12
ISSN 0856 - 3861 Na. 1052 SAFAR 1434, IJUMAA JANUARI 4 - 10, 2013 BEI TShs 500/=, Kshs 50/= Sauti ya Waislamu www.annuurpapers.co.tz Ujasiria mali washika kasi Baraza Kuu Uk. 12 Kesi ya Sheikh Ponda mashahidi waingia ‘mitini’ Hakimu aamuru mmoja akamatwe Wengine watoa visingizio, majina yao yafichwa Wakili wa utetezi amlima barua DPP MAASKOFU wametakiwa kutambua kwamba Nyerere alikuwa kiongozi wa dini au siasa? Ndiye muasisi wa Mfumokristo nchini Na Bakari Mwakangwale kile kinachoelezwa na Waislamu kuhusu hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, si upotoshaji bali ni uhalisia na kwamba, yale wanayodai kuwa ni upotoshaji yamo katika vitabu mbalimbali na mwenyewe (Nyerere) hakuwahi kukanusha Inaendelea Uk. 4 HAYATI Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, amesema iwapo Tume ya Uchaguzi itafanya kazi kwa kujiamini na kuacha kufuata matakwa ya wanasiasa, itajenga imani kwa wananchi juu ya uwezekano wa kuwepo kwa chaguzi huru na za haki na kukidhi matakwa ya wananchi. Maalim Seif ametoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita nyumbani kwake Mbweni Zanzibar, wakati akizungumza na wajumbe wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar-ZEC, waliofika kwa ajili ya kumkabidhi ripoti ya utendaji wa Tume hiyo kwa kipindi cha miaka mitano, pamoja na kumuaga baada ya kumaliza muda wao wa utumishi ndani ya Wajumbe ZEC acheni kufuata matakwa ya wanasiasa Wanaomaliza muda wao wamuaga Maalim Seif Akerwa kutohakikiwa daftari la wapiga kura Na Mwandishi Wetu, Zanzibar Inaendelea Uk. 2 SHEIKH Ponda Issa Ponda akiwa katika Mahakama ya Kisutu Jumatau wiki hii. (Picha na Bakari Mwakangwale

Gazeti la Alnuur

Embed Size (px)

DESCRIPTION

Gazeti la kila wiki

Citation preview

Page 1: Gazeti la Alnuur

ISSN 0856 - 3861 Na. 1052 SAFAR 1434, IJUMAA JANUARI 4 - 10, 2013 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

Sauti ya Waislamuwww.annuurpapers.co.tz

Ujasiria mali washika kasi

Baraza KuuUk. 12

Kesi ya Sheikh Ponda mashahidi waingia ‘mitini’ Hakimu aamuru mmoja akamatweWengine watoa visingizio, majina yao yafichwaWakili wa utetezi amlima barua DPP

MAASKOFU wametakiwa k u t a m b u a k w a m b a

Nyerere alikuwa kiongozi wa dini au siasa?Ndiye muasisi wa Mfumokristo nchini

Na Bakari Mwakangwale kile kinachoelezwa na W a i s l a m u k u h u s u hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,

si upotoshaji bali ni uhalisia na kwamba, yale wanayodai kuwa ni upotoshaji yamo katika

vitabu mbalimbali na mwenyewe (Nyerere) hakuwahi kukanusha

Inaendelea Uk. 4HAYATI Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, amesema iwapo Tume ya Uchaguzi itafanya kazi kwa kujiamini na kuacha kufuata matakwa ya wanasiasa, itajenga imani kwa wananchi juu ya uwezekano wa kuwepo kwa chaguzi huru na za haki na kukidhi matakwa ya wananchi.

Maalim Seif ametoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita nyumbani kwake Mbweni Zanzibar, wakati akizungumza na wajumbe wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar-ZEC, waliofika kwa ajili ya kumkabidhi ripoti ya utendaji wa Tume hiyo kwa kipindi cha miaka mitano, pamoja na kumuaga baada ya kumaliza muda wao wa utumishi ndani ya

Wajumbe ZEC acheni kufuata matakwa ya wanasiasa Wanaomaliza muda wao wamuaga Maalim Seif Akerwa kutohakikiwa daftari la wapiga kura

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

Inaendelea Uk. 2SHEIKH Ponda Issa Ponda akiwa katika Mahakama ya Kisutu Jumatau wiki hii. (Picha na Bakari Mwakangwale

Page 2: Gazeti la Alnuur

2 AN-NUURSAFAR 1434, IJUMAA JANUARI 4 - 10, 2013

AN-NUUR S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786

Cel: 0784 370 208, 0755 260 087 , DSM. www.annuurpapers.co.tz E-mail: [email protected]

Ofisi zetu zipo: Manzese Tip TopUsangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

MAONI YETU

Tahariri/Habari/Tangazo

Wajumbe ZEC acheni kufuata matakwa ya wanasiasa Inatoka Uk. 1Tume hiyo.

Hata hivyo, Maalim Seif, amesema Tume hiyo inayomaliza muda wake mwishoni mwa mwezi huu, inaondoka huku ikiacha viporo ambavyo Tume inayokuja inapaswa kuvipa umuhimu wa kipekee.

Miongoni mwa mambo ambayo hayakuweza kutekelezwa na Tume hiyo ni pamoja na kushindwa kulifanyia uhakiki daftari la kudumu la wapiga kura kwa vipindi viwili tofauti, jambo ambalo liliahidiwa na Tume hiyo kufanyika kila ifikapo mwezi wa Oktoba.

Kamishna wa Tume hiyo Bw. Ayoub Bakar Hamad, amesema tatizo hilo lilitokana na ukosefu wa fedha za kuendeshea kazi hiyo na kwamba, kwa sasa Shirika la Umoja wa Mataifa la

UNDP tayari limekubali kutoa fedha kwa ajili ya kuendeleza kazi hiyo.

Amesema iwapo fedha hizo zitapatikana kwa wakati mapema mwezi ujao, Tume ijayo itakuwa na uwezo wa kufanya uhakiki mara mbili kwa mwaka, ili kufidia muda uliopita.

K w a u p a n d e w a k e , Mwenyekiti wa Tume hiyo Bw. Khatib Mwinyichande, amesema jitihada za makusudi zinapaswa kuchukuliwa katika kuimarisha d e m o k r a s i a y a u c h a g u z i Zanzibar.

Amesema Tume inayokuja inaweza kufanya kazi zake vizuri zaidi, iwapo wanasiasa watatoa ushirikiano wa kutosha kwa Tume hiyo sambamba na kukubali kufuata sheria zilizowekwa.

“ N a o m b a w a n a s i a s a musioneane haya, shaurianeni na kubalini kukosoana, na kubwa

zaidi ni kukubali kufuata sharia. alishauri Mwinyichande na kuongeza.

“Wanasiasa pia mnayo nafasi kubwa ya kuisaidia Tume kwa kuipa maelekezo yanayostahiki, na kufanya hivyo kunaweza kuipa nyenzo bora za kufanyika kazi”.

Naye Mkurugenzi wa Tume hiyo Bw. Salum Kassim Ali, ameahidi kuzifanyia kazi changamoto zilizojitokeza katika chaguzi zilizopita, ili kuweka mazingira bora zaidi katika chaguzi zijazo.

Pamoja na hayo, Maalim seif, alieleza haja ya Tume hiyo kuanzisha mfuko wake, ili mapato ya Tume yaingie moja kwa moja katika mfuko huo na kupunguza usumbufu wakati Tume inapohitaji fedha kwa ajili ya matumizi yake ya kawaida.

SIKU ya Jumatatu Desemba 31, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, alitangaza matokeo ya awali ya Sensa ya Watu na Makazi iliyofanyika Agosti 26 hadi Septemba 4 mwaka jana.

Rais Kikwete alituambia kuwa sasa Tanzania ina watu milioni 44,929,002 ambapo Tanzania Bara kuna watu 43,625,434 na Zanzibar kuna watu 1,303,568.

Alisema kuwa katika Sensa ya tatu ya mwaka 2002, Tanzania ilikuwa na watu milioni 34.4, hivyo kwa matokeo ya sensa hii watanzania wameongezeka watu milioni 10.5 ambao ni sawa na ongezeko la asilimia 2.6 kwa mwaka.

Rais Kikwete alisema hii ni sensa ya nne kufanyika nchini tangu kuasisiwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 1964. Sensa ya kwanza ilifanyika mwaka 1967 ambapo nchi yetu ilikuwa na watu 12,313,054. Tanzania Bara ilikuwa na watu 11,958,654 na Zanzibar watu 354,400. Kwa maana hiyo, katika miaka 45 tangu Sensa ya kwanza na hii ya sasa, Watanzania wameongezeka watu milioni 33.

Tunaambiwa kuwa taarifa za takwimu hizi ni kwa ajili ya matumizi ya kuboresha maisha ya kila Mtanzania. Kwa kutumia sense ya watu na makazi, hupatikana taarifa muhimu kwa ajili ya kutumiwa na Serikali kupanga mipango ya maendeleo ya nchi na jinsi ya kuhudumia wananchi.

Rais alisema kama kasi ya ongezeko la watu la asilimia 2.6 hal i tapungua if ikapo mwaka 2016, nchi yetu itakuwa na watu milioni 51.6. kiasi kilichomtia hofu kuwa ni mzigo mkubwa kwa taifa kwa uchumi kuwahudumia.

Hofu hii ndiyo iliyomlazimu Rais Kikwete kusisitiza kuwepo mikakati madhubuti katika mipango ya maendeleo kuanzia sasa juu ya jinsi ya kuhudumia watu hao milioni 51.6 na zaidi ya hao miaka inayofuata.

Hili ndilo lililomfanya Rais Kikwete, asisitize suala la kupanga uzazi. Akiwa na maana kwamba kinyume na hatua hiyo, hali ya maisha itashuka sana kutokana na kupanda idadi ya watu. Anaona kuwa kuna uwezekano wa serikali kushindwa kutoa huduma muafaka kwa watu wake.

Hoja yetu kwa leo imesimamia katika nukta hiyo ya Rais juu ya hofu yake ya kuongezeka watu, akilinganisha na uwezo wa serikali kuwahudumia.

K w a m t a z a m o w e t u , tunamuona Rais Kikwete kama anaamini kuwa watu wengi ni

Tatizo letu si wingi bali viongozi waadilifu

mzigo kwa serikali.Hata hivyo, katika mataifa

yaliyoendelea na yanayokua kwa kasi kiuchumi, watu wamekuwa mtaji mkubwa wa kiuchumi kwa mataifa hayo. Watu ni soko, watu ni nguvu kazi.

China, Malaysia, India, na mataifa mengi ya Bara Asia, yamekuwa yakipiga hatua kwa kasi kiuchumi, nyenzo kubwa ikiwa ni idadi kubwa ya watu.

Watu wengi ni kigezo muhimu cha kukua uchumi wa soko na nguvu kazi kwa Taifa lolote lile. Hata wanaofanya biashara, hukimbilia sehemu zenye idadi kubwa ya watu ili kupata soko.

Idadi ya sasa ya Watanzania, j a p o t u n a a m i n i w e n g i hawakuhesabiwa, lakini haiwezi kuzua hofu kwa serikali yeyote yenye mipango mizuri ya kiutawala kwa watu wake.

Tuonavyo sisi, hofu ya Rais Kikwete isingekuwepo kama angekuwa na watu waadilifu wa kumsaidia kusimamia mapato namatumizi na rasilmali za Taifa, ili kuijenga nchi kiuchumi na kuiongezea serikali nguvu ya kuwahudumia watu wake.

U k w e l i n i k w a m b a , kukosekana kwa viongozi na watendaji waadilifu, ambao wangeweza kusimamia rasilmali za nchi kwa faida, ndio sababu kubwa ya kut i l iwa shaka uwezo wa serikali kuhudumia watanzania, sio idadi yao inayokuwa.

Hata kukiwa na idadi ndogo ya watu isiyokuwa kwa kasi, lakini waliopewa dhakama na kuongoza na kusimamia mali za watanzania wakikosa uadilifu na kutokuwa watu wa kutosheka, uwezo wa kuhudumia watu hao wacheche hautakuwepo pia.

Kukosekana maadili kwa viongozi kumekua chachu ya matumizi mabaya ya rasilmali za nchi, kiasi cha kushindwa kutoa huduma nzuri na bora kwa watu wake.

Hulka za wizi, dhuluma, uf isadi , ubinafs i , kukosa uzalendo, n i matokeo ya kukithiri utamadumi mbovu kwa viongozi na watendaji, ambao wameweka uadilifu pembeni na kuvaa ubinafsi na kulitia taifa katika hasara.

Ukweli ni kwamba, Tanzania imekuwa ikipata taabu kufikia malengo yake ya kuwahudhumia watu wake, kutokana na watu waliopewa dhamana kuliingiza Taifa katika mikataba mibovu na ya kihasara kwa maslahi yao na familia zao, huku watanzania walio wengi wakiachwa kuishi katika maisha ya kilofa.

Tunaona kwamba Tanzania ambayo ina eneo la nchi kavu la kilomita za mraba 945,000, ambazo kati ya hizo, Kilomita za mraba 881,000 ni eneo la Tanzania Bara pekee yake na kilomita za mraba 2,000 ni eneo la visiwa vya Zanzibar na Pemba,

kwa ukubwa huu wa nchini, ni dhahiri kwamba kuna uhaba makubwa ya watu kulingana na ukubwa wa ardhi yetu.

China ina watu milioni 1,300, ikiwa na ukubwa wa eneo la km² 9,596,960. Malaysia ina ukubwa wa eneo la km² 329,847 tu, lakini watu wake ni 26,888,000 kwa kadirio la mwaka 2006. Sensa ya

mwaka 2000 iliyofanyika nchini humo ilionyesha kuwa kulikuwa na idadi ya watu 23,953,136. India yenyewe ina idadi ya watu bilioni 1.2

Utaona kuwa pamoja na kuwa na idadi kubwa ya watu, na nchi nyingine kuwa na ardhi ndogo, bado mataifa hayo yamekuwa ndio tishio kwa sasa katika

uchumi wa dunia.Wingi wetu si hoja ya kuwa

na hofu juu ya huduma ya serikali kwa watu wake. Tatizo ni kukosekana watu waadilifu wa kusimamia rasilmali za watanzania, ambazo ndio msingi wa mapato yanayowezesha huduma kukidhi.

