ulijibuswali langu ukasema Wizara hii ina-retain kwa kutokununuaminofu nje ya nchi trilioni 15. Sasa kama ina-retain trilioni 15,maana yake ni minofu ya samaki na minofu ya nyama, nikwanini sasa Wizara hii idhalilishwe kiasi hicho? Kwanini Wizaraya Uvuvi isipewe fedha za kutosha ili wavue vizuri au wenzetuwa mifugo au wachungaji wapewe fedha za kutosha kwaajili ya malambo, kwa ajili ya kutengewa ardhi, na kwa ajiliya kuweza kupata dawa kwa bei nafuu. Lakini matokeo yakemmewaacha hawa wachungaji wanahangaika wenyewe,hawana hata maeneo.

Page 170: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

169

Sasa mimi nasema hivi, hii Wizara ituambie,inapoomba pia hizi fedha za nyongeza, Shilingi bilioni 40 nikwa ajili ya kununua haya makaratasi na kompyuta aukuwasaidia wavuvi na wachungaji. Mimi ninachoomba nihicho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuielezea Wizarahii pia kwa sehemu nyingine. Wafugaji wanahangaika,migogoro imekuwa mikubwa, kila anayesimama hapaanazungumzia habari ya migogoro. Naomba utuambieMheshimiwa Waziri, naona unasemeshwa hapo hutakikutusikiliza, naomba utuambie, wafugaji ni lini wataachakuhangaika? Wafugaji ni lini wataacha kuhamahama? Ni liniwafugaji wataacha mateso ya kuweza kuuza minofu yao?Kwa sababu tunauza ng’ombe kwa bei ya chini halafumatokeo yake wenzetu wanauza kwa bei ya juu kwa sababundio wenye viwanda. Je, utuambie sasa, sisi ni lini viwandavyetu vitatengamaa? (Makofi)

Mheshimiwa Waziri, naona Mheshimiwa Waziri waFedha anakusumbua hapo, lakini mimi naomba aondokekwa sababu anatusumbua na sisi, nawe usiweze kutusikiliza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuelezea kwambahapa wamezungumza suala la kwamba wametengamaeneo, kuna Halmashauri zimetenga maeneo, ni uwongomtupu! Kwa Babati tu ambako ni Mkoani kwetu. Babati ipiiliyotenga hekta 20,000? Wapi? Tuambieni, Babati ipi? Sisindiyo watu wa kule kwa nini mseme uwongo. Hii taarifa yakoni ya uwongo pia. Mnaandikia mezani, mnapeana taarifaambazo siyo sahihi. Wilaya ya Hanang’ iko wapi? Kwaniniwasitengewe Wilaya ya Hanang’ wakati ina wafugaji niwengi? Simanjiro iko wapi? Kwanini wasitengewe maeneoyao ya ufugaji? Kiteto iko wapi? Maeneo ambayo Waziri yupowa Kiteto, yake pia haikuwekwa hapa kwa sababu niuwongo.

Kiteto wana mifugo mingi, lakini zimetengwa heka 400tu, ni kidogo sana! Lakini mifugo ni mingi sana. Naombautuambie hii taarifa umeitoa wapi? Waziri watu wako ni

Page 171: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

170

waongo, wanakupa taarifa za uwongo Mheshimiwa Waziri.Nawe ni lini umekwenda kufanya Mikutano na wafugaji iliwakueleze. Tuambie ni sehemu gani ulikwenda? Wilaya gani?Kama ni Wilaya ya Hanang’, uniambie ulikutana na wafugajiwa Kijiji gani ambao wanahangaika na maeneo, ukawaelezakwamba mmetengewa eneo fulani. Hawa wengineuliowatembelea ukaja kuwadanganya WaheshimiwaWabunge kwamba wametengewa eneo, ni wapi? Hiyo niuwongo kabisa! Naomba kweli Mheshimiwa Waziri, miminitatoka na wewe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naendelea kwenye suala lamalambo, fedha zimetengwa Wilaya nzima unaipa lambomoja, tena ni malambo ya mwaka 2012 ya mwaka huuhatuyaoni. Niambie Wilaya ya Hanang’ inapata linimalambo? Yale ambayo ni ya PADEP yaliyojengwa zamaniunayarekebisha lini ili yawe na maji? Kwa sababu hakunahata lambo moja lenye maji. Tunaomba utuambie,tunafanyaje kwa ajili ya malambo? Kwa sababu bilamalambo ndiyo maana ng’ombe wanahamahama, hakunamaji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niendelee na sehemu yaNARCO. Wenzetu NARCO ni shirika lililopo ndani ya Wizaraya Kilimo, Wizara ya Kilimo naomba kuwaelezeni kamahamkufuatilia; Baraza la Mawaziri mwaka 2002 Waraka Na. 2walitoa kwamba mashamba ya NARCO sasa hivi yanatakiwayagawanywe kwa blocks ili wafugaji wadogo wadogowapewe. Juzi mmetangaza Mkata. Mlipotangaza Mkata,mmeweka mambo magumu. Mnataka wawekezaji kutokanje wawekeze badala ya wawekezaji kutoka ndani. WakatiSerikali hii ilisema hatutawapa wawekezaji kutoka nje baliwatakuwa wa ndani.

Sasa hebu niambie tusaidiane hapo, Wizara ndiyommehusika. Mimi nasema Mheshimiwa Waziri wewe ndiyoumehusika kwa asilimia mia moja. Kwa nini muweke mazingiramagumu ili wafugaji wadogo wadogo wasiweze kuombakuwa Wawekezaji kwenye mashamba ya NARCO? Kwaninimnawawekeza watu wa nje? Tutaangalia kwa shamba la

Page 172: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

171

NARCO la Mkata. Kama atawekwa mtu wa Oman, maanayake mnauza nchi hii. Tunataka watu wa Kilosa waingie,Watanzania waingie ndiyo wawekezaji lakini sio kutokaOman. Maana yake tumeona list ya majina lakini hatujui ninani anapewa. Kwa kuwa hatujui ni nani anapewa na sisituna uhakika anayepewa ni yule mwenye hela kubwa; sasakama mmekwenda kwenye hela kubwa mewaachawafugaji wadogo wadogo wana ng’ombe, NARCOwangekuwa wanashiriki pamoja na kuchunga na wawekezajiwa mashamba hayo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nizungumzie sualala Uvuvi kidogo, na namwomba Mheshimiwa Waziri kwasababu haya yametokea kwenye Mkoa wa Manyara;kufungwa kwa maziwa. Wavuvi wanategemea uvuvi tu nawachuuzi wana tegemea uvuvi tu. Mkiwafungia maziwa: Je,hawa Wavuvi hawafi na njaa? Mmewapa mbadala nini?Matokeo yake watu wanahangaika wanakuwa wezi! Hivi niutaratibu wa namna gani wa Wizara kufunga maziwa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunataka kujua, kwa sababumaziwa yote katika Mikoa karibia mitatu, wanasema Mkoawa Manyara, Tanga na Kilimanjaro wamefunga maziwa kwamiezi sita. Unategemea wale wataishije kama siyo kuwatesa?Tuambieni mbadala wa kuwasaidia wale ambao walikuwani wavuvi na walilipa leseni. Je, Serikali inasemaje kwa kulipaleseni? Wale wachuuzi: Je, wanaishije ili waweze kukimumaisha yao. Kwa nini Serikali inajichukulia tu hatua au kilamtu anaweza kuamua kufunga ziwa? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu hayayametokea kwenye ziwa Basotu, ziwa Babati, ziwa Burungepamoja na ziwa la Nyumba ya Mungu. Tunaomba msaadawenu na mtuambie tunawasaidiaje wananchiwanaohangaika na maisha yao? Matokeo yakewanafungwa na kusingiziwa kesi za ajabu ajabu kwa sababuwatu wamelipia leseni, wanadai leseni zao walipwe na badohawalipwi, wengine wanalipishwa faini za ajabu ajabu.Tunaomba msaada wa Wizara.

Page 173: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

172

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kumalizia, naombakusema kwamba siungi mkono hoja, na ninasema kwambaWaziri huwezi kazi ya mifugo kwa sababu umeshindwa…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Rose ni kengele ya pili,naomba uheshimu muda.

Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea. NaombaWaheshimiwa Wabunge muwe mnajali kengele ya muda.

Nilisema nitamwita Mheshimiwa Mfutakamba nanikasema nitamwita Mheshimiwa Malocha, mnisamehe sana,nimeangalia vibaya kwenye orodha yangu. MheshimiwaMalocha hajaomba kuchangia Wizara hii, lakini badala yakeatachangia Mheshimiwa Kilufi ambaye yupo kwenye orodhaya Wabunge wa CCM. Mheshimiwa Mfutakamba atafuatiwana Mheshimiwa Kilufi.

MHE. ATHUMANI R. MFUTAKAMBA: MheshimiwaMwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi nichangie katikaWizara hii muhimu ya Mifugo na Uvuvi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme tu kwamba Wizarahii inahitaji kuwa na Wakala wa Miundombinu ya Ufugaji. Kwamaana hiyo, Wizara hii ni lazima iongezewe pesa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, majukumu ya Wizara hii nimakubwa. Kama bajeti finyu hii waliyopewa tutakuwatunawalaumu, tunamlaumu Mheshimiwa Waziri, tunamlaumuNaibu Waziri na tunamlaumu Katibu Mkuu, waongezewefedha ili waweze kufanya kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nina imani kubwa naMheshimiwa Dkt. David Mathayo, sina matatizo naye kabisa,ni mtalaam aliyebobea, na Naibu wake ni mzoefu mkubwapamoja na Katibu Mkuu wao Dkt. Charles Nyamlundwa.Tuwape support, tuwasaidie ili Wizara hii iweze kuwa na fedha

Page 174: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

173

za kutosha na kuanzisha Wakala wa Miundombinu ya Ufugaji.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la Serikali au nchikuagiza samaki au kuagiza nyama kutoka nje, hili halikubaliki.Hili halikubaliki kwa sababu wao wakiongezewa pesawataweza kufanya kazi. Nanong’onezwa hapa, watawezajekazi? Nataka kusema hivi, tuwape bajeti ya kutosha, halafutuangalie kama hawatendi. Hiyo ndiyo haja yangu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala la kuwezakujipanga. Mimi mwaka 2009 nilikuwa DC Kilolo, tulifanyasafari ya China, mimi ndiye niliyeongoza msafara huo, nilikuwana Wawakilishi kutoka Zanzibar kwenye masuala ya uvuvi,lakini kutoka Bara ilikuwa ni masuala ya kilimo cha Chai. Lakinituliporudi hapa tulikuja na Mwekezaji wa Ranchi ya Ruvukuanzisha kiwanda cha nyama.

Nataka Mheshimiwa Waziri aniambie nini kilitokea,kwa sababu wale watu wlaisema wana fedha, wanatakakuja kuwekeza hapa, na nilikuwa naamini kile kiwandakingekuwa tayari sasa 2013. Ninahitaji majibu kwa suala hilola kiwanda cha nyama; nini kimetokea?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakuja suala la pasturedevelopment. Tarehe 27 Oktoba, 2010, Rais wa Jamhuri yaMuungano - Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, paleIsikizya, Ilolasimba, alitoa kauli kwamba kutakuwa na mpangokabambe wa kuanzisha maeneo ya malisho. Ninashukurusana katika kitabu cha hotuba ya Waziri, nimeona kabisaukurasa wa picha kule mwishoni, nimeona eneo ambalozinapandwa nyasi aina ya mikunde kwa ajili ya malisho.

Nimeona Kongwa malundo ya majani ya kulisha hiimifugo. Naomba utaratibu huu, bajeti zitosheleze. MimiIgalula nina Kata 10. Zile Kata zote 10 ni za Wafugaji, Loya,Goweko, Nsololo, Kigwa, Miswaki, Lutende, Igalula kote niwafugaji. Lakini wanatangatanga, mazingira yanaharibika,miti inakatwa, vyanzo vya maji vinaharibika. Ni lazima Wizaraisimamie mpango wa matumizi bora ya ardhi ili tuweze

Page 175: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

174

kuweka maneo ya wafugaji, maeneo ya kilimo, na tuwezekuhifadhi mazingira ili maji yaweze kuendelea kupatikana.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaweza kupata jangwaharaka sana Jimbo la Igalula na sehemu nyingine zote.Uwekwe utaratibu maalum utakaosaidia maeneo ambayokutakuwa na malambo, kutakuwa na majosho na maeneohayo tuweze kuangalia utaratibu mzima wa viwanda vyakusindika nyama na viwanda vya kusindika ngozi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, haiwezekani jamani tuagizenyama kutoka nje ya nchi wakati sisi ni nchi ya tatu kwa wingiwa mifugo. Ethiopia na Sudan, nikubali kabisa kwambawenzetu utaratibu mzuri wanao wa matumizi bora ya ardhi.Botswana kila mfugaji sharti moja la kuwa na mifugo, ni lazimauwe na kisima uwe na bore hole. Nasi tufuate utaratibu ulekwa sababu ndugu zetu wanatangatanga kwa sababuwanatafuta maji, wanatafuta mbuga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mbuga hizo hizo tunatakakulima mpunga, mbuga hizo hizo tunataka kulima mahindi.Lakini sasa kama kwato za ng’ombe zitakwenda kwenyemaeneo kama hayo; nimekaa Iringa nimeona Ihefu, Ihefuuharibifu ni mkubwa. Lakini hawa wafugajiwanapotangatanga, kwa nini tuwalaumu? Ni lazimatuwawekee mazingira, lazima tuwawekee miundombinuambayo hawatakuwa na sababu ya kwenda kwa jiraniyangu Ifakara, hawatakuwa na sababu ya kwendaMorogoro, hawatakuwa na sababu ya kuja Igalula kamamaeneo yao kutakuwa na bow holes za kutosha, watakukwana eneo la malisho, malisho ya kupanda, ambayo kiangaziwatavuna kama ninavyoona malundo hayo ya nyasi za kulamifugo Wilaya ya Kongwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, elimu ya utunzaji wamazingira ni muhimu sana. Wafugaji, wakulima lazima elimuhii iweze kuendelea. Ndugu zangu wengi wametoka Simiyu,wametoka Geita, wametoka Mwanza, wametoka Bariadi,wamekuja wote Igalula na mifugo, nami nawakaribisha.

Page 176: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

175

Lakini Sasa mifugo inanilemea kwenye Jimbo la Igalula.Nitafanyaje na mimi ni mtu rahimu, mtu mkarimu? Lakini sasamazingira yanaharibika. Wao wanasema lazima akikaanyumbani kwake pale kilomita moja awaone ng’ombe wakewanavyokuja. Kwa hiyo, lazima akate miti kuangalia kulembali. Haiwezekani!

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kwa hiyo, naiomba Serikalikwa sababu mimi nimekuwa Mjumbe wa Kamati ya TAMISEMI,fedha hata zinazotolewa Sekretarieti za Mikoa kusimamiamasuala ya mifugo, ni kidogo sana. Haiwezekani! naombasana Bajeti iongezwe ili Wizara hii iweze kufanya kazi kikamilifu.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nije kwenye suala la Kilolo.Kilolo nilikuwa DC Mawambala; kwa kutumia ufugaji wakisasa, yuko ng’ombe ana tani moja; siyo ng’ombe mmoja,wako wengi; yako mashamba yale mazuri na kuna wafugajiwengine wanakuja kujifunza pale shamba la ASAS shambala Philips na kule Mawambala. Tuwapeleke wafugaji wetukwa utaratibu waende NAIC (National Artificial InseminationCenter) kujifunza ufugaji bora ili tuwe na mifugo boramichache. Ng’ombe wachache lakini waonenepa vizuri. Kuleng’ombe mmoja ana kilo 1,000. Anatoa maziwa lita 35.Asubuhi lita 15, jioni amekula nyasi lita 20. Hili linawezekana!Tutumie wataalamu wetu wa ugani wa mifugo, wasikaemaofisini, waende kila Kata, kila Kijiji wafanye kazi na wafugajina hili tatizo litapunguza ile idadi ya mifugo kuwa mingi natutaweza kupata tija kubwa katika uchumi wa nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimetembea, nilikwendaThailand, sehemu zenye maji maji, sehemu zenye mabwawa,samaki wengi wanapatikana kutoka kwenye hayamabwawa. Sijaona jitihada kubwa kutoka kwenye Wizarakatika kusaidia kilimo cha ufugaji wa samaki kwenye vijijihusika. Tupeleke ile mbegu ndogo ya wale samaki tuwezekufuga na hii itasaidia pia. Tusiendelee tu kuchoma nyavu,tuwawezeshe hawa wavuvi kuwapa nyenzo bora za kufugana tuwape elimu. (Makofi)

Page 177: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

176

Kuna wengine bahati mbaya wanavua samaki kwadynamites. Yuko rafiki yangu mmoja karibu na Sea Cliff pale,kila siku akikaa kwenye balcony anaona bahari inalipuka puuhapo Dar es Salaam. Tuwe na watu ambao watadhibiti hawawatu kwa sababu wanaharibu mazalia ya samaki,wanaharibu mazingira yetu, lakini pia tuwawezeshe na piatuwaelimishe. Tukikamata nyavu, tukizichoma, yule mtutunampa elimu, kwamba wewe uvuaji wako utakuwa hivina nyenzo ni hizi, sheria taratibu na kanuni zifuatwe kulindamazingira ya bahari na raslimali zao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuongeze pesa Wizara hii iliiweze kutenda kazi zake kikamilifu. Kwa hayo machachenaunga mkono hoja, kwa sababu nataka hawa wafanye kaziMheshimiwa Dkt. David Mathayo na Naibu wake MheshimiwaOle-Nangoro na Katibu Mkuu Dkt. Charles Nyamrunda, NaibuKatibu Mkuu, Prof. Makungu, wanaweza kazi hawa.Tuwaongezee pesa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Tunakushukuru sana Mheshimiwa Dkt.Mfutakamba kwa mchango wako na kwa kujali muda vizuri.Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea sasa, namwitamchangiaji anayefuata kama nilivyosema, namwitaMheshimiwa Kilufi - Mbunge wa Mbarali, lakini atafuatiwa naMheshimiwa Sylvester Mabumba Masele na atafuatiwa naMheshimiwa Mkiwa Kiwanga.