SHULE YA ALJEBRA ISLAMIC SEMINARY ILIYOPO KIBADA KIGAMBONI DAR ES SALAAM INAPENDA KUKUTAARIFU

KUWA IMEANZISHA SHULE YA MSINGI ENGLISH MEDIUM.

UKIWA KAMA MZAZI, MLEZI AU MDAU WA ELIMU UNAKARIBISHWA KWENYE KIKAO CHA KUTAMBULISHA SHULE RASMI, KIKAO KITAFANYIKA SHULENI SIKU YA

JUMAPILI TAREHE 6/1/2013 KUANZIA SAA 3 ASUBUHI HADI SAA 6 MCHANA.

KWA MAWASILIANO ZAIDI PIGA SIMU NAMBA: 0715/0752/0688 260241 AU 0655/0768 176700

TAFADHALI ATAKAYESOMA TANGAZI HILI AMTAARIFU NA MWENZAKE

WOTE MNAKARIBISHWA

WABILLAH TAWFIIQ

MKUU WA SHULE

Bismillahir Rahmaanir Rahiim

ALJEBRA ISLAMIC SEMINARYKIKAO CHA WAZAZI, WALEZI

NA WADAU WENGINE WA ELIMU

Page 3: Gazeti la Alnuur

3 AN-NUURSAFAR 1434, IJUMAA JANUARI 4 - 10, 2013Habari

Kesi ya Sheikh Ponda mashahidi waingia ‘mitini’ MASHAHIDI wa upande wa mlalamikaji katika kesi inayomkabili Sheikh Ponda I s sa Ponda na wenzake, wameshindwa k u f i k a M a h a k a m a n i Desemba 31, 2012, kutoa u s h a h i d i w a o k a t i k a mashtaka yanayowakabili watuhumiwa hao.

K u f u a t i a k u s h i n d w a kufika mahakamani hapo kutoa ushahidi wao kama walivyotakiwa, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Victoria Nongwa, alitoa hati ya kukamatwa mashahidi ambao awali walisaini hati ya kuitwa mahakamani kutoa ushahidi wao, lakini siku ya kusikilizwa kesi hawakutokea m a h a k a m a n i h a p o n a hawakutoa taarifa yoyote.

Kesi hiyo, ambayo ilipangwa kusikilizwa Jumatatu ya wiki iliyopita mahakamani hapo, iliahirishwa na Hakimu Victoria Nongwa, hadi tarehe 14, 2013, kwa ajili ya kutajwa, ambapo itasikilizwa Januari 17, 2013 kwa kuendelea kusikiliza mashahidi wa upande wa mashtaka.

Kwa mara ya mwisho, kesi hiyo ilisikilizwa Desemba 13, 2012, ambapo Sheikh wa Bakwata , Mkoa wa Shinyanga, Ismail Habibu Makusanya, alitoa ushahidi kwa upande wa mlalamikaji na iliahirishwa hadi Desemba 31, 2012, ambapo ilikuwa ni kwa ajili ya kuendelea kusikiliza mashahidi zaidi wa upande wa mlalamikaji.

Awali Mwanasheria wa Serikali, Tumaini Kweka, aliieleza Mahakama kwamba, al i i ta mashahidi watatu kwa ajili ya kufika kutoa ushahidi wao, lakini wote wameshindwa kufika licha ya kwamba mmoja alisaini hati ya kuitwa mahakamani kutoa ushahidi.

“Leo kesi imeitwa kuja kusikil izwa, upande wa Jamhuri unaendelea kuleta mashahidi, lakini kutokana na sababu ambazo hata sisi Jamhuri tunashangaa, hawajatokea. Niliita mashahidi watatu kati ya hao mmoja alisaini samansi.” Alisema Wakili wa Serikali, ikiieleza Mahakama.

Akitoa sababu za kutokufika kwa mashahidi hao, Wakili Kweka, alisema shahidi mmoja alimpa taarifa kuwa amesafiri, mwingine alidai ni mgonjwa hivyo hakusaini kabisa samansi na shahidi mwingine alisaini samansi na kuahidi kufika, lakini mpaka muda huu wa kuanza

Na Bakari Mwakangwale kesi hatufahamu ni kwanini hajafika.

Hata hivyo wakili Kweka hakuwa tayari kutaja majina ya mashahidi hao.

B a a d a e a l i i o m b a Mahakama i ta je ta rehe nyingine ya kusikilizwa kesi hiyo ili aweze kuwapata na kuwapeleka mashahidi hao mahakamani kwa ajili ya kutoa ushahidi wao dhidi ya mashtaka yanayowakabili Sheikh Ponda na wenzake.

Kwa upande wake, wakili wa Sheikh Ponda na wenzake, Bw. Juma Nassoro, alihoji kuwa katika kesi iliyopita, (yaani Desemba 13, 2012) wakil i wa Jamhuri Bw. Kweka, aliieleza mahakama kuwa kesi hiyo itakuwa na mashahidi wasiopungua arobaini kwa upande wa mlalamikaji, hivyo inakuwa je wameitwa mashahidi watatu tu na wameshindwa kutokea mahakamani na hawajulikani walipo?

Baada ya kuulizwa na Hakimu, kauli ya Wakili Kweka, ilibadilika na kutoa sababu kuwa mmoja kasafiri na mwingine anaumwa, jambo ambalo Bw. Nassoro alidai si sahihi.

“Hii si sahihi Mheshimiwa Hakimu, kutoa maelezo hayo hata huyo aliyesaini samansi pia hajatokea, inaonyesha udhaifu kwani hata mwenye kesi Hafidhi (Mlalamikaji) hajafika.” Alisema Nassoro.

Hakimu Victoria Nongwa, alitoa amri ya kukamatwa shahidi aliyesaini samansi na kushindwa kufika mahakamani bila taarifa, ili ajieleze kwa nini alishindwa kutokea.

Mpaka sasa Mashahidi watatu tu wa upande wa mashataka ndio walioweza k u t o a u s h a h i d i w a o mahakamni hapo.

Nao ni Sheikh Suleiman Lolila, Katibu wa Bakwata Makao Makuu , She ikh Ismail Habib Makusanya, Sheikh wa Bakwata mkoa wa Shinyanga na Bw. Suleiman Nassor Mohammed, mmoja wa wamiliki wa kampuni ya Agritanza, ambayo ndiyo iliyopewa ekari nne za kiwanja cha Markaz Chang’ombe.

H a k i m u N o n g w a , alipendekeza kesi hiyo iendelee kusikilizwa Januari 17, 2013. Januari 14, mwaka huu, kesi hiyo itarejea Mahakani hapo kwa ajili ya kutajwa kwa mujibu wa sheria.

H a k i m u N o n g w a , a l i b a i n i s h a k w a m b a watakaokwenda Mahakamani hapo Januari 14, 2013, ni Sheikh Ponda na Mukadam Swaleh ambao wapo mahabusa mpaka sasa.

Washtak iwa wengine waliopo nje kwa dhamana, w a m e t a k i w a k u f i k a Mahakamani hapo Januari 17, 2013, siku ambayo kesi hiyo itaendelea kwa kusikiliza mashahidi wa upande wa mashtaka.

Akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kuahirishwa kwa kesi hiyo, Wakili wa Sheikh Ponda, Juma Nassoro, alionyesha kushangazwa na mwenendo wa kesi hiyo kwa upande wa walalamikaji.

Alisema, mbali ya mashahidi wanaoanza kukwepa kufika na kutoa ushahidi wao, lakini hata Hafidhi, ambaye ndiye mlalamikaji amekuwa hafiki Mahakamani bila sababu za msingi.

Aidha alisikitishwa na ki tendo cha upande wa mashtaka kushindwa hata kutaja majina na idadi halisi ya mashahidi, jambo alilodai kuwa si la kawaida kwani hata katika kesi za mauaji, mashahidi huwa wanatajwa tofauti na wale wa kesi ya mteja wake.

Alipoulizwa na An-nuur juu ya mustakali wa dhamana kwa wateja wake (Sheikh Ponda na Mukadam), alisema bado Jamhuri inadai kuwa inaona watahatarisha amani endapo watakuwa nje. Hata hivyo alisema, wameandika barua kulalamikia suala hilo kwa DPP lakini bado hawajapata majibu yoyote.

Alisema katika barua h i y o , w a m e m w e l e z a DPP kwamba kuendelea kumshikilia Sheikh Ponda na Mukadam, ni kinyume cha

haki za binadam kwa sababu haiwezekani katika kesi moja washtakiwa wengine wote wapate dhamana na wengine wanyimwe haki hiyo.

Alisema kitendo hicho ni cha kukandamiza haki za msingi za binadamu kwa sababu katika mtiririko wa maelezo ya kesi, hakuna hata mmoja anayezungumzia kuvurugwa amani ya nchi, zaidi mashahidi wanazungumzia uhalal i au kutokuwapo uhalali wa kuuzwa kiwanja cha Markazi Chang’ombe.

Kwamba hakuna sehemu yeyote ambayo inaonyesha kiwanja hicho kinagusa maslahi ya Taifa.

“Tumeandika barua kwa DPP, Desemba 24, 2012, yenye kumbukumbu namba LJ/CC/245/2012, tumeomba k w a m b a D P P a o n d o e pingamizi lake la dhamana kwa sababu kesi na mtiririko wake unavyokwenda, hakuna

lolote linaloonyesha maslahi ya Taifa au usalama wa nchi unaweza kuhatarika kwa Sheikh Ponda na Sheikh Mukadam kuwa nje kwa dhamana. Nao wapewe haki hiyo kama ambavyo wenzao waliopatiwa dhamana katika shauri hilo hilo.” Alisema Wakili Nassoro.

Wakili Nasoro alisema, u s h a h i d i u n a o t o l e w a unaonyesha kabisa kuwa ni mashtaka ya kawaida kwani alidai kwamba, hata maelezo ya Bw. Hafidhi, (aliyenunua k i w a n j a ) a l i y o y a t a o a Polisi Chang’ombe akiwa mlalamikaji, hakuna mahala panapoeleza kuna kuhatarisha maslahi ya Taifa au Usalama wa Taifa.

Al i sema nd io maana amemuomba DPP, a toe pingamizi lake ili Mahakama iweze kuweka wazi dhamana kwa washtakiwa ili wapate haki yao ya dhamana.

1.2259 sqm - 8 Milion2.1470 sqm - 4.5Milion3.1341 sqm - 4 Milion4.1566 sqm - 5Milion5. 1115 sqm - 3.5Milion6. 1136 sqm - 3.6Milion

Vipo Barabara ya Kongowe-SogaKilomita moja toka barabara ya Morogoro.

Simu No.0755 090 754/0715 090 754.

Viwanja vilivyopimwa vinauzwaKongowe Kibaha

WAKILI wa Sheikh Ponda Issa Ponda, Juma Nassoro akiongea na Waislamu nje ya Mahakama ya Kisutu Jumatatu wiki hii. (Picha na Bakari Mwakangwale)

Page 4: Gazeti la Alnuur

4 AN-NUURSAFAR 1434, IJUMAA JANUARI 4 - 10, 2013Habari

Nyerere alikuwa kiongozi wa dini au siasa?Inatoka Uk. 1

alipokuwa hai.Aidha wamefahamishwa

k w a m b a , i n a p o s e m w a kuwa haya t i Mwal imu Nyerere alikuwa muasisi wa Mfumokristo, umekuwepo ushah id i kami l i h ivyo haisemwi kwa kuzusha tu au kumpakazia na kwamba, ndiyo sababu Kanisa Katoliki nchin i l ina taka kumpa utakatifu kutokana na kazi nzuri alilolifanyia Kanisa hilo alipokuwa madarakani.

Akihutubia ndani ya Masjid Idrisa, uliopo Kariakoo jijini Dar mara baada ya swala ya Ijumaa wiki iliyopita, Maalim Bassaleh, aliwataka Maaskofu nchini, kueleza kwa uwazi sababu za kubariki utakatifu wa hayati Julius Kambarage Nyerere, wakati hakuwa kiongozi wa dini.

Alisema kabla ya kutaka kumkingia kifua Mwalimu Nyerere ambaye aliyekuwa kiongozi wa siasa, ni vyema kwanza wakaeleza misingi ya kumsimika utakatifu mkatoliki ambaye hakuwa kiongozi wa Kanisa.

“Lakini tuliulize hilo Kanisa Katoliki, kwamba je, Mwalimu Nyerere, alikuwa kiongozi wa dini au kiongozi wa Siasa? Kama wa siasa, vipi Kanisa hilo linataka kumpa cheo cha utakatifu, cheo ambacho kinalihusu Kanisa hilo tu, wakati alikuwa ni kiongozi wa umma na si wa dini.” Alisema na kuhoji Maalim Bassaleh.

Alisema kwa kawaida, Wakatoliki huwapa utakatifu watu ambao walikuwa nguzo (mihimili) ya Kanisa Katoliki na ambao wamefanya kazi zilizotukuka wakiwa ni Wachungaji au Watawa au watumishi wa kanisa waliowahi kujitolea kwa muda mrefu katika Kanisa.

Akinukuu kitabu cha Rais mstaafu wa Zanzibar, Mzee Aboud Jumbe, ambaye alifanya kazi ya kwa karibu na mwalimu, Maalim Bassaleh alisema katika kitabu chake hicho cha ‘The Partnership’, ameeleza kwamba mwalimu Nyerere, alikuja kuimarisha Mfumokristo katika utawala wake kutokana na nafasi aliyokuwa nayo na zaidi alilipendelea Kanisa lake Katoliki.

Alisema Alhaji Jumbe, aliyaeleza hayo kwa kutumia

ushahidi wa Padri Mkristo wa Kikatoliki, Dk. Sivalon, aliyefanya utafiti kuhusu Kanisa Katoliki na siasa za Tanganyika, ambapo kwa uwazi na mapana Padri huyo ameonyesha ni vipi mwalimu Nyerere, wakati wa utawala wake alivyokuwa akilipendelea Kanisa Katoliki nchini.

Ufafanuzi wa Maalim Bassaleh umekuja kufuatia yaliyoelezwa katika tamko la Jumuia ya Maaskofu lililotolewa Kurasini Jijini Dar es Salaam siku za hivi karibuni.

Katika tamko hilo, pia walijadili hali ya kuzorota kwa mahusiano baina ya dini mbili kubwa hapa nchini, Uislamu na Ukristo, kisha walieleza juu ya hatari inayolinyemelea Taifa kutokana na hali hiyo.