MHE. MODESTUS D. KILUFI: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba nikushukuru sana kwa kunipa nafasi hii ili na miminiweze kuchangia Wizara hii. Naomba nichukue nafasi hiikuwapa pole sana wafugaji wote waliopo katika nchi hii, kwamazingira magumu ya ufugaji ambayo wanayapata nabado hakuna hatua yoyote ya msingi ambayo imechukuliwakuhakikisha wafugaji hawa nao wanaishi kama Watanzaniawengine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mifugo ndiyo tegemeo letusisi wote humu ndani. Hakuna mtu mwingine anayenda

Page 178: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

177

buchani akauliza nyama kutoka labda kwa wanyama waporini. Anauliza nyama ya ng’ombe, nyama ya mbuzi nanyama ya kondoo. Lakini huyu anayetufanya tupate kitoweohicho ndio tumemwacha kama mtoto yatima. Hii haikubalikikabisa. Lazima tufike mahali sasa tukubali kwamba uundwempango maalum, Wizara ijipange, iandae mkakati ambaoutaonyesha namna gani tunawasaidia wafugaji waliopokatika nchi hii. Haiwezekani tukaendelea kuzungumza tuhumu Bungeni, kila siku tunasema wafugaji wanateseka,wanateseka, lakini hakuna hatua ya msingi ambayoinaonekana katika kuondoa tatizo hili la wafugaji katika nchihii. Wafugaji wanaishi kama wakimbizi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumefanya bidii sanakupanua hifadhi zetu za Taifa kwa maana ya wanyamapori,tunashindwaje kuweka eneo kwa ajili ya mifugo yetu ambaotunapata kitoweo kila siku? Mimi sijaridhika kabisa. NadhaniWizara lazima iseme kitu, ilete mpango ambao tutaridhikakuona namna gani tunaweka mazingira mazuri ya ufugajikatika nchi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napata taabu sana, nchi hiiwafugaji wakishirikishwa wana uwezo wa kushiriki kuchimbamalambo. Wanao! Wanachongoja ni mpango tu wa Serikali.Hakuna mpango madhubuti unaoonesha ushirikishwaji kwawafugaji katika kuondoa matati yao, haupo. Wafugaji nikama hawana Wizara, afadhali hata ingebaki kamailivyokuwa zamani. Kwa sababu gani? Tulitegemea Wizarahii ya Mifugo sasa itakuwa karibu kabisa na kuondoa matatizoya wafugaji, lakini imekuwa ni kinyume kabisa. Wizara hii miminasema sitaunga mkono kama sitapata majibu ya msingikuonyesha ni mpango gani mkakati umeandaliwa ili kuwekamazingira mazuri ya wafugaji katika nchi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kule Mbarali, kwa bahatinzuri, nasema nzuri, tumesogelewa na Hifadhi. Tumekubali.Wananchi wameondoka, tumenusuru Ihefu, tumekubali.Lakini mpaka leo hii taabu wanayopata wafugaji walehaipimiki hata kwenye mizani. Kila siku kwa sababu mpakahaueleweki na mimi nimepiga kelele mpaka nimechoka,

Page 179: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

178

jamani tuweke mpaka, wafugaji wanaumia, lakini mpakasasa bado Wizara hainisaidii. Maana yake Wizara ya Maliasilina Utalii ina majukumu mengi, inawezekana, lakini ingepatanguvu hata ya Wizara husika kwa taabu wanayopatawafugaji kwenye mipaka, pengine ingewezekana hawawatu wa Hifadhi wakafanya utaratibu wa haraka wa kuonamipaka kwenye maeneo yanayopakana na wananchiinaandaliwa mapema ili wafugaji wasipate shida. Hakunampaka unaoonekana. Lakini mfugaji akikutwa pale,ng’ombe mmoja faini Sh. 25,000/=, ng’ombe mmojaSh. 10,000/= wafugaji wanaumia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini Wizara haionimatatizo haya ikasimama na yenyewe? Kwa nini Wizara hiihaioni kilio cha wafugaji? Kama haiwezekani, basi miminiombe iundwe Kamati Maalum kwa ajili ya kuchunguzamatatizo ya wafugaji. Vinginevyo, hawa wafugaji itafikamahali watakimbia nchi hii. Kama tunaweza kulipa fedhakuhamisha wananchi kwa ajili ya kupisha kupanua Hifadhikwa ajili ya wanyamapori, tunashindwaje kufanya hivyo kwaajili ya kutenga maeneo ya wafugaji? (Makofi)

Kwa nini tusiwashirikishe hawa wafugaji kwenyekuchimba malambo kwenye maeneo yao wakaona na waowanawajibika kuchangia? Kwa nini mpango huo usije hapa?Sasa sisi kama Wabunge tunaiteteaje Wizara? Hakunampango mkakati unaoonekana kwa ajili ya kunusuruwafugaji, hatuuoni uko wapi? Kama kungekuwa na mpango,sisi tungesimama imara kuwasaidia. Tungesimama imarakuhakikisha Serikali inatoa bajeti kwa ajili ya kusaidiakuhakikisha mpango huu mkakati unatimia. Lakini sasa mimisijaona jitihada kabisa. Watanisamehe. Kilio cha wafugajikatika nchi hii hakitakwenda hivi hivi, haiwezekani kabisa.Wananchi hawa wanapata mateso makubwa sana.

Ndugu zangu kama hamwamini, kama kuna matatizoambayo ni sawa na maafa ni pamoja na kilio cha wafugajikatika nchi hii. Wanatozwa faini huko mipakani; tulikuwa namashamba ya Taifa NARCO, tumewapa watuwanayachezea tu, hakuna kazi ya maana inayofanyika kule.

Page 180: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

179

Naomba Wizara kuanzia sasa waache kubaki ofisini, wapitekwa wafugaji wakaone matatizo yao. Wapite wazungukehii nchi waone matatizo ya wafugaji. Washirikiane naowaainishe maeneo ya kujenga malambo, wawashirikishewale watachangia. Mifugo siyo kwamba ni bidhaa ambayohaiuziki, inawezekana kabisa! Nchi hii tunaonekana kamatuna ng’ombe wengi sana, lakini sisi siyo wa kwanza katikaBara la Afrika kuwa na mifugo mingi. Zipo nchi ambazo zinamifugo mingi, lakini hawapati taabu wafugaji wao kama sisi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema hivi kama sitapatamajibu ya kuridhisha juu ya mipango kamili na thabiti kwaajili ya kuboresha hii Wizara ya Mifugo na Uvuvi, sitaungamkono kuipitisha hoja ya Wizara hii. Sisi Wabunge tunaotokamaeneo ya wafugaji, adha ya wafugaji tunaijua. Taabuwanayoipata tunaifahamu. Wameshindwa tu kuja Bungenikuandamana. Wengeweza, wangekuja hapa. Wangekujakabisa, wangefika! (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo hili ni serious. Kamalilikuwa linachukuliwa kwa mzaha mzaha, naomba kuanziasasa ndugu zangu Waheshimiwa Wabunge tuungane,tuhakikishe tunawaokoa hawa wafugaji wetu. Haiwezekaniwakapata taabu katika nchi hii, wakakaa kama wakimbizina sisi viongozi wao tupo. Serikali ni ya kwetu, kwa nini isisikie?Kwanini tusiungane tukatenga maeneo ya wafugaji?(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kilio cha wafugaji hakiwezikwenda hivi hivi. Sisi tunaotoka maeneo, tuliojitoa… (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mbunge hiyo ni kengeleya pili.

MHE. MODESTUS D. KILUFI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nitaunga mkono hoja baada ya maelekezo na majibu yaMheshimiwa Waziri kuona kwamba…

Page 181: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

180

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mbunge hiyo tayari nikengele ya pili. Waheshimiwa Wabunge tunaendelea namchangiaji anayefuata. Nilisema atafuata MheshimiwaSylvester Masele na Mheshimiwa Mkiwa ajiandae. Naombatena kuwakumbusha kutunza muda.

MHE. SYLVESTER MABUMBA MASELE: MheshimiwaMwenyekiti, napenda nikushukuru kwa kunipa muda huuniweze kuchangia hoja hii. Kwanza siungi mkono hoja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesema siungi mkono hojakwa sababu zifuatazo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa Wabunge wa CCMwatakumbuka tulipokutana na Mwenyekiti wa Taifa waChama chetu alisema, fedha siyo tatizo. Kama unazo kaziambazo zinaridhisha jamii na wananchi wa Tanzania, kamawewe huna uwezo wa kutafuta pesa, umwambie yeyeatazitafuta pesa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa leo hii tunaposemabajeti ya Wizara ni ndogo, Mheshimiwa Waziri na Watendajiwake wameridhika. Hii inaonesha ni namna gani siowazalendo, wananchi wetu wanateseka, wanaranda randakila mahali, hakuna wa kuwatetea. Kwa hiyo, naomba sanaMheshimiwa Waziri, ameorodhesha wahisani wengi pagembili. Hebu atuambie, katika sekta zote mbili; maana yekeyeye ana sekta zake kuu mbili, mifugo na uvuvi.Amewashajiisha namna gani ili waweze kuisaidia Wizarayake? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu wahisani hawatunategemeana sana na wao. Sasa kama wao wamekujakumuunga mkono kwa kuorodhesha hapa wote kwambawanashirikiana na yeye, ni fedha kiasi gani ambazowamesaidia kwenye mifugo na kwenye uvuvi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye mifugo, kwanzaatusaidie, ameshirikiana vipi kutenga maeneo ambayowafugaji watatumia kulisha wanyama wao? Lakini la pili,

Page 182: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

181

amesaidia kiasi gani wafugaji ili wasihame hame, kuwa namabwawa ya kutosha ili wanyama hao wapate maji, lakinivile vile kuwa na majosho ili wanyama hawa waepukane namaradhi? Lakini la tatu, ametuelezea hapa mamilioni yawanyama tulio nao Tanzania. Hao wahisani ambaoamewaorodhesha hapa, ni wangapi wamejitokeza kujengaviwanda vya kusindika mazao ya wanyama? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naungana na wasemajiwote waliopita kwamba sekta hii imekosa wasimamizi.Tunahitaji kuhakikisha rasilimali ya wanyama inabadili maishaya wafugaji na Tanzania kwa ujumla. Lakini hakuna ubunifu.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nadhani kama kwelisisi ni wazalendo, na kama kweli Wizara hii haijaridhika napesa ambazo imetengewa, na tuone Mheshimiwa Waziri naWasaidizi wake wakisimama hapa kujiuzulu. Lakini kwasababu wako kwa ajili ya mishahara yao, wafugaji na wavuvisio kipaumbele kwao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni aibu kwamba Tanzaniainaagiza samaki. Nina taarifa hapa ya utafiti iliyofadhiliwana FAO ya mwaka 2007 ambako inaonyesha wazi kwambaTanzania inaagiza hata samaki, pamoja na ukweli kwambatuna maziwa makubwa matatu Victoria, Tanganyika naNyasa; tuna maziwa madogo Rukwa, Eyasi, Momera kuleArusha; lakini tuna ukanda mkuu wa Bahari na tuna mitomingi sana. Pamoja na yote hayo, bado tunaagiza samaki.Tunatumia zaidi ya bilioni kuagiza samaki. Ni aibu kwaTanzania.