M a a l i m B a s s a l e h , alisema katika kipengele hicho, amewataka Waislamu kuwapongeze Maaskofu hao kwa kuiona hali hiyo na kisha kutoa wito wa kuyashughulikia haraka yale yanayoashiria hatari sambamba na kuboresha mahusiano mema baina ya Waislamu na Wakristo.

“ K a m a n d u g u z e t u Maaskofu watakuwa wakweli, basi huo ni mwanzo mzuri wa kujenga msingi mwema wa amani ya kweli katika nchi yetu na wala isiwe amani ya kifaurongo (aina ya mti ukiguswa husinyaa baada ya muda huchanua)”. Alisema

Maalim Bassaleh.Pamoja na kuwapongeza

Maaskofu kwa kuiona hatari iliyo mbele, lakini alidai makundi hayo yanatofautiana kwa kiasi kikubwa katika kiini cha matatizo hayo na suluhisho lake.

Akichambua tamko hilo, Maalim Bassaleh, alisema makundi hayo yanaanza kuachana pale ambapo Maaskofu hao wanapokataa kuwepo kwa Mfumo Kristo ulioota mizizi katika dola, wakidai kwamba ni dhana potevu.

“Jukwaa la Wakristo nchini tunakanusha wazi wazi na kuelezea bayana kuwa nchi hii haiongozi kwa Mfumo Kristo, kwa watu walio makini hakuna kificho kuwa viongozi wote waandamizi wa ngazi ya juu serikalini awamu ya sasa asilimia tisini ni Waislamu.

“Dhana ya kuwepo Mfumo Kristo ni uongo na ni dhana potevu, maneno hayo ni agenda za waamini wenye imani kali na waliojiandaa kwa mapambano maovu.” Alinukuu sehemu ya tamko hilo.

A k i f a f a n u a n e n o ‘Mfumokr is to’ Maal im Bassaleh, alisema ni mfumo kandamizi dhidi ya Uislamu na Waislamu, japo kuwa kwa misingi ya kiserikali mfumo huo haupo rasmi, lakini kiutendaji mfumo huo umefanywa kuwa ni mila, desturi na utamaduni

wa watendaji walio wengi serikalini na katika taasisi zake, ambazo mara nyingi zinatumika kuwakandamiza na kudhulumu haki za Waislamu.

Al i sema mfumo huo umekuwa kama utamaduni na umeenezwa hadi katika mashirika ya umma na katika Taasisi za kijamii.

Mara kadhaa watekelezaji wa Mfumokristo wamekuwa wakikiuka hata Katiba na sheria za nchi, hususani masuala hayo yanapogusa Waislamu na Uislamu.

Maalim Bassaleh alisema kwa utaratibu huo, hata kama Maaskofu wamenisha kuwa Rais na watendaji wa ngazi za juu wote ni Waislamu, lakini kutokana na Mfumokristo, wote waliotajwa wanatatizika katika kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Wakijisafisha kuhusu suala la MoU, Maaskofu hao wanadai katika tamko lao kwamba mkataba huo ni baina ya Makanisa ya Tanzania na Makanisa ya Ujerumani na kwamba, serikali ilihusishwa tu.

Katika maelezo yao kuhusu MoU, wao wamedai kuwa MoU ya mwaka 1992, ni kwa ajili ya huduma ya kijamii zinazotolewa na Makanisa kwa Watanzania wote, ikiwa ni pamoja na huduma za hospitali, vituo vya afya, zahanati na shule mbalimbali zinazoendeshwa na Makanisa nchini.

Maalim Bassaleh alihoji, ikiwa mkataba huo ni wa Makanisa na kwamba serikali ilihusishwa tu, itahusishwa vipi katika masuala ya dini wakati Serikali yenyewe haina dini?

Inafahamika kwamba kwamba hao Maaskofu, wamekuwa wakiigomea Serikali kujihusisha na Mahakama ya Kadhi na suala la OIC kwa Waislamu, wakidai serikali haina dini.

“Mbona Serikali hiyo inahusishwa katika mikataba ya Makanisa ya Ulaya na yale ya humu nchini, lakini hawataki ihusihwe na OIC, ambayo nayo ikija i t a tengeneza barabara , madaraja, na watakaopita ni watu wote bila kuangalia waliovaa kofia, kanzu au kilemba, kusaidia taasisi za huduma za kijamii ya watanzania wote bila kujali dini zao kama inavyodaiwa kufanywa na taasisi za makanisa?.” Alihoji Maalim Bassaleh.

H a t a h i v y o M a a l i m Bassaleh alisema maaskofu hawataki kusema kweli juu ya mkataba wao wa MoU kati yao na serikali.

A l i s e m a , m a e l e z o wanayoyatoa Maaskofu ni tofauti na mkataba wenyewe ambao unasema, “S is i tuliotia saini zetu ambao ndio wahusika katika maridhiano hayo, kwa kutaja Makanisa yaliyoungana chini ya Baraza la Makanisa Tanzania na B a r a z a l a M a a s k o f u Tanzania.

“Ambayo katika mkataba huu yatakuwa yanajulikana kama ni Makanisa kwa upande mmoja na Serikali ya Muungano wa Jamhuri wa Tanzania, itatambulika kama ni Serikali kwa upande wa pili”. Alinukuu sehemu ya mkataba huo kati ya serikali na makanisa.

Alisema, kutokana na kipengele hicho, inaonyesha makubaliano hayo ni ya pande mbili ambapo upande wa kwanza ni wa Makanisa, ambayo yameungana pamoja na upande wa pili ni wa Serikali. Katika Makanisa yaliyotajwa hapo, hakuna Kanisa la Kijerumani.

Alisema kwa kupitia mkataba huo, Makanisa yanatumia pesa za Serikali ambazo ni za walipa kodi wote. Mwaka wa fedha wa 2008-2009, Serikali ilitumia mamilioni ya fedha kwa ajili ya kufadhili Mahospitali na taasisi nyingine za huduma za afya zinazomilikiwa na Makanisa kwa ajili ya kulipa mishahara wafanya kazi.

MAALIM Ally Bassaleh akiongea na Waislamu katika viwanja vya Biafra, jijini Dar es Salaam.

Page 5: Gazeti la Alnuur

5 AN-NUURSAFAR 1434, IJUMAA JANUARI 4 - 10, 2013Habari za Kimataifa

LONDONLICHA ya kutangazwa kwa propaganda mbaya kama dini ya magaidi, U i s l a m u u n a k u w a kwa kasi katika nchi za Magharibi ambazo kwa kawaida wanaishi wakristo wengi.

Uingereza imekuwa mfano mzuri wa hali hii ambapo Wakristo wengi wanabadili dini na kuwa Waislamu na kuufanya U i s l a m u k u w a d i n i inayokuwa kwa kasi zaidi katika majimbo ya nchi hiyo.

Kushamiri kwa Uislamu kumebainika hivi karibuni kufuatia sensa iliyofanyika hivi karibuni Uingereza, a m b a y o s i k w a m b a imebainisha ukuaji wa haraka wa Uislamu, lakini pia kumeifanya Uislamu kuwa dini ya pili nchini humo.

Mmoja wa watathmini

TEHRANJeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limefanyia majaribio makombora mawili ya Qader (Uwezo) na Nour (Nuru) katika mazoezi ya kijeshi yaliyofahamika kama ‘Velayat 91’.

Kamanda wa Kitengo cha Makombora cha Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Admeli

Iran yafanyia majaribio makombora mapya Ali Vafadar, amesema aina hizo mbili za makombora hayo yametengenezwa nchini humo na wataalamu Wairan wenyewe.

A m e o n g e z a k u w a m a k o m b o r a h a y o yameimarisha kiwango cha uwezo wa Jeshi la Wanamaji la Iran baharini.

Mazoezi hayo hayo ya siku sita yalianza Ijumaa, Desemba 28, na yamefanyika katika

eneo la fukweni, baharini na angani, kwenye lango la Hormuz, Bahari ya Oman, Kaskazini mwa Bahari ya Hindi, Ghuba ya Aden na lango la Babul Mandab.

Kamanda wa Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Admeli Habibullah Sayyari, amesema mazoezi hayo ya kijeshi yamebeba ujumbe wa urafiki na udugu kwa mataifa rafiki na onyo kali kwa maadui.

WASHINGTONHABARI kutoka Marekani zinabainisha kuwa, viongozi wa kisiasa wa vyama vya Republican na Democrats, wameendelea kulumbana kutokana na hali mbaya ya uchumi wa nchi hiyo.

Mvutano huo umetokea kuhusu juu ya namna gani ya kutatua matatizo ya kiuchumi i l i kuweza kuwapunguzia wananchi mzigo wa mgogoro wa kiuchumi.

Mkuu wa taasisi ya Centre for Corporate Policy, ya Washington Bw. Charlie Cray, amesema kuwa jamii ya watu wa tabaka la kati nchini Marekani, ndio waathirika wa malumbano ya kisiasa nchini humo.

Ameongeza kuwa, hali hiyo imezidisha ongezeko la ukosefu wa ajira na mgogoro wa kiuchumi nchini humo. Mtaalamu huyo wa masuala ya kiuchumi pia amesisitiza kuwa, hali mbaya zaidi inawakabili Wamarekani wenye asili ya Kiafrika na kwamba, kiwango cha ukosefu wa ajira katika tabaka hilo kimefikia asilimia 12.4, ambapo wengi wao ni vijana walio na umri wa kati ya miaka 18 hadi 29.

Rais Barack Obama amekuwa akishinikiza mpango wake wa kuiongeza kodi kwa matajiri nchini humo, ikiwa nikatika harakati zake za kujaribu kupunguza nakisi ya bajeti ya nchi hiyo na kuongeza pato la serikali.

Wakristo Uingereza wasilimu kwa kasiWaufanya Uislamu kukua kwa kasi zaidi

amesema, “dalili zote ni kwamba idadi kubwa ya Waingereza ambao wamekulia katika Ukristo w a n a k u w a Wa i s l a m . Hii inaonyesha ni jinsi gani idadi ya Waislamu inaongezeka huku ile ya Wakristo ikipungua…kiwango hiki kinatarajiwa kuendelea.”

K w a m u j i b u w a matokeo ya sensa hiyo, Waislamu sasa wanakuwa asilimia tano ya idadi ya watu wote wa Uingereza. Viwango vya ukuaji vya hivi karibuni vimeonyesha kuwa idadi ya Waislamu inaweza kuwa maradufu hadi kufikia sensa ijayo ambayo itafanyika mwaka 2021, na hapo wanatarajiwa kuwa asilimia kumi ya idadi ya watu wote.

Katika kipindi hicho,

idadi ya Waislamu England na Wales inakadiriwa kuongezeka kwa asilimia 80 (sawa na milioni 1.2), kutoka milioni 1.5 mwaka 2001 hadi milioni 2.7 mwaka 2011, na kuufanya Uislamu dini ya pili kwa ukubwa Uingereza.

W a t a f i t i w e n g i wanaamini kuwa idadi k a m i l i y a Wa i s l a m Uingereza inaweza kuwa kubwa kuliko iliyojitokeza katika data za sensa hiyo. Hii ni kwasababu swali la dini lilikuwa swali la hiari katika sensa hiyo ya mwaka 2011 na asilimia 7.2 ya watu hawakujibu swali hilo.

D i n i y a t a t u k w a ukubwa England na Wales ni Hinduism (817,000), wakifuatiwa na Sikhism (423,000) , Buddhism

(248,000) na Judaism (263,000), ilieleza ripoti ya sensa hiyo.

Katika sensa hiyo, idadi ya watu milioni 56.07 walihesabiwa, idadi ya waliojieleza wenyewe kuwa ni Wakristo ilishuka kutoka asilimia 72 mwaka 2001 hadi kufikia asilimia 59 mwaka 2011. Idadi ya Waislamu iliongezeka kutoka asilimia 3 hadi kufikia asilimia 5 katika muongo mmoja.

Takwimu za sensa hiyo zimeonyesha kuwa idadi ya Wakristo England na Wales imeshuka kwa silimia 11 (milioni 4.1) katika karne iliyopita, aidha inaonyesha kupungua kutoka milioni 37.3 mwaka 2001 hadi milioni 33.2 mwaka 2011.

T a k w i m u h i z o zilionyesha dhahiri kuwa

Uislamu unakuwa kwa kasi na idadi kubwa ya wasiokuwa Waislamu wameamua kuufuata , ingawa watu wa Magharibi wanauona kama ni dini ya magaidi na kusambaza propaganda potofu dhidi ya Waislamu.

WAZIRI Mkuu wa Uingereza, David Cameroon

Marekani yaonyesha kujizatiti kijeshi Afrika

MAREKANI imetuma vikosi vyake nchini Chad, katika hatua ambayo inaonekana wazi kuwa ni kuzidi kujizatiti kijeshi barani Afrika.

S a b a b u i l i y o t a j w a n a Marekani ya kutuma vikosi vyake nchini Chad, ni wasiwasi wa Washington kuhusu usalama wa raia wake kutokana na kuzidi kusonga mbele waasi katika nchi Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambayo ni jirani na Chad.

Katika barua yake kwa maspika wa mabunge mawili ya Marekani, Rais Barack Obama wa nchi hiyo amesema kuwa, raia kadhaa wa Marekani wameondolewa katika mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bangui, tangu Desemba 27 na hivi sasa kikosi cha wanajeshi 50 wa Marekani kimetumwa nchini Chad.

Watu wanaokosoa hatua hiyo ya Marekani wanasema kuwa, hawaoni sababu ya Washington kutuma kikosi cha jeshi, tena katika nchi ambayo haina machafuko kwa madai kuwa nchi jirani ina machafuko.

Itakumbukwa kuwa Marekani na Ufaransa zilikataa mwito wa Rais Francois Bozize, wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wa kutaka kusaidiwa kukabiliana na waasi wa kundi la SELEKA.

Uchumi waibua malumbano ya kisiasa Marekani

Page 6: Gazeti la Alnuur

6 AN-NUURSAFAR 1434, IJUMAA JANUARI 4 - 10, 2013Makala

WAZUNGU wana msemo wao usemao, “Ukitaka kumuua mbwa mpe j ina baya” . Jambo la kushangaza basi, katika uzoefu wa maisha ya mwanadamu si mara nyingi falsafa na ukweli uliomo katika methali kutumika kama falsafa ya nchi au taifa fulani.

Lakini kwa sababu moja au nyengine, kuna misemo miwili mitatu hivi inaonekana kubakia kuwa misemo tu, bali imekuwa kama falsafa inayoongoza maisha na malengo ya watu hapa duniani.