Ninaomba Mheshimiwa Waziri akija hapa atuambieni mikakati gani wanaitumia hata kwa hao wavuvikuwawezesha kuwa na zana za kileo siyo kwenda kuchukuanyavu na kuchoma moto. Mimi naomba maeneo ya wafugajiwote tuhamasishe wafugaji kama vile wanafunziwanavyoandamana kwenda kumsumbua Waziri wetu waElimu na wafugaji waongoze ng’ombe wao wamfuate WaziriOfisini kwake. (Makofi)

Page 183: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

182

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndipo Waziri ataweza kuonauchungu wanaoupata watu hawa. Akienda tu na LandCruiser lake, V8, na nini, V8 hili ni kwa sababu ya pesa zawalipa kodi. Naomba sana Mheshimiwa Mwenyekiti, wafugajina wavuvi hawa kama tungewasaidia, hata manenoambayo yanatoka hapa yasingetokea hapa tena. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini tuna hizi Ranch za Taifaambako tumeambiwa hapa, atuambie, basi kutokana naranch za Taifa hil i ni viwanda vingapi ambavyovimehamasishwa kujengwa au ambavyo sasa hivi tunavyoau ambavyo amefufua Mheshimiwa Waziri toka akalie nafasiile kwa sababu kwa elimu hatuna hofu naye. Lakini kwenyeuthubutu, tuna hofu. Kwenye uthubutu tuna hofu kwambahawezi kuanzisha jambo hata moja ili watu wakajifunza.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, angeanza japo na Mikoamiwili tu ili baadae tuone sasa kwamba kuna haja yakumsaidia Waziri apanue Mikoa mingine. Leo hii ni aibukwamba tunakaa hapa tunaweka mikakati kwa ajili yawanyama pori ambao kwa hakika wakati wa ukame kuleSerengeti na Ngorongoro wanakwenda Kenya na kule Kenyakurudi kwao huku ni hiari yao, inakuwa ni mali ya Kenya. Lakinihawa wafugaji wenye ng’ombe tuna hakika ni mali yaWatanzania. Lakini kwa nini hatuweki mkakati kwa hawawafugaji tuweka mikakati mikubwa kwa wanyamaporiambao wakati wa ukame kama ninavyosema wana-migrate,na waki-migrate, wengine wanauawa kule wanang’olewameno yale yanauzwa na wengine ndiyo wananufaisha sektaza kiutalii katika nchi ambazo wana-migrate.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba tuwahurumiewafugaji. Lakini pia tunaposema tuhurumie wafugaji lazimatuisaidie Mikoa. Naomba Mheshimiwa Waziri akija kujumuishaaniambie ni lini alifanya mikutano na Wakuu wa Mikoakuhamasisha namna gani wao kwa kuanzia watahudumiawafugaji? Kwa sababu, kama alivyosema MheshimiwaMfutakamba, tumekaa Kamati ya TAMISEMI, tumeangaliabajeti ile, lakini hatujaona wapi Mheshimiwa Waziri wa Mifugo

Page 184: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

183

na Uvuvi amekuwa mkereketwa kushirikiana na Wakuu waMikoa. Zaidi sana wanahangaika sana wale. Tukikaa hapatunasema Mkuu wa Mkoa fulani hafai, lakini kumbe kunaWizara ambazo zingeweza kuwasaidia wakawawanapunguza lawama hizi za kuhudumia wafugaji katikamaeneo yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wafugaji hawa kwa upandemwingine ni kura za CCM. Lakini tunapodharau kura zile,itakula kwetu. Ni jambo dogo sana, wakiingia wenzetuwakawapa maneno ya matumaini, watatuasi sisi. Rafiki wakweli ni yule anayeshughulikia kero zako. Maneno matupuhayavunji mfupa, kwa hiyo, watu watatukimbia. Mwaka 2015haiko mbali. Naomba tuanze sasa, mna maneno matamukweli! Big Result Now! Big Result Now, how? Sehemu kubwaya wafugaji hatuwajali, hatuwasaidii na hata wavuvi wetuhatuwasaidii, rasilimali ya samaki inaporwa. Tuna udhibiti ganikwenye bahari kuu? Kama walivyosema wenzangu, hiiExclusive Economic Zone tunahudumia vipi? Tuna vyombovingapi kwenda ku-monitor meli zinazokuja kule ndani?Hakuna! (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wanavua samaki wana-dissapper Japan wapi, baadae eti tuna import tani saba zasamaki. Shame on us. Naomba tubadilike. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusemamachache haya, naomba nisubiri majibu ya MheshimiwaWaziri, vinginevyo siungi mkono hoja. Ahsante sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Massele.Waheshimiwa Wabunge, naendelea na orodha yangu. Sasanitamwita Mheshimiwa Mkiwa na Mheshimiwa Diana Chilolo,ajiandae.

MHE. MKIWA A. KIMWANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Awali ya yote napenda kumshukuru MwenyeziMungu aliyenipa uhai na nguvu kwa siku hii ya leo na miminikasimama kwenye Bunge lako hili, kuchangia Wizara iliyokombele yetu.

Page 185: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

184

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningependa kusema nenomoja. Wizara hii nafikir i kama sijakosea, haijui niniinachokisimamia. Kwa nini nasema hivyo? Wavuvi wanapigakelele, wafugaji wanapiga kelele. Sasa hivi ni kipi ambachohasa kinasimamiwa kwenye Wizara hii ambacho kinauafadhali tukasema angalau huku kuna nafuu? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kidogo kuongeleawavuvi wa Ziwa Victoria. Hii ni mara ya pili kama siyo ya tatunimesimama kwenye Bunge hili na kumwomba MheshimiwaWaziri ashirikiane na TAMISEMI ili mvuvi anapoweza kukataleseni ya mwaka mmoja, leseni hiyo anapotoka Wilaya mojakwenda Wilaya nyingine asiombwe tena mchango unaozidilaki, laki na kitu, kwa sababu Ziwa ni hilo hilo la Victoria. Wakatianaweza akatoka Wilaya ya Ilemela akaenda Wilaya yaUkerewe akaombwa tena fedha nyingine. Lakini upande wamagari, ukishalipia tu kodi utatembea Tanzania nzima,hakuna mtu atakuuliza wewe umelipia wapi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hii inawakwazawavuvi na kama Halmashauri wanategemea wavuvi ndiyowaweze kuchangia katika mapato ya Halmashauri,tunawaumiza wavuvi na hasa ukizingatia wavuvi hawawanavua kizamani, hamna mtu anawawezesha, hawanaelimu, hawana mikopo, lakini wanachangia pato la Taifa kwaakili zao wenyewe bila kusaidiwa na mtu yoyote. MheshimiwaWaziri wa Mifugo na Uvuvi ninakuomba kaa na Wizara yaTAMISEMI, kama ni kiwango cha kulipia leseni, kiwe kiwangokimoja, ilimradi mtu akishalipa aweze kuvua ndani ya ZiwaVictoria bila kikwazo chochote. Wavuvi hawa wanaumia.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wavuvi wa Ziwa Victoriakwanza bado wana vua kizamani lakini wanachangia patola Taifa. Tunaambiwa katika pato la Taifa uvuvi unachangia1.4% lakini zaidi ya 60% zinatoka Ziwa Victoria. ZinapotokaZiwa Victoria, tunaposema kwamba kazi yetu sasa Wizaraya uvuvi imekuwa ni kukamata nyavu na kuchoma.Tunaomba nyavu mlizoshika madukani hazitoshi mkakaguemagodauni, mkakague maduka na nyavu za milimita sita

Page 186: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

185

zinauzwa dukani, lakini zikiwa dukani siyo haramu, haramu tuzikishaingia kwenye maji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunawaomba sasamkakague godauni zote nyavu zinazotengenezwa nchini,nyavu zinazotoka nje ya nchi kwa sababu zinalipiwa na VATkwa sababu Serikali inapata fedha, ili mweze kuanzia haponafikiri wavuvi wakikosa hizo nyavu haramu hawatawezakuchukua nyavu haramu wakaingiza ndani ya maji. Isiweikiingia ndani ya maji haramu, ikiwa dukani ni halali na piakodi mnataka, ushuru mnachukua; hivi huyu mvuvi akimbiliewapi? Hana pa kukimbilia, tunawaomba sasa mkae chini,Wizara yako, Wizara ya TAMISEMI mwambizane, muwezekuwahurumia wavuvi hawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kusemakwamba kuna doria, hakuna doria inayofanywa kwenye ZiwaVictoria. Wavuvi wanavamiwa na majambazi, wanaibiwamashine zao, wavuvi wanakaa visiwani; siku moja naombaMheshimiwa Mathayo aje tumpeleke Bezi, tumpeleke visiwavya mbali ili akaone ni namna gani wavuvi wanapatamatatizo na siyo awe anakuja anaishia nchi kavu.