Kwa mfano, msemo mkongwe wa Wazungu u ta f s i r ikao kama ‘wagawe, uwatawale’ umetumika ipasavyo katika kuzitawala nchi na Jumuiya mbalimbali duniani. Waingereza waliweza kuitawala dunia kwa msemo huu. Na Wamarekani wameweza kufanya watakalo duniani kwa kutumia falsafa hii. Pia Watanganyika wameweza kuitawala Zanzibar kimabavu kwa kutumia fasalafa hii pia. Wametugawa na kututawala.

Wakati hubadilisha mambo. Kwa muda wa miongo ipatayo sita (six decades) tangu uhuru, falsafa hii imekuwa ikifichwa kutumiwa kwake. Inafichwa sio

Hujuma dhidi ya Waislamu wa Zanzibar

SHEIKH Farid Had na viongozi wenzake wa UAMSHO wakiwa katika karandinga la Polisi.

Na Mwandishi Wetu kama haipo, ipo lakini dunia ya sasa ya utandawazi na haki za binadamu, falsafa hii haipati nguvu ya kutembea utupu hadharani tena kama ilivyokuwa mwanzo.

Na kwa vi le s i laha hi i imekwisha nguvu, tumeletewa si laha nyengine isemayo, ‘Ukitaka kumuuwa mbwa, mpe jina baya!’

Zanzibar, katika ramani ya siasa za dunia imekuwa ikifanyiwa kila bidii na njama ili iwe sawa na Palestina, au mataifa mengine ya Kiislamu yaliyoharibiwa na Mayahudi na Manasara kupitia mataifa yao makubwa. Yaani Zanzibar inatakiwa isiwe na utaifa wala utambulisho wowote. Na hilo lilikuwa karibu mno kufanikiwa. Lakini kabla ya kufikia hatua hiyo, wazanzibari wameamka.

Wakaanza kudai haki zao. Na kwa vile wanzanzibari hawalengwi wala kuthibitikiwa na kuwa na haki ya kudai chao, pao, lao, wala ya kwao, hili limekuwa kosa. Sasa tunabatizwa kwa kila jina baya ili kuhalalisha kuangamizwa kwetu.

Tu n a i t w a m a g a i d i n a Waislamu wenye msimamo mkali. Tunaitwa hivi katika k i p i n d i a m b a c h o d u n i a imejengwa iamini kila Muislamu ni adui asiye na haki ya kuishi

katika mgongo wa dunia hii.Kwa kusherehesha mjadala

huu, katika siku za hivi karibuni, Zanzibar imekuwa ikiharibiwa sifa na jina lake kwa maksudi na vyombo vitatu. Kwanza, Kanisa ambalo limekuja Zanzibar sio kwa kufanya ibada, bali kuifitinisha Zanzibar mbele ya jamii za Kimataifa. Kanisa lilikuwapo Zanzibar tangu na kabla ya kuja kwa Edward Steere hapa Zanzibar.

Kulikuwa kimya ilhali Waislamu walikuwepo, tena na wasomi wakubwa wa enzi hizo wakiwa hai hapa Zanzibar. Ilikuwa kimya na wala hakukuwa na Mzanzibari aliyewahi kuingilia uhuru wa kuabudu kwa wana Kanisa. Na hivi ndivyo ilivyo mpaka leo. Zanzibar ni nchi pekee duniani iliyo na ustahamilivu mkubwa wa kidini (Religious tolerance) kuliko nchi yoyote.

Kwa vile wanaonekana Wazanzibari hawapendi ugomvi na wenzao wa Kikristo, la kufanya ni kuwapachika kila aina ya sifa mbovu ili kuwachafua, hata kama hawamchokozi mtu. Kanisa, Zanzibar hufanya kila liwezalo, kuhakisha wanawakorofisha Waislamu ili wajibu mapigo, wawaharabie sifa na malengo yao yatimie.

Hili lilishindikana na sasa kuna

njama za maksudi za kufanya matukio yao wenyewe kama vile kutia moto baa, makanisa yao, na hata kujeruhiana na kisha wakasingizia Waislamu wa Zanzibar, ambao wengi wao hawana habari na Wakristo waliopo. Wazanzibari wa sasa wametiwa dhiki za maisha kiasi kwamba hata hizo sala tano ni shida kuzisimamisha, seuze kugombana na kanisa.

Chombo cha pili ni Serikali, ambayo ili kulinda maslahi ya Muungano, imeifanya Zanzibar kuwa ni eneo la hatari kidini na kisiasa. Na bila kujua athari ya maneno wanayosema mbele ya jamii za kimataifa, serikali imethubutu kuitangazia dunia kuwa Zanzibar kuna magaidi na wanaharakati wa Kiislamu wenye msimamo mkali.

Huu ni ubaya ulio dhahiri wa Serikali dhidi ya wananchi wake wenyewe. Serikali haitambui kuwa kufanya hivi sio kuharibu taswira ya Zanzibar na Waislamu tu, bali hata nchi nzima, na kuathiri shughuli nyingi za kiuchumi, lakini nani anafikiri hayo. Tupo kisiasa zaidi.

Taasisi ya tatu, Mayahudi na Manasara ambao kazi yao ni kuleta fitina katika ardhi, hasa hasa ardhi za Kiislamu. Watu hawa ambao wengi ni wazungu, huja hapa kama watalii na baadae

kuanza kupanga hujuma na mitandao ya fitina zisizomithilika dhidi ya Waislamu. Baada ya hujuma zao hizo kutimia, ndio utaona wanatumia vyombo vya habari kuitangazia dunia kuwa Zanzibar kuna ‘ugaidi’ Waislamu wanawaonea wakristo. Hii ni fitna tupu.

Zanzibar hakuna lolote kati ya hayo wanayoyataja. Na jambo la kushangaza, hakuna kiongozi wetu hata mmoja anayekanusha upuuzi na kasumba hizi. Leo hii Wazungu ndio wanaoongoza kwa kutembea uchi hapa Zanzibar. Waislamu wako kimya. Wao wapo hapa pia kuishawishi nchi hii ikubali ndoa za mashoga. Mambo ambayo huko kwao yameshawashinda, wanatuletea sisi huku.

Wazungu ndio walioleta nakama ya mahoteli, kuigiza na kuingiza mikanda ya ngono, na ndio wanaojazana hapa mwezi wa Ramadhani kuja kula mchana barabarani ili kuwaudhi Waislamu. Hakuna anayesema. Tunafanyiwa maudhi na karaha ndani ya nchi yetu, bila kuheshimu mila na desturi za nchi yetu. Ukisema Serikalini unajibiwa, ‘Serikali haina dini’.

Wanzanzibari tumekuwa watumwa, watwana katika nchi yetu kwa wageni wajao kwetu. Na bahati mbaya Waislamu wakisimama kudai haya, Serikali husimama kidedea kuwalaani Waislamu na kuwahujumu kupita kiasi. Serikali haijali wala kutambua kuwa katika nchi kama Zanzibar ambapo Waislamu ni wengi, mila na desturi za Waislamu hao hazina budi kulindwa na kuheshimiwa na kila mtu, licha ya kuwa serikali haina dini, lakini viongozi wanayo dini.

Nionavyo, ni wajibu wa kila Muislamu, awe kiongozi wa siasa, wa nchi au raia wa kawaida, ni wajibu kwake kuilinda dini hii. Tuelewe kwamba wenzetu wasiokuwa Waislamu, wameanda l iwa kuvuruga juhudi zote za kuimarisha na kuisimamisha dini ya Kiislamu. Na mbinu wanayoitumia ni hii ya kutuita majina mabaya ili kuhalalisha maovu yao.

Wazanzibari na Waislamu wote, tuwe macho na tusimame na kamba ya mwenyezi Mungu b i l a ku fa r ik i ana . Kwan i tutakaposimama kumnusuru M o l a w e t u , a t a t u n u s u r u na kuzithibisha nyoyo zetu. Tukumbuke kwamba, wenzetu w a s i o k u w a Wa i s l a m u hawapendezewi na ustaarabu na utamaduni sahihi wa dini hii, na ndio Mola mtukufu anaposema ‘Hawataridhika hao Mayahudi na Manasara, mpaka muwafuate mila na nyendo zao’.

Wallwahu a-alam!

Page 7: Gazeti la Alnuur

7 AN-NUURSAFAR 1434, IJUMAA JANUARI 4 - 10, 2013Makala

D e s e m b a 2 7 , 2 0 1 2 - ‘Mtandao wa kupashana habari’Siku tatu kabla ya kijana wa miaka 20 Adam Lanza kumwua mama yake, na halafu akafyatua risasi katika darasa li l i lojaa watoto wa chekechea h u k o C o n n e c t i c u t n c h i n i M a r e k a n i , mwanangu Michael (jina limebadilishwa) mwenye umri wa miaka 13 alikosa basi la kumpeleka shule kwa sababu alikuwa amevaa k a p t u r a y e n y e r a n g i zisizostahili.

“Naweza kuvaa kaptura hii,” alisema, sauti yake ikiongeza ukali, chembe nyeusi ya katikati ya jicho ikimeza ukanda wa bluu unaozunguka.

“Kaptura hii ni buluu ya bahari,” nilimwambia. “Sare za shule yako ni kaptura nyeusi au za khaki, basi.”

“Waliniambia naweza kuvaa hizi,” aling’ang’ania. “Wewe ni dogi mpumbavu, Naweza kuvaa kaptura yoyote ninayotaka. Hii ni Amerika. Nina haki zangu.”

“Huwezi kuvaa chochote unachotaka,” nilisema, kwa sauti ya upole, kumwelewesha. “Na kwa vyovyote huwezi kuniita dogi mpumbavu. Hutatumia chochote cha ki-elektroniki siku nzima, Sasa ingia kwenye gari nikupeleke shuleni.”

Naishi na mtoto ambaye n i m g o n j w a w a a k i l i . Nampenda mwanangu. Lakini ananitisha.

Wiki kadhaa zilizopita, Michael alinishikia kisu na kutishia kuniua na halafu ajiue baada ya kumwambia arudishe vitabu vya maktaba alivyochelewesha. Wadogo zake wa miaka 7 na 9 wanafahamu mipango ya usalama - walikimbil ia gari na kufunga milango kabla sijawaambia wafanye hivyo. Nilifaulu kukitoa kisu mikononi mwa Michael, na kwa uangalifu nikaokota chochote chenye ncha kali ndani ya nyumba na kuweka katika kasha ambalo kila nikisafiri naondoka nalo. Na muda wote huo alikuwa akiendelea kunitukana kwa sauti kubwa na kutishia kuniua au kunidhuru.

Ugomvi huo uliisha wakati maofisa watatu wa polisi wenye vifua vipana na mganga msa id i z i wa l ipombana mwanangu aingie kwenye kiti cha gari la wagonjwa la gharama kubwa kupelekwa katika chumba cha dharura cha karibu. Hospitali ya magonjwa ya akili haikuwa na vitanda vyovyote siku hiyo, na Michael akatulia vyema katika

Watoto wauaji, na familia zenye hofu MarekaniBaada ya mauaji mengine ya kutisha na

janga la kitaifa, ni rahisi kuzungumzia bunduki. Lakini ni wakati pia wa kujadili

magonjwa ya akili

Na Mama mwanaharakati

chumba cha dharura. Hivyo wakaturudisha nyumbani na maelekezo ya kutumia Zyprexa na kufika tena hospitalini hapo kumwona daktari wa magonjwa ya watoto wa kituo hicho.

Bado hatufahamu tatizo na Michael ni nini. Kila aina ya ugonjwa wa watoto na mvurugiko wa akili na tiba yake vimejaribiwa, bila mabadiliko, katika mikutano na maofisa walezi wa watoto watukutu, wasimamizi jamii na washauri, na waalimu na watawala wa shule.

A m e k u w a a k i t u m i a mchanganyiko wa dawa za kuzuia kuchanganyikiwa na za kupooza mawazo, mpangilio wa dawa unaotoka Russia kutibu magonjwa ya hulka. Hakuna mabadiliko.

‘Alipokuwa anaingia darasa la saba (ni mwanzo wa elimu ya kati, sekondari) Michael alikubaliwa katika mchepuo wa masomo yaliyoharakishwa kwa watoto wenye vipaji katika hisabati na sayansi. Uwezo wake wa kuelewa ni nje ya kawaida. Akiwa anajisikia vizuri, atakufanya usikilize akiongea chochote, iwe ni habari za Uyunani ya kale au tofauti kati ya fizikia ya Einstein na Newton, au riwaya mashuhuri. Muda mwingi zaidi hali yake ni nzuri. Lakini anapobadilika, chunga sana. Na huwezi kujua ni kitu gani kitamtibua.

Wiki kadhaa baada ya kuingia shule hiyo mpya, Michael alianza kuonyesha hulka ya kushangaza na kutishia watoto shuleni. Tuliamua kumhamisha kuingia mafunzo yenye vizuizi vikali katika wilaya, mazingira ya shule ambako watoto wasioweza kufuata m a d a r a s a y a k a w a i d a wanawekwa katika uangalizi bila malipo kuanzia saa moja na nusu asubuhi hadi saa nane kasoro kumi alasiri Jumatatu hadi Ijumaa hadi wafikie umri wa miaka 18.

Asubuhi hiyo ya ugomvi wa kaptura, Michael aliendelea kubishana na mimi katika gari. Mara anaomba radhi na kuonekana kusikitishwa na a l i chofanya . Kabla hatujaingia katika eneo la

kuegesha magari la shuleni kwake, akasema, “Mama samahani, nasikitika sana, Naweza kutumia michezo ya video baadaye leo?”

“ H a t a k i d o g o , ” ni l imwambia . “Huwezi kufanya ulichofanya asubuhi hii na udhani unaweza kupata zawadi zako za elektroniki mapema kiasi hicho.”

Uso wake ukigeuka baridi, na macho yake yakiwa na hasira iliyopimwa. “Basi nitajiua,” alisema. “Nitaruka nje kutoka katika gari na kujiua.”

Ilitosha. Baada ya kutoa kisu, nilimwambia kuwa kama akisema tena maneno hayo nitampeleka moja kwa moja hospitali ya magonjwa ya akili, bila lakini au labda. Sikumjibu, ila kuingiza gari katika njia mkabala, kugeukia kushoto badala ya kulia.

“Unanipeleka wapi?” aliuliza, akianza kuwa na wasiwasi . “Unakwenda wapi?”

“Unajua tunapokwenda,” nilijibu.

“ H a k u n a ! H u w e z i kunifanya hivyo! Unanipeleka motoni! Unanipeleka motoni moja kwa moja!”

Nilisimamisha gari mbele ya hospitali, nikimpungia kwa nguvu mhudumu mmoja wa kliniki aliyekuwa amesimama nje. “Ita polisi,” nilisema, “Fanya haraka.”

Michael alikuwa sasa chakaramu kabisa, akipiga kelele na kupiga huku na kule. Nilimbana kwa karibu ili asiweze kutoroka kutoka kwenye gari, Alinipiga mara kadhaa na kupiga kiwiko chake katika kufua changu kwa chini. Bado nina nguvu kuliko yeye lakini haitachukua muda.

Polisi walifika haraka na kumbeba mwanangu akipiga kelele na mateke hadi ndani kabisa ya hospitali. Nilianza kutetemeka, na machozi yakaanza kurengarenga machoni wakati najaza fomu - “Kulikuwa na matatizo yoyote kati yako na . . . mwanao ana umri gani ...... kulikuwa na matatizo na....hivi mwanao ameshawahi ku.... mwanao ana....”

Angalau sasa tuna bima ya afya. Hivi karibuni nilikubali kuanza kazi katika chuo kimoja cha karibu, nikaacha kufanya kazi za kujitegemea kwani unapokuwa na mtoto kama huyu, unahitaji mafao. Utafanya lolote kupata

mafao, Hakuna mpango wa bima ambao utakubali kuweka bima ya maisha kwa mazingira hama haya.

K w a s i k u k a d h a a , mwanangu aling’ang’ania kuwa nilikuwa nadanganya - kuwa nilitunga tukio hilo lote ili niweze kumwondoa. Siku ya kwanza, nilipokwenda k u m w o n a , a l i s e m a “Nakuchukia, Na nitajilipiza mara nitakapotoka humu.”

Kufikia siku ya tatu, alikuwa tena mwanangu mtulivu, anayefurahisha, akiomba msamaha na kuahidi kubadilika, Nimesikia ahadi hizo miaka mingi. Siziamini tena hata kidogo.

Katika fomu za kumwingiza m g o n j w a , a n a p o u l i z a , ‘Nini matazamio yako ya tiba?” niliandika “Nahitaji msaada.”

Na ninauhitaji. Tatizo hili ni kubwa mno kulibeba mwenyewe. Mara nyingine hakuna la kufanya dhahiri, Hivyo unatumainia tu hali iwe nzuri na kutazamia kuwa kwa kuangalia ulikotoka, labda maana yake itaeleweka.

Naelezea jambo hili kwa sababu mimi ni mama wa Adam Lanza. Ni mama wa Dylan Klebold na mama wa Eric Harris. Ni mama wa Jason Holmes, Ni mama wa Jared Loughner. Ni mama wa Seung Hui Cho. Na wavulana hawa - na mama zao - wanahitaji msaada. Kufuatia msiba mwingine wa kutisha wa kitaifa, ni rahisi kuzungumzia bunduki. Lakini ni wakati wa kuzungumza kuhusu magonjwa ya akili.

Mother Jones anasema kuwa tangu mwaka 1982, mauaji ya watu wengi kwa kutumia silaha yametokea m a r a 6 1 k o t e n c h i n i . (http://www.motherjones.com/politics/2012/07/mass-shootings-map)

Kati ya hayo, wauaji 43 wal ikuwa wanaume Wazungu, na mmoja tu alikuwa mwanamke. Mama Jones aliangalia kama wauaji walipata bunduki zao kihalali (wengi zaidi walizipata kihalali). Lakini dalili hizi za wazi za ugonjwa wa akili zituwezeshe tuangalie ni watu wangapi nchini Marekani wanaishi kwa woga, kama mimi.

Nilipomuuliza msaidizi wa kijamii wa mwanangu nini naweza kufanya, alisema ambacho tu naweza kufanya n i kupeleka mashi taka

mahakamani. “Akirudishwa k a t i k a m z u n g u k o w a kufungwa, watafuat i l ia nakala za alikopitia,” alisema. “Ndiyo njia pekee ambako u n a w e z a k u h a k i k i s h a kunafanyika lolote. Hakuna atakayekusikiliza labda uwe na mashtaka.”

Siamini kuwa mwanangu a n a f a a k u k a a j e l a . Mkanganyiko wa mazingira unamfanya aharibikiwe z a i d i a k i i n g i l i a n a n a vinavyomsumbua na haugusi chochote katika tatizo la awali. Lakini inaelekea kuwa Marekani inatumia jela kama jawabu la watu wote wenye magonjwa ya akili. Kwa mujibu wa shirika la Human Rights Watch, idadi ya wagonjwa wa akili wanatumikia vifungo iliongezeka mara nne kuanzia 2000 hadi 2006 na inaendelea kuongezeka. Cha ziada, kiwango cha ugonjwa wa akili kwa waliofungwa ni mara tano zaidi (asilimia 56) ukilinganisha na watu walio huru.

(h t tp : / /www.hrw.org/n e w s / 2 0 0 6 / 0 9 / 0 5 / u s -number-mentally-ill-prisons-quadrupled)

Baada ya vituo cha misaada na tiba vya serikali kufungwa, jela ndiyo njia pekee iliyobaki kwa wenye magonjwa ya akili - kisiwa cha Rikers, jela ya Los Angeles County (wilaya), na ile ya Cook jimboni Illinois vilikuwa na vituo vikubwa zaidi vya kutibu wenye magonjwa ya akili mwaka 2011.

( h t t p : / / w w w . n p r .org/2011/09/04/140167676/nations-jails-struggle-with-mentally-ill-prisoners)

H a k u n a a n a y e t a k a kumpeleka mtoto wa miaka 13 mwenye kipaji anayempenda Harry Potter na mkusanyiko wa midoli ya wanyama ya kulalia, jela. Lakini katika jamii yetu, ambayo haitaki kusikia habari za magonjwa ya akili na mparaganyiko katika mfumo wake wa tiba, haitupatii njia nyingine yoyote. Hivyo mgonjwa mwingine anaye teseka moyoni anavamia mgahawa wa ‘\chips-kuku’ anafyatua risasi, au ‘supermarket.’ darasa la chekechea, Na tunakamua mikono yetu tunasema ‘Hii lazima ikomeshwe.’

Nakubaliana kuwa lazima hali hii ikome. Ni mwanzo wa kuanza mazungumzo ya kina, yenye maana, kuhusu magonjwa ya akili. Ndiyo njia pekee ambayo taifa letu linaweza kupona kikamilifu.

Mungu nisaidie. Mungu msaidie Michael. Mungu tusaidie sote.

Mama mwanaharakatiMimi napenda sana

kinanda, wanangu wanne, na michezo ya kubuni ya elekroniki, ingawa siyo kwa mpangilio huo.

Page 8: Gazeti la Alnuur

8 AN-NUURSAFAR 1434, IJUMAA JANUARI 4 - 10, 2013

Makala/Tangazo

Uongozi wa Shule ya Answaar Islamic Model School inawatangazia waislamu wote nafasi za masomo kwa mwaka 2013, kama ifuatavyo.

1. Shule ya awali ( Nursery School) Kg - 1 and Kg 11 Umri kuanzia miaka mitatu na nusu na kuendelea.2. Shule ya msingi ( Primary School) Darasa la kwanza hadi la Sita, kwa wale wanaotaka

kuhamia nafasi pia zipo.ADA: shule ya awali ( Nursery school) 550,000/= kwa mwaka.Shule ya msingi (Primary school).i) Darasa la kwanza hadi la tano ni Tsh. 650,000/=ii) Darasa la sita na la saba Tsh. 750,000/= ada inalipwa kwa awamu tatu.- Shule ipo kinondoni Studio/ karibu na vijana Social Hall

au nyuma ya vijana.- fomu zinapatikana shuleni Kinondoni studio Masjid

Answaar.- Tarehe ya USAILI ni Tarehe 6/01/2013, usaili utafanyika

shuleni Answaar Islamic Model School, Siku ya Kufungua shule ni Tarehe 14/01/2013.

Kwa mawasiliano zaidi piga simu. 0767- 121555,0777-790283, 0712 790283. Au Email [email protected] au tembelea Tovuti yetu: www.answaarislamic.co.tz

Mlete mwanao apate elimu na malezi bora ya Kiislamu

ANSWAAR ISLAMIC MODEL SCHOOL

HABARI za Musa si ngeni kwa wanaosoma vitabu vya historia na vya dini. Musa alikuwa muongozi wa wana wa Israil. Mheshimiwa Firauni, aliwakilisha tawala za kidikteta. Namwita mheshimiwa kwa makusudi kwa sababu ndiyo wanavyopenda kujiita watu hawa (watawala).

Hawajuwi kwamba mtu huwa mheshimiwa kwa kujiheshimu.

F i r a u n i a n a w a k i l i s h a tawala mbalimbali za kidikteta zinazoendesha serikali kwa mabavu na ukandamizaji, kama vile kuwaonea wananchi, kuwabana na kuwadhulumu wananchi kwa maslahi binafsi ya mtawala na kikundi kidogo kinacho muunga mkono.

K i b a y a z a i d i , t a w a l a zinazoongozwa Kifirauni huwa hazijali raia na mara nyingi hutatua matatizo kwa kutumia rungu la dola ambalo huchukua nafasi ya majadiliano.

Wingi wa matukio katika kisa cha Musa, unatufanya tuweze kutafakari masuala ya msingi, ambayo Wazanzibari tunaweza kujifunza na kuyaangalia kama kioo cha kujitazamia, ili penye kuharibika tujue na kutafuta namna ya kurekebisha.

Matukio ya kisa hicho yatufae kwa lengo la kuendeleza umoja na ustawi wa jamii yetu. Kuja kwa Musa kulisaidia kuchochea na kuamsha ari ya mapambano dhidi ya maovu. Mifumo ya kidikteta bado ingalipo na watawala kama Firauni bado wapo, wakila kuku chini ya ulinzi mkali unaogharimiwa na walipa kodi.

Na wananchi walala hoi bado wapo kwa wingi katika maeneo mbalimbali ya nchi, wakiendelea kutaabika na kusulubika katika hali ya uonevu, dhiki na kukata tamaa. Maskini hawa, hakuna wa kuwahurumia.

Tujiulize, Musa aliwezaje kuwa hodari mpaka kushinda vita dhidi ya unyanyasaji, dhulma, ufisadi na maonevu?

Huku tukio kubwa kabisa likiwa ni kumshinda mungu – mtu Firauni, mtawala aliyejaa kiburi, aliyetisha na kuogopwa na kujizolea umaarufu kwa watu wake kama jemedari wa vita asiye shindwa.

Bila shaka siri ya Mussa kushinda dhulima, unyanyasaji na utesaji wa Firauni ilikua ni kumuogopa Mola wake peke yake. Mola wake naye akavifanya vitu vyote vilivyokuwa juu ya uso wa ardhi vimuogope Musa na wale wote wasio muogopa Mola. Walifanywa waviogope

Na Ibrahim Mohammed Hussein

Zanzibar bado inamuhitaji Musa atayetuonesha mchawivitu vyote juu ya ardhi.

Mussa mwana demokrasia, anaufundisha u l imwengu uelewe kwamba, utawala ni dhamana inayohitaji uadilifu, na sehemu kubwa katika uadilifu ni ushirikishwaji wa kila mmoja kwa nafasi ya ufahamu, utaalamu alionao.

I l i kuya f ik i a ma lengo yake kwa ufanisi anaamua kupendekeza ndugu yake Haruni, amsaidie katika ukalimani na kazi nyingine za ushauri.

Kisa cha Musa kinafundisha kwamba, kupitia utaratibu wa sheria pekee ndio unaweza kuwasimamisha watu katika uadilifu, hisia za kupendana na kusaidiana, kutumainiana na kushikamana. Aliwafundisha wana wa Israil kufanya kazi kwa bidii kama njia moja wapo ya kujenga taifa imara.

Funzo jengine tunalolipata katika kisa cha Musa ni kwamba katika mapambano dhidi ya udikteta, si laha kubwa ni ujasiri, mbinu, ukakamavu na uwerevu. Hekima aliyopewa Musa na Mola wake, ilishinda vita vya nyoka wa Firauni walioongozwa na baraza la wachawi, akaipiga Bahari ya Sham kwenda ng’ambo ya pili.

Mussa aliongoza mapambano katika haki na kuyazamisha maovu na waovu baharini.

Jambo hili tumelikosa hapa kwetu licha kuwepo mamia, kama sio maelfu ya wasomi tulionao. Wasomi wetu wamefanya nini kuonesha kwamba wapo na wanajali masilahi ya watu wa nchi hii?

V i o n g o z i w e n g i wameshindwa kuifaa jamii, wamebaki silolote wala chochote zaidi ya kufurahikia maslahi baada ya kuwakamua wanyonge na kuhodhi rasilmali za nchi.

Wamebaki kimya bila ya kukemea ubeberu unaendeshwa na baadhi ya viongozi wasio pendelea umoja na utulivu wa nchi hii. Viongozi wameweka pamba maskioni, hawataki kusikia kilio na matakwa yenye nguvu za hoja kutoka kwa wenye nchi.

W a n a n c h i w a n a d a i kuonyeshwa mkataba wa Muungano ili wapate kuandika katiba mpya. Serikali haikuona umuhimu wowote juu ya mkataba huo. Wao wamesimamia Sera ya CCM Serikali mbili. Kwa mkataba gani huo?

Vipi utaiandika katiba wakati hujawahi kuona mkataba wenyewe? Kipi kilichokupa imani kwamba mkataba umeeleza nini na kwa makubaliano gani au kwa muda gani?

Ni sahihi kabisa kukataa Muungano wa katiba wakati m k a t a b a w a m u u n g a n o hapana aliyeuona. Hapa ndipo niliposema Zanzibar inahitaji Musa atakayetuonyesha mchawi, akiitoa nchi bila ya mkataba, na kama ilitolewa kwa mkataba, uko wapo?

Kwa nini walazimishwe wananchi waandike katiba huku wakikataliwa madai yao

ya kutaka kuonyeshwa mkataba? Bila ya kuoneshwa mkataba ni vigumu kuota tunakoelekea. Nchi inaendeshwa kwa matakwa ya watawala tulio nao.

Viongozi wanaongozwa na utashi wa matamanio ya nafsi au ubinafsi katika kutumikia umma. Wanaosinzia Bungeni na kwenye vikao muhimu vya maamuzi katu hawatoweza kuikomboa Zanzibar kiuchumi.