Sasa tunaomba aje tuvuke wote na mitumbwi akaonewavuvi wanavyopata shida, michango wanayochangishwalakini hakuna huduma yoyote inayoendelea ya kijamiikwenye maeneo hayo. Hata mwanamke akitaka kujifunguausiku inakuwa tatizo, mpaka avushwe kwa mtumbwiapalekwe nchi kavu. Tunaomba sasa asiishie nchi kavu. Ajeapande mitumbwi wanayopanda wavuvi kwa sababu ndiyowatu wake alionao kwenye Wizara yake ili aweze kuwasemeana aweze kuona matatizo waliyonayo, huenda na yeyeakapatwa na huruma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa naomba nichangiekidogo uvuvi wa bahari kuu. Uvuvi wa bahari kuu mwaka 2009ulipewa mamlaka ya uvuvi wa bahari kuu, lakini tangu 2009Mheshimiwa Waziri upewe Mamlaka hiyo mpaka leohujapewa kibali cha kuajiri wafanyakazi wa mamlaka hiyo.Wamekuwa na wafanyakazi wa kuazima tu katika Vitengo

Page 187: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

186

vya uvuvi. Kuna tatizo gani, mnashindwa kuipa hii mamlakamliyoiteua kibali cha kuajiri wafanyakazi ili waweze kufanyakazi zao kwa uhakika? Wamebakia na wafanyakazi watano,tena wafanyakazi wenyewe wa kuazima! Serikali ya Jamhuriya Muungano wanaazima na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.Wafanyakazi wenyewe ni watano, hivi wanafanya kazi gani?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningeomba MheshimiwaMathayo utakapokuja uniambie, ni kwa nini hutoi vibali vyahawa, ukawapa hii mamlaka ikaweza kuajiri wafanyakaziwakaweza kuendeleza uvuvi katika bahari kuu? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama hiyo haitoshi, katikabahari kuu kuna Sheria ambayo inasajili meli za kigeni. Baadaya kusajili inabidi itakapoingia kuvua lazima irudi kwenyebandari ili ikaguliwe imevuna kiasi gani. Iende aidha bandariya Zanzibar, iende bandari ya Dar es Salaam, Mtwara auTanga. Sheria hii ina vifungu vyake.

Kama meli i l iyopewa leseni haikufanya hivyo,inatakiwa mwenye meli huyo atozwe Shilingi bilioni moja amaafungwe miaka 20 kwa kukiuka Sheria hiyo. MheshimiwaWaziri katika hotuba yake ametuambia ndiyo wanaanza sasakuja kukaguliwa, ndiyo wanaanza. Hiyo miaka yotemliyokuwa mnasajili ukija hapa utuambie ni meli ngapizimepigwa faini ya Shilingi bilioni moja na ni wamiliki wa melingapi wamefungwa miaka isiyopongua 20, au mambo yotemawili kwa pamoja? Uje utuambie kwa sababu hiiinatukosesha Tanzania mapato, wavuvi hawa wanakuja,Sheria zipo Wizara mnashindwa kusimamia Sheria. Mtuambiemna njama gani za kushindwa kusimamia Sheria zilizotungwana sisi wenyewe? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika ukurasa wa 59Mheshimiwa Waziri amesema wanafanya doria. Wana ndegeinafanya doria kwa masaa 180. Lakini doria hii inayofanywakwa masaa 180 kwa utafiti wangu, saa moja ya ndege hiyowanalipa dola 2,000 kwa saa moja, tuzidishe mara 180 ili tujueni Shilingi ngapi Serikali inapata hasara. Siyo chini ya Shilingimilioni mia tano sabini na kitu, Serikali inaingia hasara, tena

Page 188: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

187

ukaguzi huo unafanyika usiku, wakati usiku meli hiyo hatakama itaonwa na hiyo ndege, siyo rahisi kuikamata.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunaiomba Serikaliitafute mbinu nyingine ya kuweza kukamata hawa wavuviharamu ni wengi ambao wanakuwa kwenye bahari kuu, lakinihawawezi kuvua bila kukaguliwa na bila kutozwa fine. Hii yoteinaendana na sisi wenyewe kuwa wazembe, kushindwakusimamia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nirudi kwenyemifugo kidogo. Mheshimiwa Waziri amekuja hapa akatutoleatakwimu za mifugo. Mimi naomba nimwulize MheshimiwaWaziri hivi, sensa ya mifugo Wizarani kwako mara ya mwishoumeifanya lini? Utakapokuja utuambie sensa ya mifugoWizarani kwako kwa mara ya mwisho imefanyika lini? Kwakumbukumbu zangu ni miaka 20 iliyopita. Sheria inasemasensa inatakiwa ifanywe kila baada ya miaka kumi ya mifugo,lakini wewe kila siku ukija unakuja na takwimu; takwimu hiziunazokuja nazo zisizokuwa na uhakika ndizo hizi zinashindwakujua tuna mifugo kiasi gani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii mifugo Mheshimiwa Waziriajue iko chini yake. Wavuvi wanaonewa, wavuviwananyanyaswa, wavuvi wanauliwa kwa haki zao. Yeyekama Waziri wa Mifugo anawatetea vipi wavuvi hawa?Anajua. Kuna Wakuu wa Wilaya wanachukua mamilioni kwawavuvi. Je, hujui? Kama unajua, umechukua hatua gani kwawafugaji hawa? Mimi mwenyewe nimeshuhudia mfugajiamekamatiwa ng’ombe 75, anapewa risiti ya ng’ombewatano. Ng’ombe wengine wote wanakwenda bure,Wenyeviti wa Vijiji, Wenyeviti wa Wilaya wanachukua fedha,wanawachukulia Wasukuma ng’ombe zao. Kwani Wasukumawana makosa gani hapa duniani? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba, mnasemawavune mifugo, mwatafutie njia ya kuvuna mifugo, siyoumwambie mtu tu vuna mfugo, hajui apeleke wapi. Ahsante.(Makofi)

Page 189: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

188

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Nakushukuru Mheshimiwa Mkiwa,kengele hiyo ni ya pili. Nakushukuru sana. Nilisema nitamwitaMheshimiwa Diana, naona hayupo. Basi naomba nimwiteMheshimiwa Opulukwa, halafu Mheshimiwa Pambaajiandae.

MHE. MESHACK J. OPULUKWA: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante kwa kunipa na mimi nafasi ili niwezekuchangia bajeti hii ya Wizara ya Mifugo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili nisisahau, kwanza siungimkono hoja. Nilikuwa naangalia kitabu cha bajeti Volume IVkwenye ile vote namba 99, wakati naangalia hiki kitabunikadhani kwamba nilikuwa nasoma matokeo ya kidato channe ya mwaka 2012 kabla ya kufanyiwa marekebisho, kwasababu nilikuwa naona zero ni nyingi sana. Nikaangalia vote,subvote 4486 zero kila mahali sifuri, sifuri nikafananisha hizi nadivision four ambazo zilifanyiwa marekebisho juzi na leo hiimatokeo yameweza kupanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama bajeti hiihaitaongezwa na kama zile fedha ambazo Kamati imeombakwamba ziongezwe kwenye Wizara hii ili angalau kazi ziende;kama hazitakwenda sitaunga mkono kabisa hoja hii. Lakinisiyo kuunga mkono tu hoja hii, lakini hata kama fedhazitaongezwa ili niweze kuunga mkono, lazima sasa niwezekuona maeneo ambayo yamesahaulika kwenye Jimbo laMeatu, Jimbo ninalotoka mimi hakuna majosho, hakunamabwawa, ukienda kule Ng’wangundo, Bukundi, Mwabuzo,Mwamalole, Mwamanimba, Nkoma, hawa watu wanahitajimaji kwa ajili ya mifugo yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa naunga mkono hoja hiinamna gani wakati ambapo kwenye Jimbo langu na kwenyeWilaya yangu hawa watu bado hawajasikilizwa?

Page 190: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

189

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nashangaa sanaSerikali ya Chama cha Mapinduzi kwa sababu ndiyo Serikalii l iyopo madarakani. Sera ya Chama cha Mapinduziwanasema ni kupunguza mifugo kwa sababu mifugoinaharibu mazingira.

Sisi kwetu wafugaji na hasa ukienda Meatu naukienda Simiyu, ukienda Shinyanga, ng’ombe ndiyo benkiyetu. Ni sawa na Mbunge mwingine au mtu mwingine yeyoteanachukua fedha zake anapeleka benki kwa ajili ya kwendakujihifadhi pale. Sisi benki yetu ni ng’ombe. Unapokuwa nang’ombe utauza ng’ombe utapeleka mtoto shule atasoma;unapokuwa na ng’ombe utauza utapata fedha utajenganyumba ya bati; unapouza ng’ombe utapata pesautapeleka mtoto hospitali atatibiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo tunaambiwa punguzang’ombe. Mimi naomba hii sera ya Serikali kwa kweli badalaya kupunguza ng’ombe, iwe ni kuongeza ng’ombe na walasiyo kupunguza ng’ombe. Wakati nasoma kitabu cha hotubaya Mheshimwia Waziri kuna sehemu inasema Sekta ya Mifugo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kunukuu kidogo.Inasema: “Sekta ya Mifugo ni moja kati ya sekta zilizopewaumuhimu katika kutekeleza mkakati wa kukuza uchumi nakupunguza umaskini”. Inasema, mifugo inatoa ajira. Kamatunapunguza mifugo, ajira itapatikana wapi? Watotowatakwenda kuchunga ng’ombe wapi? Hii ni ajira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi kama nina mifugoyangu itachungwa na nani kwa sababu tunaamini kwambaajira siyo ajira ya kukaa darasani, siyo white collar job pekeyake! Ajira ziko nyingi, lakini tunawaambia leo watuwapunguze mifugo, wapunguze ng’ombe waendelee kuwamasikini, waendelee kutawaliwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nasema ili tuwezekuwatendea haki Watanzania wengi ambao ni wafugaji,wanaotoka maeneo ya wafugaji, ni lazima bajeti hii iwezekuongezwa kama ambavyo Kamati imependekeza lakini pia