Zanzibar inamuhitaji Musa atakayeonyesha wachawi na kuwashinda, Musa atakayekuwa tayari kusikiliza na kupokea maoni na ushauri, atakayesikia na kufanyia kazi malalamiko ya wananchi wake.

Mheshimiwa Jaji Joseph Warioba, aliwahi kukizindua kitabu cha ‘TUTAFIKA’ Mei 2003. Kitabu hicho kilitoa nadharia ya kumezwa kwa Zanzibar na kuwa jimbo la Mashariki (Eastern Province), k a t i k a m f u m o m p y a w a Kiserikali wa Tanzania .

Hayo ni mawazo na mtizamo wa yaliyomo katika kitabu hicho, ambacho ndio kimetoa nadharia hiyo katika kile kinachoelezwa kama, kuitazama Tanzania katika kipindi cha miaka 20 ijayo . Kitabu hichi kilichapishwa na Tanzania Printers Limited (2003).

Kitabu hicho kina azma ya kuitayarisha Tanzania juu ya matokeo ya baadae, ili iweze kuwa ni kinga ya matukio ya ghafla katika maeneo ya

kiuchumi, kijamii na kisiasa. Kitabu hicho kimegawanywa katika maeneo makuu matatu, nayo ni ya ‘Yale Yale’ ‘Mibaka Uchumi’ na ‘Amka Kumekucha’ .

Katika twasira ndogo ya ‘Ya le Ya le ’ i nae lezewa namna ambavyo Watanzania walivyokata tamaa na kutoamini kuwa, nchi inaweza kubadilika na kushindwa kuwashirikisha vijana juu ya kuchukua nafasi yao kujitengenezea khatima yao na ya nchi.

Katika ‘Mibaka Uchumi’ kinachoelezewa ni juu ya uchumi utayokuwa umeshikiliwa na mapapa makubwa ya ndani na nje huku rushwa ikiwa imetawala kabisa, wafadhili kuwa na sauti kupita kiasi hata kuamua kutoa maamuzi ya kila aina ndani ya nchi.

Kwenye ‘Amka Kumekucha’ ni taswira ambayo inaonyesha namna ambavyo Tanzania ya kesho itakavyokuwa, na hapo ndipo inapoonekana kuwa kutakuwa na matatizo ya kisiasa yatakayoanzia na suala la rushwa, mgawanyo wa madaraka na kuwepo tishio la kupasuka kwa Chama Cha Mapinduzi ( CCM) .

Twasira hiyo inasema, hapo ndipo ambapo kutakuwa na shinikizo kubwa ambazo zitasababisha kwa mara ya kwanza, Tanzania kuitisha

kura ya maoni (Referendum) na majadiliano makali ya kitaifa yatafwata. Kinaeleza kuwa kubwa litakalokua katika mada ni kuundwa kwa Serikali ya Shirikisho la Jamuhuri ya Tanzania.

Waandaj i wa twasira h iyo wanasema, hapo ndipo muundo wa shirikisho utakapokuwa tayar i na Tanzania itakuwa na majimbo matano yakiwa ni Kusini, Kati, Kaskazini, Magharibi na jimbo la Mashariki, ambalo litakuwa na mikoa ya sasa ya Tanga Lindi, Dar es Salaam na Zanzibar yenyewe.

Kitabu hicho cha ‘Tutafika’ a m b a c h o k i l i t o l e w a bure, ni dhihirisho kuwa tayari mikakati imeanza kuandaliwa, ili kujenga njia ya makusudi kuelekea katika lengo la kuwa na mabadiliko makubwa . Mabad i l i ko yatakayojumuisha pamoja na mambo mengine, suala la Zanzibar inachukuliwa yote ndani ya Tanganyika ya sasa.

Wenzetu wamo katika kulikamilisha lengo la kuichukua Zanzibar milele na milele.

Zanzibar inahitaji Musa aliye Mzanzibar aliyerithi damu ya uzalendo toka tumboni kwa mama yake. Vyenginevyo, tusije kuusaidia mpango wao kupitia sera ya CCM mwishowe ikawa ni vilio.

0715 - 498363

Page 9: Gazeti la Alnuur

9 AN-NUURSAFAR 1434, IJUMAA JANUARI 4 - 10, 2013Makala

DESEMBA 25 mwaka 2012, Maaskofu wa makanisa takriban yote hapa nchini, walitoa maneno mazito ya vitisho, kejeli na vijembe kupitia ibada zao za Krismasi dhidi ya Serikali ya Tanzania na Waislamu. Maneno hayo kimsingi yametokana na maazimio ya kikao cha nne cha Jukwaa la Wakristo Tanzania TCF, kilichoketi Desemba 6 mwaka 2012, Kurasini jijini Dar es salaam.

Ukisoma tamko la Maaskofu kwa makini, kimsingi hakuna hoja yoyote ya maana inayoweza kudumisha amani ya Watanzania. Kwa sababu amani haijengwi kwa kufumbia macho dhulma. Waislamu kwa muda mrefu wamekuwa wakilalamikia dhulma wanazofanyiwa na mfumo usio rasmi serikalini, ambao unawapendelea Wakristo. Waislamu wamekuwa wakitoa ushahidi wa kihistoria, kisayansi, kimazingira na hata kitakwimu kuhusu dhulma hizo.

Lakini k ichekesho cha mwaka, zaidi ya Maaskofu 35 wanakutana jijini Dar es salaam, wanajadiliana kisha wanaona watoke na vitisho, kejeli na vijembe dhidi ya Waislamu na Serikali, badala ya kuleta hoja za msingi zitakazolinusuru taifa na hatari za upendeleo wa kidini, unaofanywa na mawakala wa kanisa serikalini!

Ta m k o l a M a a s k o f u limeonyesha hofu kwamba Waislamu wameshagundua dhulma wanazofanyiwa. Na anayewadhulumu pia wanamjua. Sasa Maaskofu wanajaribu kuficha uhal ifu wao kwa kutumia vitisho, propaganda, porojo na vijembe. Hiyo ni namna ya kujihamu tu (Defence Mechanism).

Siyo lengo langu hasa kujibu tamko la Maaskofu kupitia maka la h i i . Kwa sababu tamko lenyewe, kwa kiasi kikubwa, halikuzingatia ukweli wala uhalisia wa mambo, na limesimamia zaidi kwenye propaganda na porojo. Ni sawa na maneno ya kwenye khanga!

Wanataka kuchora picha potofu kwenye jamii kwamba Wakristo nchini Tanzania wanaonewa sana na Waislamu! Makanisa yao yanachomwa, wakati serikali ikiaangalia tu! Wanajaribu kupandikiza fikra potofu kwenye jamii kwamba Wakristo ndiyo watu wa amani na Waislamu ni watu wa vurugu! Wanadhani wanaweza kugeuza ukweli kuwa uongo na uongo kuwa ukweli!

Ni ukwel i us iopingika kwamba Waislamu wa Tanzania wamedhulumiwa na Mfumo Kristo ulioasisiwa na baba wa taifa. Ukweli huu kamwe hautakuwa uongo kwa sababu

Hongera Waislamu, Maaskofu wanagwaya!Na Said Rajab.

ya propaganda na porojo za Maaskofu. Na tatizo hili lisiposhughulikiwa kwa dhati, lazima litaleta maafa huko mbele. Waislamu wanapigania haki yao i l iyodhulumiwa na katika hili, wanaonekana hawamuogopi yeyote. Hilo Maaskofu walifahamu vizuri sana.

Nawapongeza sana Waislamu wa Tanzania kwa juhudi zao za muda mrefu za kubainisha d h u l m a w a n a z o f a n y i w a na Mfumo Kristo, ambazo pamoja na kupuuzwa, lakini sasa zimeanza kuzaa matunda. Harakati za Waislamu za miaka mingi za kupigania haki yao iliyoporwa na mawakala wa kanisa serikalini, haziwezi kuishia hewani. Maaskofu wameliona hilo na bila shaka hofu yao ni kwa sababu Waislamu wameshagundua ubaya wao.

Ki tendo cha Maaskofu kushindwa kujibu hoja za Waislamu kuhusu dhulma za Mfumo Kristo, na badala yake kuleta porojo za kuhamisha ajenda, ni ushindi mkubwa kwa hoja za Waislamu. Tafsiri yake ni kwamba Maaskofu hawana la kusema kuhusu ukweli wa madai ya Waislamu. Mwanzoni

waliamua kuwapuuza Waislamu, wakidhani madai yao yangejifia yenyewe kifo cha kawaida.

Lakini wal iposhuhudia wanavyoendelea kusimama kidete kupaza sauti zao, sasa wameanza kutoa maazimio ya woga kuf icha uhal i fu uliofanyika. Wanataka kuzima sauti za wanaokandamizwa na hilo kamwe halitawezekana. Wanafanana na Maquraysh wa Makka, ambao walidhani wangeweza kuzuia ujumbe wa Qur’an kwa kuwakataza watu wasiisikilize:

‘Na walisema waliokufuru: “ M s i s i k i l i z e Q u r ’ a n h i i inaposomwa na ipigieni makelele isomwapo, huenda mkashinda” Qur 41:26.

Lakini jambo la kuzingatia, kama vile Maqurayshi wa Makkah, ambao hawakuwa na uwezo wa kupambana na Qur’an kwa hoja za kiakili, Maaskofu wa Tanzania nao hawana uwezo wa kupambanisha hoja na Waislamu. Vurugu zao zote dhidi ya Waislamu siyo za kifikra, zaidi ni propaganda na porojo za kuficha ukweli!

Lugha zao zimejaa chuki na fitna dhidi ya Waislamu. Kila mnapotaka kujadiliana

kwa haki, kitaalamu, kisomi na kiuadilifu, hawako tayari na zaidi wataendelea kutoa m a e l e k e z o n a m a s h t a k a serikalini. (Uchonganishi).

M f a n o h a l i s i w a h i l o ulishawahi kutokea hapa nchini, wakati Rais Ali Hassan Mwinyi alipowakutanisha Masheikh na Maaskofu Ikulu jijini Dar es salaam, kuzungumzia tatizo la mihadhara ya kashfa. Maaskofu wa l i kuwa wak i l a l amika , waki ibana Ser ika l i ip ige m a r u f u k u m i h a d h a r a y a Waislamu waliyodai kuwa inakashifu Ukristo. Waislamu kwa upande wao, walipinga dai la Maaskofu, wakileta hoja kwamba hawakashifu Ukristo, bali wanaelimisha watu kwa kutumia maandiko matakatifu.

Busara za Mzee Mwinyi z i k a m u e l e k e z a k u w a i t a Wahadh i r i wa Ki i s l amu, w a n a o d a i w a k u u k a s h i f u Ukristo upande mmoja, na Maaskofu wanaolalamika upande mwingine, ili kujadiliana kidugu, kiuadilifu na kitaalamu, lengo likiwa kubaini ukweli ili kuondoa mgogoro uliojitokeza.

Maaskofu hawakuwa tayari kudhihirisha! Hawakuwa na hoja zinazothibiti na kwa bahati pale propaganda haikuwa na nafasi. Matokeo yake malengo ya mkutano ule hayakufikiwa. Hawakurudi tena Ikulu kusaka muafaka hadi Mzee Mwinyi alipostaafu!

Tizama, lakini angalia, alipoingia Rais Mwingine Ikulu, waliendesha kampeni zile zile za propaganda ya ‘mihadhara ya kashfa’ kupitia vyombo vya habari, na matokeo yake Serikali ikaenda kuua Waislamu wasio na hatia pale Msikiti wa Mwembechai mwaka 1998.

Wa i s l a m u w a l i u a w a Mwembechai kwa sababu tu ya chuki, fitina, propaganda, porojo na ulaghai wa Maaskofu.

Wa i s l amu wa l ipo i t aka Serikali kuunda Tume ya uchunguzi wa mauaj i ya Mwembechai, ili kubaini ukweli wake, Rais Benjamin Mkapa alisema “hajaona haja na hoja” ya kuunda Tume hiyo. Hivyo ndivyo walivyo.

Lakini Prof. Hamza Njozi, alipoandika kitabu kubainisha u k w e l i w a M a u a j i y a Mwembechai, ili Ulimwengu ufahamu kilichotokea, Serikali ya yule yule, ambaye “hakuona haja na hoja” ya kuunda Tume ya uchunguzi akapiga kukipiga marufuku kusambazwa kitabu hicho nchini! Hawasemi ukweli, lakini pia hawataki hata watu wengine waseme ukweli huo! Hivyo ndivyo walivyo!

Siyo s ifa ya Maaskofu kulinda na kudumisha amani.

Sifa kubwa ya Maaskofu imekuwa ni kudumaza akili za watu ili waweze kutawaliwa au kudhulumiwa. Sote tunafahamu jinsi Kanisa lilivyotumika kuingiza ukoloni barani Afrika. Wamissionari wa Kikristo (Mapadri na Maaskofu) ndiyo waliopalilia Ukoloni Afrika.

Alipata kusema Askofu Desmond Tutu wa Afrika Kusini, jinsi wakoloni walivyotumia kanisa kuingia nchini mwake: “Walipokuja sisi tulikuwa na ardhi na wao walikuwa na Biblia, tulipogutuka tukajikuta tumebaki na Biblia na wao wamebaki na ardhi”.

Maaskofu hawatasema ukweli kwamba Makanisa nchini Tanganyika yaliikataa TANU; mara mbili mwaka 1958 mjini Sumbawanga na mwaka 1965 mjini Mbulu. Makanisa yalikuwa yakifanya kazi kwa karibu sana na Serikali ya kikoloni, ambayo ndiyo iliyomlea Mwalimu Nyerere, ili aje kuwa Rais wa kwanza wa Tanganyika baada ya Waingereza kuondoka.

Baada ya uhuru kupatikana, nchi ikiwa chini ya uongozi wa Mwal imu Nyerere , Wakr i s to wa Tanzan ia wanavuna kile ambacho hawakupanda. Wanafurahia matunda ya uhuru kila sekta kutokana na Mfumo Kristo ulioasisiwa na Mwalimu Nyerere, akiungwa mkono na mataifa ya Magharibi. Leo wanataka kuaminisha watu kuwa wao ndio wazalendo zaidi kuliko Waislamu!

Maaskofu wanaeneza propaganda za sumu kwamba Waislamu wanahatarisha a m a n i n a u m o j a w a Watanzania, licha ya ukweli kwamba amani na umoja huo imekuwa ikitunzwa na Waislamu, tangu kipindi cha harakati za kupigania uhuru na baada ya uhuru kupatikana.

Inajulikana vizuri kwamba, u k i w a o n d o a m a r e h e m u Hassan bin Amir na Sheikh Zubeir Mtemvu, Waislamu wa Tanganyika walikataa kukiunga mkono chama chao wenyewe cha ‘All-Muslim National Union of Tanganyika’ (AMNUT), ili kulinda umoja wa kitaifa chini ya TANU, ambacho Rais wake alikuwa Nyerere, Mkatoliki.

Lakini hali inavyoonekana, Maaskofu wamejiandaa kuleta macha fuko makubwa ya kidini hapa nchini, ili wapate kizingizio cha kuwachinja Waislamu wanaopigania haki zao, kwa kutumia mawakala wao serikalini.

Lakini Waislamu hawana sababu hata moja ya kupigana vita isiyo na macho, ambayo nadhani Maaskofu wanaitafuta kwa udi na uvumba hapa Tanzania.

Ila katika mapambano ya kupigania haki, Waislamu hawarudi nyuma na wako tayari.

ASKOFU Laizer

Page 10: Gazeti la Alnuur

10 AN-NUURSAFAR 1434, IJUMAA JANUARI 4 - 10, 2013Habari/Tamgazp

RAIS Mstaafu wa awamu ya pili, Alh-haji Ali Hassan M w i n y i , a m e w a t a k a Waislamu kushughulika zaidi na utafutaji wa elimu kwani kufanya hivyo ndio siri kubwa ya kupata maendeleo ya jamii nzima na taifa kwa ujumla.

Alhaji Mwinyi, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kongamano hilo, aliyasema hayo al ipokuwa aki toa nasaha zake kwa Waislamu waliohudhuria kongamano la Kuzaliwa Mtume Muhammad (S.a.w) lililofanyika Lushoto Jijini Tanga.

Amesema kuwa, jambo lolote haliwezi kufanikiwa bila kuwa na elimu nalo, hivyo aliwataka Waislamu kujikita katika kutafuta elimu na kutoa elimu ili kuweza kuleta maendeleo ya Taifa kwa ujumla.

Aliongeza kuwa Uislamu haukutenganisha elimu, hivyo ni vyema Waislamu wakatoa kipaumbele kwa masomo yote, ili kuweza kuandaa Waislamu walio na maadili mema na wenye uelewa wa dini yao.

A i d h a a m e w a t a k a Waislamu kutambua kua elimu ndio siri ya maendeleo kwa taifa na dunia nzima, na ndio maana elimu katika Uislamu imefanywa kuwa jambo la lazima, kama ambavyo Mtume Muhammad

Lushoto wafanya kongamano kubwa la WaislamuNa Mwandishi Wetu (s.a.w) aliposhushiwa aya

ya kwanza ya kusoma na wala hakuainishiwa kitu gani asome.

Naye mwanachuoni mkubwa kutoka nchini Kenya, Sheikh Sharifu Ahmad Al- Badawi, ambaye alikuwa miongoni mwa w a n a c h u o n i w a k u b w a waliohudhuria kongamano hilo, alipokuwa akiwasilisha mada yake aliwataka Waislam kuwafundisha watoto kuijua vema Qur’an na kuihifadhi kwa ufasaha, ili kuwa na kizazi bora chenye kumhofu Mola pamoja na kumjua m w e n y e z i M u n g u n a kuitumikia dunia yao kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu.

Amewataka wazazi na walezi kuhakikisha kuwa watoto wao wanasoma sawasawa na walimu wao nao wana utaalamu na uelewa mkubwa wa masomo wanayofundisha ili watoto wapate elimu sahihi.

K w a u p a n d e w a k e , Mkurugenz i wa Ki tuo cha Kiislamu cha Markaz Chang’ombe, Jijini Dar es Salaam Dk. Ossama M a h a m o u d I s m a i l i , amewakumbusha Waislam kufuata yale yote aliyoyafanya Mtume (s.a.w).

Aidha wanapoazimisha mazazi ya Mtume (S.A.W) iwe ni moja ya njia za kuhuisha upendo uadilifu na msamaha wa Kiislam, na

kwa kufanya hivyo itakuwa ni sawa na kuiga tabia za Mtume (S.A.W) juu ya uadilifu wake, upole na msamaha aliokuwa akiwasamehe wale waliokuwa wakimkosea.

Sheikh Osama, alisema kuwa kumbukumbu ya Mazazi ya Mtume yanayofanyika kila mwaka, yawe na athari kwa Waislamu ili kuthibitisha matunda ya kujifunza na k u m f u a t a M t u m e k w a vitendo.

Al i sema mafundisho yanayopa t ikana ka t ika historia ya Mtume, hayawezi k u p a t i k a n a k a m a m t u atakuwa hajausoma Uislamu na Qur an, historia ( Sira ya Mtume) na hadithi za Mtume Muhammad (s.a.w).

Naye Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, a m e k u m b u s h a j u u y a Waislamu kuyafanyia kazi yote yaliyoongelewa katika Kongamano hilo. Aidha alitoa

pongezi zake za dhati kwa Sharifu Hussein Al-Badawi, kwa juhudi zake kubwa za kuendeleza dini ya Mwenyezi Mungu na kuitetea.

K o n g a m a n o h i l o l i l ifanyika Desemba 2 mwaka huu Wilayani Lushoto Tanga na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini na kisiasa, pamoja na mamia ya Waislamu kutoka Lushoto na vijiji vya jirani.

RAIS Mstaafu wa awamu ya pili, Alh-haji Ali Hassan Mwinyi (wanne kutoka kulia) akiwa katika kongamano la Waislamu Lushoto, mkoani Tanga. Watatu kulia ni Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Amir Kificho, kushoto kwake ni Sheikh Alhad Musa.Wa kwanza kulia ni Sheikh Ismail Osama, Mkurugenzi wa chuo cha Markaz Chang'ombe

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, amesema wananch i wanah i ta j i kuelimishwa zaidi juu ya uhifadhi wa mazingira ili kuweza kuyalinda na kuepuka kuyachafua.

Amesema uchafuzi wa mazingira mara nyingi umekuwa ukisababishwa na wananchi wenyewe, jambo ambalo linapaswa kupigwa vita kwa wananchi hao kupatiwa elimu ya sahihi mazingira i l i kuepusha uharibifu huo.

Maalim Seif alisema hayo wakati akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Bi. Chiku Galawa, mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Tanga

Maalim Seif asisitiza elimu ya kuhifadhi mazingiraNa Mwandishi Wetu,

Tangakwa ziara ya siku mbili.

Amesema iwapo wananchi wataelimishwa ipasavyo kuhusu umuhimu na faida za kuhifadhi mazingira, wataweza kujiepusha na uharibifu, hasa ukataji wa miti kiholela bila ya kuzingatia athari za kimazingira.

Naye Mkuu wa Mkoa w a Ta n g a , B i . C h i k u Galawa, alisema uharibifu wa mazingira ni moja kati ya changamoto kubwa zinazoukabili mkoa huo, jambo ambalo linarejesha n y u m a m a e n d e l e o y a kiuchumi katika mkoa.

Alisema serikali ya mkoa inatafuta njia mbadala ya kutumia nishati nyingine ili kupunguza matumizi ya kuni na mkaa, ambayo yanachangia zaidi ukataji wa miti kiholela.

“Iwapo serikali itazuia matumizi ya mkaa na kuni,

serikali na wananchi watapata nafasi ya kufikiria nishati mbadala ya kutumia kwa ajili ya kupikia. Lakini tukiendelea kutumia kuni, mawazo yetu yatabakia hapo hapo tu na tutaendelea kutumia kuni kila siku”, alisema Bi. Galawa.

Mkuu huyo wa mkoa abainisha kuwa, ukataji miti kiholela mkoani humo, umekuwa ukichangia kuwepo kwa athari za mabadiliko ya tabianchi, yanayosababisha upungufu wa mvua pamoja na kuongezeka kwa hali ya joto.

Hata hivyo Bi. Galawa alisema mkoa huo umepiga hatua kimaendeleo, ikiwa ni pamoja na kuimarika kwa miundombinu ya barabara.

Akiwa Mkoani Tanga, Maalim Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF anatarajiwa

kuhutubia mikutano mitatu ya hadhara katika viwanja

vya Tangamano, Kwadiboma Sokoni na Handeni.

Masjid Muzdalifa Mbezi kwa Yusufu inawashukuru waislamu wote waliofanikisha ujenzi wa msikiti kufikia mahala hapa ulipofikia. Lakini pamoja na shukrani hizo bado tunaomba msada kwa waislamu wenye moyo wa kujitolea waendelee kutusaidia ili tukamilishe ulipobakia kwa uwezo wa Allah Inshaalah.

Kwa yeyote mwenye kutaka kuchangia chochote ulicho nacho wasiliana nasi kwa namba hizi 0717 649313/ 0713 673216/ 0715 874127 au 0657 531367 au unaweza kufika katika msikitini.

Page 11: Gazeti la Alnuur

11 AN-NUURSAFAR 1434, IJUMAA JANUARI 4 - 10, 2013Makala/Habari

S H U K U R A N I z o t e anas tah ik i Mwenyez i Mungu, na inatosha na rehema na amani ziwafikie waja wa Mwenyezi Mungu ambao amewachagua.

Baada ya utangulizi huo, miongoni mwa vyanzo ambavyo vimechungwa sana na Uislamu ni upande wa hukumu za kisheria, Juu ya wepesi na kuondoa ugumu na kutatua mambo katika dini, na miongoni mwa mambo magumu ambayo yamefahamika katika baadhi ya dini zilizopita.

M w e n y e z i M u n g u amewafundisha waumini kumuomba yeye. “Ewe Mola wetu, usitubebeshe t u s i y o y a w e z a k a m a

Wepesi wa hukumu za kisheria

Na Sheikh Abubakar Selemani

ul ivyowabebesha wale waliokuwa kabla yetu”. Surat Bakara, aya ya 286. Na Magumu ni yale yaliyo mazito.

Kuyafikiria yaliyokuwa kabla yetu miongoni mwa sheria zil izopita katika hukumu ngumu. Umma huu umepunguziwa kwa kuondolewa magumu mengi yaliyokuwepo, nayo ni bahati kubwa.

Kwani hakuna dini yoyote ikiwa hakuna kumuabudu Mungu. Lakini dini zilizopita kwa upande wa wafuasi wake, ilikuwa inawaamrisha kuukera mwili na kuuadhibu. Na malengo yaliyokuwa kwa waumini wake ni kujiumiza katika mwili. Na mwili unapozidi maumivu yake inakuwa ndio kujisafisha roho yake na kuosha nafsi.

Imekuja sheria ya Kiislam ili kuondoa mambo hayo magumu, na amejulishwa Mtume (saw) juu ya mambo hayo katika vitabu vya watu wa mwanzo, ambayo ni tofauti (Anawaamrisha mema na kuwakataza maovu, na kuwahalalishia yalio mazuri na kuwakataza wao mabaya na kuwaondolea magumu). Surat Aaraf, aya ya 157.

Amej is i fu Mwenyezi

Mungu juu ya Mtume wake kwa watu akasema, “Kwa hakika amekuja kwenu Mtume kutokana na nyinyi, anaathirika na yale mlionayo, mwenye pupa na mambo yenu waumini, ni mpole mwenye huruma). Surat Tauba, aya ya 128.

Amesema Mtume (S.A.W) “nimeletwa kwa dini nyepesi yenye msamaha”. Dini hii ni nyepesi katika imani, ni nyepesi katika maamrisho yake na hukumu. Na Mwenyezi Mungu ameuhusisha umma huu na msamaha na uwepesi kwa sababu ni hukumu na ujumbe wa watu wote. Na kwa dunia nzima na kwa nyakati zote.

Na ujumbe huu kwa kuwa ni kwa ajili ya watu wote na ni wa kudumu, hapana budi aufanye Mwenyezi Mungu mwenye hekima k a t i k a h u k u m u z a k e , uwepesi na urahisi na upole unaokubaliana na watu na zama hizi na mahitaji yake.

Na haya yapo wazi katika hukumu za kisheria peke yake. Amesema Mwenyezi Mungu mtukufu, “Enyi ambao mlioamini, rukuuni na sujuduni na muabuduni Mola wenu na fanyeni kheri kwa hakika mtafaulu, na piganeni

jihadi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, ubora wa jihadi yeye amewateuweni nyinyi. Na hakufanya Mwenyezi Mungu kwenu katika dini ugumu) Surat al-Haji, aya ya 77 hadi 78.

Na anasema mwishoni mwa aya ya Udhu, “Hataki Mwenyezi kuweka uzito na ugumu kwenu. Lakini anataka mjisafishe na atimize neema zake kwenu, ili mpate kushukuru” Surat Maida, aya ya 6.

Na anasema mwisho wa aya ya Funga, “Anataka Mwenyezi Mungu kwenu uwepesi na wala hataki kwenu uzito”. Surat Al-Bakarat, aya ya 185.

“Ana taka Mwenyez i Mungu kuwafanyia wepesi na ameumbwa binadamu ni dhaifu” Surat Nnisai, aya 28.

Na amewatuma Mtume (S.A.W) Muadhina Aba Mussa Al-Ashariyi, wakawe viongozi nchini Yemen ikiwa ni miongoni mwa usia wake Mtume kwao. (Wafanyieni wepesi na wala msitie uzito, na wabashirieni na wala msiwagawe, na mkubaliane na wala msitofautiane).

Na miongoni mwa sifa zake Mtume (S.A.W), alikuwa

hapewi mambo ya kuchagua isipokuwa huchagua lililo jepesi zaidi likiwa halina makosa (madhambi). Na miongoni mwa maneno yake Mtume (S.A.W) ni kuwa, “Dini hii ni nyepesi na wala hatoitia ugumu yeyote isipokuwa itamshinda. Basi jisogezeni katika mema. Na ikiwa muongozo wa Uislam ni uwepesi katika hukumu za kisheria na Muislamu yeyote atakayeweka uzito na ugumu atakuwa ametoka nje ya dini ya Kiislam”.

Na kwa hivyo ndipo aliposimama Mtume Mtukufu m b e l e y a w a n a o w e k a ugumu katika Uislamu na akawaambia juu ya kuangamia kwao na ubaya wa mambo yao akasema, “Zindukeni na jueni kuwa wameangamia wenye kuitia uzito dini”.