Page 191: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

190

lazima Meatu ikumbukwe kwenye mambo ambayo hayakokatika kitabu cha bajeti cha Mheshimiwa Waziri ili angalautuweze kwenda sambamba pamoja na Wabunge wengine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningependa kuongeleakwamba katika kitabu cha bajeti hii kwenye ule ukurasa wa85 Mheshimiwa Waziri ame-indicate kwamba Meatuimetengewa hekta 11,000 kwa ajili ya wafugaji peke yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi natoka Meatu nanahudhuria pia vikao vya Baraza la Madiwani, hizi hekta11,000 hazipo! Kama zipo, ziko wapi? Kama zipo labda zipoheka mbili au tatu, ndiyo maana wafugaji wa Meatu,wafugaji wa Simiyu, wafugaji wa Bariadi wanahama kila sikuwako Sumbawanga, wako Mbeya, wako Rufiji, wakoMorogoro kwa sababu hakuna maeneo ya kulisha mifugoyao. Nilikuwa naomba sasa ili angalau wananchi hawa, iliangalau haya maeneo anayosema hekta 11,000 kwambazipo, Mheshimiwa Waziri baada ya Bunge hili kuisha uendeMeatu ukajiridhishe na hizi hekta 11,000 zinazoelezwa.Nadhani Watendaji wako ndio wamekuandikia hotuba hii,lakini wewe bila kufuatilia wala kuangalia, ukaitoa kamailivyo. Hakuna hekta 11,000 kwa Meatu na ndiyo maanawananchi wanateseka sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mara nyingi huwa sipendikupigiwa kengele. Napenda kusema neno la mwisho.Watanzania wengi, wananchi wengi na karibia dunia nzimawanapenda nyama na hasa nyama ya ng’ombe na nyamaya mbuzi. Ukienda kwenye ma-deep frezers ya watumbalimbali na Mawaziri wetu akiwemo na wewe labdaMheshimiwa Mwenyekiti ukiwemo utakuta friji imejaa nyama,lakini cha ajabu hawa mifugo, hawa ng’ombe hii nyamandiyo inapigiwa vita kila siku watu wapunguze ng’ombe.Nilikuwa naomba, hebu tuwajali watu hawa, wametesekakwa muda mrefu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naungana mkono naWaheshimiwa Wabunge wote ambao wamesema hawaungimkono hoja hii. Ahsante sana kwa kunipa nafasi. (Makofi)

Page 192: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

191

MWENYEKITI: Nakushukuru sana MheshimiwaOpulukwa kwa mchango wako.

Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea. Nilisemanitamwita Mheshimiwa Saleh A. Pamba, atafuatiwa naMheshimiwa Amina Makilagi, na kama muda utatosha,namwona Mheshimiwa Diana Chilolo amerejea, nadhanialikuwa na udhuru. Basi tutaona.

MHE. SALEH A. PAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii ambayosikuitegemea. Awali ya yote, naomba kuunga mkono hoja.Naunga mkono hoja kwa sababu Wabunge wotewaliozungumza kuanzia asubuhi, wamezungumzia juu yasuala la bajeti ndogo ya Wizara hii. Serikali yetu ni sikivu, Serikaliya Chama cha Mapinduzi ni sikivu, inasikia kilio cha wananchiwake, inasikia kilio cha wafugaji, inasikia kilio cha wavuvi. Ninauhakika kabisa kwamba Serikali yetu sikivu itaongeza bajetihii ili Mheshimiwa Waziri aweze kufanya kazi yeke vizuri.Ninaamini kabisa bila wasiwasi wowote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitaanza pale ambapoamemalizia Mheshimiwa Kitandula. Mheshimiwa Kitandulaalizungumzia juu ya masuala na takwimu na Taarifa ya UvuviDuniani iliyotolewa na FAO mwaka 2012. Alizungumzia juu yatakwimu zile ambazo sitaki kuzirudia, lakini natakanizungumzie kitu kimoja kikubwa kabisa ambachoamekizungumzia, nalo ni suala la ufugaji wa samaki. (Makofi)

Ufugaji wa Samaki katika takwimu alizozungumziaunachangia takribani nusu ya samaki wote wanaouzwaduniani. Ufugaji huu unachangia fedha karibu dola bilioni 119.Sasa nataka kuiangalia nchi yetu tuko wapi, hasa katikaufugaji wa samaki? Hasa nataka kuangalia nchi za Kiafrika,ili niweze kuleta msisitizo kwa Wizara hii kwamba suala laufugaji wa samaki ni muhimu sana na lazima lifanyiwe kazina lazima liwe katika mipango. (Makofi)

Katika nchi kumi zinazofuga samaki, au zinazoongozakwa ufugaji Afrika, ya kwanza ni Misri, inazalisha tani 900,000;

Page 193: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

192

ya pili, Nigeria, inazalisha tani 200,535; ya tatu, Uganda, tani12,000; Zambia, tani 10,000, Ghana, tani 10,000; Madgascar,tani 6,000; Tunisia tani elfu 5,000; Malawi, tani 3,000; nyinginezote za Kiafrika ni tani 21,000 pamoja na Tanzania. Maanayake nini? Maana yake ni kwamba, Tanzania nchi iliyo namaziwa makuu matatu; Victoria, Nyasa na Tanganyika; Mito,Maziwa madogo madogo, hatujafanya jitiada za kutoshakatika sekta hii. Naoimba Wizara katika mipango yake,ihakikishe kwamba, suala la ufugaji wa samaki, ambalo nisuala muhimu linalo-contribute takribani asilimia 50 ya samakizote duniani, wanatokana na ufugaji. Suala hili lazima walitiliemkazo katika mipango yao yote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda nizungumzieharaka haraka katika eneo la uvuvi wa bahari kuu.Tumeanzisha Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari kuu mwaka 2009.Mamlaka hii inafanya kazi kwa matatizo kama Wabungewengi walivyo zungumzia. Haina meli ya doria. Nadhani bajetihiyo itakayoongezwa, naiomba Wizara, kwamba kitu chakwanza cha kufanya ni lazima wanunue meli ya doria, ilikusudi waweze kupambana na majangili walioko katikabahari kuu. Kwa sababu tunapoteza fedha nyingi sana, dola1,900,000 zinazotolewa na leseni tu, hazitoshi hata kidogo!Tunapoteza takribani dola zaidi ya bilioni 100, kutokana nasamaki wetu wanaovuliwa katika bahari kuu, ambaotunashindwa kukamata Meli hizi, na tunashindwa kupataroyalty katika meli hizi.

Kwa hiyo, bajeti hiyo itakayoongezwa, naamini kabisaSerikali itaongeza bajeti hii. Fedha hizo suala la kwanzaambalo Wizara hii lazima ifanye, ni lazima inunue meli kubwaya kupambana na majagili baharini, ili kusudi tuweze kupatafedha katika nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niende harakaharaka kwenye suala la wavuvi wadogo wadogo. Katikamikakati ya Wizara, na nimesoma bajeti ya MheshimiwaWaziri, sijaona mkakati hasa wa kuwasaidia wavuvi wadogowadogo. Badala yake, Wavuvi wadogo wadogo katika nchiyetu, maeneo mbalimbali, pamoja na wavuvi wa Pangani,

Page 194: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

193

hawapati misaada ya kutosha kutoka Serikalini. Wenzetu waWizara wanachofanya ni doria, kukamata nyavu nakadhalika. Kama mvuvi mdogo mdogo hujampa nyavu yakisasa, unafikiri afanye nini? Sasa nataka nitoe pendekezokwamba, ili tuweze kufaidika na wavuvi wadogo wadogo,na ili tuweze kuwasaidia, tufanye kama walivyofanya katikaWizara ya Kilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara ya Kilimo wana kituwanakiita Mfuko wa Pembejeo, Agricultural Inputs Fund. Ulemfuko wavuvi wanakwenda kukopa, wanapata mikoponafuu, wanalipa kwa muda mrefu, ili kusudi waweze kupatavifaa vya kisasa. Haisaidii kuchoma nyavu za wavuvi wadogowadogo, huko ni kuwaonea kama hukuwapa uwezo wakuweza kupata zana na boti za kisasa na kadhalika. (Makofi)

Kwa hiyo, naomba Mheshimiwa Waziri kwamba hiliuliweke katika mipango yako, na fedha utakazopata zanyongeza, uanzishe mara moja Mfuko wa Wavuvi WadogoWadogo ili waweze kupata fedha hizi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho ambalo natakakuzungumzia, Mheshimiwa Waziri mwaka 2012 ulituahidikwamba utatusaidia katika Wilaya ya Pangani kwambautatupatia Kituo cha Mitamba, Kituo cha ng’ombe bora. Hilohalijafanyika. Kwa hiyo, nakuomba Mheshimiwa Waziri,wananchi wa Pangani sasa hivi ni wafugaji wazuri, wanafugakisasa, wanapata kila mwezi karibu Shilingi milioni 150zinazoingia mfukoni kwa wafugaji wadogo wadogo, lakinitunahitaji kituo hiki ili kusudi tuweze kupata mitamba ambayoitatusaidia kupata ng’ombe bora na kuongeza uzalishaji wamaziwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho kabisa ni suala lakutunza mazingira. Uvuvi haramu unaendelea, uvuvi haramukatika mito, uvuvi haramu katika maziwa; lazima Wizaraitenge fedha za kutosha za kuhakikisha kwamba,wanapambana na waharibifu wa mazingira. Kwa sababusamaki hawa, ni renewable resource. Kama tukiwatunza vizuri,tutaendelea kupata samaki wengi zaidi. Kwa hiyo, suala la

Page 195: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

194

kutunza mazingira ni eneo mojawapo ambalo nafikiri nimuhimu sana ili kusudi uvuvi wetu wa baharini, katika maziwa,katika mito, na maeneo yote mengine, unakuwa endelevu.

Naomba Mheshimiwa Waziri kwa kumalizia, nisemekwamba, ninaamini kabisa kwamba Wizara hii ina mipangomizuri, mimi mwenyewe nimeiona mipango hiyo katikafisheries masterplan ambayo wameitengeneza, nimeonamipango hiyo mizuri katika livestock development program,haya yote ya majosho, kupanga maeneo mbalimbali yawafugaji na wakulima na kadhalika yote yanawezekana.Naomba Wabunge wenzangu, tuisaidie Wizara, waweze kwakuanzia angalau hiyo Shilingi bilioni 40 ambayo wameiomba,waweze kuendelea na mpango wao huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja asilimiamia kwa mia. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Amina Makilagi!

MHE. AMINA N. MAKILAGI: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana kwa kunipa nafasi ili niweze kutoa mchangowangu katika sekta hii muhimu sana kwa maendeleo ya Taifaletu na Sekta ya Uvuvi na Mifugo, Sekta ambayo kamatutaijengea miundombinu mizuri ya kutosha, inawezakuchangia pato la Taifa na tukaondokana na tatizo la kuwaombaomba; Tukaondokana na tatizo la kutegemeawafanyabiashara wachache ndiyo walipe kodi na tuendeshenchi yetu ya Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kwanza niungemkono bajeti hii asilimia mia moja, kwa sababu mimi ni mdauya Kamati hii ya Mifugo na Uvuvi na naomba niunge mkonokabisa moja kwa moja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mara baada ya kuungamkono, naomba sasa na mimi niungane na wenzangu wotewaliosema kwamba bajeti ya Wizara hii kwa kweli ni ndogo.Ni ndogo ukilinganisha na mahitaji ya Wizara hii, ukilinganishaumuhimu wa sekta hii na ukilinganisha hata na ukubwa wa

Page 196: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

195

Wizara yenyewe. Mimi kusema ukweli, nimefuatilia michangoya Waheshimiwa Wabunge wengi. Nilivyokuwa naitazama,wengi wanafikiri pengine Mheshimiwa Waziri, watendajiwake, siyo wa kiwango cha kuridhisha, pengine Katibu Mkuuna Watendaji wenzake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi mwenzenu nipokwenye Kamati. Naomba niwaombe WaheshimiwaWabunge tuwapongeze hawa Watendaji wetu; MheshimwiaWaziri, Katibu Mkuu na Watendaji wake wote kwa kufanyakazi katika mazingira magumu. Nafikiri ni ukweli usiopingikakwamba wote tumeiangalia bajeti hii. Hivi wangefanya nini,asilimia 56 ya fedha walizozipata katika fedha zilizoidhinishwana Bunge lako Tukufu. Hivi wangefanya nini katika fedha zamaendeleo? Kiasi walichopata ni asilimi 36 tu! (Makofi)

Kusema ukweli, hata kama wangekuwa na miujizaya namna gani, wasingeweza ku-perform vizuri. Mimi nilikuwanaomba niwashawishi Wabunge wenzangu, tuwapongezehawa Watendaji wetu na Viongozi wetu kwa kazi kubwa nangumu wanayoifanya katika mazingira magumu sana, kwakweli ya kupigiwa mfano. Wangekuwa kama sio watu makini,ingekuwa Wizara imeshaanguka kabisa kutokana na halininavyoiona hapa. Kwa sababu wako makini,wanachokipata wanakitumia; tena nataka niwaambie hawaWatendaji wa Sekta ya Mifugo na Uvuvi ni Watendaji ambaowana wito.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nimekuwa nakutananao, huwa nawaona jinsi ambavyo wana uchungu;unawaona jinsi ambavyo wanataka kushuka huku vijijiniwakafanye kazi; unaona jinsi ambavyo wana hamu yakwenda kujenga malambo kwa ajili ya wafugaji; lakini ukijakwenye bajeti, hawapati kitu. Kwa kweli wanashindwakusonga mbele.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba WaheshimiwaWabunge wenzangu, hebu tuwatie moyo hawa Watendajiwetu, tuwasaidie kama ambavyo mmesema hapa. Serikalisasa isikie kilio cha Watendaji, isikie kilio ha Kamati, ichukue

Page 197: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

196

maoni yote ya Kamati kama ambavyo tumeyaleta hapa,tupewe Shil ingi bil ioni 40 na nawaomba wenzanguwaliochangia hapa, hata ikiwezekana zaidi kamawalivyoziomba zote, ili sasa wakirudi waweze kutenda kwamanufaa ya Taifa letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nizungumzie sasamigogoro ya wakulima na wafugaji. Jambo hili la migogoroya wakulima na wafugaji kwa kweli limekuwa ni jambo sugu,jambo ambalo kila tunapokutana hapa, linajirudia, lakini kwakweli hatujaona hatua za makusudi za hizi Wizara mtambuka.Kamati ya Mifugo tumejieleza vizuri, kwamba jambo hili lakupima ardhi kwa ajili ya wafugaji; jambo la kupima ardhikwa ajili ya wakulima, huwezi ukaachia Sekta ya Mifugo pekeyake. TAMISEMI wako wapi? (Makofi)

Maana ukisema pia TAMISEMI unaachia Halmashauripeke yake, kuna Halmashauri nyingine hapa nchini, hali yauchumi wao ni mdogo. Kuna migogoro pale niliwahi kusemaBunge lilopita, kwamba pale Rufiji na maeneo mengine,huwezi ukasema Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji, kwa mapatoyake peke yake au Kisarawe au maeneo mengine wao ndiyowatenge maeneo ya wakulima, watengeneze bajeti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilizungumza kwenye Bungelilopita na hapa ninarudia; na kwenye Sekta ya Ardhinimesema na hapa tena narudia kwa mara nyingine. HebuSerikali itafute fedha popote, ipeleke kwenye Halmashaurizetu, kwa ajili ya kutenga maeneo ya wakulima na wafugajiili kuondoa hii migogoro inayotokea mara kwa mara na kuletamaafa katika nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hotuba yaMheshimiwa Waziri na katika Kamati yetu hapa tumetoaushauri, huoni kabisa mkakati wa kupunguza hii migogoro.Wafugaji wa Mwanza, wafugaji wa Geita, Wafugaji waShinyanga, na hata Mara na wote hawa niliowataja,utawaambiaje akae pale, hakuna lambo? Atakaa palenamna gani, hakuna majosho? Hakuna madawa!Wanahamahama kwa sababu ya haya matatizo yaliyopo.

Page 198: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

197

Tunaiomba Serikali kusema ukweli i j itahidi kadriinavyowezekana, kama ambavyo Kamati ya Kilimo na Uvuviimeshauri, Serikali itafute fedha kwa ajili ya kujengamiundombinu ya mifugo, ili wafugaji waendelee kukaa katikamaeneo waliyopo, waachane na hii tabia ya kuhamahama.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkoa wa Mara ni miongonimwa Mikoa ya wafugaji, ambao sio wa kuhamahama. Lakiniwale wa Mkoa wa Mara wanafanya uvumilivu kwa sababuwakati mwingine wanawakimbiza mtoni, wakati mwinginekuna vijilambo. Kadri hali ninavyoiona na wenyewe wataanzakuhamahama. Sasa hivi mnazungumzia Wasukumawanahama, wanatembea, sasa wanakuja na Wakurya,wanakuja na Wajaluo, tutakwenda wapi? Wajita naowanakuja sasa, maana hata kule mifugo imeshakuwa mingi,hawana elimu ya kufuga mifugo ya kisasa, hawana malambona majasho, na wao wanataka kuhama kwa ajili ya kwendamaeneo mengine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa naomba sana,hebu tupeleke hii elimu ya ufugaji. Tujitahidi sasa kupelekaelimu hii ya ufugaji kwa Tanzania nzima na Serikali itafutefedha za kutosha kwenda kutoa elimu kwa wakulima nawafugaji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, natoa mfano, Mkoa waPwani, Mtwara, Tanga na hata kule Katavi na Rukwawalikohamia wafugaji, wale utamaduni wao haukuwa wakufuga. Leo mmekwenda kuwachanganya na wafugaji,hakuna elimu yoyote, matokeo yake sasa Wazaramo naWakwere wanaona kama siyo wenzao na migogoro ndiyoinapoanzia. Hivi hii elimu nil iyoidai mwaka 2012,mmeshapeleka wapi? Je, kuna mkakati gani? Nilikuwanaiomba Serikali itutafute fedha kwa ajili ya kwendakuelimisha watu wetu, ili migogoro hii iweze kupungua.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niendelee kusemakwamba, Sekta ya Mifugo na Uvuvi kwa kweli ni sekta muhimu

Page 199: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

198

sana. Kama tutawekeza kama wenzetu wa Kenya hapa jiraniwalivyofanya; wenzetu Wakenya, wamejielekeza katika sualazima la kuchimba malambo, wakawapatia vijana, hawawaliotoka Vyuo Vikuu wako mbali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa naongea na mtummoja mvuvi hapo Kibaha, ananiambia mama, mimi katikamiezi sita, nina uhakika wa kupata Shilingi milioni 60, bwawadogo kabisa, nilishangaa. Akanihamasisha! Hivi kamatungetenga fedha kwa ajili ya kuchimba mabwawatukawasaidia kuwapa vijana wetu, vikundi vya akina mamana vijana, wakaendelea kufuga samaki za kutosha, soko lipo.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa kwa kweli tutapataajira, pato la Taifa litaongezeka na hawa wanawake navijana wataondoka katika suala zima la umasikini. Nilikuwanaiomba Serikali kwa kweli ijielekeze kutafuta fedha kwa ajiliya kujenga haya malambo, ili kuwapataia vijana nawanawake ili kuimarisha uchumi wao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nizungumzie sualazima la uimalishaji wa Sekta ya Viwanda ya kusindika mazaoya mifugo na uvuvi. Mimi kwanza nilipenda Mheshimiwa Waziriatakapokuwa akifanya majumuisho, atupe tena maelezokwa pamoja kama ulivyotueleza kwenye Kamati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi huu mkakati wa kufufuaviwanda vya maziwa uko wapi? Umepotelea wapi? Kiwandakiko kule Musoma, tunashukuru kwa jitihada zinazoendeleajuzi nimeona kwenye Kamati na hapa taarifa inaonyesha.Vile vichache vichache havitoshi! Nilikuwa naiomba Serikaliitafute fedha nyingi kabisa kwenye mabenki, iwakopeshewazalendo wa Tanzania, walio tayari kujenga viwanda katikanchi yetu, kwa ajili ya kusindika mazao ya samaki, mazao yamifugo ili kuleta tija kwa Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi tunaona shida gani,kuchukua benki ya CRDB, tukatenga hata Shilingi bilioni mbili,tukawatafuta Wazalendo hata watatu, tukawakabidhi, hebu

Page 200: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

199

kajenge kiwanda kule Mara, hebu kajenge kiwanda kuleSingida kwa ajili ya kusindika mazao ya mifugo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nafikiri tukifanya hivyo,na wenzetu ndivyo walivyofanya. Tusikae kutegemea hawawafanyabiashara. Kila mtu ajihamasishe, suala la kujengaviwanda linahitaji fedha, linahitaji ujasiri, ni lazima Serikaliiwawezeshe ili kuleta tija kwa Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nizungumzie sualala wafanyakazi wetu katika sekta hii muhimu sana. Kamamlivyoona kwenye taarifa na hata kama Kamati ambavyotumesema hapa, katika Wagani nchi nzima ni zaidi ya 17,000na tulionao ni 5,000 tu. Lakini tunapombana MheshimiwaWaziri kwenye Kamati mara atuambie TAMISEMI, maraatuambie Utumishi, hana Mamlaka yoyote. Anasemaameshapeleka barua huko, hajapata majibu. Mimi natakawakati mnafanya majumuisho, kama ni TAMISEMI watuambie,upo mkakati gani wa kuajiri wagani?