Amesema hivi mara tatu. Na hakuwa mwenye kurudia maneno isipokuwa kwa ubora wa maneno hayo na hatari ya madhumuni yake.

Amepokea Bin Abbas (R.A) kutoka kwa Mtume, “Jiepusheni na kuongeza mambo katika dini kwani wameangamia waliopita kabla yenu kwa kuongeza vitu katika dini”.

Dini ambayo imejazwa Qur-ani kwa waliopewa na amesema Mwenyezi Mungu mtukufu, “Sema enyi mliopewa kitabu msiongeze katika dini yenu ya haki, na wala msifuate matamanio ya watu waliopotea kabla na wakawapoteza wengi na wakapotea katika njia iliyonyooka”. Surat Mainda, aya ya 77.

Amepokea Abu Daudi toka kwa Sahali Bin Abii Umma kwamba, ameingia yeye na baba yake kwa Anasi, wakati wa uongozi wa Omari Bin Abul-Azizi, naye akiwa Amiri wao, naye alikuwa akiswali swala nyepesi kwa muda wa dakika moja, ni kama swala ya msafiri au inakaribiana na hiyo na alipotoa salamu akaniambia, hakika Mtume (S.A.W) alikuwa anasema “Msitie ugumu wenyewe ili asije kuweka ugumu kwenu Mwenyezi Mungu, kwani wapo watu walitia ugumu wenyewe Mwenyezi Mungu akawawekea ugumu kwao”.

Hilo ndilo lililobakia katika nyumba zao za ibada na viongozi wao wakajizushia na wala hatukuwalazimisha sisi wao.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu ajaalie tuwe wenye kuyajua mambo na kuyafanyia kazi na kuyafundisha wengine na wayafuate kwa ubora zaidi na wayakubali.

ZAIDI ya vijana 2000 walioathirika na matumizi ya dawa za kulevya Zanzibar wamepatiwa huduma ya kuwawezesha kuacha matumizi ya dawa hizo, ambapo zaidi ya vijana 400 wameweza kuacha kabisa matumizi ya dawa hizo na wanaendelea na harakati zao za kimaendeleo.

Hayo yameelezwa na Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maal im S e i f u S h a r i f H a m a d , Jumapili iliyopita wakati akizindua Tume ya Kitaifa ya Kuratibu na Kudhibiti wa Dawa za Kulevya, katika hafla iliyofanyika Jumba la Wananchi Forodhani.

Tume hiyo imeanzishwa kufuatia mabadiliko ya sheria namba 12 ya mwaka 2011, juu ya udhibiti wa dawa za kulevya, ambayo kwa sasa inatoa mamlaka kamili ya kisheria katika mambano dhidi ya dawa za kulevya

Vijana 2000 wapatiwa matibabu dawa za kulevya Z’barZaidi ya 400 waacha kabisa Na Mwandishi Wetu,

Zanzibar

nchini.Ser ikal i ya Zanzibar

imeamua kuandaa programu mbalimbali kwa ajili ya kudhibiti matumizi ya dawa za kulevya, chini ya ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa huduma za nyumba za kurekebisha tabia “sober houses” kwa ajili ya vijana walioamua kuachana na matumizi ya dawa hizo.

Alisema hayo ni mafanikio y a l i y o p a t i k a n a t a n g u kuanzishwa kwa mpango huo kwa miaka mitatu iliyopita.

Hata hivyo Maalim Seif amesema mafanikio hayo hayatokuwa endelevu iwapo harakati za usafirishaji, uingizaji na matumizi ya dawa za kulevya hazitoendelea kupigwa vita.

Alisema kuna hatari ya vijana kuendelea kuwa wahanga wa matumizi ya dawa za kulevya iwapo juhudi za serikali za kuleta

maendeleo hazitakuwa na tija.

Aliongeza kuwa hatma ya Taifa inategemea zaidi vijana wenye mwelekeo makini na waliojiepusha na matumizi ya mihadharati kwa vile wao ndio nguvu kazi kubwa ya

taifa.Amewata wajumbe wa

Tume hiyo kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo yaliyomo kwenye kauli mbiu ya “Zanzibar bila ya dawa za kulevya inawezekana”.

Februari mwisho wa kuhamia digitali ZanzibarInatoka Uk. 1Channel zipatazo 36 zitapatikana kwa uhakika ambapo kutakuwa Channel za hapa nchin i , michezo, burudani ya tamthilia na sinema za Kiswahili, Kiarabu Kihindi na Kizungu. Alisema pia kutakuwa na Channel nyingi za habari kama vile BBC, CNN, Al-jazira, Deutschewelle, CCTV na nyenginezo.

Waz i r i huyo a l i s ema serikali ya Mapinduzi Zanzibar inafanya kila jitihada, kuona kwamba wananchi hawana sababu ya kuhamanika na kununua ving’amuzi ghali na

dhaifu hivyo aliwahakikishia kwamba, wataalamu wa serikali wanahangaika ili kuona kituo cha televisheni cha ZBC TV wanaendelea kukiona bila ya usumbufu hadi Februari 28,2013.

Waziri Mbarouk, alisema mabadiliko ya mfumo wa matangazo ya analogue kwenda digital, yamekuja kufuatia agizo lililotolewa na Shirikisho la Mawasiliano la Afrika Mashariki (EACO) kuwa, nchi wanachama wa Shirikisho hilo zinatakiwa ziwe zimehamia katika mfumo wa digital ifikapo mwaka huu.

Page 12: Gazeti la Alnuur

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.

AN-NUUR12 SAFAR 1434, IJUMAA JANUARI 4 - 10, 2013

Usikose nakala yako ya AN-NUUR kila

Ijumaa

KATIBU Mkuu wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu (T) Sheikh Ramadhan Sanze, amewaasa Wais lamu kwamba huu si wakati wa kulalamika kupitia historia na mwenendo wao nchini, bali ni wakati wa kupanga mikakati ya kutenda.

Sheikh Sanze , ametoa ushauri huo mwishoni mwa wiki iliyopita katika kituo cha Kiislamu, Mwenge Jijini Dar es salama, wakati alipokuwa akizungumza katika mahafali ya nne ya kuhitimu wakufunzi wa Kutayba, yanayoendeshwa na kusimamiwa na Baraza hilo kwa lengo kuendesha vikundi vya fedha vya Kutayba Saccos na Kutayba Vikundi.

Sheikh Sanze, al isema k w a m u d a m r e f u s a s a Waislamu wamekuwa katika hali ya kulalamika kuwa wamedhulumiwa baada ya kupigania uhuru, jambo ambalo linawapotezea muda wa kufikiri juu ya hatua za kuchukua baada ya kubaini dhulma hizo.

Alisema historia hiyo ipo sahihi na itabakia hivyo tu, lakini haitusaidia isipokuwa ni kuitumia kwa kupata ari ya kufanya vizuri zaidi.” Alisema Sheikh Sanze.

Alibainisha kwamba kwa sasa hakuna haja ya kulalamika wala kunung’unika baada ya kubaini kuwa kuna tatizo, zaidi Waislamu wajipange upya ili mambo yao yaende.

“Mwenyezi Mungu katika Qur an, amewataka Waislamu wasihuzunike, wasilalamike wala wasiogope kwa kuwa wao wapo juu, lakini ikiwa tu ni waumini”. Alitoa somo Sheikh Sanze.

Kupitia Kutayba Vikundi na Kutayba Saccos, sasa Waislamu wameanza kuonyesha njia ya kutambulika kwenye vyombo vya fedha , kwani tayar i wameanza kuwakimbi l ia baada ya kuona kuna watu wameanza kuonyesha juhyudi zao wenyewe, hivyo wanaona wakisaidiwa watafanya vizuri zaidi.

Alisema awali mpango huo ulikuwa katika vichwa, kisha kuhamishiwa katika makaratasi na baadae uliingizwa katika utendaji na matokeo yake yameonekana kwani hapakuwa na utaratibu kama huo kwa Waislamu nchini.

Sheikh Sanze alifafanua zaidi kwamba unapouwezesha umma wa Kiislamu, unakuwa umewezesha zaidi ya asilimia 50 ya Watanzania, na zaidi utakuwa umeisaidia Serikali tawala kuinua hali za kiuchumi wa raia wake.

Mpaka sasa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu (T), chini ya Kutayba

Ujasiria mali washika kasi Baraza KuuZaidi ya milioni 400 zatolewa mikopo Na Bakari Mwakangwale imewezekana kuwakopesha

Waislamu kupitia vikundi zaidi ya shilingi milioni mia tano.

Akitoa nasaha zake kwa wakufunzi wa mafunzo ya wanakutayba, Sheikh Sanze, aliwaeleza wahitimu hao kuwa, kuhitimu kwao ni mwanzo wa mafanikio makubwa iwapo wanataka.

Kwa upande wake Sheikh Mtoe, alitanabaisha kwamba pamoja na mafanikio yenye tija ambayo yanaanza kuonekana k w a Wa i s l a m u k a t i k a kujiletea maendeleo, lakini wasijisahau kwani kuna wenzao wameshapiga hatua kubwa kuliko hiyo waliyofikia.

Aliwataka wakufunzi hao kuhakikisha ki la mmoja, ahakikishe kwamba mipango na mikakati hiyo ya Kutayba Vikundi na Kutayba Saccos, anaifikisha katika Msikiti wake na kuizalisha kwa wengine ambao hawajabahatika kuipata taaluma hiyo.

Naye Ustadhi Iddi Uvuruge, ambaye ni Meneja mikopo wa Kutayba Saccos, alisema mpaka sasa wana matawi takriban 23 katika mikoa yote nchini na baadhi ya Wilaya.

Alisema kupitia Kutayba, zaidi ya shilingi Milioni mia nne, zimetolewa kama mikopo kwa wanachama mbalimbali wa Kutayba Saccos nchini.

Ustadhi Uvuruge, aliitaja mikopo hiyo kuwa ni pesa tasilimu, vifaa vya ujenzi, pikipiki zaidi ya mia moja, magari, bajaji pamoja na nyumba.

Akianisha aina ya mikopo wanayoitoa, aliitaja kuwa ni Karbanhasana (mikopo mema), inayohusiana na pesa tasilimu kuanzia elfu ishirini hadi milioni moja. Katika mkopo huu, mwanachama akikopa kiasi hicho anatakiwa kurejesha kiasi hicho hicho bila kuongeza kiasi chochote.

Aina ya pili ya mikopo ni Mudhwaraba (Mikopo ya kibiashara). Hii ni mikopo inayozidi kiasi cha shilingi milioni moja. Mkopo huu haitolewi pesa tasilimu, bali mwanachama hukopeshwa bidhaa, vifaa, magari au hata nyumba kulingana na mahitaji ya mwanachama.

Akizungumzia changamoto wanazokumbana nazo, meneja huyo alisema baada ya huduma hiyo kuwafikia Waislamu wengi nchini, kumekuwa na ongezeko kubwa la Waislamu kutoka sehemu mbalimbali wanaohitaji kufikiwa au kufungua Kutayba zao.

Changamoto ny ing ine ni uelewa mdogo wa jamii hususani katika mikopo hii ya Mudhwaraba, ambapo ule utaratibu wa kununua kitu kisha ukamkopesha mwanachama kwa bei ya juu anadhani kuwa bado hiyo ni riba.

WA Z I R I w a H a b a r i , Utamaduni, Utalii na Michezo Bw. Said Ally Mbarouk, amesema kuwa uhamaji kutoka katika mfumo wa matangazo wa analogue kwenda digital utakamilika rasmi ifikapo Februari 28 mwaka huu, ambapo mitambo ya analogue katika kanda ya mikoa mitano ya Zanzibar itazimwa. Bw. Mbarouk, aliyaeleza hayo wakati akizungumza na waandishi wa Habari katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Kikwajuni, mjini Zanzibar.

Alisema kuwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Kamisheni ya Utangazaji Zanzibar (ZBC), pamoja na taasisi zinazohusika na shughuli za utangazaji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, zimeshauriana juu ya namna Taifa la Tanzania litakavyoingia katika mfumo wa digital kwa

Februari mwisho wa kuhamia digitali Zanzibar Na Nassor Khamis,

Zanzibarawamu, ambapo kwa Zanzibar utakamilika Februari mwakani badala ya mwishoni mwa mwaka huu.

Katika kukamilisha kuingia katika mfumo wa utangazaji wa digital, Waziri Mbarouk alisema kuwa Wizara ya Habari imefanya kazi kwa mafanikio makubwa ikiwemo kujenga kituo cha usambazaji mawimbi (signal) katika eneo la Rahaleo pamoja kutayarisha maeneo ya kurushia matangazo ya digital katika visiwa vya Unguja na Pemba.

Aidha alisema kuwa Wizara imeandaa utaratibu wa kuwepo msambazaji mawimbi (signal) wa serikali ambao utafanya kazi kwa ubia na Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, Shirika la Utangazaji Zanzibar na Wizara ya Fedha Uchumi na Mipango ya Maendeleo, pamoja na kuandaa utaratibu wa upatikanaji wa ving’amuzi na maudhui kwa bei nafuu.

Aidha alisema kuwa uzinduzi wa mitambo na matangazo ya digital utafanyika wakati

wa sherehe za Mapinduzi, ambapo tukio hilo limepangwa kufanyika Machi 08, 2013 Rahaleo, mjini Zanzibar pamoja na kusambazwa kwa ving’amuzi katika wilaya zote za Zanzibar kwa ajili ya majabio.

“Tutasambaza ving’amuzi vichache katika Wilaya zote za Unguja na Pemba, ili mafundi wetu waweze kuangalia kama matangazo hayo yanaweza kupokewa katika pembe zote za Zanzibar.”alisema Waziri Mbarouk.

Alisema kuwa ving’muzi kwa ajili ya matumizi ya wananchi vitaanza kuuzwa mwishoni mwa mwezi wa Januari kwa bei ya shilingi 50,000, vikiwa na punguzo la shilingi 22,000 kutoka bei halisi ya ving’amizi hivyo na kutakuwa na kulipia ada ya shilingi 8,000 kwa mwezi mmoja.

Vi n g ’ a m u z i 3 0 0 , 0 0 0 vinatarajiwa kuuzwa katika kipindi cha miaka miwili.

Alisema kuwa ving’amuzi hivyo vitakavyosambazwa,

KATIBU Mkuu wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu (T) Sheikh Ramadhan Sanze.

Inaendelea Uk. 11