Kama ni suala la Utumishi, watuambie. Katika huumpango mzuri alikokuja nao Waziri wa TAMISEMI na Waziriwa Utumishi, watueleze, katika ajira zitakazotengenezwamwaka huu, Wagani wangapi ni wa Mifugo, na Waganiwangapi ni wa uvuvi? Kwa sababu, bila hawa wataalamitakuwa sawa sawa na kutwanga maji kwenye kinu. Nilikuwanaiomba sana Serikali hebu ijielekeze kutafuta fedha kwa ajiliya kuajiri Wagani wa kutosha na hili jambo libaki kuwa historia.Haiwezekani kila wakati tunapokuja tatizo ni la Wagani, tatizoni la Wagani linajirudia mara kwa mara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nizungumziesuala la Uimarishaji wa sekta ya ….

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa Mzungumzaji)

MHE. AMINA N. MAKILAGI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nadhani ni kengele ya kwanza hiyo.

Page 201: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

200

MWENYEKITI: Ni kengele ya pili Mheshimiwa.

MHE. AMINA N. MAKILAGI: Mheshimiwa Mwenyekiti,Naunga mkono hoja, ahsante sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Nakushukuru sana Mheshimiwa AminaMakilagi kwa kukubushwa na kukumbuka muda umepita.Mheshimiwa Diana kwa dakika tatu nne.

MHE. DIANA M. CHILOLO: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii nami niweze kutoamchango wangu.

Kabla sijatoa mawazo yangu, napenda niungane naWaheshimiwa Wabunge wenzangu wote waliotanguliakwamba, bajeti ya Wizara ya Uvuvi na Mifugo ni ndogo.Jamani naiomba Serikali iwe inaangalia maeneo ambayoyanagusa Watanzania walio wengi moja kwa moja. Hatunaujanja na wafugaji, hatuna ujanja na wavuvi, hatuna ujanjana wakulima, lazima tuangalie maeneo haya. Tutaendeleakugombana na Watanzania mpaka lini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi naomba, nilimwonaNaibu Waziri alikuja kunong’ona na Waziri pale, ninaaminikuna kapu la hela labda amepeleka. Mimi nashangaMheshimiwa Rose Kamili ulikuwa unagomba bure, pale kunahela imekwenda. Naomba kesho Mheshimiwa Waziriatuambie ameongezewa Shilingi ngapi, ili wavuvi, wafugajiwafurahi, na waweze kufanya kazi vizuri kwa sababuwatakuwa na uwezesho?

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niongeleeKiwanda changu cha Singida cha kusindika maziwa. Tunakiwanda kidogo cha kusindika maziwa Singida katika Kijiji chaMsepuka Wilaya ya Ikungi. Mheshimiwa Waziri, ndani ya bajetihii, tembelea kiwanda hiki kidogo. Kiwanda hakinamiundombinu, hakina wataalam, kina mazingira magumu nakinahitaji uwezesho. Nakuomba utembelee Singida na mimiunichukue nikusindikize uende uone hali halisi ya kiwanda hiki.(Makofi)

Page 202: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

201

Mheshimiwa Mwenyekiti, siyo kiwanda hicho tu, paleMsunguwa, Tarafa ya Isepuka, tuna kiwanda cha kuwambangozi. Kiwanda hicho nacho hivyo hivyo ni duni kabisa, hakinawataalam, hakina miundombinu, yaani kinahitaji uwezesho.Tena vinakaa eneo moja kama Bunge hili hapa. Ninakuombauondoke uende uvione hivi viwanda, tunatakiwa kuvinusuru,kwa sababu tayari Halmashauri na Wilaya ilishawekeza pale,na Mkoa umetazama pale, ninaomba na Serikali itazamepale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niongelee suala lakuku. Jamani Tanzania nzima tunalisha kuku watu wana-Singida. Kuku wanapitishwa hapa wamening’inizwa bilahuruma. Kwa nini tunawatesa namna hiyo? Tuangaliemazingira ya kuwabeba kuku, na ikiwezekana kuku hawa,tutengeneze kiwanda cha kusindika nyama za kuku Singida.Tuache tabia ya kuwatesa hawa ndege wadogo, nao piawanahitaji kulindwa. Tutengeneze kiwanda Singida, tusindikenyama za kuku, tusindike nyama nchi nzima, tusambaze nchinzima, watu wale kuku, kuku wa asili ambao hawana maradhiwala tatizo lolote la kumdhuru binadamu, siyo sawa na kukuwa kisasa ambao wanatumia madawa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakuomba sana,Mheshimiwa Waziri asikie ombi langu la wana-Singida kuhusukuku. Tunahitaji kiwanda cha kuku Singida. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niungane na wenzangukuhusu ugonvi wa wafugaji na wakulima, sasa upate muafakana uishe. Wafungaji wategewe maeneo ya kufugia, iliwaache kuchungia kwenye mashamba; wanadumazamashamba. Mashamba yanaharibika kwa sababu yang’ombe kupita humo kila siku. Kunakuwa na ugumu wakulima kwa sababu ya mifugo kukanyaga humo kila siku.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Singida tuna Ziwa Kitangiri,tuna Maziwa mawili pale mjini; Ziwa Singida na Ziwa Kindai.Maziwa haya hayana samaki. Hivi jamani, si kuna kupandikizasamaki! Nakuomba Mheshimiwa Waziri na wataalam wako,

Page 203: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

202

wakague haya maziwa; Kitangiri, na Ziwa la Singida pale mjini,na Ziwa Kindai tupandikiziwe samaki ili vijana waweze kujiajirikatika maziwa haya, na wana-Singida waweze kupatakitoweo cha samaki, tuweze kuwapa na majirani zetu waMikoa inayotuzunguka kama Tabora, Manyara, Shinyangana kwingine. Tunaweza tukalisha! Jamani, Tanzania hakunaumaskini. Mungu alitupendelea tukapewa kila aina yarasilimali, ni sisi wenyewe ndio tunashindwa. (Makofi)

Mheshimiwa Waziri tunaomba, wewe ni kijanamchapakazi, una Naibu Waziri mchapakazi, hebu pitia hayamaziwa, fanya utafiti, weka Samaki pale, tayari vijanawatakupenda, kwa sababu watajiajiri. (Makofi)

Mheshimwia Mwenyekiti, niongelee kuhusu machinjioya kisasa. Katika Mikoa ambayo inafuga ng’ombe kwa wingiau mifugo kwa wingi ni pamoja na Singida, Singida ni Mkoawa nne. Naomba sana jamani, tutengenezewe machinjio yakisasa ili na sisi tuweze kula nyama ambazo zimekaa katikamazingira safi kuliko kuchinja ovyo ovyo, holela namna hii.Kama wenzetu hapa Dodoma wana machinjio ya kisasa,Singida kuna tatizo gani? Tunaomba tupewe machinjio yakisasa. (Makofi)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, kablasijaahirisha shughuli hizi, nimepokea tangazo la kuwepo kwamechi ya Timu ya Bunge kesho. Sasa nimepokea tangazokutoka kwa Mwenyekiti wa Bunge Sports Club, MheshimiwaIddi M. Azzan, anaomba niwakumbushe WaheshimiwaWabunge wote, wakiwemo wachezaji na washabiki wotewa timu zetu za Bunge, kwamba, kesho timu zote mbilizitakuwa na mchezo na NSSF wakifanya zoezi la kujiandaana mechi zao.

Sasa wameniambia hapa, timu ya football ya Bunge,itaongozwa na mshambuliaji wao mahiri, Mheshimiwa Capt.John Komba, ataongoza timu ya football. Ameniambia hapakwamba timu ya netball itaongozwa na goal keeper waomahiri, ambaye ni Mheshimiwa Maria Hewa. (Kicheko/Makofi)

Page 204: 31 MEI, 2013 MREMA 1.pmd

31 MEI, 2013

203

Kwa hiyo, Waheshimiwa Wabunge, nami naunganamkono kabisa na Mheshimiwa Azzan kama hawa ndiowataongoza timu zetu kesho, na kama Prof. Maji Marefuamefanya mambo yake, basi nadhani mambo yatakuwamazuri sana kesho. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, baada ya tangazo hilo, sasanaahirisha shughuli za Bunge mpaka kesho siku ya Jumamosisaa 3.00 asubuhi ndani ya Ukumbi huu wa Bunge.

(Saa 1.45 usiku Bunge liliahirishwa hadi siku ya Jumamosi,Tarehe 1 Juni, 2013 Saa Tatu Asubuhi)